Saturday, November 29, 2008

Them, I, & Them. MORGAN HERITAGE ......... A Man Is Still A Man

Nikiwa na Gramps Morgan baada ya onesho lao la kutangaza albamu yao mpya ya Mission In Progress.
"A man is still a man whether him wear jacket and tie, or walk barefoot.The only difference is whether him good or evil.
A man is still a man whether him rich or poor black or white for sure.The only difference is whether him good or evil."
Pengine liwe funzo kuwa hatuwezi kuwaweka watu kimakundi kwa mwonekano wao wa nje. Ni yale wawazayo na kutenda na namna yanavyoathiri jamii ndivyo tunavyoweza kuwaweka katika makundi makuu mawili ambayo ni watenda mema ama mabaya. Hapa Morgan Heritage wanatukumbusha kuwa maisha ama namna tuendeshavyo maisha yetu na kupata kipato chetu cha kila siku si sababu ya kuwafanya wengine wadharauliwe ama wengine kujiona bora zaidi kwa kuwa tu wanafanya kazi masaa machache na muda ambao kila mtu anautamani. Ndivyo Jah Petes asemavyo kwenye ubeti wa kwanza kuwa "Lots of different people on the streets wiping car glass windows. This is what they do day to day just to get a little food to eat. Then you have others wearing suit and tie, work a good nine to five. And they take it for granted that they're living a better life" Ni kote kote duniani ambako kuna watu ambao hawawathamini watu kwa vile tu maisha yao ni "mema" zaidi ya wenzao. Ni jambo ambalo wengi wanasahau kuwa aliyewapa wao ndiye anayeendelea kufungua milango kwa wengine wanaoonekana kama hawana (sijasema amewanyima wengine), na kuwa kila mtu ana namna amzidivyo mwenzake katika mambo fulani mbele ya jamii fulani. Tutambue kuwa tofauti za rangi ya ngozi zetu hazimaanishi lolote juu ya yale tuwezayo kutenda kwai sote twaamuliwa na Mungu mmoja, hivyo twastahili kuchunga yale tutendayo kwa wale tusiowajua. Petes anaendelea kusema "I say the color of our skin don't mean a thing if we do good or commit to sin.We're all judged by the same, and Jah is his holy name.So lets all be aware of how we entertain angels unaware.For angels do move through men, whether here or from there". Kwa hiyo bila kujali Daraja la Maisha, Imani wala Rangi za mwili wetu, twapaswa kutambua kuwa tuna jukumu la kuishi maisha sahihi yenye heshima na kuwajali wengine kwa kuwa sote tu sawa mbele ya macho ya Muumba. Na haya ndiyo asemayo Gramps anapoimba kwenye "bridge" kuwa "Everyman has freedom, ya.For the wealth of a man. Be sure when living life. We treat all men right.For we are all of the same. In the MOST HIGH'S EYES"
Ni vema tukajifunza kuwathamini na kuwaheshimu watu FOR WHO THEY'RE AND NOT WHAT THEY ARE sababu the only Difference is whether them good or evil
Bofya Player hapa chini kusikiliza wimbo huu.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, November 27, 2008

Hotuba: Julius Kambarage Nyerere (pt 3/3) MWISHO

Sehemu hii ni ya tatu na ya mwisho katika mfululizo wa hotuba ya Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa katika hoteli ya Kilimanjaro (Kempinski) siku ya Jumanne, tarehe 14 Machi 1995. Kwa marejeo ya sehemu ya kwanza bofya hapa na kwa sehemu ya pili bofya hapa . Sehemu ya tatu ipo hapa .
Subi

Wednesday, November 26, 2008

What if we "what ifs" positively?

Pengine swali la kwanza ni "What if Mubelwa angeandika heading hii kwa kiswahili?'
Na ningejibu kuwa yawezekana usingevutiwa nayo, ama isingeweza kuleta maana nitakayo, labda usingethubutu hata kusoma maana yawezekana umeshtushwa na kichwa hiki cha habari u labda unasoma maana unataka kuelewa yamaanisha nini kwa kuwa ni kama haieleweki.
SAFI.
Ndilo lengo kukufanya usome maana ukiangalia uwezekano wa maswali mengi, utagundua kuwa yatakuwa ni "negatives" zaidi.
Lakini hapa lengo si kueleza sababu ya kichwa cha habari. Hapa nataka kuuliza mawili matatu juu ya hali halisi ya utata ambayo imekuwa ikituyumbisha katika maisha yetu. Ni ile hali ya kuogopa na kuhisi kitu kisicho cha mafanikio kitatokea katika kile ambacho mtu anataka kufanya.
Kuwa na ile hali ya kutanguliza kushindwa katika mipango mipya na ni hali hiyo ambayo inatukatisha tamaa na kutukwamisha wengi.
 Kuna mtu aliniambia "your mental picture will determine your actual future" na ni katika hili tunapojijengea maanguko kwenye mipango yetu mipya kwa kuuliza "what if" isipofanikiwa? Labda tujiulize ni mara ngapi tumetaka kufanya kitu kisha tukaamua kuacha kwa kuambiwa hatutafanikisha ama kujiambia wenyewe "itakuwaje nisipofanikisha?" Tusilojua ni kuwa kwa kutofanya ama kuanza kufanya vitu hatutakutana na CHANGAMOTO zilizo muhimu katika kukua, kukomaa, kupevuka na kuendelea kwetu.
Ina maana kwa kutofanya yale tupendayo tukihofia kutofanikiwa tunajifungia milango ya kuendelea kwenye maisha yetu na hilo linafanya wengi wasiopenda kujaribu ama wanaoshindwa kujaribu kwa kuhofia majibu mabaya ya "what if?' kushindwa kutimiza ndoto zao kwa kufanya kazi wasizo na mwito nazo, jambo linalowafanya wakose ubunifu unaostahili na kisha kuifanya kazi kutokuwa ya furaha kama ambavyo ingestahili.
Hili linayafanya matokeo ya kazi kutokuwa katika kiwango kinachotakiwa na kusababisha jamii kutopata "matunda" halisi ya kazi hizo.
Natambua kuwa jamii ingenufaika kama kila mtu angeweza kufanya kile apendacho na ni rahisi kufanya hivyo tukiacha kukatishana tamaa kwa kutilia mkazo na kuulizana "matokeo hasi" (negative results) za kile tutakacho kufanya. Mtambuzi Shabani Kaluse aliwahi kuzungumzia juu ya hofu ya kesho kuwa kama dubwana la kutisha
Sasa naamini twatambua kuwa kuna maswali ya kujiuliza katika harakati zetu za kuikwamua jamii na langu ni "what if we 'what ifs' positively"? Nadhani itasaidia kuwafanya watu waamini katika ndoto zao na kufanikisha mengi kwenye jamii.
Ni mtazamo tu

Tuesday, November 25, 2008

Wazazi katika uchaguzi wa majina.

Pengine niifanye hii kuwa "SPECIAL". Na kama ntaulizwa kwanini ntajibu ni kwa kuwa ni kutoka kwa watu special juu ya kitu special. Yaani waliochagua jina nao wana la kusema kuhusu uchaguzi wa jina. Wazazi wangu wanasema

"Ni kweli kuwa ni vigumu kumwambia mtoto maana ya jina pale unapompa lakini ni kweli pia kuwa mtoto akipata ufahamu anaweza ama kujisikia vema au vibaya kutokana na jina alilopewa na wazazi, hii huwalazimisha wazazi kutafakari maana kabla ya kutoa jina. Maana hata kama jina laonekana kuwa limepinda au la kimizengwe, huwa kuna sababu za jina hilo na wazazi wakiulizwa maana wanaweza kusema. Ni vema kuchagua kwa makini jina la mtoto, maana katika kutoa jina si vema kuangalia mambo ya karibu sana na yanayopita, bali ni vema kujua kuwa jina lenye laana hulaani na lenye baraka hubariki.
Tunakutakia yaliyo mema na kama jina lako lilivyo basi uendelee kubarikiwa na kuneemeka. Hizi ni sala za wazazi wako."

Maoni ya mchambuzi Kaluse katika Majina.

