Tuesday, March 30, 2010

Robo mwaka inakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???

Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.
Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo.
Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo.
Nafurahi kuwasiliana na kila mmoja wetu kuweza kuwaza changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii na kisha tujiulize kama tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu. Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa). Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ambalo ni JAMII. Awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona, ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue ilipo huduma. Afunzaye mapishi, mitandao, mavwazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.
Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.
Lakini je, mwaka huu ambao unamaliza robo yake ya kwanza wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu? Tumeshuhudia KUTHAMINIKA KWA KAZI ZA BLOGGERS kwa aina mbalimbali.
Tuliona wenzetu wakitunukiwa vyeti vya kuthamini kazi zao, tumesikia wengine (kupitia utambulisho wa blog zao) wamepata nafasi ya kushiriki vipindi vya idhaa za kimataifa kufanya uchambuzi wa habari. Hivi juzi tumemuona Kaka Michuzi akishiriki Diaspora huko London kwa nafasi yake kama blogger. Hizi ni chachu kwetu kuwa kuna kuonekana mchango wa kile tufanyacho na pia kuna kukua kwa ueleweka wa kazi zetu.
Ninalowaza ni VIPI TUNAWEZA KUWEKA NGUVU NA JITIHADA ZETU PAMOJA KUWEZA KUITUMIKIA VEMA JAMII?
Mafanikio ya blogger mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA na tunalostahili kufanya ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoianza robo ya pili ya mwaka 2010, tuangalie nyuma na kujiuliza, robo ya mwaka inakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??


Na hii iwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

Monday, March 29, 2010

Miaka 4 tangu kifo cha Shaaban Ally Mhoja Kishiwa (TX MOSHI WILLIAM)

Leo ni miaka 4 kamili tangu ulimwengu wa muziki nchini kuondokewa na moja ya nguzo zake. Tx Moshi William.
Mtandao wa Msondo Ngoma Band umeweka wasifu wake kwa ufupi kama ifuatavyo

Shaaban Ally Mhoja Kishiwa (TX MOSHI WILLIAM) he was born in 1954 at Hare small town along the road to Tanga City in Tanzania.

TX Moshi had four children, called Hassan, Maika, Ramadhai and Mahada.

He started music when he visited primary school at Hale in Tanga. Then he was performing music in small bands at Hale. In the 1970‘s he joined the Police Jazz up to 1982 when he became member of Juwwata Jazz Band, OTTU JAZZ BAND and then Msondo Ngoma Music band whereby he was among the owner of the band.

He died on 29th march 2006 at Muhimbili National Medical center. Due an accident he had in February 2006 and got injured his left leg.

During his membership at Police Jazz he had composed many songs, some of them are Mayasa, Dunia, Unalewa bila Kipimo and other kinds.

At Juwata/Ottu jazz band he composed a lot of song such as Asha mwana Seif, Hamida, Ashibae, Cheusi Mangala, piga ua talaka utatoa and others.

For his band, Msondo Ngoma Music Band he composed Kaza moyo, Ajali, and others.

The death of TX Moshi William leaves a big vaccum in our band. We‘ll not forget him forever.

GOD BLESS THE FAMILY OF TX MOSH WILLIAM!

Katika kukumbuka siku hii, naambatanisha kazi chache ambazo Moshi Williams alishiriki vema.
MSAFIRI KAKIRI


AJUZA

TUPATUPA

TUTAENDELEA KUKUMBUKA Tx Moshi William kwa kazi zako

Kwanini zilipendwa na vipi za sasa zitapendwa?

