Tuesday, May 24, 2011

Maonyesho ya ndege (taswira & video)

Ulinzi ulikuwepo wa kutosha tu.
U2S Dragon. Ndege inayoruka mpaka futi 70,000 kutoka usawa wa bahari. Mara mbili ya umbali urukwao na ndege za kawaida. Rubani katika ndege hii huvaa mavazi maalum kujikinga na mionzi ya jua na joto.
Haka kanaruka bila rubani. Na bado kanafyatua mizinga. Yaaani
Hili lidege la ki-rusi. Na chini ni "landing gear" yake ya nyuma.
KISHA......

Hizi ndege ni za kundi linalojiita Geico Skytypers na wanaandika maneno angani kwa kutumia moshi wa ndege. Tazama baadhi ya waliyoandika TENA KWA UFASAHA
Hiyo ni moja ya injini nne za ndege ya C-5M Galaxy. Ambayo kama anavyozungumza rubani wake hapa chini, inatumia paundi elfu ishirini za mafuta kwa saa moja iwapo angani.....
TAZAMA HAPA CHINI NILICHOJARIBU KUREKODI KWENYE VIDEO

Saturday, May 21, 2011

Give Thanks and Praises...COME DOWN FATHER

"In my heart I know that you wont let ur chosen people suffer, (too long) I know u would never let us down.
Many times I coulda pick up a gun, I coulda go out a street and play big john, that's no fun no, sure ain't no fun, oooh no, cause I think
What would happen if the other man, thinks the same, then bullets fall like rain, It's no fun no, no it's no fun.
Oh I see greed and I see selfishness, everyman is for themself. Only u can talk to them father, cause they listen to no one else.
Come Down Father"
Ndivyo asikikavyo kuimba Beres Hammond katika wimbo huo ambao ni kama maombi kwa yale yaendeleayo duniani. Beres anaendelea kumuomba Mungu juu ya wenye mamlaka ambao sasa wanajigeuza miungu-watu akisema "To the hearts of those responsible, let them know their actions are despicable. Remind them that is u who wears the crown" Na pia anawakanya wale wenye kudhani wataweza kuikimbia hukumu ya mabaya wanaoendelea kuyatenda kuwa "Oh, unto the ones who think you can do these wrongs and get away, Woe unto u, and watch out for ur day"


Msikilize mwenyewe Beres Hammond akimuomba Mungu arejee kusawazisha hali


KISHA BURUDIKA (TENA) NA VIDEO HIZI ZA AFRIKA MASHARIKI
ATEGISIN by Emmy Kosgei

OMULIRO by Judith Babirye

KIATU KIVUE by Anastazia Mukabwa & Rose Muhando

SALUTI by Dady Owen & Friends

TAUNET NELEL by Emmy Kosgei

Friday, May 20, 2011

Them, I & Them......NEVER GIVE UP....Luciano

Luciano kwenye onesho lake Zanzibar On The Waterfront 2008 Them, I & Them nayo ilikuwepo kudaka hili na lile"Many of life's failures are people who did not realize how close they were to success when they gave up." Thomas A. Edison (1847 - 1931)Nukuu hii ina ukweli mwingi na wa maana maishani mwetu hivi sasa. Wapo wengi ambao kutokana na mfumo wa maisha ulivyo na mkanganyiko wa uchumi wa sasa wameamua kuachana na kile wanachoamini na kukipenda na kujikuta wanajipotezea nafasi za kusonga mbele katika kukamilisha "mafanikio" yao maishani.
Pia nukuu hiyo hapo juu yanikumbusha kile alichokiimba hayati Lucky Dube katika wimbo wake TOUCH YOUR DREAM alipouliza "have you ever see the dream walking?, have you ever hear the dream talking? ....You are THE MASTER of your dream, if you pull the right string it'll be talking to you, don't hesitate, grab the chance before it's too late .... REACH OUT AND TOUCH YOUR DREAM"Tunalokumbushwa hapa ni kuwa maisha yetu yako mikononi mwetu. Tunaweza kuamua kufanyia kazi kile kilichopo mawazoni mwetu (ambacho wengine wanakiita NDOTO) na kisha kukifanya kuwa kweli (na hapo watakibatiza jina la UFUNUO).
Ama twaweza kubaki na "kumbukumbu" ya tulichokiota na kushindwa kusonga mbele.
Lakini maisha yetu hayajaumbwa kuwa marahisi na ndivyo ilivyo na inavyotakiwa iwe. Kwa maana nyingine, kupambana na majaribu ni sehemu ya maisha tuliyopangiwa.
Ni katika hili, tunakutana na Jephter Washington McClymont ambaye anafahamika zaidi kama LUCIANO, anapotueleza kuwa MAISHA YAMEPANGWA NA MUNGU na kupanda na kushuka ni sehemu ya maisha.
Ukisikiliza ubeti wa kwanza, Luciano anazungumzia wakati ambao maisha hutuendea vema nasi tukadhani ni haki yetu kuwa hivyo nasi kusahau kuwa MUNGU ndiye chanzo cha mtiririko wa maisha yetu na ni wajibu wa kila mmoja kulitambua hilo.
Anasema "Just like a river moving water on and on to the sea. Like an Ocean always in motion, that is how you got to be. Just like the wind that blows on a constant flow that gives us life wherever we go. Like the sun that shines and allows our days to go.. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW."
Na katika kiitikio, Luciano anaendelea kutusisitiza kuwa licha ya ugumu wote huo, twatakiwa kuendelea kupigania kile tuaminicho mioyoni mwetu akisema "you should never give up, NEVER GIVE UP. Just keep on tyring. Never give up, believe in what you're doing. You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Lakini pia Luciano anaelezea wakati ambao mambo huwa yanakwenda kombo na baadae kuja kunyooka akituasa kuwa huo "ndio mfumo wa maisha" ambao MUNGU ameupanga na kwa kuwa yeye ndiye chanzo cha yoe, "hatutakiwi kushangaa".
Anasema "sometimes the crops refuses to bear and the harvest isn't really there. No rain the soil is cracked and dry, mothernature seems to die. Then one day shower came and the earth smiled again...... DON'T BE SUPRISED, 'CAUSE THAT'S NATURAL FLOW. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW"
Na kwa wale ndugu zangu wote walio katika magumu ya uchumi, maradhi, ukiwa, kuuguliwa, ama harakati nyingine zionekanazo kukwamisha kile ambacho umekuwa ukipanga kufanya kwa muda mrefu, nakwambia alivyosema Luciano kuwa "You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Msikilize HAPA katika wimbo wake huo NEVER GIVE UP uliopo kwenye albamu yake ya Jah Is Navigator
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Wednesday, May 18, 2011

Chemsha bongo...Mjini ni wapi?