Kutokana na mazoea kuna ukweli juu ya hilo( la majina kuathiri mstakabali wa maisha yetu.). Niliwahi kufanya utafiti wakati fulani juu ya dhana hiyo, nikaja kugundua kuwa majina yamepewa nguvu kutokan na watu kuamini katika hizo imani. Kiutambuzi jambo lolote likipewa nafasi katika jamii na kuaminiwa linakuwa na nguvu, ndio sababu ya watu wengi habudu mizimu na kwendakutambika katika makaburi kwa kuamini kwamba mambo yao yataanyooka, na hii inahusisha hata wale watu walioshika dini. Kwa kuwa wameaminishwa kwamba bila kutambikiamizimu hakuna kufanikiwa, basi dhana hiyo inakaa kwenye ubongo wa kina na hapo ndipo imani hiyo inapokuwa na nguvu kwelikweli. Kwa mfano uliotolewa na dada Yasinta, yote hiyo ni imani za kutengeneza tu, hakuna ukweli wowote.Kwangu mimi jina ni jina hakuna jina baya balitafsiri zetu ndio mbaya. Nimeshangaa kumsikia mwana utambuzi mwenzangu Kamala kwamba ilibidi aachane na jina lake la ubatizo kwa sababu eti lilikuwa halimfai, kwa bahati mbaya hakusema kwamba lilikuwa halimfai kivipi? kama angesema lilikuwa na mkosi, ningejua nimsaidie vipi mwanutambuzi mwenzangu lakini hakutoa sababu.Ipo mifano mingi inayodhibitisha nguvu hizi za kutengeneza>Kwa mfano Nchini Marekani, wanaamini kwamba mtu hawezi kupata Urais kama jina lake halina herufi G, O au W, na ndio sababu ukichunguza marais waliotawala katika nchi ile majina yao hayakosi herufi hizo. Na hapa nchini kwetu inaaminiwa kuwa Herufi M ndio inatawala, kwa hiyo ukichunguza marais wetu wote majina yao yana Herufi M.MWALIMU JULIAS KAMBARAGE NYEREREALI HASSANI MWINYIBENJAMINI WILLIAM MKAPAJAKAYA MRISHO KIKWETE.Na hata kwa upande wa mawaziri wakuu ni hivyo hivyo.Naomba kuwasilisha.
Mtambuzi, Shabani Kaluse

Shabani Kaluse ni Mtambuzi anaye-blog habari za kina juu ya utambuzi kupitia blog yake unayoweza kuitembelea kwa kubofya hapa

Monday, November 24, 2008

Ni kweli majina yetu huathiri mustakabali wa maisha yetu?


Kama maana tusomazo ndizo halisi. Basi swafi.

  Kama kweli majina huathiri maisha yajayo, basi siku saba baada ya kuzaliwa nilishasaidiwa kuchagua mustakabali (future) yangu
Unapopewa kazi ya kumtafutia mwana jina huwa unaanza na nini? Haya umeshajua jinsia kinachofuata ni nini? Historia ya maisha ya wazazi? Tukio kuu la wakati huo? Jina la wazazi wa wazazi wake ama?
Sijapata nafasi ya kuuliza hili kwa wazazi wangu kujua walikuwa na majina mangapi ya kuchagua na kwanini walifikia uamuzi wa kuniita niitwavyo na si vingine? Labda nikijua hilo na kujua kwanini wanaitwa waitwavyo itaepusha ama itanipa nafasi ya kutumia ama kutotumia majina yao kwa wanangu na ama nikiwaeleza wanangu juu ya majina yangu wataweza kujua kama kuna umuhimu wa kutumia ama kutotumia majina yangu kwa watoto wao.
Tunajua kuwa jina lako laweza kuwa chanzo cha kukosa baadhi ya itu ama nafasi. Kwani si bado tunakumbuka jinsi jina la kati la Rais Mteule wa Marekani la Hussein lilivyokuwa likitumiwa kuwatisha watu wasimchague? Lakini pia swali ni kwamba, ni kweli kuwa tabia za ndani za watu zaweza kuathiriwa na jina la mtu? Yaani kumuita mtoto SHIDA ama MATATIZO ama TABU kunaweza kusababisha awe na maisha ya hivyo? Kwani ukimuita mtoto OSAMA inampa tabia za kigaidi? Ama kumuita mwana HITLER kunaweza kumfanya awe mkatili kwa jamii fulani? Sasa mbona kuna watu wanapata watoto na kukata baadhi ya majina wakiamini kuwa watoto wao hawatakuwa watu wema wakiitwa majina hayo? Lakini pia, ni kweli kuwa majina hufanya tabia za watu zifanane? Yaani tukitafuta kina Mubelwa kama kumi kuna uwezekano tukawa na mfanano wa tabia? Ni kweli? Na kama ni kweli hufanana kwa tafsiri ipi? Mfano tafsiriya Mubelwa kikwetu ni tofauti na ile ipatikanayo kwa wanazuoni wa majina? Tumeona wengine wamezaliwa na kuitwa Obama siku ya uchaguzi wa Marekani, sijui tutegemee nini wakikua na sijui kwa utaratibu wa kuwaita majina ya babu zai itakuwaje kwa wajukuu zao kuitwa Obama bila hata kujua kwanini babu zao wameitwa hivyo. Na sina hakika kama kuitwa tu bila hata kujua maana ya jina lao (kama ilivyo kwa wengi) kunaweza kumfanya mtoto aamini maisha yake yanaenda na maana ya jina lake. Vipi walioitwa CCM? VALENTINE je? Ambaye alizaliwa tarehe 14 Februari; nami nimwite mwanangu Valentine kwa kuwa mwenye jina ni rafiki sana hata kama kazaliwa Oktoba 8?
  Well! Nimekuwa na bahati sana maishani mwangu na jina langu lamaanisha hivyo katika tafsiri ya kikwetu, lakini sina hakika kama nimeona hivyo kwa kuwa natamani iwe kweli ama ni kweli iko hivyo kwa kuwa wazazi wangu waliniita jina langu.
Hapa sina hakika kama naliona tatizo, ila bado naamini kuwa kama lipo, basi kila alionaye ataona tatizo.
Blessings

Saturday, November 22, 2008

Katika Jina la Demokrasia.

Salamu za marejeo toka kwake Msangi Mdogo

Wapendwa katika jina la Watanzania. Amani iwe juu yenu. natumai wote muwazima.
Hii ni kuwataarifu rasmi kuwa, baada ya kimya cha muda mrefu sana, mahangaiko ya hapa na pale na mambo mengine, hatimaye ndugu, kijana, mpiganaji, muungwana na mpigikaji mwenzenu nimerejea ulingoni. najua kuna ambao walikuwa wangali wakinisaka katika www.msangimdogo.blogspot.com....... na najua kuwa kuna wale ambao watakuwa huenda ni wapya kabisa katika taarifa hizi. Ila nyote kwa ujumla, napenda kuwataarifu rasmi kwa, maskani yangu kwa sasa ni www.uchambuzi.blogspot.com
Kuna kitabu cha wageni pale, makala zangu zilizotangulia ambazo zilitoka katika sehemu mbalimbali nilizozurura nakadhalika. Ila hatimaye, nimeamua kutulia hapo. nawakaribisheni sanjari na kuwaomba muwafikishie ujumbe huu "Blogaz" wenzenu ambao mnawafahamu, pamoja na kuniwekea taarifa hizi katika blogi zenu kwa wale watakaoweza.
Mwisho kabisa, naomba wale ambao viungo vyao (link za blogi zao), haziko katika blogi yangu, wanitumie kwa mail ili niweze kuviweka pale, maana nataka kila mtu niwe na anwani ya kuingia kwenye maskani yake kwa urahisi. na kwa wale ambao wana nembo, pia wanaweza kunitumia ili zikae pale kama zilivyo za dada katabazi, Bongo Celebs nk.
Amani iwe juu yenu
Msangi, Ramadhani S.

Kaka. Ni katika jina jema lenye Amani, Heshima na Upendo twakukaribisha tena. Uwanja ni mwema, msafi na wenye uelimishaji. Blogs zaendelea kukwamua na kuonesha yale ambayo yanatakiwa na jamii na kwa namna hii tunaelekea ambako tutajivunia kuwa kweli sasa hizi ni Blog za jamii, kwa jamii. Na hii yastahili kuwa CHANGAMOTO YETU sote wenye kumiliki Blogs. Yaani kuwa sauti za wale wasioweza kujisemea.
  Tuko Pamoja Kaka

  

Thursday, November 20, 2008

Hotuba: Mwl Julius Kambarage Nyerere Pt 2


Wiki iliyopita tuliisikiliza sehemu ya kwanza ya hotuba bofya hapa kuirejea aliyoitoa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hoteli ya Kilimanjaro (Kempinski) mnamo siku ya Jumanne mwezi wa Machi tarehe ya 14 ya mwaka 1995.
Hii Bofya hapa ni sehemu ya pili kati ya sehemu tatu za hotuba hiyo.

Subi
www.nukta77.com & nukta77.blogspot.com

Asante sana Da Subi

Tuesday, November 18, 2008

Natamani kuwa mwalimu. Shule iwe UN na wanafunzi ma-Raisi

Ingenichukua muda kusahihisha Homeworks, lakini wote wangefanya VEMA dunia ingekuwa sehemu bora ya kuishi kuliko ilivyo sasa.

