tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post7157017783411420182..comments2023-09-22T16:29:14.938-04:00Comments on "The Way You See The Problem Is The Problem": Uswahili, Mswahili na Kiswahili...Ni nini nani na kipi?Mzee wa Changamotohttp://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comBlogger7125tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-68429775847055656562012-08-17T22:30:56.468-04:002012-08-17T22:30:56.468-04:00Neno mswahili linamaana zaidi ya moja maana ya kwa...Neno mswahili linamaana zaidi ya moja maana ya kwanza mswahili ni mtu anae zungumza kiswahili.maana ya pili ni mtu anayeishi pwani ya afrika mashariki.lakini kwa maana za kimtaani mswahili ni mtu asiye kuwa mkweli.

pcmakerhttps://www.blogger.com/profile/11911602245892572359noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-33429420120665079612011-01-25T07:13:58.772-05:002011-01-25T07:13:58.772-05:00hapa patamu ngoja tujifunze zaidi!uswahilini kunav...hapa patamu ngoja tujifunze zaidi!uswahilini kunavituko,mswahili sana yule,acha mambo ya kiswahili wewe, jamani tusiwe waswahili!!!!
hao wote au sote tunaongea kiswahili na majibu au maneno tunayotamka ni kama hayo na mengine mengi!!!!!!!!!Rachel Siwahttps://www.blogger.com/profile/03819895731823514877noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-84195744766648111012011-01-23T17:42:19.310-05:002011-01-23T17:42:19.310-05:00Kwangu Mswahili hutegemea na msemaji. Kwanza hakun...Kwangu Mswahili hutegemea na msemaji. Kwanza hakuna kabila la waswahili. Maana tunaambiwa kiswahili ni lugha itokanayo na mchanganyiko na muingiliano wa watu mbali mbali kwenye ukanda wa pwani. Hivyo nukta ya kwanza ni kwamba hakuna kabila la waswahili.
Mie hujiita mswahili hasa ninapokuwa na hawa wazungu nikimaanisha muafrika. Nilipokuwa naishi Kenya niliwahi kuwaita wenyeji wangu waswahli wakachukia. Maana kwao mswahili ni mtu asiyestaarabika.
Baada ya kuwaelimisha nini maana ya kuwa mswahili, sikuona tena wakichukia pale nilipowaita waswahili.
Kwa mfano, niliwaambia kuwa adui mkubwa wa mswahili ni mtu anayemnyemelea mkewe au binti yake.
Niligundua kuwa kwao mke au mume kwa baadhi ya makabila si kitu cha thamani sana ukilinganisha na fedha.
Hii ilitokea baada ya rafiki yangu mkikuyu kuniambia kuwa naweza kuchukua hata mke au binti wa rafiki yangu ilmradi kuna chapaa. Nilishangaa nusu kufa.
Hivyo kwangu mswahili ni muafrika wa kawaida anayeishi kwa mila na tamaduni za kiswahili.
Wanangu wamezaliwa Kanada, Lakini bado huwezi kuwaita wazungu au waamerika kwa sababu ya kuzaliwa tu.Wala huwezi kuwaita wanyasa kwa vile hawajui kinyasa na mimi si mnyasa pure ikizingatiwa kuwa mama yangu hakuwa mnyasa. Naitwa mnyasa kwa sababu ya urathi wa baba kuwa alikuwa mnyasa pure.Hivyo, kwa vile nimekulia Dar es salaam huwa napenda kujiona mswahili.
Kuondoa dhana nzima ya ule uswahili wa hasara kama vile majungu, kutojali muda na matusi, waswahili wa Dar hujaribu kutofautisha uswahili na uzaramo ingawa na uzaramo si mbaya.
Kama alivyosema mwalimu Matondo, unaweza kuandika msahafu kuhusiana na dhana hii na usimalize.
Kwa hiyo wabongo mkiitwa waswahili na wakenye wakati mwingine ni kutokana na kiswahahili chenu mulua.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-60912783788281771972011-01-22T14:38:37.515-05:002011-01-22T14:38:37.515-05:00mimi ni shabiki mkubwa wa Kiswahili....huwa nasuuz...mimi ni shabiki mkubwa wa Kiswahili....huwa nasuuzika sana nizisikilizapo tungo kama hizo.Fadhy Mtangahttps://www.blogger.com/profile/10322331153810581894noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-78518135294788233782011-01-22T11:53:05.303-05:002011-01-22T11:53:05.303-05:00Mmmh!Mmmh!Simon Kitururuhttps://www.blogger.com/profile/08443099916542057958noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-27878851980725158622011-01-22T02:53:36.665-05:002011-01-22T02:53:36.665-05:00Mmmh, mimi nirudia usemi usemao `mkataa utamaduni ...Mmmh, mimi nirudia usemi usemao `mkataa utamaduni wake ni mtumwa' kwanini nimeanza hivi, kwasababu katika jamii zetu watu wamekuwa wakitumia neno `uswahili' kwa tafsiri mbaya, na hili chimbukolake ni `kiswahili'.
Najua wanamaanisha watu wa pwani, na zile tabia zo ambazo ni kinyume na maadili zikautwa `uswahili' ...lakini je tabia mbaya za makabila yetu zinaitwa `kabila letu...' ni nadra sana, ...
Sasa kwanini watu wakafikia hatua ya kukinasibisha kiswahili , au uswahili kwenye matendo mabaya. Upo usemi usemao, `ukitaka kumuua mbwa muite kwanza maneno mabaya. Hawa walioanzisika tala-lala hizi za uswahili ni wapinzani wa lugha ya kiswahili...!
LAKINI Wahenga husema chema chajiuza kibaya chajitembeza, leo hii kiswahili kinapanuka, hawa jamaa wanaima chini kwa aibu...kwasababu huu ni utamaduni wetu, sehmu hizi za Africa masharaki, tena na kati, na sasa ...ipo siku mtasikia ni miongoni mwa lugha za kimataifa!
Mengine kutokana na hoja hii yapo wazi, kiswahili ni lugha, mswahili ni mtumiai wa lugha hii, na uswahili ni yale matendo ya wanaoutumia lugha hii, lakini je ndio maana yake inavyotafsiriwa...hapana kwani wanasema `ukutukanaye hakuchagulii tusi..' AU NIMEKOSEA JAMANI...NI hayo tu mkuu!emu-threehttp://miram3.blogspot.com/noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-40562706943707249842011-01-22T01:00:53.486-05:002011-01-22T01:00:53.486-05:00Watu wameshawahi kuandika tasnifu za shahada za uz...Watu wameshawahi kuandika tasnifu za shahada za uzamivu kabisa kuhusu maswali haya. Si maswali rahisi kuyajibu hasa kwa wakati huu ambapo Kiswahili kimejitandaza duniani kote.