Juzi kwenye ukurasa wa Facebook wa mdogo wangu nilikutana na maelezo yasemayo "While individuals embrace each other in rural, they stay apart in Urban."
Kisha nikawaza kuwa MJINI NI WAPI? Nikaweka majibu kuwa "Hivi Mjini ni wapi? Nikiwa Nyakibale niliona Omuluhamila kama mjini. Kufika pale nikaona Kaagya kama mjini, Na Kaagya wanaona Kashozi kama mjini na wa Kashozi wanaona Bukoba Mjini ndio kumekucha. Aliye Bikoba mjini anaamini Mwanza ndio kwen...yewe (tena anywhere in Mwanza) na aliye Mwanza anaamini Arusha ama Dar ama etc ndio haswaaaaa. Aliye Dar Kibondemaji anaamini Kariako ndio mjini na wa Kariakoo anaangalia Masaki. Wa Masaki anatazama Nairobi na nje ya nchi hata Marekani na hata hapa Marekani kuna aliye DC ama Los Angeles na bado anautafuta mji. KWANI MJINI NI WAPI? Labda hata ndani a nyumba yenu kuna mjini ambapo ni Master bedroom na aliye humo naye anaamini choo cha humo ndimo mjini mwake. KWA MAANA NYINGINE, LABDA MJI NA KIJIJI NI FIKRA TU. Kwa kuwa anayekula raha sana duniani na kuamini ana kila kitu, anaambiw na kuwa KUNA MBINGUNI KULIKO NA MANONO KULIKO ANAYOPATA. Labda huko ndio MJINI. Lakini tukifia huko hatutaambiwa kuna "mji mwingine?" NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUU..."
Na bado nawaza..........MJINI NI WAPI?

Monday, May 16, 2011

Majibu ya MMILIKI WA TUZO ZA BLOG TANZANIA

Hivi karibuni niliandika kuhusu Tuzo za Blog Tanzania na kutoa MTAZAMO NA MSIMAMO WANGU (hapa) na sasa mmiliki / mwongozaji wa blogu inayotayarisha tuzo hizo amejibu kuhusu mtazamo wangu. Nami napenda kuweka maoni yake hapa
FRIDAY, 13 MAY, 2011
Admin said...
Wow! Nilikua sijapata muda wa kusoma link ulizoacha kwenye blog yetu. Leo ndio nimepata muda nimepitia huku sasa hivi ndio nikaona umeandika maoni yako kuhusu tunzo yetu. Kwanza nikupe shukurani kwa vile kuandika post kuhusu kitu fulani sio jambo dogo..

Ila ninalotaka kusema ni kuwa kila mtu anaruhusiwa kutoa mawazo yake na kueleza jinsi anavyofikiria. Sasa na mimi kwa upande wangu naweza nisikubaliane na hata kitu kimoja unachosema au nikubaliane na vichache tu.

1.Unavyosema la muhimu ni kuwa na umoja wa wanablog kwanza sikuelewi una maana gani. Unajua umoja wa kitu chochote haulazimishwi? Na kila mtu au watu wanaojiunga katika umoja fulani ni kwa kutokana na jinsi wanavyoona huo umoja utawasaida vipi kutokana na kanuni za umoja huo. Wanawake fulani wakikaa wakaamua waanzishe umoja wa wanawake wanaoblog, je utamlazimisha kila mwanamke anayeblog ajiunge na umoja huo? Kama hataki je watu waliokua kwenye umoja huo watamfikiriaje mtu ambaye hayupo kwenye umoja huo? Je watamtenga, watachukia blog yake, watafikiria kuwa anajiona yeye yuko juu zaidi kuliko wale waliojiunga kwenye huo umoja au waanzilishi wa huo umoja? Hivyo sioni sababu ya kulazimisha kuanzisha umoja wowote kama watu hawako tayari au hawajui umuhimu wa umoja fulani. Ujue kuwa umoja wowote unaoanzishwa iwe kwenye nchi, makazini, kwenye makanisa au misikiti ni kwa manufaa ya wanachama kama sivyo basi hauna maana. Na mimi ninavyofahamu kuna kundi la watu wanaokutana jijini Dar Es Salaam kujadili blog zao kila mara. Sasa hilo kundi sijui nao utawaambia kwanini mnakusanyika wenyewe bila kutangaza au kutwambia na sisi tujiunge? Hivyo umoja unaouzungumzia si ajabu upo lakini ni kwa watu fulani. Hivyo na wewe unaweza ukaanzisha umoja na kuutangaza humu na kueleza madhumuni na faida za umoja huo ili wenye kuona unawafaa wataamua kujiunga au la. Usikae na kuimba wimbo wa “tuanzishe umoja, tunzishe umoja” tu. Wewe kama mwana blogger unatakiwa ndio useme jamani nimeanzisha umoja huu, madhumini yetu ni haya na kanuni zetu ni hizi hivyo mwenye kutaka kujiunaga atajiunga.

2.Halafu unavyosema kabla ya tunzo kwanza tufundishane umuhimu wa blog kwa jamii…Sasa kama ni hivyo Oscar awards ambayo ni tunzo ya juu sana katika ulimwengu wa filamu nao wasingeanzisha hiyo tunzo mpaka leo wakisubiri watu wafahamu umuhimu wa filamu katika jamii. Hivyo hilo sitakubaliana na wewe pia kabisa kwa vile mpaka leo kuna filamu hazina maudhui yeyote katika jamii zaidi ya kufurahisha tu. Na hilo utalikuta kwenye blog nyingi tu, sio zote zitakua za kufundisha jamii kuna blogs ambazo zitakua zinafurahisha tu lakini zote zitashirikishwa katika mashindano. Na ni juu ya waanzilishi wa Oscar awards kuchagua ni filamu gani wazishirikishe na gani wasizishirikishe. Hawalazimishwi na watu wa filamu. Watu wa filamu ndio wanajitahidi kutengeneza filamu zao kwa ubora zaidi ili zitambulike humo. Na sisi hapa hatutalazimishwa na mtu yeyote ni wajibu wetu kuiweka award yetu katika kiwango cha juu. Na uzuri wa award yetu ni kuwa watu wanaosoma hizi blogs ndio watakao chagua wenyewe. Tumeshazoea kuona vyombo vya habari vinavyojua kumpalilia mtu kwa vile ni fulani au anajulikana na watu fulani kuliko mtu mwingine anayefanya mengi lakini kwa vile hamjui yeyote yeye jina lake halipitishwi mahali popote. Hayo yapo sana tu lakini hapa kwetu ni people’s choice hata yule mtu ambaye amejitahidi sana kujitangaza na hakuonekana tunampa jukwaa la kuonekana.