Napenda old style ya ualimu ambapo walimu walikuwa wanajua uwezo wa takribani kila mwanafunzi. Walikuwa wanahakikisha kuwa kila mtu anafanya "homework" yake na walikuwa wanasahihisha siku inayofuata. Walimu walikuwa na uwezo wa kutambua kama umefanya mwenyewe homework yako ama umefanyiwa. Halafu kingine nilichokuwa napenda ni ile style ya kubandika matokeo darasani. Yaani kujua nani kawa wa kwanza na nani wa mwisho. Hapo ilikuwa ni lazima usome sana maana ni kuangalia nani ana VEMA nyingi na nani anaongoza darasa. Lakini kwa mtazamo wangu ilikuwa na faida maana yaliyotendeka ilikuwa ni CHANGAMOTO KWETU kuongeza juhudi katika masomo.
Style hii ningeipata nikaweza kuitumia UN naamini ingesaidia saana. Yaani kuhakikisha kila maraisi wanapoondoka wanapewa "homework" ya kufanya nchini mwao na wakirejea kwa "darasa" (kikao) kijacho kwanza tunaangalia nani kafanya nini na kafanikiwa mangapi kisha tunasonga mbele. Yaani kujua nani anajua na kutatua matatizo ya nchini mwake na kuwasaidia wananchi wake na pia tungejua nani hana ajualo kuhusu shida na mahitaji ya wale awaongozao. Ingetuwezesha kujua nani yuko mstari wa mbele kubadilishana mawazo (pale nitakapowapa group discussion ya kukokotoa maswali) na kutumia "ideas" za wenzake kufanya homework zake kuwasaidia wananchi wake. NINA UHAKIKA kwa mfumo huu lazima ULIMWENGU ungekuwa hatua kadhaa mbele kuelekea kwenye mafanikio ya kutatua shida za wenye uhitaji.
Kwani wanapokutana huwa hawapewi majukumu ya kutekeleza? Ama wakipewa wanaweza kuyatekeleza bila kuwaeleza wananchi? Lakini kama ni majukumu kwa wananchi si tungeona mabadiliko huko tuliko? Namaanisha hata kama hatuambiwi si tungejua kuwa "ujenzi wa hizi zahanati ni manufaa ya raisi kwenda kwenye mkutano wa mwaka huu?" Najiuliza kama kuna mwananchi anayeweza kujibu akiulizwa amenufaika nini na raisi wake kwenda kwenye vikao vya Umoja wa Mataifa na vingi" Sisemi hatujanufaika, ila kama manufaa hatuyaoni bayana na hatuambiwi pia, sijui tufikirieje matumizi ya kodi zetu!

Anyway, japo kuna ukweli ndani yake, lakini nafikiri hii ni njozi. Never Mind!!!

Monday, November 17, 2008

HAPPY BIRTHDAY MAMA


" We each get just one MOTHER to love a lifetime through, One MOTHER to encourage us in everything we do. But one MOTHER is so many People blended into one. A source of inspiration and happiness and fun. A MOTHER hears out every word. She listens with her heart, shares and always cares, thinks of others first and she'll love us just like always even when we're at our worst. She brings such happiness with kindness she gives and creates a GOOD EXAMPLE simply with the life she lives. YES! We only have ONE MOTHER to look up to and to praise and NO ONE ELSE IN ALL THE WORLD can MATCH HER LOVING WAYS"

Namna siku zinavyokwenda ndivyo tunavyozidi kuangalia nyuma na kutambua umuhimu wa yale yote mliyokuwa mkitufundisha. Tunayatambua kwa kuwa yanatusaidia sana maishani popote tulipo ambako ni mbali nanyi.
Ni malezi ambayo mlitupatia katika muda wote tuliokuwa chini ya uangalizi wenu ambayo yanatuwezesha kuishi popote tuendapo na ni msingi wa Heshima na Upendo pamoja na Imani mliyotujengea ambayo inatuongoza vema wakati wote.

Tangu siku hii ya kwanza uliponitwaa mikononi mwako mpaka siku hii tunayopishana kidogo kimo, bado waendelea kuwa Mama yuleyule mwenye upendo usiopimika.
Mama; waweza kutokuwa maarufu kama wengine, kutoonekana na kusikika kama wengine, lakini utambue kuwa hata katika usiri wa maisha yako, wewe bado ni SHUJAA wa maisha yetu na wale wote tuhusianao nao na kwa hakika TUNAJIVUNIA wewe kuwa MAMA yetu. Tunakupenda na kukuthamini na tunakutakia kila la kheri katika kukumbuka siku yako ya kuzaliwa na pia katika miaka ijayo yenye afya na nguvu tele.

HAPPY BIRTHDAY MAMA
Na huu ni wimbo kwa Mama, toka kwao Boys II Men . Blessings

Sunday, November 16, 2008

Rockaway Subi

Thanx alot Sis Subi. Najua wapenda za kale, nami nakukumbusha alizokumbusha Beres Hammond kwenye wimbo wake Rockaway. Remember ol' good days?
One done, one down and many more to go.
Thanx again Subi


Chorus
Oh yeah, oh I miss those days yes
I miss those days yeah
Remember the songs
Used to make you rock away
Those were the days
When love used to reign, hey
We danced all night to the songs they played
Weekend come again, do it just the same

Verse 1

Now I feel it to my heart
Being such a golden time had to part yes
Now there's hardly any safe place left to go
Someone's bound to come
And try to spoil the show, oh oh

Chorus

Remember the songs
Used to make you rock away
Those were the days
When love used to reighn
We danced all night to the songs they played
Weekend come again
We do it just the same, hey

Verse 2

Hail John Holt, Alton Ellis, Delroy Wilson, Dennis Brown, hey hey
Big Youth, Josey Wales,
Daddy Roy would wake the town, yeah
And you had to hold your woman real close When Smokey starts to sing
Temptations, Marvin Gaye,
Spinners all the way
Aretha Franklin
Patti Labelle used to make me drift away
Play Stevie play, Sam Cooke anyday, yeah
We dance all night to the songs they played
Weekend come again do it just the same

Right now we need a brand new start
People everywhere need more music,
From the heart
And if there remains such a place
That I can go
Will someone tell me tell me I want to know

Chorus

Remember the songs
Used to make you rock away
Those were the days
When love used to reign
We danced all night to the songs they played
Weekend come again
We do it just the same, hey
Remember the songs
Used to make you rock away
Those were the days
When love used to reighn
Danced all night to the songs they played
Weekend come again
We do it just the same
Remember the nights

Chorus

Remember the songs
Used to make you rock away
Those were the days
When love used to reighn
Danced all night to the songs they played
Weekend come again
We do it just the same, hey
Remember the songs

Saturday, November 15, 2008

Ni Maandamano yasioenda ama maonesho ya maombi?

Picha zote toka kwa Kaka Bernard Rwebangira wa www.bongopicha.blogspot.com
"Assert your right to make a few mistakes. If people can't accept your imperfections, that's their fault" Dr David M.Burns
" I am careful not to confuse excellence with perfection. Excellence i can reach for; but perfection is GOD's business" Michael J Fox
Naamini jina la Blog (The way you see the problem is the problem) na nukuu za hapo juu zitaongoza mtazamo wa hili nionalo mimi.
Nimelelewa katika mazingira na familia iliyothamini dini na imani na hakuna dini isiyohimiza maombi. Hivyo nami nimekua nikitambua na kufanya maombi, na sio tu kwa namna waonavyo wazazi na ama walezi, bali kwa mujibu wa kitabu Kitakatifu tuaminicho. Ni kitabu hicho hicho kinachozungumzia juu ya KUFUNGA NA KUOMBA pamoja na KUOMBA KWA ROHO NA KWELI.
Na ni katika haya ninapopata shaka na namna baadhi ya sehemu za maombi zinavyoendesha shughuli zao. Kufunga na kuomba halisi (ninavyofahamu mimi) ni kule ambako unakufanya ilhali humfanyi mtu mwingine asiyejua kinachoendelea katika "programu" yako ya siku kuona udhaifu wa mwili ama sura. Yaani asiyehusika asitambue mfungo kwa unyonge ama udhaifu wa mwili wako. Ni kufanya mfungo na maombi bila kuwa kikwazo ama shaka kwa wengine. Na Kuomba kwa roho na kweli ni kule ambako unakuwa sehemu ambayo umetoa muda, mwili na mawazo yako kwa ajili hiyo. Ni sehemu ambayo haikufanyi ufikirie kingine zaidi ya "muungano" wako na MUNGU.
Sasa nikirejea kwenye mkusanyiko kama huu ambao Jumapili iliyopita ulikutana kwa nia njema ya kuiombea serikali kufanya maamuzi bora nabaki na maswali kadhaa.
1: Hivi ni kweli kwamba waumini walikuwa wengi kiasi cha kuhitaji sehemu kama Mnazi Moja? Ama ni kutaka kuweka nguvu za pamoja katika maombi? Lakini si kama wana "sharika" wangeomba huko waliko na kusikika? Naamini kuwa MAOMBI YANA NGUVU NA MWENDO KASI kuliko tunavyoweza kufikiri.
2: Kama Waislamu nao wataendesha yao Ijumaa, kisha Hindu nao wakawa na yao kuunga mkono ama kupinga, kisha Wayahudi wakafanya, Bahai nao wakasaka siku yao, na wengine wenye imani tofauti wakaamua kufanya maombi yao, tutabaki tukiona hayo kama maombi ama majibishano? Na kama kuna uwezekano huo kwanini yaanzishwe?
3: Hivi kunakuwepo kuomba kwa roho na kweli wakati unajua kuna Kamera za picha na video, Kelele za magari na wapiga debe, dhihaka na pilika za siku zikiendelea? Kweli watu wata-concentrate kwenye maombi ya dhati bila kuogopa kuwekwa kwenye kumbukumbu ama wengine wataacha kuigiza kuwa katika maombi halisi ili wawekwe kwenye hizo kumbukumbu zitakazowaonesha kwenye magazeti, mitandao na televisheni mbalimbali?
Sina hakika na mtazamo wa wengine na sidhani kama ni lazima niendane na mtazamo wao maana kama hili ni tatizo basi kila mtu analiona toka katika upande wake na namna tuonavyo ndilo tatizo, na kama huoni tatizo katika hili, basi utaona tatizo kwa mimi kuliona tatizo na hilo litakuwa tatizo, maana namna uonavyo tatizo ndilo tatizo.
Kwangu sijaona umuhimu wa kufanya maombi ya kuiombea Serikali tena mahala kama Mnazi Mmoja. Naona tofauti ndogo saana ya hili na MAANDAMANO YASIYOENDA AMA KUTEMBEA na najitahidi kutoamini kilichopo kichwani kuwa kama hakukuwa na maombi halisi kulingana na mazingira, basi haya yaliyopangwa kuwa maombi kwa serikali yalikuwa MAONESHO YA MAOMBI
MUHIMU: Hapo juu ni mtazamo wangu na ushauri wangu ni kwamba, Ukiona tatizo soma jina la blog, ukidhani nimekosea soma nukuu ya kwanza na kama unadhani nafikiri niko sahihi angalia nukuu ya pili.
J'mosi njema