Kumekuwa na kutokueleweka kwa jina ZILIPENDWA ambako wapo waliodhani humaanisha nyimbo za kale sana na wengine wakiamini kuwa zimkuwa kiwakilishi cha nyimbo zote za kale huku wakiamini kuwa nyimbo zote za kale zilipendwa na kukubalika. Siamini katika fikra zote hapo juu.
Lakini licha ya kutokubaliana na kauli nzima ya ZILIPENDWA, ninaloona wasanii wetu wanapoteza ni KWANINI NYIMBO HIZO ZILIPENDWA NA NI VIPI ZA KWAO ZITAPENDWA.
Na leo ntajikita zaidi kwa wasanii wa "bendi za kisasa" na kuangalia kwanini tungo zao nyingi "zinapotea" katika ramani ya muziki kirahisi
Labda nianze kwa kuwarejesha nyuma kidogo mpaka Sept 30, 2008 ambapo niliandika nikiuliza Ni kipi tulichopoteza kwenye muziki wetu kisichorejesheka? (Irejee hapa) ambapo niliingia kwa kiasi kuuliza kama wasanii wetu wanafikiria kwa umakini kabla hawajabadili "midundo" ya miziki yao. Na nilitoa mfano wa Komandoo Hamza Kalala na Hussein Jumbe ambao wakiwa na bendi zao awali walivuma na kutunga nyimbo ambazo zinavutia kusikiliza hata sasa, lakini baada ya kuhamia "dansi ya kisasa" wamejikuta wakilazimika kufuata wapendacho mashabiki ambao hata hawajui wanapenda nini. Mwisho wa siku, wasanii WANAJIPOTEZA.
Ni sababu hii hii ninayoiona kwenye nyimbo hizi ziitwazo zilipendwa. Kwanza si nyimbo zote zilizoimbwa zamani zilizokubalika na kupendwa japo twajua kuwa kutokana na utaratibu uliokuwepo wa kuhariri kabla ya kurekodi, nyimbo nyingi zilizungumzia matatizo ama masuala halisi yaikumbayo jamii na hivyo KUPENDWA.
Haijalishi wimbo umeimbwa mwaka gani, kama utakuwa umeimbwa kugusa mahitaji na shida za jamii ni lazima utapendwa na kudumu. Ukisikiliza hizi ziitwazo "bendi za kisasa" na kusikiliza nyimbo zao zitokazo katika albamu za kwanza utafurahia mpangilio wa vyombo na maudhui (labda kwa kuwa huwa wana muda mrefu wa mazoezi) na mfano halisi ni nyimbo kama Mtaji wa Maskini wa TOT-Band ambao mpaka leo waweza hesabika kuwa kati ya nyimbo bora kabisa za bendi hiyo. Adolph Mbinga, Sister V (Much Respect to you Sis) Mimi na Rogert Hegga baada ya mahojiano 100.5 Times Fm 2002. Mbinga ameshiriki kupiga gitaa la solo katika nyimbo zote mbili za Fadhila kwa Wazazi
Lakini pia nyimbo kama Kisa Cha Mpemba uliobeba jina la albamu ya kwanza ya African Stars Band ulikuwa na bado una ujumbe wa kuelimisha leo hii. Lakini pia zipo nyimbo ambazo licha ya kuzungmzia masuala binafsi, bado zinaakisi maisha halisi ya wengi na mfano halisi ni nyimbo hizi zilizotungwa naye Rogert Hegga ziitwazo FADHILA KWA WAZAZI. Sehemu ya kwanza ilizungumzia mpango wa kuwatunza na kuwaenzi wazazi wakingali hai na sehemu ya pili yazungumzia namna ambavyo mambo yanaweza badilika kuliko tunavyodhani.

Kisha sehemu ya pili aliyoimba akiwa Mchinga Sound hapa chini

Mbali na Rogert Hega, tumuangalie Badi Bakule ambaye akiwa na African Revolution alitunga na kushiriki kuimba wimbo huu uitwao MTUMAI CHA NDUGU ambao hautachuja mpaka wale wote walio na tabia kama za CHANDE watakapobadilika na kuanza kufanya kazi. Na huu ni mfano wa nyimbo ambazo ZITAPENDWA milele kwani zimegusa meengi yaliyo ya kweli na halisi ndani ya jamii yetu.