Hata tukiachana na Mswahili, pengine tujiulize tu Mhaya ni nani? Ni yule anayezungumza lugha ya Kihaya kwa ufasaha kama Kamala? Au ni mtu anayeujali na kuuthamini Uhaya - hata kama hafahamu Kihaya na utamaduni wa Kihaya? Vipi kuhusu kijana wa kizazi cha dot.com ambaye hafahamu Kihaya wala mila na desturi za Wahaya (mf. umuhimu wa senene). Bado tunaweza kumwita kuwa ni Mhaya? Ni nini kinachomfanya mtu aitwe Mhaya. Wewe Muberwa ni Mhaya? Kwa nini?

Kuna makala moja nzuri sana kuhusu jambo hili imeandikwa na Profesa John Mugane wa Chuo Kikuu cha Harvard ambayo inaongelea kwa ufasaha kuhusu suala hili. Na kwa watu kama Ngugi wa Thiong'o, wewe kama huwezi kuongea lugha ya kabila lako basi huna haki ya kusema ni memba wa kabila hilo!

Sehemu iliyobakia ya swali lako ni ya kifalsafa na inahusisha mambo mengi yakiwemo mfumo wa kinyonyaji na mahusiano ya kihasama kati ya makampuni ya Kimagharibi ambayo yanafaidika na biashara ya kondomu na vyandarua kwa kusaidiana na viongozi wetu wachache wenye njaa. Hili naliachia wachambuzi wengine walijadili kwa kina na pengine nami nitapata mawili matatu ya kujifunza na hatimaye kuongezea. Leo tunazugwa kwa kuletewa vyandarua na kondomu za "bure", na kama ulivyosema msisitizo hasa siyo katika kiini cha tatizo bali ni katika dalili tu. Na hili ni mojawapo ya matatizo makubwa ya Afrika. Na kwa jinsi tulivyotawaliwa kifikra, yaani tumekuwa kama vile hatuwezi kufikiri na kuja na masuluhisho yetu wenyewe - au kupendekeza masuluhisho tunayodhani kwamba yatagusa kiini cha matatizo yetu...Tumezoea vya bure na kuamuliwa mambo kama watoto wadogo na baada ya muda cha moto tunakiona. Hata huu upuuzi wa Dowans na Richmond tunaohangaika nao unaingia katika mkumbo huu huu.

Unakumbuka pia kuna kipindi fulani kulikuwa na ukame sana na maji katika bwawa la Mtera yalishuka sana. Baadhi ya wanasiasa walipendekeza eti kuleta wataalamu wa kuleta mvua kutoka Vietnam kuja kufanya "cloud seeding" ili mvua inyeshe karibu na bwana hilo ili lijae na mgao wa umeme hatimaye uwe historia. Kwa masuluhisho kama haya ni wazi kwamba tunavyoyaona matatizo yetu pengine ndiyo tatizo.

Nimebwabwaja vya kutosha. Ngoja niachie na wengine.Masangu Matondo Nzuzullima (MMN)https://www.blogger.com/profile/17267350894732424957noreply@blogger.com