Friday, November 14, 2008

Them, I &Them. MAXI PRIEST ......... Cry For The Children

"Slow down everyone pay attention let us reason for awhile, I'm worried about this everyday killing that is turning into style. Don't try to convince its normal, playing with human lives. I Don't know about you but I know its brings tears to my eyes.
Ndivyo anavyoanza hivyo Maxi Priest kwenye wimbo wake huo unaozungumzia athari za vita kwa watoto na Mama zao. Ni mambo ambayo tunaona yanaendelea sehemu nyingi ulimwenguni ambako watoto wasiojua hili wala lile kuhusu vita wanalazimika kukimbia kila dakika kusalimisha maisha yao. Ni maisha hayo ambayo anayawakilisha kwa wahusika kuwa kuwauliza wafikiriacho kwa kuwa yeye sio tu analia, bali anaomba kuwa sala zijibiwe wawe huru kama asemavyo "And I cry for the childrenAnd I pray for themThat someday consciousness will once againBe the answer to our prayers "

ABC Image
Lakini Maxi ameanza kwa swali kwa viongozi wanaojitahidi kuifanya vita kama sehemu ya maisha tunayotakiwa tuikubali, na sasa anaendelea kuwauliza juu ya uwezekano wa siku tutakayoamka na kuliona jua bila hofu ya maovu na hujuma akiuliza "How many more lives do you need for your game? Cause we're counting. How many more mothers will you leave in pain?
Cause it's mounting. Could you give me a time or a day, how much longer will we have to wait, will there be sunshine and no trace of crime when I wake? Now I'm tired"
BBC Image
Ni "uchovu wa kuona maovu" alionao Maxi ambao kila mmoja anaushuhudia sasa hivi kwa watoto kugeuzwa chambo cha mauaji ya wakatili wachache wanaotaka kutawala na kusahau wao ni nani na wanawafanyia ukatili kina nani. Kupoteza utu wao kwa kusaka ubora na uimara wa maovu yao na hapa anasisitiza kuwa "Now I'm tired of all the goings on around us everyday. How did the little bitty innocent babies become pray, and by the way how could we allow ourselves to go so far, I'm almost certain we've forgotten who we are, I'm wide awake in a dream that never ends, and my heart cries out for help everyday".
Sina la ziada kwa kazi aliyoifanya Maxi Priest hapa. Ni AMANI, HESHIMA NA UPENDO na kwa hakika ndivyo Maxi Priest na kundi lake (THEM) wanavyoelezea hayo ambayo mimi (I) nimeyaona na kuyaweka kwa wahusika (THEM)

Waweza kujua zaidi juu ya Maxi kwa kubofya http://www.maxipriest.com/index2.htm . Bofya player hapa chini kusikiliza ujumbe mzito wake Maxi.

BLESSINGS

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, November 13, 2008

ISHIKE Radio part 10 from Dona Productions


ISHIKE Radio part 10 is uploaded and it has tons of New TZ/KE music.
Click the link http://www.djdona.com/mp3/DJ%20Dona%20ISHIKE%20RADIO%20Part%2010%20(YES%20WE%20CAN%20EDITION).mp3

Tracklisting
1. Intro
2. AY Feat P Square - Freeze
3. STL (Stella Mwangi) - Dreamer
4. Wahu feat Bobby Wine - Little things you do
5. Nonini Feat lady Bee- Kumbuka
6. K-Nel Feat Ben - ISHIKE RADIO Freestyle
7. Ngwair - Nipe Deal
8. Mejja, Mad Traxx, Jimwat - Mezesha
9. Chid Benz- King Kong
10. Big Pin feat Collo - Kadem
11. Bebe Cool Feat Gasuza- Sexy Thing
12. Mwasiti and Chid Benz - Haoo
13. Mad Traxx Feat Wyre- Serious
14. Fid Q Feat AY - Shimo Limetema
15. Kleptomaniax- Magnetic
16. Langa Feat Chidi Benz - Ninaposimama
17. Kaya - Fire Fire
18. Cloud Tissa Feat Nameless - Physically Fit
19. J Sha 4 - Play
20. Afande Sele- Heshima
21. Inspector Harun - Ndoa Haina Doa
22. Shena Feat Z-Anto - Fursa
23. Black Rhyno - Black Chata
24. Bombaa Clan - Does U R Mother Know
25. Blu 3 - Together
26. Kleptomaniacs Feat Ulopa - Psycho
27. Skool Fizz - Huku Majuu
28. Prezzo Feat Taz - Tupendane
29. Matonya feat FID Q - Taxi Babu
30. Ray C Ft Chidi Benz-Nihurumie
31. UB Feat Mr Lenny - Pesa
32. P-Square - Game Over
33. Grace - Anfuukula
34. Noorah - Mapenzi Sinema
35. Hydro - Swing That Back
36. Jua Cali featuring Mejja, Alahola, Rady, Ru, K-Solja and Linda
37. Alfayo - Physical
38. Bella - Faasi
39. G-Flow - Pepeta
40. Outro

Lazima tupande ndio tuvune. Yaani tuwekeze ndio tunufaike.

"Everyone wants to go in heaven; but nobody wants to die" Ni mameno ya Winston Hubert McIntosh ama Peter Tosh alipoimba kwenye Equal Rights. Kwa ufupi naona kama linalohimizwa hapa ni suala la kutaka kuweka bayana kuwa kama unahitaji chochote lazima kuwekeza gharama zitakiwazo.
Natazama "mfumo" wa serikali uliopo na najiuliza kama unatoa changamoto kwa watendaji kusaidia walio na uhitaji. Yaani kama Rais na wabunge wote wanachaguliwa kwa wakti mmoja ina maana ikitokea wabunge wakawa wengi kutoka katika chama cha Rais basi hata wasipotekeleza ilani za uchaguzi hakuna wa kuhoji kwa nguvu bungeni. Lakini pia najiuliza kama serikali ni kwa ajili ya wananchi si ina maana wanatakiwa wafanye kila lililo ndani ya uwezo wao kuwezesha wananchi kufanikiwa? Unadhani itawezekana kama kufanya kila liwezekanalo itamaanisha serikali kuhatarisha nguvu zake za kiutawala? Kimsingi tutasema NDIO lakini kiitifaki itakuwa HAPANA.
Lakini bado najiuliza kama tungekuwa na chaguzi tofauti, kwa maana Marais na wakuu wa mikoa wakachaguliwa miaka miwili na nusu kabla ya wabunge na madiwani si ingekuwa safi? Kwamba kwa nusu muhula tunawaangalia na kuwasoma viongozi waliopo madarakani na kama hawatekelezi lolote "tunawamwagia upupu" kwa kujaza wapinzani wao kwenye uchaguzi ujao. Ndhani hii ingeamsha UTEKELEZAJIwa ilani za uchaguzi na pia ingewasaidia wananchi kupata kile wanachohitaji kutoka kwa wawakilishi na viongozi wao.
Najua watasema ni gharama, lakini kama ndizo zitakazowasaidia wananchi kutoka kwenye umaskini na ujinga kwanini zisitumike? Kuna gharama gani zaidi ya kuwa na taifa lenye uhitaji mkubwa leo kama ambavyo ilikuwa miaka 37 iliyopita?
Gharama lazima zitumike kuokoa taifa maana NI LAZIMA TUPANDE NDIO TUVUNE, YAANI TUWEKEZE NDIPO TUNUFAIKE

Wednesday, November 12, 2008

Hatuwathamini kwa kuwa hatuwajui. Kwanini?