3. Na unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani. Mtu anaweza kuwa na mawazo yake fulani lakini kile anachokichapisha kwa watu ni tofauti kabisa na kuna wengine kwa kufuata mkumbo wa huku na kule basi waliloanza nalo sio lile wanalo sasa hivi. Hivyo baada ya watu kuwakilisha blog zao tutakaa chini kuona kama kila blog iliyopitishwa inastahili kuwekwa katika hiyo category.
SUNDAY, 15 MAY, 2011

KISHA AKAENDELEA
Admin said...
Halafu ukishapangia watu nani apewe tunzo ya juu na nani anastahili zaidi kuliko mwingine hiyo si sawa kabisa. Kila mtu anayefanya jambo lolote linalosaidia jamii kwa njia moja au nyingine anastahili pongezi. Kuna watu wengi sana wanatoa michango yao katika jamii lakini labda kwa vile uwezo wao ni mdogo basi michango yao haisikiki au haifiki katika ngazi za kitaifa nao ikifika siku ya kutambuliwa utawapengua na kusema nyie hamstahili kwa vile mmesaidia huko vijijini tu na wala sio zaidi? Ina maanisha kama mtu amesaidia kuokoa maisha ya mtoto aliyekua afe huko kijijini na mtu aliyesaidia maisha ya mtoto aliyekua afe mjini ni yupi anastahili pongezi zaidi? Je wanatofauti hao watu katika ustawi wa jamii? Ndio maana kuna awards na life time achievement awards nadhani unaelewa tofauti kati ya hayo mawili. Award inapigiwa kura lakini life time achievement awards inateuliwa. Kama ingekua hapa tunachotoa life time achievement award na wewe ukapendekeza jina la mtu fulani ningekuelewa vingine sitakuelewa au nitaanza kufikiri au una agenda fulani. Kuna watu wanastahili tunzo ya life time kwa michango yao wameitoa kwa muda mrefu katika jamii lakini usimkatishe tamaa yule mtu anayeanza tu kutoa mchango wake katika jamii kwa kutomtambua au kwa vile hana zana wala uwezo wa kufanya makubwa ili taifa kumtambua mchango wake. Hata kama ni mchango wake ni mdogo tu unaoishia katika kijiji chake anastahili pongezi sawa kama yule mwenye uwezo na kufanya mambo makubwa zaidi. Watu wote wanaofanya jambo lolote kwenye jamii linalosaidia kuboresha ubora wa maisha ya watu wanastahili kutambuliwa na kupongezwa.


Lingine ni lile ulivyosema tuwekeze “kuhamisha maandiko yetu kutoka kwenye blogu kuelekea kwenye MAGAZETI yanayosomeka na wengi” . Hapa sikubaliani na wewe kabisa. Cha muhimu ni vyombo vya habari kuhakikisha kuwa wanaweka habari zao kwenye mitandao kwa vile kuna watu wengi wako nje ya nchi na wana kiu za habari za nyumbani na wahazipati hivyo ndio maana unaona blog za bongo nyingi ni za habari tu kwa vile ndio wanaona kuna watu wengie wanakimbilia huko. Either walio bongo wanataka habari za nje ya nchi na walio nje ya nchi wanataka habari za bongo. Kwa kusema tutafute njia ya kupeleka blog kwenye magazeti unatakiwa kujua kuwa kila nchi inasheria zake za uhuru wa habari. Na kila gazeti linasimama kufuata sheria za nchi na sheria za malengo ya magazeti yao. Magazeti kama sio ya serikali basi hufanya kazi kwa ajili ya biashara tu. Usitegemee gazeti la watu binafsi liko kwa ajili yako liko kwa ajili ya kuchapisha habari itakayouza gazeti lao na kupata faida. Hivyo hata kama kuna vitu watu wanatuma viwekwe kwenye magazeti lakini haviweki kwa ajili labada ya kanuni zao, hazifikii ubora wa habari zao au kwa sababu zao nyingine. Hivyo ukisema kila linalokua blogged na watu huku kwa vile unafikiria ni bora basi linahitaji kusomwa na wale hata wasiokua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao inaweza ikawa n vizuri lakini sio kila blog ina maudhui. Sasa kila kinachowekwa kwenye blog kikiwekwa kwenye gazeti patakalika kweli. Cha muhimu ni wewe kama una mawazo hayo basi anzisha kitu kama blog magazine na uwe unachapisha blog yako au post za blog za watu wengine ambazo unaziona ni muhimu kwa kujenga taifa lakini nafahamu baada ya muda ili kuuza gazeti lako hata wewew utakua unachapisha vitu unavyoona vinauza gazeti lako tu. You know that is the way life is….wengi huwa wanaanza kwa madhumunimazuri lakini baadaye wanakua greedy na kusahau maadili ya biashara zao…Na pia ukumbuke kila nchi ina sheria zake za mambo ya habari. Ndio maana kuna email ya mtu ambaye aliishi Tanzania na kuweza kufahamu lugha ya Kiswahili. Katika pita pita akaona hii tunzo yetu na alifurahi sana kwa vile huko nchi yake aliko wao kwa bado hawawatambui hii kabisa na wau wanaoblog wanachukiwa sana tu na hata na serikali. Hivyo hata sisi nchini kwetu sidhani kuwa kuna gazeti litaweza kusurvive hata mwenzi mmoja likiwa linahapisha baadhi ya topics zinazowekwa humu kwenye blogs…
SUNDAY, 15 MAY, 2011

Ndugu yangu ADMIN......Kabla sijaendelea na yangu wacha nikupe ya wenzangu ambao kwa bahati mbaya maoni yao yalifutika kutokana na tatizo la BLOGGER juma lililopita, lakini bado yapo kwenye email


Mfalme Mrope has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

nani yuko kwenye kamati ya kuteua hizi blogs na ni nani mpiga kura na pia mpendekezaji ni nani na tangazo la hii kampeni lilitolewa lini? na ati? Michuzi iko kwenye best designed blogs?? HUH?
Posted by Mfalme Mrope to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Wed, May 11, 2011 at 11:23 PM

Yasinta Ngonyani has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

nanukuu.."NA HIVI NDIVYO NIONAVYO TATIZO, LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO" mwisho wa nukuu. haswa ni tatizo.
Naungana na kaka Mrope nani alipiga kura? na nani aliamua kila kitu?...
Posted by Yasinta Ngonyani to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 3:21 AM

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

Mimi nilipoona tangazo hili wala sikutaka kusema cho chote. Ingekuwa vizuri hao waandaaji wakajaribu kuwasiliana na wanablogu wote ili tukashirikishwa.

