tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post1781135821250140783..comments2023-09-22T16:29:14.938-04:00Comments on "The Way You See The Problem Is The Problem": Unasoma upate kazi, kisha wafanya kazi miaka tele kulipia masomo hayo.Mzee wa Changamotohttp://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-24593149958361188272010-03-09T23:07:12.849-05:002010-03-09T23:07:12.849-05:00Yote kwa yote mimi nadhani huu ni utaratibu unaosa...Yote kwa yote mimi nadhani huu ni utaratibu unaosaidia vijana wao kupata elimu ya juu. Bila utaratibu huu serikali ingebidi ibebe mzigo wa kulipia gharama za elimu - mtindo ambao ni kinyume na mfumo wao wa ubepari dume wanaouendesha hapa. Akina Rush Limbaugh, Glen Beck, Ann Coulter, O'Reilly na "vichaa" wengine wa kihafidhina bila shaka wangeehuka kama hili lingetokea. <br /><br />Kama gharama hizi ni sababu mama inayowafanya madaktari watoze ada ghali namna hii (drip moja tu ya maji inaweza kukugharimu dola 500 halafu bili inaandikwa kwa kutumia bonge la msamiati wa kitiba), pengine serikali ingeweza kutafuta utaratibu wa kuwapunguzia mzigo wa deni la mkopo wa masomo yao. <br /><br />Hii inaturudisha kwenye mzunguko fumano usio na fundo na ukiangalia vizuri unaweza usione hasa nani anayestahili kulaumiwa hapa. Na anayefaidika na mfumo huu si daktari wala mgonjwa bali hayo makampuni yanayotoa mikopo pamoja na makampuni ya bima. Nadhani hali imekuwa mbaya mpaka baraza la Congress limeamua kuingilia kati ili kujaribu kuona kama kuna uwezekano wa kupunguza riba katika mikopo inayotolewa kwa wanafunzi. Ubepari...Huwa natamani sana kama Karl Marx angekuwa sahihi katika utabiri wake....Masangu Matondo Nzuzullima (MMN)https://www.blogger.com/profile/17267350894732424957noreply@blogger.com