"Everyman must know their past, so we can stand firm in the future" Na haya yalisemwa na Morgan Heritage walipoimba juu ya KNOW YOUR PAST katika albamu yao ya More Teaching. Ni haya tunayokosa katika kujitambua ambayo "yanapelekea" kutotambua mlingano wa tulipo na tutokako. Na huu ni ukweli.
Hivi sasa inapofika Ijumaa, mimi na wenzangu wapenda "za kale" ama wengine wanaziita "zilipendwa" tunajimwaga ukurasa huu wa BONGO CELEBRITY kupata burudani hiyo. Ukiingia kwenye sehemu ya maoni utaona watu wanauliza hivi aliyeimba huo ni nani? Aliwahi kupigia bendi gani na wengine kutoa majina na miaka isiyo na hakika. Inasikitisha kuwa wasanii wetu NGULI ambao wamesaidia kuielimisha jamii, kuiburudisha na hata kutimiza matakwa ya viongozi kwa kuwakusanyia hadhira wanapojiandaa kuhutubia ama kukamilisha azma zao kama za Gezaulole wanasahaulika kwa kuwa tu wahusika hawafanyi wanalotakiwa. MASWALI NILIYONAYO
HIVI CHAMA CHA MUZIKI WA DANSI TANZANIA (CHAMUDATA) wako wapi kushindwa kuandaa, kutunza na kuenzi taarifa za wanamuziki wa Dansi nchini?
Kweli leo hii watu wanakosa habari, historia na hata kazi za wasanii walioiweka Tanzania kwenye ramani ya muziki barani kwetu? Leo hii tunakosa kuwajua kina Marijani Rajabu, Balisidya, Mbaraka Mwinshehe, Moshi William, Eddie Sheggy, Adam Bakari, Hemdi Maneti, Ndala Kasheba, Selemani Mwanyiro, Abeli Baltazar na wengine kwa kuwa tu hakuna pa kupata kumbukumbu zao?
Kweli kazi na maisha ya hawa wasanii mahiri yanapauka na kupotea kwa kuwa tu hakuna pa kupata kumbukumbu zao?
Kwanini Chamudata wasiwe na tovuti ya kueleza maisha ya wasanii WOTE wenye uanachama?
Nitasema ukweli kuwa wasanii waliojenga msingi wa sanaa nchini hawaheshimiki na kujulikana kwa kuwa wahusika hawafanyi wanalotakiwa kufanya.
Ni jambo la kusikitisha kuona wasanii wetu wamefanya kazi kuubwa sana wakati wa maisha na wapo wanoendelea kufanya hivyo, lakini HATUWATHAMINI KWA KUWA HATUWAJUI. Na swali ni Kwenini?
Huu ni MTAZAMO WA CHANGAMOTO YETU KWETU na ndivyo namna nionavyo tatizo. Labda ndilo tatizo.

Tuesday, November 11, 2008

Iwe "bifu" la kweli ama "gemu". Ubunifu bado ni ziro

Katika toleo langu la tarehe 30 mwezi Septemba niliandika yale ambayo kwa mtazamo wangu yanaathiri sanaa ya muziki wa sasa nchini Tanzania. Niliandika yale ambayo tumepoteza katika sanaa na ambayo tunaendelea kupoteza kila siku just kwa kuwa tunataka ama kuiga yatokayo nje ya nchi, ama kutengeneza pesa za haraka.

Lakini kuna kitu ambacho sio tu sikukifafanua vema, bali sikukikemea pia na kwa kuwa kinaendelea kujitokeza naona ni vema kuiweka bayana CHANGAMOTO YETU hiyo ili kuweza kukabiliana nayo.

Nimekuwa mfuatiliaji wa muziki kwa muda sasa na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wasanii wanavyokuj na tungo mbalimbali kutafuta heshima. Na kuna watungao yaliyomo kwenye jamii, kuna watungao kuburudisha na kuelimisha na kuna wale ambao wenzao wakishatunga, wao wanaibuka na tungo za kuwajibu. SI mnakumbuka Ngoni Tribe walivyojibu wimbo wa Jay Dee wa WANAUME KAMA MABINTI? Ama mwakumbuka "series" hii ya Sister P alivyopanda chati na ANAKUJA iliyoonekana kumjibu Zay-B. Naye Zay-B akafifia mpaka alipomjibu Inspekta Haruni kwenye wimbo wake NIPO GADO. Sasa majuzi Inspekta naye baada ya kuwa chini kafufuka na tungo ya kumjibu MwanaFA na wimbo wake NDOA HAINA DOA ambao waonekana kufanya vema kama ambavyo nyingine zote zilizofanya.

Hapa nieleweke kuwa sipingi kujibizana na huku kujibizana hakujaanza leo. Kujibizana imekuwa sehemu ya BIASHARA YA MUZIKI kwa miaka mingi na sehemu nyingi na wakati mwingine hupangwa ili kuboresha mauzo japo inapokuwa kweli huishia kusiko kwema kama ilivyokuwa kwa makundi ya Pwani ya Mashariki na Magharibi ya Marekani. Ila suala ni kuwa yaonekana utunzi wa wote hawa na wengine ambao sijawataja ni wa kusuasua na haiwezi kuwa rahisi kwa yeyote ambaye hajawahi kusikiwa wimbo unaojibiwa atakuwa hapati picha kamili na halisi ya kiimbwacho. Yaani ni "kukariri" sehemu ya maneno ya wimbo wa kwanza na kuyajibu moja kwa moja na ndio maana wanaojua wimbo uliojibiwa wala hawahitaji maelezo ya msanii kujua alikuwa akiimba nini ama akimuimba nani!

Labda niwakumbushe kuwa hata Tanzania majibizano hayakuanza jana na wala hayakuanzia kwenye Bongo Fleva ama Taarabu. Ila zamani nyimbo zilikuwa zina picha ambayo kama ulikuwa ukijua kinachoendelea basi ungejua kinachozungumzwa na kama hujui kinachojibiwa hapo unakuwa na taswira nyingiiine kabisa tena yenye mafunzo tofauti na mema kwa jamii. Kwa wale ambao hamkuwahi "kuchimba" maudhui halisi ya nyimbo, mnakumbuka MV. Mapenzi II ya Sikinde? Mnajua ilikuwa dongo kwa walioikimbia Sikinde kwenda kuanzisha Safari Sound? Je Chatu Mkali iliyowajibu Sikinde? Unakumbuka nyimbo Msafiri Kakiri ya Juwata? Unajua ilikuwa ni ujumbe kwa nani? Na Talaka Rejea ya Sikinde? Unajua lilikuwa jibu kwa nani? Lakini kama hujui kuwa kuna majibizano katika nyimbo hizo, huoni pia kuwa kuna mafunzo ya tofauti kwenye Mv Mapenzi inayoelezwa kama meli kwenye bahari yenye dhoruba, ama Chatu na sifa zake za uwindaji msituni, ama mtalakiwa anavyoeleza juu ya talaka rejea aliyopewa? Kwa taarifa yenu, hayo yote yalikuwa madongo lakini bado yalifikisha ujumbe kwa wahusika, yakaelimisha wasiohusika na ndio maana nasema watunzi wetu wa zamani walikuwa makini katika kazi zao na licha ya kuwa na zana duni za kutendea kazi, bado waliweza kuwa na ubunifu wa hali ya juu. Hata kwenye Taarabu kina Sanamu la Michelin, Mambo Iko Huku na nyingine zilikuwa zikiburudisha wasiojua majibizano na kufikisha ujumbe kwa walengwa.

Wasanii wa sasa lazima wakubali kuwa Pesa na kusaka matamasha ya haraka vinawapeleka pabaya. Ndio maana wote kati ya niliowataja hapo juu "hufa" baada ya "single" zao kuchokwa maana majibizano ya kitoto hayadumu.

Sitaki kujua kama kinachoendelea huwa ni "bifu" la kweli ama ni "gemu" la kusaka shows na attention ya media, lakini kwa lolote liwalo, UBUNIFU WENU BADO NI ZIRO.


Ni mtazamo wangu na ndivyo nionavyo tatizo, na yawezekana namna nionavyo ndilo tatizo.