Mzee wa Changamoto: Hakikisha post hii inawafikia hao waandaaji. Ingekuwa vizuri kama nasi wanablogu tulioko nje tukashirikishwa. Mimi binafsi ningependa kuona vigezo vinavyotumika katika uteuzi. Asante sana kwa kuliona hili.
Posted by Masangu to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 9:02 AM

Malkiory Matiya has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":
- Hide quoted text -

Yaelekea bloggers wa kitanzania tuishio nje tumeshapokonywa uraia wetu na waandaaji wa tuzo hii. Inashangaza kuona blogs ambazo ni chachu katika kuelimisha watanzania popote pale duniani, ndizo zimepigwa chini. Na zaidi ya yote zile blogs ambazo hufanya uchambuzi yakinifu katika masuala ya siasa, utawala bora nazo zimepigwa chini. Kuna kila sababu ya kutilia shaka Lengo, nia, madhumuni na vigezo vya tuzo hii.
Posted by Malkiory Matiya to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 1:14 PM

NITAENDELEA NA MAONI YA KWENYE FACEBOOK BAADAE.
Lakini kama nilivyosema katika POST YENYEWE, kwamba 'NDIVYO NIONAVYO TATIZO....NA LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDILO TATIZO'

Sunday, May 15, 2011

Kwa mlio karibu na Washington DC


Mwishoni mwa juma hili, Wizara ya Ulinzi hapa Marekani itaendesha maonyesho ya majeshi yake katika kambi ya jeshi la anga ya Andrews (Andrews Air Force Base) hapa Maryland.
Haya ni maonyesho mazuri ambayo yanakupa muda na nafasi ya kuona ndege, magari, mizinga nk na pia kupata nafasi ya jypata maelezo na mahojiano toka kwa wanajeshi. Kama nilivyopata nafasi hiyo mwaka jana na kurekodi VIDEO HII

Na pia kuona DEMO za ndege kama hii video ya AV-8B Harrier

Kujua mengi kuhusu maonyesho haya yanayotokea kila wikiendi ya tatu ya mwezi Mei, BOFYA HAPA na kwa ratiba kamili ya matukio siku hiyo BOFYA HAPA
NA HIZI NI BAADHI YA TASWIRA ZA MAONYESHO YA MWAKA JANA
Ndani ya Cockpit ya C-17
Na mmoja wa marubani wa vita ya pili ya dunia
Blue Angels zikiwa kwenye maonyesho
Waruka kwa miamvuli
Helikopta za jeshi katika maonyesho

Friday, May 13, 2011

Duh!!!!

Baada ya BLOGGER kwenda halijojo kwa muda, naona imerejea, ile post kadhaa zimewekwa DRAFT na haziingii hata ninapojaribu kuzi-post tena.
Wamesema wanashughulikia na zote zitarejea.
POLENI KWA KUKOSA "UHONDO"

Tuesday, May 10, 2011

Ati nini? Soma mwenyewe uone

Niliwahi kusimuliwa kuhusu rafiki wa mwanafunzi mwenzangu ambaye hujifunza kupiga gitaa wakati anaendesha. NDIO. Gitaaa. Watu wakashangaa. Lakini hii niliyotumiwa leo sikuwahi kufikiria. Ati mtu anajinyoa "hoohah" yake ilhali anaendesha? Soma hiki kisha waza ALIWAZA NINI?
IMEANDIKWA NA Celia Rivenbark. Mwandishi wa vitabu kadhaa kikiwemo "You Can't Drink All Day If You Don't Start in the Morning," Kujua zaidi kuhusu yeye, tembelea tovuti yake HAPA

By now I'm sure that most of you have heard about the Florida woman who caused a two-vehicle wreck because she was shaving her bikini area while driving.
Guess that makes the time you drove with your elbows while eating a Whopper seem downright virtuous, doesn't it? Florida Highway Patrol troopers said the car Megan Barnes was driving crashed into the back of a pickup truck at about 45 mph. Her reaction time was slowed down because she was too busy grooming her hoohah to pay attention to the road. Oh, like that's never happened to you?
Ms. Barnes told the investigating officer that she was on her way to a date and "wanted to be ready for the visit."
Yes, she wanted to look her best. All over. Except, well, we've seen Ms. Barnes' mug shot and she appears to have a face that would stop a clock and raise hell with small watches, bless her heart. To be blunt, I don't think a perfectly groomed love rug could possibly make that much difference.It could've been worse, I suppose. Ms. Barnes could've been waxing her bikini area as she drove along in her T-bird (Yes, fun, fun, fun till the po-lice took her T-bird awaaaaaayy) on those scenic bridges. Imagine the horror if she'd tossed the used wax strips out the window. The manatees might have tried to adopt them.
Hons, I've driven on this particular stretch of highway between Miami and Key West and it's flat-out beautiful with crystal blue water, gorgeous mangroves and cloudless skies.
Not once have I been so bored that I decided I'd rather drag a sharp blade over my nether regions just to have something to do. There are so many "You might be a redneck if" elements to the story of Megan Barnes, but my favorite is that, while performing this extremely personal grooming ritual, she asked her EX HUSBAND to steer the car so she could concentrate ("Help me out, Buford, I'm gonna make it look like a LIGHTNING BOLT!")
What a guy! Not only did he hold the steering wheel so she could concentrate on primping for her big date with ANOTHER MAN, but when the cops arrived, he tried to switch places and claim he'd been driving.Trouble was, he had burns on his chest from the airbag that had deployed on THE PASSENGER SIDE ONLY. Oops.

To no one's particular surprise, the Highway Patrol quickly discovered that Ms. Barnes didn't have a valid driver's license. Oh, and, the day before, she'd been convicted of DUI and driving with a suspended license. Oh, and her car had been seized and had no insurance or registration. Oh, and she was on probation. Oh, and SHE'S A FLIPPIN' LUNATIC!
Albeit an impeccably groomed one

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

Monday, May 9, 2011

TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu

Hivi majuzi nilikuwa nasoma habari kwwenye blogu hii ya Dina Ismail kuhusu kuteuliwa kwa blogu yake kuingia katika Tuzo za Blogu Bora Tanzania.
NIKAMPONGEZA.
Kisha nikatembelea tovuti inayoandaa TUZO hizo na kukuta kuwa wanaandaa tuzo hizo. NINAWAPONGEZA.
Lakini kama nilivoandika kwenye maoni, KABLA HATUJAWA NA TUZO ZA BLOGU BORA tutekeleze ambayo naamini ni muhimu KUWEKANA SAWA kwa wateua na wateuliwa. Naulizia ama kuelezea VIGEZO kadhaa.
-Kwanza BLOGU NI NINI? Na ni vipi tunaweza kuziunganisha ama kuzitenganisha na "forums" mbalimbali kama Jamii ama Wanabidii?
-BLOGU ZINA JUKUMU GANI na ZINAWAFIKIA VIPI WALENGWA? Ni kweli kuwa blogu zetu zinajipenyeza kuelekea kwenye uhitaji?
-BLOGU ZINATHAMINIKA kwa umaarufu wa wamiliki ama maudhui kwa jamii?
-UBORA WA BLOGU NI UPI? Idadi ya watembeleaji? Kama ndivyo basi Ze Utamu yaweza kuwa blogu bora zaidi kupata kutokea kwa waTanzania. Ama ni MAUDHUI yenye kuifaa jamii?
-UPI UELEWA WA WATEUZI? Wateuzi watakaoteua ni bloggers ama wasomaji?

