Wednesday, July 20, 2011

Enziiiii!!! Tunapoteza nini tunapoongeza nini?

Enzi zangu. Hii ilikuwa ni "one shot" baada ya maandalizi ya kutosha. Hahahahaaaaa. Back in time.
Kwa miongo miwili iliyopita kumekuwa na mabadiliko makubwa saana ya teknolojia. Nakumbuka "enzi" hizo mambo kama kupiga picha ilikuwa ni suala la miadi na mpigaji (kama hukuwa na kamera ndani na naamini wengi hawakuwa nazo), kisha unafanya "zoezi" la style halafu akija unapiga na kusubiri kwa muda (kulingana na ulipo) kabla hujapata picha yako. Nadhani hii ilitufanya tuwe makini saana maana hatukutaka kupoteza picha ama kupiga piucha ambayo tutalazimika kuilipia hata kama hatuitaki.
Lakini sasa kwa teknolojia iliyopo, unaweza kupiga picha 1000 kisha ukachagua moja ya kutumia.
Hivi hatujapoteza kitu kutokana na teknolojia hii? Pengine "za kale" zilitupa maandalizi mazuri katika kujiandaa kupiga picha na mengine mengi ambayo sasa tunayaweka pembeni kwa kuwa tu kuna "teknolojia". Hatutumii ramani tena, tunategemea GPS, hatupiki, ni fast food tuuu. Hatunywi maji yenye usafi wa asili, bali twataka kununua yaliyochujwa toka kwenye maji taka. Hatutembeleani, ni email na jumbe fupi na simu. Hatuaminiani, kila kitu ni kwa "wino wa mashahidi". Hatupendani kwa dhati, mwenye nacho ndiye apendwaye. Yaaani ni mabadiliko kwa kwenda mbele (japo yaturudisha nyuma)Mambo mengi tuyaonayo ya kizamani hunirejesha "back in time" MSIKILIZE INNOCENT GALINOMA HAPA KATIKA WIMBO WAKE ALIOUITA BACK IN TIME

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

swali ni je tunakwenda na wakati au wakati unakwenda na sisi au hatuko kote kote. furaha ni kuweka wazi masuala ya kiroho yakajulikana kwa wengi yaliyojulikana kwa wachache

lakini sasa pozi za picha usinikumbushe sana, nilikuwa hodari katika hilo na sasa uhodari wangu umekufa

Rachel Siwa said...

kaka umetoka mwenye na mikono mfukoni!!!!!