Blessings

Monday, November 10, 2008

Hongera Miriam Odemba

Miss Earth 2008 Karla Henry
Miss Earth Tz Miriam Odemba

Mshiriki na mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kumsaka Miss Earth 2008 Miriam Odemba amefanya kile ambacho wengi walimtabiria. Kuwa miongoni mwa washindi wa shindano hilo.
Odemba ambaye ameshika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho kilichofika tamati jioni ya leo huko jijini Angeles, Pampanga nchini Phillipines, ameweza kuitangaza vema Tanzania kwa kushinda pia tuzo ndogo ya Miss Aficionado ambapo alikuwa mshiriki pekee toka Afrika aliyeshinda moja kati ya tuzo hizo 27 zilizowekwa kwenye kundi la Special and Minor Awards.
Kwa Odemba hii ni CHANGAMOTO nyingine baada ya kuwa amepitia maisha ya aina nyingi yenye vikwazo vingi na hatimaye akaweza kuvipita na kurejea katika kile anachokimudu zaidi. Urembo na Mitindo.
Twampongeza kwa kurejea katika kile amuducho na kumsihi kutumia taji hilo kama balozi mwema wa Taifa kutangaza hali ya kimazingira ambayo imekuwa mbiu kuu ya mashindano hayo yanayosemekana kuwa moja kati ya mashindano makubwa zaidi ya ulimbwende kwa idadi ya ushiriki wa nchi na washiriki wake hujihusisha zaidi na masuala ya kimazingira.
Mshindi wa shindano la mwaka huu ni Miss Phillipines Karla Paula Henry ambaye kabla ya kutwaa taji hilo, alishashinda Tuzo za Miss Earth Designers Award na Miss Photogenic.
Hongera Saaana Odemba

Sunday, November 9, 2008

Buriani Mhe. RICHARD S. NYAULAWA Marehemu Mhe Richard Nyaulawa
Katika picha hii ya March 20 2008, Makamu wa Ris Dk Ali Mohamed Shein na Mama Mwanamwema Shein wakimfariji Mbunge wa Mbeya Vijijini Mheshimiwa Richard Nyaulawa ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Indraprastha Apollo kwa matibabu ya Saratani (Cancer) ya utumbo wakati Dk Shein alipotembelea hospitalini hapo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo.

Nilipata bahati ya kumfahamu Mhe. Richard Nyaulawa kwa kufanya kazi katika kampuni ambayo alikuwa mmoja wa wakurugenzi wake ya Bussiness Times iliyo chini ya Bussiness Care Group of Comnpanies. Habari za kufariki kwake zilizotolewa leo zimekuwa za kusikitisha saana hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa bado anaendelea kuitumikia jamii na hasa jimboni mwake. Mbali na ubunge pia alikuwa mjasiriamali aliyeheshimika saana kwa kusaidia kunazisha na kuongoza baadhi ya makampuni yaliyojihusisha na masuala ya biashara na uchumi na pia kama mhadhiri katika Chuo cha Biashara jijini Dar.
Amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kwa awamu iliyoanza mwaka 2005.
Kila mtu anaweza kuwa na jema la kusema kuhusu Mhe. Nyaulawa, lakini kwa sasa naungana na ndugu, jamaa, marafiki, wanafunzi na wafanyakazi wenzake katika wakati huu mgumu na wa masikitiko.


MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI

Friday, November 7, 2008

Them, I & Them. NASIO .......... Truth Will Reveal

"You see their faces but you never know their thoughts,.. you see their actions but you never know their reactins, Time and Time-alone will prove the story and every eye will see, TRUTH WILL REVEAL"
Nimesema saana juu ya Nasio. Mmoja kati ya "darubini" kali za maisha ya wengi kupitia muziki halisi wa Reggae. Na japo nilimzungumzia wiki iliyopita, basi hapa ninaye tena katika kibao hiki TRUTH WILL REVEAL kutoka albamu yake ya Revolution.
Na namzungumzia kutokana na mambo matatu yaliyotokea wiki hii. Kwanza sitaweza kuweka pembeni historia iliyowekwa na uchaguzi hapa nchini, pili mazungumzo ya amani ya Congo huko Kenya na tatu watuhumiwa wa pesa za EPA waliofikishwa mahakamani huko nyumbani.
Umati mkubwa nyakati za kampeni. Ukitaka kujua wawazalo juu ya mgombea, angalia matokeo. Kama unabisha muulize Mrema (1995)
Kwa hapa Marekani tumeona namna ambavyo uchaguzi umegeuka kuwa funzo kwa wengi. Kuwaonesha kuwa MABADILIKO yajapo hayazuiwi kwa vitisho wala mtazamo wa mtu. Watu walipiga kura za maoni kwa namna ya kuweka uwiano na wengine hata kutopiga kabisa ilhali wakijua walichonacho mioyoni mwao. Hilo liliwapa watu mtazamo kuwa uchaguzi ungekuwa mgumu kiasi na wengine kubashiri mambo kugeuka siku ya mwisho kulingana na "enthusiasm" waliyokuwa wakiiona kwenye kampeni zao. Walilosahau ni hilo lililoimbwa na Nasio ambalo pia nimeliandika hapo juu. Walidanganywa na sura bila kujua mawazo, na kuangalia matendo bila kujua madhara yake na wakati ulipofika kila mtu akafanya kilichokuwa mioyoni na UKWELI UKADHIHIRIKA kiasi hata cha kuwashangaza walioshindwa. NASIO ALIKUWA NA BADO YUKO SAHIHI.
Naona sura sijui wawazalo. Ni amani, ama kumwadhibu mhusika ama posho? Time and time-alone will prove the story. Picha kwa hisani ya Michuzi
Huko Nairobi ambako mazungumzo ya "kutafuta amani" ya Kongo yanaendelea. Na kama ambavyo nimeshasema tangu awali ni kuwa njia m'badala za kusaka amani zinawaweka wananchi wenye uhitaji wa amani hiyo katika wakati mgumu zaidi. Ni mazungumzo ya viongozi kusaka amani yasiyohusisha pande mbili zinazosababisha machafuko. Wamekutana bila kiongozi wa "waasi" kwa vile tu "ni mkutano wa viongozi". Hapa mtazamo wangu ni kama vile "wanasuuza maji" maana kwa kufanya hivyo hutapata maji masafi bali utachafua na yale uliyokuwa nayo. Kukutana na viongozi huku mkimwacha yule mumuitaye muasi akiendelea kuasi na kuua sijui kunaletaje amani kule aliko? Na njia ya kukutana inayotumika ndio iliyokataliwa na serikali kukutana na muasi. Trust me, mkutano ni sehemu yenye amani, usafiri mzuri, ulinzi wa kutosha, mlo mwema na uliokamilika na mavazi mwanana lakini hawa kinamama, walemavu na watoto wanaendelea kudidimia katika maisha ya kutembea kuisaka dakika ijayo wakiwa hai. "Time and time-alone will prove the story and every eye will see". Picha na NYTimes
Wako kwenye "kitimoto' cha EPA. Wanawaza nini? Watasema. Truth will reveal
Sasa hawa watuhumiwa wa EPA nao sijui wanawaza nini vichwani mwao? Ni watuhumiwa na naamini miongoni mwao (kama sio wote) kuna wanaojua ukweli wa tuhuma zinazowakabili. Je ni wao? Kama ni wao walifanya haya peke yao? Ni akili zao ama waliagizwa? Ni kweli kuwa hawa ndio waliochukua mapesa yote? Kuna wengine? Nao ni tabaka la kati kama hawa? Na kama ndio mbona hawaonekani kumiliki na kurejesha pesa zote hizo? Kuna wengine? Ni waheshimiwa? Nasubiri wakianza kuanika ukweli wa mambo. Ni yaleyale aliyoimba Nasio kuwa "you see their faces but you never know their thoughts... time and time-alone will prove the story, and every eye will see. TRUTH WILL REVEAL.