KATIKA ORODHA ILIYOTOLEWA......
Ningependa kuona TUZO YA HESHIMA KWA KAKA NDESANJO MACHA. Muasisi wa blogu za kiswahili na ambaye anaendelea na mambo ya tovuti katika kukikuza na kukiendeleza kiswahili. Lakini pia naamini njia iliyo sahihi katika kufanya tuzo,
KWANZA NI KUWEKA UMOJA WA BLOGGERS. Ukweli ni kuwa hata bloggers wenyewe wamegawanyika kwa makundi. Hatuna umoja.
PILI KUWASILIANA NA BLOGGERS WOTE kuhusu tuzo hizi. Ina maana wote wajue kinachoendelea. Ni vibaya kusema ni tuzo za blogu bora ilhali wapo wanao-blogu na hawajui kuwa kuna tuzo. Kwa hiyo waandaaji watafute orodha ya blogu zote ili kuhakikisha mnazijua.
TATU...CATEGORIES. Namheshimu na kumpa pole kakangu Profesa Matondo ambaye amezigawa blogu zote kwa mujibu wa habari zao. Ninalopendekeza ni kuwa bloggers wote waandikiwe emails na kuuliza kuhusu CATEGORIES za blogu zao ili kuhakikisha kuwa kila blog inatambulika kuwa iko kwenye CATEGORY gani na kama itapendekezwa katika category isiyo, basi irekebishwe. Ni lazima blogs ziwekwe kwenye sehemu husika ili thamani ya tuzo iendane na category yake.
Kisha tuhimize UMOJA BAINA YA BLOGGERS. Ni wazi kuwa bloggers wengi hawana ushirikiano na pengine hawapendi kushirikiana. Ni kama kuna matabaka ya blogs na zaidi ni kama vile matabaka haya si kwa content ya blog, bali umaarufu wa blogger. Lakini tunatakiwa kwanza kuhimiza umoja kwani KAMA HATUNA UMOJA, HATUTATHAMINI USHINDI WA WATAKAOSHINDA. Na kama HATUNA NIA MOJA YA KU-BLOGU, basi itakuwa ni FASHENI.
Kwa mnaopenda kujaza fomu ya kushiriki ama kushirikishwa, BOFYA HAPA na kama unataka kusoma orodha ya waliochaguliwa basi BOFYA HAPA

NDIVYO NIONAVYO TATIZO....NA LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDILO TATIZO

