tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post7660227466336147973..comments2023-09-22T16:29:14.938-04:00Comments on "The Way You See The Problem Is The Problem": MAHOJIANO: NOVA KAMBOTA NA ASKOFU SYLVESTER GAMANYWAMzee wa Changamotohttp://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-8951285990647982277.post-83425764386363482892011-06-11T21:30:17.525-04:002011-06-11T21:30:17.525-04:00Siasa katika dini ndio sababu mimi siendi kanisani...Siasa katika dini ndio sababu mimi siendi kanisani; na maiti yangu italiwa na funza jalalani ikibidi mpaka hapo nikiwapata viongozi wadhehebu au imani yenye kuitika "NAAM" au "HAPANA" na sio kutubabaisha sisi Waafrika katika hali ngumu tulionao leo ya kuletewa na wakoloni madawa ya kulevya watoto wetu kama sio kuletewa vijidudu vya ukimwi wakati wengine bado "wanamwomba Mungu" awaeleze eti kweli bomu limeripuka au la!

Naam, Mkuu! Kwa maoni yangu, Askofu huyu (kwa heshima lakini), anacheza mchezo wakisiasa pale anapoulizwa juu ya madai yake JK.

Kwanini adai yeye anamwuliza kwanza Mungu ampe jibu kwa swali kuhusu madawa ya kulevya kanisani? Kwani Mungu hakumpa yeye Baba Askofu akili kusudi atumie? Mbona Yesu alipoambiwa na Shetani aache mikate ya duniani bali atengeneze ya kwake kwa kutumia mawe, alikataa (ikiwa na maana kile Mungu aliekupa kama akili ukitumie na usikidharau nakwenda kumomba Mungu kingine kwa kudai wewe ni Mtakatifu au Mtoto Wake)?

Mimi naona Baba Askofu (tena kwa heshima kubwa) anaogopa tu akisema ukweli (na kuitika "Ndio, JK, wapo baadhi yetu!")atakosana na hao viongozi wadini wanaofikiriwa kuuza hayo madawa ya kulevya na huenda wakamdhuru. Sasa uoga na imani haviendi pamoja kamwe!

Baba Askofu pia anaogopa akidai "Hamna kitu kama kilivyosemwa na JK", wengi wafuasi wa dhehebu lake wataacha kuhudhuria kanisa kwani watamuona mwongo yeye mwenyewe, kwani yaliesemwa na JK ni kitu kinachojulikana kotekote Barani Afrika hasa ya Kusini, sio Tanzania tu!

Haya basi, Baba Askofu, endelea kumwomba Mungu akupe jibu. Lakini sisi tumekwisha kukuambia: watu hao kama alivyosema Mkuu Wanchi wapo kama kawa. Bomu unaedai wewe limeripuka kanisani ni moja tu: ile mantiki yako ya kudai hayo yote unayasikia mara ya kwanza leo kwa JK!Goodman Manyanya Phirihttps://www.blogger.com/profile/15369122107376580214noreply@blogger.com