BLESSINGS

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, November 6, 2008

"Not over until it's done"


"..once you got life there's a chance you'll be able to overcome. Where there's will, there's a way, IT'S NOT OVER UNTIL IT'S DONE, if you believe you will achieve, everything can just turn around" Hayo ni maneno yaliyoimbwa naye mkongwe wa Lover Rock Beres Hammond katika wimbo wake Not Over Until It's Done.
Maneno hasa ndio ambayo hunipa moyo pale ninapokuwa na ndoto ama mipango na kisha kuhisi kuwa ninakumbana na vikwazo mbalimbali katika kuyatekeleza. Na ndipo nikumbukapo kuwa It's not over until it's done. Na ukimsikiliza zaidi kwenye wimbo huo anaendelea kusema kuwa "while you are wondering what suit to wear, the family's worry is what a meal to share" na hiyo hunipa mwanga kuwa pamoja na matatizo tuliyonayo, lakini wengine wana zaidi. Kwa hiyo badala ya kulalamika basi tuendelea kukamilisha mikakati ya kufanikisha ndoto zetu. Na kwa juhudi, maarifa, utii na imani kutakuwa na njia sahihi ya kutufikisha kule tutakako kwenda. Lakini juu ya yote kuwe na Baraka zake akupaye uhai.
Nimesema haya kutokana na ushindi wa Rais Mteule wa Marekani Mhe Barack Obama.
Hajatoka kwenye familia ya kitajiri, hakuwa katika familia yenye jina kubwa (kama kina Martin Luther ama Malcom X), hakulelewa malezi ya wazazi wote kumfanya awe na mtu wa kuiga majukumu ya kimalezi ya mwanaume, hakutoka katika jimbo lenye uwezeshwaji mkubwa na wala si mtu aliye ndani ya siasa kuu za nchi kwa muda mrefu. Lakini kwa miezi 21 aliyopiga kampeni, ameonesha nia halisi ya kushinda uchaguzi huu na mara zote katika harakati zake amekuwa akikumbana na "kigingi" cha kuwa yeye ni mweusi na isingekuwa rahisi kwa raia wabaguzi wa nchi hii kumpa kura. Alichofanya ni kuamini katika nia yake ya kuwa kiongozi wa nchi na yanaweza kusemwa yasemwayo lakini "it's not over until it's done". Na watu wakasema kuwa historia haiwezi kubadilika kwa mtu ambaye hajawa na uzoefu wa kuongoza hata jimbo lake akapewa dhamana ya kuongoza taifa hili lenye ukubwa wa matatizo zaidi ya wema, lakini msemo unaonekana kuwa uleule kuwa "it's not over until it's done". Wamemhusisha na Magaidi, kutumia jina lake la pili la Hussein kama njia ya kuwatisha watu, kuzungumza juu ya uwezo wake mdogo katika masuala ya kimataifa lakini alionekana kujiamini katika kile atendacho akiamini kuwa mwisho wake ni Nov 4 na kwa kuwa ilikuwa haijafika, kwake ni yaleyale "it's not over until it's done".
Obama amekuwa na mafanikio makubwa saana katika "kuiunganisha jamii" tangu akiwa Community Orgernizer huko Chicago. Ni uwezo huohuo alioutumia katika kujipanga na kueleza vema mtazamo, msimamo, imani, changamoto na matarajio yake na namna anavyojipanga kukabiliana na hayo yote katika kipindi cha utawala akipewa dhamana. Alionesha kujipanga vema katika ku-organize kampeni na kuvunja rekodi ya kukusanya kiasi kikubwa saana cha pesa kwa ajili ya kampeni kitu kilichowafanya wapinzani wake waanze kutaka kufanya uchunguzi kama watu hao hutoa pesa zao wenyewe na kwa hiari. Lakini hakusita kuonesha kuwa ana lengo na kwa kuwa muda ulikuwa haujafika, "it's not over until it's done"
Ni Jumanne ya wiki hii, tuliposhuhudia kile kilichowaliza wengi. Kuona ambacho miaka mitano iliyopita hakikuwa hata mawazoni mwa watu. Kile ambacho wengi hatukutegemea kutokea katika kizazi chetu. Tukaona kwa ushindi wa wingi wa kura na kura za kimajimbo tena kwa historia ya wapiga kura wengi tangu mwaka 1908, Barak Obama akachaguliwa kuwa Rais wa 44 wa Marekani, Rais wa kwanza mwenye asil ya Afrika na kwa hilo akadhihirisha kuwa "anything can just turn around"
CHANGAMOTO YETU ni kujifunza kutoka katika njia aliyoionesha badala ya kutegemea kuleta mabadiliko Barani na nchini mwetu. Kuamini katika kuvunja mipaka iwekwayo na "maadui" na kuamini katika kile sahihi kilichopo ndani ya mioyo yetu. Namaanisha kuwa wengi hawaoni mafisadi wakiweza kusafishwa nchini Tanzania, hawaoni kama rushwa yaweza kuondolewa nchini Tanzania, hawaoni viongozi wazembe wakiwajibishwa nchini Tanzania, hawaoni mtu akigusa na kuinua maisha ya wahitaji wengi wa vijijini nchini Tanzania na wala hawaoni mageuzi ya kweli kuelekea matumaini kwa waTanzania wengi, lakini nionalo mimi ni kuwa "IT'S NOT OVER UNTIL IT'S DONE"

BLESSINGS

Tuesday, November 4, 2008

Kushinda si kazi. Akishashinda sasa!!!!!!

Barack Obama wa Democrat Party
John Mcain wa Republican Party
Ralph Nader.. Independent
Bob Barr wa Libertarian Party
Cynthia McKinney wa Green Party

Leo ndio leo kwenye siasa ya Marekani na ulimwenguni kwa ujumla. Ni kwa kuwa kwa namna yoyote ile ama kwa yeyote atakayechaguliwa kuongoza nchi hii, basi lazima ataweka rekodi. Ama atakuwa Barak Obama ambaye atakuwa mwenye asili ya Afrika kukwaa nafasi hiyo, ama atakuwa John Mcain ambaye atakuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi kushika wadhifa huo, ama wasio na nafasi kama Ralph Nader atakayekuwa mgombea huru ama Cynthia McKinney na Bob Barr ambao wanatoka kwenye vyama vichanga ama vidogo hapa nchini. Lakini twajua kabisa kuwa nafasi kubwa ipo kati ya Barak Obama ama John Mcain.
John Mcain alionekana kuwa nyuma saana ya Obama lakini ni kama anakuja tena kwa kasi ya ajabu kujaza mapengo. Kwa wale wamjuao ama wafuatiliao siasa za hapa wanafahamu kuwa Mcain ameshafanya hiyo kuwa style yake. Anajiona kama "underdog" anayefanya vema saana na anazidi kudhihirisha hilo. Na kuna uwezekano wa mtu kupata kura nyingi lakini asiwe Rais nchi hii kama ambavyo ilitokea mwaka 2000. Yanaweza kutokea mwaka huu? Si swali la kuweka pembeni maana lolote laweza kutokea kwenye uchaguzi ulio na ushindani wa ajabu na wa chinichini kama huu
Tatizo ni kwamba yawezekana akawa anajifunika shuka kukiwa kumekucha lakini pia yawezekana kura za maoni haziko sahihi. Sasa kama kura zingekuwa ama zitakuwa kama zinavyoonesha kwenye maoni, basi Barack Obama ataweka historia ya kuwa mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwa Rais. Na hilo litawezekana baada ya miezi 21 ya kampeni za hali na mali na hatimaye kuweza kupita vigingi vikubwa vya siasa kikiwepo Hillary Clinton na kama akiweza hiki cha Mcain.
Sasa Obama akishinda ndio hasa kazi itakapokuwa na kuna "marundiko" ya lawama nioyaonayo.

1: Naamini kuna wanaomuona kama nabii vile wakiamini kuwa ushindi wake wa leo unaweza kuanza kuleta mabadiliko kesho. Hilo naona ni kama "rundiko" la lawama zijazo.

2: Watu wengi wanamuunga mkono kwenye uchaguzi ili aweke historia. Yaani orodha ya waliojiandikisha inavunja rekodi kuanzia watu wazima, vijana na mpaka wasio na makazi ambao wanaamini ataweka mabadiliko. Tatizo ni kwamba wangapi wako tayari kushirikiana naye kuleta hayo mabadiliko? Kama hakuna, basi hilo analo na ni "rundiko" la pili la lawama.
3: "Rafiki" yangu alisema "ngoja Obama ashinde labda tutapata nafuu Afrika" Nikajiuliza kuwa "mnategemea akishinda ahamishie Ikulu yake Afrika nini? Mataifa ya nje nayo yanamuona kama muunganishaji na mpatanishi mwenye uwezo na ushawishi mkubwa kimaongezi, lakini hapa nyumbani kuna chuki iliyojengeka kimatabaka na ki-rangi ambayo imejidhihirisha kidooogo kwa wale wachache wenye tabia hiyo mbovu kupanga mikakati mibaya kuharibu sifa za watu weusi. Kwa hiyo ni changamoto nyingine aliyonayo kama akishinda.
4: Lakini kwa yeyote atakayeshinda, CHANGAMOTO KUBWA ni kutafuta suluhisho la Mashariki-ya-kati, Vita vinavyoendelea Iak na Afghanistan na mkanganyiko wa uchumi unaoonekana kuimung'unya dunia hivi sasa

Kwa vyovyote iwavyo, Amani, Heshima na Upendo vitawale na kisha aliye na ushawishi wa kuwaongoza wengi na apewe dhamana tuone atakapotupeleka.
Uchaguzi ni leo, lakini kama ukishinda, CHANGAMOTO iliyo mbele yako si lele mama.

Monday, November 3, 2008

Washindi wa Bahati Nasibu ya Benki ya Posta wapatikana

Meneja wa benki ya posta tawi la Bukoba Maduhu Makoye akimzawadia muuguzi msaidizi wa hospitali ya mkoa wa Kagera Judith Kaindoa zawadi ya friji baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa bahati nasibu iliyochezeshwa na benki hiyo.