Bendi walizopitia wasanii hawa baada ya kutunga nyimbo hizi zimerekodi nyimbo kadhaa lakini HAZITAMBULIKI kwa kuwa hazikugusa maisha halisi ya jamii na ndio maana hazikupendwa na hazitapendwa.
Ushauri kwa wasanii ni kukaa chini na kutunga nyimbo ziigusazo jamii na zenye kuisaidia jamii kujikomboa katika matatizo mbalimbali ikumbanayo nayo. Kwa kufanya hivi atakuwa wamekamilisha kazi yao kuu kama DARUBINI YA JAMII ionayo mambo na kuyachambua na pia kusaidia kuyatatua kwa njia iwagusao wengi kwa wakati mmoja.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa** . Ama ili kuweza kujua tasnia nzima ya muziki na wanamuziki wa Tanzania BOFYA HAPA

Sunday, March 28, 2010

Give Thanks and Praises. Jah Glory by Nasio

Kila niangaliapo utendaji kazi wa mwanadamu na kisha nikaangalia tofauti yetu na wengine na hata viumbe najikuta nikishangazwa nalo. Mazingira ya maisha yetu nayo ni kitu cha kushangaza saana hasa yanavyotofautiana mahala mpaka mahala na pia yanavyowawezesha walio maeneo yake kuishi vema wakiyatumia na kuyatunza vema.
Ni mambo mengi ambayo kwa ujumla niyaangaliapo na kuyatafakari hunifanya nirejeshe SIFA NA SHUKRANI kwa yule nimwaminiye.
Sina hakika kwako lakini hata uwezo wa kusoma haya niliyoandika ni kitu cha kushukuru na kukipa sifa.
Narejesha sifa na shukrani kwake.
Nasio Fontaine anaimba JAH GLORY. Anasema anashukuru kwa kila uumbaji auonao tangu mawio mpaka machweo. Tizama na usikilize pia.
JUMAPILI NJEMA

Saturday, March 27, 2010

Asemalo kaka Freddy Macha......NALO NENO

Picha kwa hisani ya ukurasa huu wa mahojiano yake na mtandao wa BONGO CELEBRITY
Wiki hii imekuwa na BARAKA kweli kwangu. Achilia mbali ugumu wa maisha ambayo yako kila mahali na pengine kwa asilimia kubwa ya watu hivi sasa, lakini nimeendelea kuona baraka za aliye juu kwa kukutana na kufunzana na wengi. Na kati ya ambao nimebahatika kuwasiliana naye kwa mara ya kwanza ndani ya juma hili ni Mwandishi Makini na mkongwe Kaka Freddy Macha ambaye baada ya mawasiliano mafupi, nilimuomba apitie "kibaraza" hiki nikiamini kuwa atapata mambo atakayonishauri kuweza kuboresha. Niliamini hivyo kwa kuwa nimeona akifanya hivyo katika blogu kadhaa alizotembelea na amekuwa akishauri kile ambacho ninaamini ni sahihi. Na ndivyo alivyofanya. Alipopata nafasi aliipitia na kushauri mambo ambayo nimekubaliana na ushauri wake na naanza kuyatendea kazi.
Lakini alikwenda zaidi ya hapo na kutoa ushauri / changamoto (katika mfumo wa maoni) katika toleo lililopita hasa kuhusu AJALI ZA BARABARANI. Nakumbuka tarehe 2 Disemba mwaka jana niliweka toleo hapa lenye kichwa cha habari Blogu ni shule. Wafunzao ndio wafunzwao (bofya hapa kujikumbusha) na hilo limedhihirika zaidi kwa changamoto hii aliyoitoa Kaka Freddy aliposema
"Kuna haja ya wanahabari na waelemishaji jamii wote kuungana na kuanza kampeni kabambe kuhusiana na udereva wa kizembe, rushwa, magari yasiyofaa kuwa barabarani, nk. Mpaka jamaa wa nchi jirani zilizokuwa mbovu zamani kutuzidi, leo wameanza kuulizia mitaani Ulaya: "Oh nasikia ajali za magari zimezidi kwenu Matizedi."
Hii si aibu? Tanzania nchi ya amani imegeuka nchi ya ajali za vipanya, fuko na nzige? Kampeni yaweza kufanywa hivi. Wanahabari, waandishi, waalimu na waelemishaji kupiga kelele, kuungana kukemea hili tatizo. Mbona UKIMWI umekemewa (Oh vaeni mipira na soksi) ; mbona wanasiasa wabovu (mafisadi) wanasemwa...vipi vibaka wanapigwa hadi wakauawa kwa kuiba nyanya mbili sokoni? Kwanini dereva anayekimbiza kipanya cha "Hiace" hadi akaua hakemewi na waandishi na wale wenye "mikono" ya waelemishaji na vyombo vya habari? Mbona abiria wanakufa na tai, wanajikaza kisabuni; wanakubali eti ajali na uzembe huu eti ni sehemu ya majaaliwa ya " Ubongo" na "Wanabongo"?"