Sunday, May 8, 2011

Kwa Mama yangu, Mamaa wangu, Mama wa kwetu na Mama zetu

ASANTENI......Katika MAISHA YANGU, kila mtu ana umuhimu. Na kila mtu ni sehemu ya ukuaji wangu japo umuhimu na ukuaji huo waweza kuwa ama kuja kwa aina na malengo tofauti. Lakini "mwisho wa siku" nakuwa nimejifunza na nimeerevuka zaidi ya nilivyokuwa kabla. NDIVYO NIFAHAMUVYO KUHUSU MAISHA.
Lakini pia nataka kukiri kuwa maisha yangu ya kila siku yamekuwa zao na endelezo la kinamama ambao katika ngazi na matukio mbalimbali maishani wamekuwa sehemu kubwa ya suluhisho. Simaanishi kuwa kinababa hawapo (kwani kinamama hawa wamekuwa walivyo kutokana na kinababa walio upande wao), lakini kwa kuwa leo ni siku ya kinamama hapa Marekani (naamini haiadhimishwi pamoja duniani kote), naomba nizungumzie nafasi yao maishani mwangu. Mama yetu.....HAKUNA KAMA YEYE. Mama wa kwetu (dada zetu) ambao wote sasa ni WAZAZI. Nawapenda nyooote na nawatakia kila siku iliyo ya mafanikio kwani kwangu mimi, kila siku ni siku yenu, ni siku niwakumbukao na kuwaombea.
Kwanza nianze na Mama yetu mpeeenzi. Ambaye katika miaka 18 ya mwanzo maishani mwangu amekuwa MSINGI IMARA wa mimi kuwa nilivyo. Beres Hammond alipata kuwaelezea wanawake akisema kwa wakati mmoja, mwanamke anaweza kuwa "tough as a rock, but soft like a rose petal". Na hayo nayaona kwa Mama yetu. Kwa nyakati tofauti nilidhani kuwa sahihi zaidi yake lakini baadae nilikuja kuelewa kwanini amekuwa namna alivyo na kwanini alitenda alivyotenda na mwisho kuwaza "kwanini alitenda yoote aliyotenda kwa ajili yangu? SINA NINALOWEZA KUMUOMBA MUNGU ANIONGEZEE KWA MAMA YANGU.
Lakini pia kuna Mama mkwe wangu (ambaye leo nayarejea malezi yake kwa kutumia mwanae ambaye ni mke wangu na ambaye anaakisi maisha halisi aliyokulia). Mama huyu ndiye aliyeleta kile niitacho FURAHA YA KWELI maishani mwangu. Amelea mtu ambaye sasa ni suluhisho halisi na kila nimuangaliapo mke wangu na kuzungumza na Mama Mkwe wangu nahisi mwenye BARAKA ya kipekee kupokea "tunda la malezi yake". Mamaa wangu. Mama wa mwanangu na "stress buster" wangu. Ndio....MKE WANGU..... HAPPY MOTHER'S DAY
Nirejee kwa Mama wa mtoto wangu. Huyu ndiye "STRESS BUSTER" kwangu. Ni makao makuu ya furaha yangu na dampo la mawazo yangu. Kwa huyu sina ninaloweza kusema mengi kwani ndiye anifanyaye niendelee kuwa vile ambavyo wazazi na walezi wangu waliweka msingi huo.
Maisha yangu yalipitia malezi ya Mama zangu wadogo na Dada zangu. Hawa nao ni sehemu kubwa ya maisha niliyo sasa. Nikiwa mhangaikaji asiyeonekana kuwa na mafanikio ya karibu maishani, waliendelea kunishauri, kunipa moyo na kunisaidia katika kile nilichoamini kuwa ni fanikio langu lijalo. Kwa asilimia kubwa najivunia uwepo wao na kwa kuwa kwa pamoja wote wamekuwa MSAADA MNYOOFU kwangu kwa kuwa na suluhisho lisilohitaji mimi kudhihirisha kitu ili kulifikia. WALIKUWA, WAMEKUWA NA NAAMINI WATAENDELEA KUWA UPANDE WANGU.
Lakini pia nina Dada wadogo ambao nao kwa nafasi waliyokuwa nayo walikuwa chachu saana ya mimi kufanikisha nitakalo. Nakumbuka nikiwa Times Fm kuna wakati ambao "feedback" pekee ambayo ningeipata ni kutoka kwa Kaka na Dada zangu wadogo ambao walijitahidi kunisikiliza kila uchao na kunipongeza ama kunicheka "nilipochemsha" jambo ambalo liliongeza ufanisi kwangu. Kwa hiyo kwa kina Dada Abeella, Byela, Atu, Juliana na wengine (ambao mmeshakuwa Mama Wadogo na mashangazi), nawashukuru, nawapenda na natambua kuwa mmekuwa sehemu kuu ya changamoto zilizonifikisha hapa nilipo.
Kuna Dada zangu wa hiari ambao kiiiila siku nawasiliana nao. Iwe ni kwa kusoma kwenye mitandao yao ama wao kusoma kwangu. Iwe ni kwa kuwasiliana kwenye facebook, messenger, msn ama aina yoyote ya mawasiliani ya kijamii. NAWAPENDA SAANA.
Mmekuwa nguzo muhimu ya kile nionacho kama mafanikio na mmefanikisha kuboreka kwa HIMAYA HII ambayo ni sehemu ya maisha yangu pia. Kwa kina mtabibu wa blog, Dada Subi, Da Yasinta wa Maisha na Mafanikio na Dada "muamshaji" Koero wa Vukani, Da Sophy wa Bambataa, Dada Agnes wa Kiduchu, Da Sarp wa Angalia Bongo, Da Faith wa "Ulimwengu Mdogo", mwanamke wa shoka Da MiJAH, Dadangu Dina wa Marios, Da Edna wa "mchakato wa maisha" (strive for life), Dada Happy Katabazi uwapaye hofu viongozi kwa kalamuyo, Dada Jackline Charles, Dada mpiganaji Judith Wambura, Dada zangu wajasiriamali Marium Yazawa na Shamim wa Zeze, Dada mwenye wito wa mitindo na mavazi Scola wa Passion4fashion, mshairi wa kutazama Upande wa Pili Da Serina, Dada Sophie wa Sophie Club, Dadangu Mpenzi Mary Damian na Da mkubwa Chemi wa Swahili Time. Dada-Rafiki Makrina a.k.a Mama Paul nawe shukrani kwa uwepo wako.
Kwa kinamama nyooote mliogusa maisha yangu kwa namna yoyote ile, nawapenda na kila siku naona na kudhihirishiwa thamani yenu. Lakini leo kwa kuwa wametenga siku ya kuwaenzi hapa, NAWAOMBEA MAFANIKIO KATIKA KILA JEMA MTENDALO.
Kwa kinamama mlioonesha njia sahihi tangu awali, twawashukuru kwa mwanga mliotuwashia.
Kwa kinamama ambao mnatufunza kuhusu "upande wa pili wa dunia" nanyi pia twashukuru kuwa uwepo wenu watukumbusha kuwa dunia haijajazwa na wale watendao tupendayo tu. Mwanamke wa shoka (mtarajiwa) Paulina. AKISI ya kinamama wengi waliotulea sisi wazazi wake
Kwa kinamama watarajiwa, twatambua mwajifunza njia sahihi na twaamini mtaonesha usahihi huo wakati ukifika.
Lakini kwa ujumla wake, HAKUNA KAMA MAMA.
Msikilize Beres Hammond anaposema "What a woman"

Friday, May 6, 2011

Them, I & Them...AFRICA UNITE....Bob Marley

Alifariki tarehe 11 mwezi wa tano mwaka 1981. Tarehe ya kufariki kwake ni kati ya sababu zinazofanya mwezi huu kusherehekewa kama mwezi wa amani na pia kuwa na matamasha mengi ya kumuenzi Mfalme huyu wa Reggae duniani.
Waweza kuwa na tafsiri yako ya Bob Marley na pengine hata hadhi utakayompa kulingana na mtazamo wako kwakwe, lakini ushahidi wa kazi yake waonesha kuwa alikuwa zaidi ya mwanafalsafa, zaidi ya mtabiri, zaidi ya muona mbali na aliyeona njia sahihi za kuikwamua dunia miongo kadhaa iliyopita, aliyehimiza kuhusu KUJITAMBUA kama njia ya kutuweka huru na askari wa jeshi la amani aliyetumia kazi yake kama silaha halisi.
Aliimba katika wimbo wake aliouita Real Situation kuhusu wanyang'anyi wa mali za watu wanaoamini kuwa "the total destruction is the only solution" na tunaona yatokeayo ulimwenguni sasa. Katika wimbo huo huo alisema "Give them an inch, they take a yard; Give them a yard, they take a mile" akiwaeleza wale ambao wakipata kisa cha kuingia nchini mwako hawatoki na kila siku watakuwa na sababu ya kuendelea kuwepo kuinyonya nchi. Ndio tuonayo leo.
Lakini pamoja na mengi aliyoonya, Bob aliliasa bara la Afrika na wana wa Afrika kuungana kama njia pekee ya kuweza kusonga mbele. Japo wapo waliopinga alilosema (kwa kuhukumu muonekano wake), alilosema lilifanyiwa kazi (kinadharia) takribani miaka 21 baada ya kifo chake. Waligundua ukweli wa alilosema na kujitahidi kujipachika uasili wa wazo japo yajulikana alisema nani, kwanini na ili kiwe nini.
Bob aliweka bayana katika wimbo wake wa AFRICA UNITE kuwa kuna umuhimu na ulazima wa kuungana kikweli kwani twahitaji ku"Unite for the benefit of your children, Unite for it’s later than you think". Kibaya ni kuwa WATAWALA wetu wajiitao viongozi na ambao wana upeo mdogo zaidi ya Bob hawasikilizi usia wa kutupeleka tutakako.Wanacheza POLI=TRIX
Kumzungumzia Bob na nyimbo zake hakuhitaji ukurasa wa pekee, bali blog ama tovuti kamili kwa ajili yake, ila kwa leo naomba tuhitimishe mwezi kwa kumsikiliza katika wimbo huu.

