tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post3323839739185489016..comments2023-09-22T16:29:14.938-04:00Comments on "The Way You See The Problem Is The Problem": Kabla hatujapata Rais wa upinzani, ......YATOKANAYOMzee wa Changamotohttp://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comBlogger4125tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-37075491264878227972010-12-08T17:55:36.126-05:002010-12-08T17:55:36.126-05:00Thanx Anon.
I can be reached at changamoto@gmail.c...Thanx Anon.
I can be reached at changamoto@gmail.com
BlessingsMzee wa Changamotohttps://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-70123771118103342542010-12-08T13:20:12.469-05:002010-12-08T13:20:12.469-05:00Wow all I can say is that you are a great writer! ...Wow all I can say is that you are a great writer! Where can I contact you if I want to hire you?Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-73547602363017994912010-09-22T12:51:25.778-04:002010-09-22T12:51:25.778-04:00fadhy katika hili la mabadiliko nakuacha uwe msema...fadhy katika hili la mabadiliko nakuacha uwe msemaji wangu. umekubali?

kinachoturudisha nyuma watanzania ni woga ambao umepandikizwa vichwani mwetu kwa vizazi vingi. leo wafanyabiashara wanaogopa wakifanya mabadiliko biashara zao zitakwenda kombo. wakulima wanadhani watakosa mbolea (mwananchi leo, mbeya vijijini). walio nje ya nchi wanadhani kukitokea mabadiliko hawatakuwa watanzania tena. wakinamama wanadhani watageuka wakina baba, wakinababa wanadhani watageuka wakina mama.

mkiwa madereva wengi kwenye chombo kimoja akichoka huyu anampisha huyu.

wapinzaji sio kuwa hawajijenga vijijini. wapo wamejaa tele isipokuwa vyama vyao havina mihela. pengine mihela itumike kuona vyama viko vijijini. lakini mihela ndio tumeikataa miaka yote kuwa sio msingi wa maendeleo nchini. wanaotoa mihela, mikapelo, mitisheti na mikanga wanaitoa wapi?

vyama vya upinzani vitajijenga kwa hoja sio kwa halua na tende.

kupinga kwangu kusubiri mno kuliwahi kunighafirisha na baadhi ya wachangiaji pale kwa Koero. time is 'nau'. pengine neno 'upinzani' lina ukakasi katika kiswahili na hivyo tunapoongea 'upinzani' katika siasa tunabeba dhana ile ilea ya ukakazi. ndio maana baadhi ya wanaharakati wanataka tuviite vyama vya ushindani. upinzani sio uadui. ni muendeleza wa ushindani katika kuleta maisha bora iwezekanavyo kwa wananchi.John Mwaipopohttps://www.blogger.com/profile/11708584279197669683noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-86103526371651967732010-09-21T04:11:31.724-04:002010-09-21T04:11:31.724-04:00Kaka Mubelwa huu ndiyo wakati ambao Watanzania kar...Kaka Mubelwa huu ndiyo wakati ambao Watanzania karibia wote ndani na nje ya nchi tunacheza mdundiko wa aina moja. Siasa na uchaguzi mkuu.

Uchaguzi mkuu unaohusiana na ustaarabu wa vyama vingi.

Wiki iliyopita niliweka maoni kwa kaka Chib, nikamwambia kuwa chaguzi zilizopita nilipiga kura kwa ushabiki. Mwaka huu nitaitumia vema kura yangu.

Kwa nini nadhani nitaitumia vema kura yangu? Kwa sababu nataka kuwa sehemu ya mabadiliko ninayopenda kuyaona. Hapo ninakumbuka busara ya Mahatma Gandhi, you must be the changes you wish to see in the world.

Awali nikiwa bado mdogo sana wa shule ya msingi, nilijiuliza sana, kwa nini Mwalimu Nyerere alitaka tuingine ktk mfumo wa vyama vingi wakati asilimia 80 ya Watanzania hawakutaka? Baadaye nikaja kumsoma vema katika kitabu chake, Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania.