Kaka Macha kasema "KUNA HAJA YA WANAHABARI....." na naamini sisi ni sehemu yao. Na hii iwe CHANGAMOTO YETU sote tulio katika tasnia ya habari kusaidia kuzuia ajali zizuilikazo
ASANTE KWAKO KAKA FREDDY KWA CHANGAMOTO HII

Kaka Freddy Macha ni mwandishi na mtunzi mahiri ambaye anajitambulisha kama mtu apendaye "michezo, afya, lugha, sanaa, fasihi na kuukomboa ulimwengu dhidi ya ujinga, umaskini na maradhi". Mkusanyiko wa habari na kazi zake waweza kuupata kwa kuanzia HAPA

Friday, March 26, 2010

Ninapowaza KUWAOMBEA VIONGOZI wapate matatizo

NIMECHOSHWA NA MAUMIVU NIHISIYO KILA NIONAPO AJALI NA NINA HAKIKA KAMA VIONGOZI AMA WENYE MAMLAKA WANGEKUWA WAMEHUSIKA KATIKA AJALI KAMA TULIZOPITIA NA KUWA NA MAUMIVU KAMA NILIYONAYO (NA WAHANGA WENGINE), WANGEFANYA JAMBO LILILO NDANI YA UWEZO WAO KUZUIA WINGI WA AJALI HIZI.
Picha zote mali ya FRANCIS DANDE wa Michuzi Blog
Kuna wakati ambao unajikuta ukiwaza visivyowazika ukiamini kuwa NDIO SULUHISHO PEKEE la matatizo tele.
Bushman aliwahi imba "in order for one to survive, sometimes you gotta take another one's life"

Najua kuwa leo ilistahili kuwa siku ya BURUDANI ya muziki wa Reggae ili kuifunza, kuielimisha na kuikomboa jamii kutoka katika utumwa wa kiakili, lakini habari iliyobandikwa jana juu ya ajali imenitibulia wiki yangu.
Ni hapa ninapokuja kujihisi nikikubaliana na msemo kuwa AISIFIAYE MVUA, IMEMNYEA. Na mimi kwa kuona taswira hizo hapo juu nimerejewa na machungu ya kinachowakuta wengi pale wanapopatwa na ajali. Najua kwa kuwa nami ni mhanga wao. Nimeandika saana kuhusu ajali iliyonikuta zaidi ya miaka 10 iliyopita na ambayo bado naendelea kuuguza athari zake. Januari 24 mwaka jana nikaandika kuwa Tumechoshwa na SALAMU ZA RAMBIRAMBI. Na sasa hatuzitaki. Na hii ni kutokana na kutokuwepo kwa sera ama mipango maalum ya kupunguza ama kuzuia ajali zitokeazo kila siku.
Tunaloona ni VIONGOZI KUTOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI kisha wasihimize kinachotakiwa kuhimizwa kusaidia kuzuia ajali hizo.
June 15 2009, SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) lilitoa ripoti yake juu ya takwimu na usalama katika barabara ilionesha kuwa watu 34.3 katika kila watu 100,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania ilhali wastani wa dunia ni watu 18.8 kati ya watu 100,000.
Jikumbushe alivyoinukuu Kaka Faustine (hapa)
Wamiliki wana magari ambayo hayastahili kuwa barabarani.
wamiliki wanatumia madereva kama vibarua na hawana mikataba nao.
Wamiliki hawawajibiki na tabia za madereva waendeshao magari ambayo yanabeba ama kupishana ama kutumia njia moja na magai ya abiria.
Wamiliki wa magari hawakamilishi matengenezo na kulinda VIGEZO muhimu juu ya ubora wa "mabati" yatumikayo kutengeneza bodi za magari.
Na bado, SERIKALI HAIFANYI LOLOTE. Sheria inasema hakuna kusafiri alfajiri mapema na usiku lakini tumeona kilichotokea hapo juu.
Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000, kulikuwa na wimbi la ujambazi wa kutumia silaha na polisi walionekana kushindwa kudhibiti mpaka waliouawa askari wenzao tukaona nguvu halisi walizonazo. Walifanya "operesheni" ambayo iliathiri majambazi na mpaka raia wanaosemekana kuwa wema wakifanya biashara zao za madini.
Kisha tukashuhudia ajali zikiendelea kuteketeza watu na viongozi "kutoa salamu za rambirambi" mpaka pale wimbi hilo lilipohamia kwa viongozi wakuu ambapo serikali ikaamka.
UKWELI NI KUWA WATENDAJI WA SERIKALI WANASTAHILI KUAMKA ILI KULINDA MAISHA YA WANANCHI (AMBAYO NI KAZI YAO KUU) NA PIA MAISHA YAO WENYEWE NA WAPENDWA WAO.
Na kama wao kuwa sehemu ya tatizo ndio njia pekee ya kupata suluhisho, basi na iwe hivyo.
Narejea kusema kuwa NIMECHOSHWA NA MAUMIVU NIHISIYO KILA NIONAPO AJALI NA NINA HAKIKA KAMA VIONGOZI AMA WENYE MAMLAKA WANGEKUWA WAMEHUSIKA KATIKA AJALI KAMA TULIZOPITIA NA KUWA NA MAUMIVU KAMA NILIYONAYO SASA, WANGEFANYA JAMBO KUZUIA AJALI HIZI.
Mpumzike kwa amani. SEE YOU IN ZION