Africa unite:
'Cause we're moving right out of Babylon,
And we're going to our Father's land, yea-ea.

How good and how pleasant it would be before God and man, yea-eah! -
To see the unification of all Africans, yeah! -
As it's been said a'ready, let it be done, yeah!
We are the children of the Rastaman;
We are the children of the Iyaman.

So-o, Africa unite:
'Cause the children (Africa unite) wanna come home.
Africa unite:
'Cause we're moving right out of Babylon, yea,
And we're grooving to our Father's land, yea-ea.

How good and how pleasant it would be before God and man
To see the unification of all Rastaman, yeah.
As it's been said a'ready, let it be done!
I tell you who we are under the sun:
We are the children of the Rastaman;
We are the children of the Iyaman.

So-o: Africa unite,
Afri - Africa unite, yeah!
Unite for the benefit (Africa unite) for the benefit of your people!
Unite for it's later (Africa unite) than you think!
Unite for the benefit (Africa unite) of my children!
Unite for it's later (Africa uniting) than you think!
Africa awaits (Africa unite) its creators!
Africa awaiting (Africa uniting) its Creator!
Africa, you're my (Africa unite) forefather cornerstone!
Unite for the Africans (Africa uniting) abroad!
Unite for the Africans (Africa unite) a yard!
/fadeout/


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, May 5, 2011

Pale teknolojia inapotubadilishia tafsiri ya maisha

Taswira toka University of Sydney Prometheus Research Team
Kuna tafsiri pana sana juu ya suala zima la URAFIKI.
Na kila mtu aweza kuwa na namna anayotafsiri, lakini mwisho wa siku, yaonesha tafsiri zoote nilizokutana nazo zahusisha KUJALIANA KWA WATU AMA PANDE HUSIKA. Ina maana yajumuisha kuwa na wakati maalum na wa kutosha wa kujitolea kwa yule uaminiye kuwa rafiki yako. Katika wimbo wa FRIENDS ulioimbwa naye Beres Hammond ambaye alizungumzia suala zima la urafiki, alisema "friends don't mean a thing if when I'm down you keep me down. Friends don't mean a thing, if I can't cry on your shoulder".
Sasa tunapozidi "kuendelea" tunaona namna ambavyo tafsiri za vitu mbalimbali vyabadilika. Oktoba 6, 2008 nilibandika toleo lenye kichwa cha habari Inapotafutwa maana mpya ya kifo kukidhi mahitaji ya afya (Irejee hapa). Yote ilikuwa katika kuangalia namna ambavyo MAENDELEO na sasa TEKNOLOJIA zinakotupeleka.
Leo nimepita kwenye ukurasa wangu wa FACEBOOK na kukuta nina marafiki 231. Nikawaza ninawasiliana na wangapi na ni wangapi ambao hata nikiandika kwenye "wall" zao wananijibu? Nina desturi ya kuwajulia hali wale ambao hawajawasiliana nami mara kwa mara na ambao hatuwasiliano kwa namna yoyote ile (ikiwa ni pamoja na kutembelea na kuacha maoni kwenye blogs zao), lakini bado nikagundua kuwa wapo ambao tangu wametuma "mwaliko" wa urafiki hawajajisumbua kujua maendeleo mengine ya "rafiki" yake mimi. Pia nikagundua kuwa wapo ambao nami sijawajibika kuwasiliana nao kama ambavyo ningependa.
NIKAJIULIZA...KWANINI SIWASILIANI NAO NA BADO NAWAWEKA KWENYE KUNDI LA RAFIKI?
Ni kweli kuwa wale tulionao kwenye rodha ya tuwaitao "marafiki" wanastahili kuitwa MARAFIKI?
Hivi tunajua WAJIBU WA RAFIKI? Tunajua TUNACHOTAKIWA KUFANYA KWA YULE TUNAYEMHESABU KUWA RAFIKI KWETU? Tunatekeleza kila tutakiwalo kutekeleza kwa wale tunaowaita marafiki?
Katika wimbo huu usindikizao hapa chini, Beres ameanza kwa kumuuliza kila ajionaye kuwa rafiki (nami nakuuliza wewe kuwa)
"Friends, what are you supposed to do? Should you build me up or break me down?
Friends what are you there for, if in my needs you're never around.
Friends what are your duties? Doesn't mean loyalty? Tell the truth even if when hurts, no matter what it may be.
Cause I got my problems and you know that I got them but still you say nothing though you know I'm hurting. Half way smiling when something is hurting and you're keeping the solution...friends don't mean a thing if when I'm down you keep me down. Friends don't mean a thing, if I can't cry on your shoulder"
Usikilize kwa umakini na kwa urefu / Ukamilifu hapa chini nawe ujiulize kuhsu URAFIKI

Tujiulize mengi katika kile tuaminicho kuwa ni MAENDELEO na hiki kiitwacho TEKNOLOJIA. Tuangalie namna ambavyo kwa mwendokasi wa kipekee, tunajipoteza kwa kufuata mfumo wa kile tuonacho kwenda na wakati.
Tujiulize MAJUKUMU yetu kwa wale wawasilianao nasi na kujua kama tunahitaji kuwa nao wote ama tuwe na wachache wanaotusaidia katika kukua kwetu na kukuza fikra zetu.

Ni CHANGAMOTO tuu katika kuyaangalia mambo kwa kile ambacho Dadangu Mija alikiita JICHO LA NDANI