NA MKEBEZI RUGALABAMU,BUKOBA
MUUGUZI msaidizi wa hospitali ya mkoa wa Kagera Judith Kaindoa ameibuka mshindi wa kwanza wa bahati nasibu iliyochezeshwa na benki ya Posta tawi la Bukoba.
Kwenye bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa na benki hiyo kuanzia julai 23 hadi septemba 30 mwaka huu muuguzi huyo alipata zawadi ya Friji ya milango miwili yenye thamani ya zaidi ya shilingi 900,000.
Zawadi hiyo kwa mshindi huyo wa kwanza ilikabidhiwa na meneja wa benki hiyo tawi la Bukoba Maduhu Makoye sambamba na washindi wengine katika sherehe fupi iliyofanyika katika jengo la Benki hiyo mwishini mwa wiki.
Washindi wengine walioshinda zawadi mbalimbali za bahati nasibu iliyochezeshwa na benki hiyo ni pamoja na Bryson Mayowa mshindi wa pili aliyepata zawadi ya television yenye thamani ya shilingi 270,000 aina ya hitachi.
Washindi wengine waliopata zawadi ni Mariath Kagambo ambaye alipata zawadi ya cherehani baada ya kuibuka mshindi wa tatu chenye thamani ya shilingi 180,000 ,mshindi wa nne ni Amani Rhodes aliyeibuka na baiskeli yenye thamani ya shilingi 130,000 na mshindi wa tani alikuwa Arosto Mstapha aliyeibuka na zawadi ya simu aina ya nokia yenye thamani ya shilingi 130,000.
Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wa bahati nasibu hiyo ulienda sambamba na uzinduzi wa promotion kabambe ambayo Benki hiyo imeanzisha inayojulikana kwa jina la Gazebo ambayo itamwezesha mteja anayefungua akaunti kwenye benki hiyo na kujiunga kwenye mija kwa mija kwenye shindano la bahati nasibu ambapo washindi watakuwa wanatangazwa kila mwisho wa wiki.
Akiongea baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi meneja wa benki hiyo alisema katika promotion ya gazebo wateja 50 wa kwanza watakaofungua akiba kwenye benki hiyo watakuwa na nafasi ya kufungua akiba kwa kiazio cha shilingi 10,000 na watapigwa picha bure.
Sambamba na hilo Maduhu alisema kuwa wateja wapya watakaofunguo akiba kwenye benki hiyo kwa kiazio cha zaidi ya shilingi 40,000 watapatiwa zawadi mbalimbali ambazo ni pamoja na tshit, kalamu na miavuli na pia watashiriki moja kwa moja kwenye bahati nasibu inayochezeshwa na benki na kupata washindi kila wiki.
Alisema katika bahati nasibu ambayo washindi wake wamepatiwa zawadi zao benki hiyo ilikuwa imetenga zaidi ya shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya washindi hao , Maduhu alisema sasa michezo ya bahati nasibu ambayo benki hiyo itaichezesha imetenga zaidi ya shilingi milioni 4.9 kwa ajili wa washindi.
Meneja huyo wa benki ya posta alisema kuwa washindi wote waliopata zawadi walipatikana kutokana na vigezo mbalimbali, alisema kuna washindi walioshinda bahati nasibu hiyo walipatikana kwa kufungua akaunti mpya na wengine walipatikana kwa kuweka fedha nyingi kwa muda mfupi kwenye akaunti zao.
Maduhu alisema benki ya posta ni benki ambayo imejizajititi kuboresha huduma zake hasa kwa wateja wake, alisema benki hiyo kwa sasa inafanya uhamasishaji wa aina mbalimbali ili iweze kuwavuti wateja wake na iweze kupata wateja wapya.
Alisema benki hiyo kwa sasa imenzisha huduma ya utumaji wa fesha kwenda nje nchi kwa gharama nafuu, Maduhu alisema kwa sasa benki hiyo inatoza dola hamsini kwa kiasi chochote cha fedha kinachotumwa kupitia kwenye benki hiyo kwenda nje ya nchi.
Habari kwa msaada wa Audax Mutiganzi

Hongera na Shukrani VGSS

Sote twaamini kuwa ukitaka kupata matunda mema basi anza kujali pale unapowekeza tangu hatua za mwanzo. Anza kutoa huduma bora na muhimu tangu anwali kuweza kukupa matunda bora na mengi. Na kwa hili ambapo BLOGU hii inaungana na wapenda maendeleo wote kuwashukuru na kuwapongeza Vodacom kwa mpango wao wa kuwaendeleza vijana katika soka. Tuna imani kuwa Francis Costa, Cosmas Mwazembe na Salum Bakar Saad watakuwa nyota njema sio tu kwa Tanzania, bali kwa ulimwengu kwa ujumla na ni hazina ya miaka ijayo kwa maisha na michezo nchini kwetu. Lakini pia tunapongeza na kushukuru kwa wale wote washiriki 11,000 waliojitokeza kuwania nafasi hizo. Twaamini kuwa kati yao wapo wengi walioona uwezo mkubwa walionao hivyo wataongeza juhudi ili waweze kufika mbali katika mchezo huo waupendao. Na twaamini kuwa kati ya hao hao 11,000, wapo walioonekana na kuelekea kunyakuliwa na timu zinazoshiriki ligi mbalimbali na kuwaendeleza ki-soka.
Shukrani Na Pongezi kwenu Vodacom kwa kunyakua vipaji toka kanda zote za nchi.

Saturday, November 1, 2008

Wow!!!!!!!!!!!!!

"They were brought here to protect us, They were brought here not to hurt. But now they hurt us everyday. You see, Police have joined forces with criminals..... How can we expect them to serve and protect the community, if they themselves are the bad guys" Hayo sijasema mimi. Aliimba Lucky Dube kwenye wimbo Life In The Movies ndani ya albamu yake ya Trinity. Si aliyaona yalitokuwa yanatokea kipindi cha ubaguzi kule Afrika Kusini. Sasa aibu kwetu kuwa yanatendeka miaka karibu 50 baada ya UHURU.
Hapa nausaka MSTARI HAFIFU unaotenganisha SHERIA na HAKI.
Nausaka maana nikiuona ntaukazia wino ili hawa Ma-askari waweze kuuona na kutambua kuwa wanachotakiwa ni kulinda sheria lakini hawana mamlaka ya kuamua haki ya mhisiwa, mkusudiwa ama mshukiwa. Na ndio maana wanamsongesha mbele kwenye vyombo vya haki kama Mahakama ili HAKI ITENDEKE. Lakini hili nalo hawalioni.
Si tu kwamba ma-askari hawalioni, ila yaonesha hata wenye kuhusika na kuwakumbusha hawa hawalioni pia. Kuna jambo nahisi na pia kuna jambo najua. Ninalohisi ni kuwa hawa Askari wanapokuwa CCP ama popote kulingana na utekelezaji wao (nikimaanisha Magereza, ama Mgambo ama Akari Polisi, Sungusungu nk) wanafundishwa juu ya kile kitwacho Code Of Ethics. Najua kuwa wanaelezwa kuwa hiyo ni kazi na si nafasi ya kunyanyasa wanyonge kutokana na mood unayokuwa nayo siku hiyo. Kutambua mipaka na haki za wale wahisiwao kuwa wakosaji. Hata mwenye kosa la mauaji bado ana haki na sio wajibu wenu kumhukumu just kuonesha ubabe. Ziggy Marley aliuliza "why we lose ourself just to find who we are?"
Ila pia NAJUA kuwa ni wachache wenye kutekeleza hayo wafunzwayo. Tumechoshwa na uborongaji na uvunjwaji wa haki za binadamu tunaofanyiwa, kuuona na kuusoma ama kuuangalia katika vyombo mbalimbali vya habari hapo nchini.
Tumeyaona haya kuanzia Zanzibar ambayo yamesambaa kwenye tovuti kama You Tube (bofya hapa uone yalivyo wazi ulimwenguni na yanavyotia kinyaa http://www.youtube.com/results?search_query=Tanzania+police+brutality+Zanzibar+Nov+2005&search_type=&aq=f) kisha tukaona kina Mzee wa Sumo walipigwa na Askari Magereza na juzi tu hapa Father Kidevu naye akwa mhanga.
Pamoja na kuwekwa mitandaoni kwa muda wote huo, bado mnaendelea kujichukulia sheria mkononi tena bila woga???? Come On.
Namuunga mkono Lucky Dube kuwa sasa huyo Polisi kishaungana na waovu kufanya uasi.
Pole Kaka Mroky na kwenu wanausalama (wale wachache wenye kuharibu sifa nzima ya jeshi) , ni CHANGAMOTO KUBADILI TABIA

Na huu ni mtazamo wangu kwa namna nionavyo Tatizo. Yawezekana ndilo Tatizo nililonalo.