Thursday, March 25, 2010

Happy Birthdate Da Agness

Ni sahihi kuwaza, kwani siku zasonga na majukumu yaongezeka
Ni siku nyingine katika maisha ambayo kwa wengine yamaaanisha mengi zaidi. Kuna kumbukumbu nyiingi maishani ambazo kwa wengine zaanza, na wengine zaendelea. Na hiyo ni sehemu ya siku yoyote ambayo kwa wengine ni "special"
Na leo ni siku muhimu kwa Da'Mdogo Agness Anderson amilikiye Blog ya Kiduchu ambaye leo anatimiza mzunguko kamili wa mwaka maishani mwake. Ni "mwaka mpya" wa maisha yake na kama mwana-blog mwenza, napenda kuungana naye katika siku hii muhimu kwake.
Labda kwa kuwa nina tu-miaka kadhaa twa kukabiliana na maisha, nikuase kuwa maisha ya sasa ni ya kukabiliana na kile chema uaminicho. Kwa sasa wapo wengi ambao watajitahidi kuja na "wazo" hili ama lile kukufanya uamini kuwa HUWEZI KUFANYA UTAKALO NA KUWA UPENDAVYO.
Hakuna la kufanya kuweza kuwakimbia hawa watu kwani "wameumbwa wawepo" na ndio ambao husababisha matatizo na UKUAJI wetu maishani. Kwa hiyo katika kuyasaka maisha mahala popote utakapoishi na vyovyote utakavyoishi, Lucky Dube kakukumbusha kuwa "Problems are there left and right. Liars, cheaters, politicians and back stabbers. Making life a little bit more unbearable". Na anaendelea kukuasa kuwa kuna mengi ya kufanikisha maishani iwapo utakuwa makini katika kutumia nafasi njema uzipatazo, kwa usahihi ukikumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa kutoa ama kupata, hivyo "you got to take what you can, when you can make the best of it."
Labda kwa kuangalia hali ilivyo sasa, kila mtu anasaka maisha na kila mtu ana taabu zake. Wapo walioshindwa kuwa wema na kufanya ya kusikitisha na kudharau zawadi kuu waliyonayo na MAISHA.
Lakini twaambia kuwa TUZO AMA ZAWADI YA MAISHA UNAYOISHEREHEKA LEO NI ZAIDI YA TATIZO LOLOTE duniani, hivyo "You could be having problems right now, but there's no problem worth your life"
Nakusikilizisha kibao chake Lucky Dube kiitwacho CELEBRATE LIFE (na maneno yake hapo chini) unaposherehekea siku yako hii muhimu
HAPPY BIRTHDATE DA'MDOGO AGGIE

We're living in the world with alot of crazy people.
We're living in the world with psychopaths.
Everyone of them wants to rule the world
Some people have the front row seat
At the top of the world
Some people have nothing but just a life
Problems are there left and right
Liars, cheaters, politicians and back stabbers
Making life a little bit more unbearable
It is a give or take world
So you got to take what you can when you can
Make the best of it. Wow!!