Wednesday, May 4, 2011

Hesabu za siasa na ki-sisasa

Mara zote ni kinyume; wengi ndio wachache na wachache ndio wengi

Hivi ulibahatika kusoma toleo la Kaka Kamala alilosema MOJA JUMLISHA MOJA SAWA NA MOJA? (BOFYA HAPA KAMA ILIKUPITA). Je maoni ya waliochangia akiwemo Ndugu Born Again Pagan?
Kuna ukweli wa hesabu za wenzetu hawa wanasiasa ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa kinyume na zile tulizozoea kwenye masomo na elimu yetu ya kawaida. Wiki hii tumeanza na habari za kuuawa kwa Osama bin Laden. Watu wakasherehekea na kurukaruka wakisema WAMEMPATA MTU ALIYEKUWA AKITISHIA USALAMA. Lakini punde baada ya MTU huyo kuuawa, hali ya usalama ikaimarishwa duniani kote. Swali nililojiuliza na ninajiuliza ni kuwa "iweje mtu anayeonekana kuwa hatari auawe na kisha hali ya usalama iwe mashakani kuliko ilivyokuwa wakati yuko hai?" Unadhani unaambiwa ukweli kuhusu HATA ya mtu huyu? Ndugu yangu mmoja aliandika kwenye ukurasa wangu wa Facebook kwamba kama Osama alikuwa MTU HATARI, basi wamepata kimoja kati ya viwili. Wamempata MTU lakini hawajazuia HATARI. Lakini katika HESABU ZA KISIASA (ambazo naona zinakwenda kinyume na hesabu zetu wananchi), ni USHINDI. KWANINI?
Kwa HESABU ZAO, ni kama vile "wengi wanakuwa wachache na wachache wanakuwa wengi." Hakuna kujali kile wanachoimba na kuahidi kukitetea wakati wa kampeni zao. Hawawajali wananchi na kwao ubinafsi ni maana nyingine ya "manufaa kwa umma"
Labda tuangalie UMOJA WA MATAIFA ambao una wanachama lukuki na unaonekana "kutawala" dunia kimaamuzi lakini bado maamuzi ya mataifa matano yenye kura ya turufu ndiyo yanayoamua dunia iende wapi, iadibike na / kuadibishwa vipi, nani awe rafiki wa nani na nani awe adui wa nani hata kama hawana jibu la kwanini iwe hivyo. Na mataifa mengine yanatulia na kuendelea kutafsiri hiyo kama DEMOKRASIA.
Tukirejea kwenye ngazi ya nchi, tunaona kuwa maslahi ya wananchi pengine ndio kitu cha mwisho kufikiriwa akilini mwa "waheshimiwa" hawa. Wanatanguliza u-mimi na hata maamuzi yao hayaonekani kuwajali wengi ambao ndio waliowachagua. Hawawajibiki, hawaonekani kuwathamini na hawako katika nyadhifa zao kushughulikia lolote lihitajiwalo nao. Kwao, kulinda heshima yao ni jambo la muhimu kuliko kujali wananchi. Wanasikia matatizo, wanayaona na kisha WANAYAPUUZA
Nasema mahesabu yao yako kinyume maana kwao wananchi ndio "minority." Kwao wanaona kama wanahitajika kumaliza mahitaji yao kwanza ndio njia sahihi na ndio maana kwangu mimi ni WATAWALA kuliko viongozi.
Sasa kwanini tunawaamini? Kwanini tunawapigia kura wakati hatuna nafasi kwao kwani jamii nzima kwao ni "minority."
Wasikilize Morgan Heritage katika kibao chao hiki, POLITICIAN hasa wanaposema "why should we trust politicians, why should we vote every election? When there's no place for we, you and me, in the secret society they call us minority."

Sunday, May 1, 2011

Waliwaza nini kutenda waliyotenda baada ya kutenda waliyowaza?

Photo Credit: Kinesis Marketing
Niliposoma haya matukio nikawaza WALIYOWAZA mpaka KUTENDA haya baada ya kuwa WAMETENDA WALIYOWAZA AWALI.
Hii ni kuhusu "watu" hawa ambao kwa fikra zilizofuata baada ya MATENDO yao wameufanya ulimwengu kuwaza WALIWAZA NINI?Tuanze na "jirani" zangu wa Pennsylvania ambapo watu wawili "walifanikiwa" kuiba toolbox nyumbani mwa mtu na bila kuchelewa wakaamua kwenda kuliuza "fastafasta". Ambalo hawakuwaza ni "wapi pa kuliuza" na matokeo yake ni kuwa wakajikuta wanaenda kazini kwa waliyemuibia na kujaribu kumuuzia. Mwenye mali alipoangalia vema, akafananisha na toolbox yake, lakini akasubiri mpaka alipofika nyumbani ambako aligundua kuwa AMEIBIWA. Polisi waliwakamata Cody Lee Littrell (32), wa Hanover, Rebecca Erinn Dice mwenye miaka 32. Habari kamili waweza kuisoma HAPA.
Leo bado niko na WAHALIFU tuuu. Tumzungumzie huyu mwingine, Christian Longo, ambaye ANATAKA KUREJESHA IMANI YAKE KWA WANAJAMII baada ya kuua mke na watoto wake watatu.
Photo Credits: NY Dailynews.com
Sasa analazimisha serikali kumkubalia kutoa viungo vyake ili vikasaidie kuokoa maisha ya watu wengine baada ya kuuawa kwa sumu. Kwa mujibu wa ukurasa huu wa MSNBC.COM, "Christian Longo, 37, says he wants to do more to take responsibility for killing his family and dumping their bodies in coastal bays nearly a decade ago than simply accepting execution by lethal injection." Yaani anawaza KUOKOA maisha ya mtu mmoja baada ya kuwa ameua wanne. ANAWAZA NINI?
Najua wengine wanaisoma hii kupitia FACEBOOK. Basi kwanza nikukumbushe nilichowahi kuandika kuhusu mitandao hii ya kijamii. Niliandika kuhusu "kisa cha mama mmoja ambaye amepoteza mafao yake baada ya taswira katika ukurasa wake wa facebook kumuonesha mwenye furaha kuliko alivyoandikishwa kazini. Hiki ni kisa cha kweli na mama huyo sasa anajuta kwa kuwa na picha hizo ambazo zimetibua malengo yake a maisha.
Unaweza kufuatilia kisa kamili HAPA . Sasa wiki hii nimesoma kuhusu hawa wengine ambao "walifanikiwa" kuiba dola 62,000 benki, kisha wakaenda kujigamba kwenye Facebook, jambo lililowarahisishia polisi kazi ya kuwanasa. Jamaa hao waliandika kwenye Facebook siku moja kabla ya kwenda kuiba kwamba "U HAVE TO PAST THE LINE SOMETIMES!! TO GET DIS MONEY!!" kisha kesho yake baada ya "mafanikio" ya uporaji huo, mmoja wao akaandika "I'M RICH (expletive)." Haikuchukua muda kwa wao kukamatwa na kukiri kutenda kosa. WALIWAZA NINI? Soma kisa kamili kilichowashangaza hata maafisa wa FBI HAPA .
Na mwisho ni HUYU "mheshimiwa" ambaye alifanya kazi ya ziada juu ya kazi ya ziada kupunguza kazi ya ziada ya kumsaka. Photo Credit: Daily Mail
Ninamzungumzia Anthony Garcia wa California ambaye baada ya mauaji aliyofanya kwenye duka moja la pombe, alienda na kuchora tatoo kifuani mwake inayoonyesha eneo zima la mauaji lilivyotokea mwaka 2004. Sasa Garcia ambaye ni mwanachama wa kundi hilo la Rivera 13, anakabiliwa na kifungo cha miaka 65. Hebu soma kwa undani habari yake HAPA.
Kwa hawa wote...nawaza kuwa WALIWAZA NINI kutenda ama kutaka kutenda haya baada ya kuwa wamewaza waliyotenda awali?
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***