Mwalimu alisema, CCM imejisahau mno. Hivyo inaelekea kuwa chama cha kidikteta. Huu ni ukweli ukweli mtupu. Kiongozi wa juu wa chama anapofikia pahala akawaona wananchi wengine wote hawana fikra wala kumbukumbu nzuri, kiasi cha kuwakatalia hakutoa lugha fulani aliyowahi kuitoa hata miezi sita haijapita, unaona chembechembe za mawazo ya Mwalimu.

Hebu tuone na hili. Chama kinachoyajali maisha ya wananchi wake, kikapanga bajeti zaidi ya bilioni 50 kufanya kampeni za anasa huku zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake wakiogelea kwenye bahari ya umasikini, tunapaswa tujiulize mara mbili. Nimekosea hapa, ninapaswa siyo tunapaswa.

Labda niseme na hili, uongozi uliokaa muda mrefu ukashindwa kujua namna ya kuzitumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wote. Nchi iliyobarikiwa mito, maliasili na ukanda mkuuuuuubwa wa pwani, milima, vilima na nyanda zenye rutuba kiasi hakuna mmea usiokubali Tanzania. Wanyama weeeengi. Bado uongozi huo ukasema hatuwezi kuendelea bila misaada. Unapaswa kufanyiwa mabadiliko.

Tunashindwa kuitazama Rwanda kwa jicho la aibu. Waliokuwa vitani miongo mingi. Wasio na bandari. Ambao ukubwa wa nchi yao ni sawa tu na ukubwa wa wilaya ya Mbozi, leo hatuwafikii kiuchumi. Sisi tunakazana kununua fenicha Dubai, magari ya bei chafu Japan na safari za anasa ndani na nje ya nchi.

Kila siku nikisimama kwenye kituo cha daladala pale Benki, jijini Mbeya, huwa nayaona maandishi makubwa kwenye uwanja wa mpira wa Sokoine. Yanasema, NCHI MASIKINI HAZIWEZI KUENDELEA KWA KUTEGEMEA MISAADA KUTOKA NCHI ZA NJE-MWALIMU J.K. NYERERE.
Tatizo mie nahama sana kwenye mada, ngoja nirudi.

Mabadiliko. Lazima yaje tu. Niliandika jana http://fadhymtanga.blogspot.com/2010/09/wakati-ukifika-umefika-tu.html

Mwaka 1992 wakati vyama vingi vinaanza, mtu mmoja Zablon I. Manzi, aliandika kitabu, Tuyaelewe Mageuzi. Yule bwana ana akili sana. Alieleza jinsi nchi zote duniani hususani za Kisoshalisti zilivyokuwa zikiyapitia mageuzi. Akatoa rekodi pale. Kama tungekisoma kitabu kile vema, tungeanza kujiandaa mapema sana kuelewa, tutake tusitake, mabadiliko hayakwepeki.

Jana nilisema tatizo tunaziogopa gharama. Ni kweli.

Wanaoziogopa gharama wacha waziogope. Sisi tutapewa moyo na kauli ya Mwalimu Nyerere, aliyoitoa panapo Novemba 5, 1980 akipokea maandamano ya vijana Ikulu kumpongeza kuchaguliwa kwake kama rais. Aliwaambia maana ya demokrasia. Akasema demokrasia siyo tu ni sauti ya wengi kusikilizwa, bali pia sauti ya wachache kuonekana.

Kura yangu, haitojali kama itakuwa katika sehemu ya sauti ya wengi kusikilizwa, ama sauti ya wachache kuonekana. Angalau itakuwa katika fungu la wao wasemao kwa uwazi kabisa kuwa, tunahitaji mabadiliko.Fadhy Mtangahttps://www.blogger.com/profile/10322331153810581894noreply@blogger.com