Chorus
say yeah!! Celebrate life
Say year!! Life is good.

We're living in the world with demented people
There's a man standing on the edge of the bridge
Ready to end it all
Some people don't know what life is worth
Some people have the front row seat at the gates of hell
You could be having problems right now
But there's no problem worth your life
People fight to stay alive every day
Cause they know, life is worth more than worries.
So you got to take what you can when can
Make the best of it, Wo!! Ho!! Wo!! Ho!!

Chorus
Say Yeah,yeah celebrate life
Say Yeah, yeah life is good.

Till fade.

Tuesday, March 23, 2010

UC Berkeley J-School opens 2010-2011 fellowships for African journalists

The Graduate School of Journalism at the University of California at Berkeley is pleased to invite applications for three yearlong fellowships for accomplished African journalists, beginning in the 2010-2011 academic year.

The fellowships will each total $36,000, including round trip airfare, professional stipends, and rent while in Berkeley.

The selected fellows will join the School’s Visiting International Scholars Program and participate in a new journalism training initiative aimed to provide high quality coverage of agricultural development issues in Africa for dissemination in U.S., African, and international media. The initiative will also offer dedicated funding for both domestic U.S. and Africa travel for research and reporting work.

Requirements:
Selected fellows must bring at least five years experience in journalism in sub-Saharan Africa, in any medium including print newspaper, magazine, television, radio, documentary, or new media format such as blogging, podcasting, and other online publishing.

Applicants also must demonstrate a proven track record of commitment to the truth-seeking craft, and a willingness to effectively investigate the problems of hunger on the continent with an aim to publish or broadcast stories about these topics and bring them to light in compelling form for audiences in Africa and around the world. A B.A. degree, at minimum, is strongly desired, along with experience and knowledge about agricultural issues in the applicant’s native country.

Selected African fellows will enroll with other Visiting Scholars in background courses at Berkeley examining the global food crisis starting in late August 2010, while also contributing their knowledge about Africa and journalism to their U.S. and international peers.

Please submit applications via the online form (click here).

To access the form, use the password: africa2010

The form provides spaces to include your resume, a one-page cover letter containing a statement of interest, and links to three examples of work.

For questions, contact africa@journalism.berkeley.edu

Deadline for applications: Monday, March 29, 2010

This opportunity is part of a two-year grant provided by the Bill & Melinda Gates Foundation to the Graduate School of Journalism at the University of California at Berkeley.


PS: Hii nimeipata leo 23.03.10
Subi
www.wavuti.com

Asante saana Dada Subi kwa kutushirikisha hili. Baraka kwako

Dunia na maji yake

Picha hii ya maktaba yake mdau John Lukuwi ikimuonesha Rais Jakaya Kikwete akizindua mmoja wa miradi ya maji katika kijiji cha Kishishi wilaya ya Urambo mkoani Tabora
Jana ilikuwa siku ya maji duniani ambapo dunia imekumbushwa namna ambavyo upatikanaji wa maji safi na salama unachangia kwa kiwango kikubwa katika kuyaboresha maisha ya kila siku ya mwanadamu. Kwa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Michigan, 70% ya dunia "imekaliwa" na maji japo bado upatikanaji wa maji safi na salama ni tatizo. Takwimu hizo zasema 97.5% ya maji yote ulimwenguni na MAJI CHUMVO hivyo kuacha asilimia 2.5 tu ya maji yasiyo na chumvi. Na 70% ya hayo yasiyo na chumvi ni barafu ama katika maeneo ya Antarctica na Greenland na asilimia kubwa ya yaliyosalia yamehifadhika kama unyevu wa udongo ama yako kina cha mbali chini ya ardhi na hivyo kutopatikana kirahisi kwa matumizi ya binadamu. Bara la Afrika bado laonekana kuwa na kiwango kidogo saana cha upatikanaji wa maji safi na salama ukilinganisha na mabara mengine na hili laendelea kuwa tatizo kwa wana-Afrika wengi.
Data from United Nations Environment Programme, GLOBAL ENVIRONMENT OUTLOOK
Duniani, mpango wa malengo ya maendeleo kwa karne ama Millennium Development Goals (MDGs) umesema uko katika harakati za kupunguza idadi ya wahitaji wa maji safi na salama kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015. Hii ni kati ya ile mipango minane iliyopangwa na viongozi wa dunia kuwa imepunguzwa kufikiwa nusu ifikapo mwaka 2015 japo yaonekana baadhi ya nchi za Afrika na hasa kusini mwa jangwa la Sahara ziko nyuma katika utekelezaji wake na haiaminiki kama zitaweza kutimiza lengo hilo la maji safi kufikia mwaka 2015. Lakini bado zipo nchi kusini mwa jangwa la Sahara ambazo zaonesha maendeleo makubwa katika suala la maji na mipango mingine. Feb 27 mwaka huu nilihudhuria Kongamano lililokuwa likijadili suala la MAJI SAFI NA SALAMA KWA BARA LA AFRIKA ambalo lilihutubiwa na watu wengi huku mgeni rasmi akiwa Balozi wa Jamhuri ya Liberia hapa nchini Marekani Mh. Nathaniel Barnes. Katika kuchangia huko, Dr. Carroll A. Baltimore Sr. ambaye ni Makamu wa kwanza wa rais wa Progressive National Baptist Convention, Incorporated (PNBC) alizungumzia uwiano wa gharama za utengenezaji wa maji ya chupa na usambazaji wa maji safi na salama kwa mamilioni ya watu kama asemavyo hapa chini.

Baada ya kongamano hilo, nilifanya mahojiano na Balozi Barnes na kumuuliza (pamoja na masuala mengine ya Afrika) suala la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wote barani Afrika. Tazama majibu yake hapa chini


BLESSINGS
Twahitaji kujitahidi kulipenda bara letu la Afrika lililo na vingi ili liweze kutusaidia.
Mzikilize Nasio akizungumzia upendo wa asili tulionao kwa bara letu la Afrika katika wimbo Africa We Love

Monday, March 22, 2010

Hongera kaka Fadhy na BLOGU YA "MWANANCHI MIMI"

Leo nasimama nikijivunia kushuhudia mabadiliko na maendeleo mengine kwenye ulimwengu huu wa ku-blog kwa Kiswahili. Ulimwengu ambao kama ilivyo kwa kitu chochote kile kilichoko katika hatua za mwanzo, waonekana uko kwenye hatua za "mpito" za kukua. Hatua ambazo kila kitu ni "mumo kwa mumo". Kama uvuvi wa kokoro ambao samaki, mawe na hata kobe wote wanakumbwa. Ni katika kipindi hiki ambacho twasema "viache vyote viote kisha magugu yatajitenga na mazao"
Ninalomaanisha hapa ni kuwa kuna blogs za wenye kujua kwanini wanafanya wafanyalo na pia kuna za wale wanaosaka kujua wanalopenda na kutaka kufanya na kuna za wale wafanyao wanalofanya kwa kuwa wenzao wanafanya ama kwa kuwa wana "access" ya kufanya wafanyalo.
Lakini leo hii, mmoja kati ya "wakongwe" (kwa muda ambao blogu zetu za kiswahili zimekuwa "hewani") anajivunia kuona blogu yake ikitimiza miaka 3. Kaka Fadhy Mtanga anaye-blog kupitia Blog ya MWANANCHI MIMI na ile ya DIWANI YA FADHILI amekuwa mshiriki mzuri wa kuonesha na kufikirisha dunia juu ya kile kilichopo "upande wa pili".
Na leo hii, blogu hii pendwa ya MWANANCHI MIMI inatimiza miaka mitatu. Sikuwa mfuatiliaji wa blogu wakati inaanza lakini nilikuja kutambua umuhimu wa blogu hii na tangu nijiunge nayo, nimejifunza na kujivunia meengi kuhusu kazi za Kaka Mtanga.
Ni kwa sababu hii na ile ya kuthamini michango ya watu mbalimbali nchini kulikonifanya kumuomba kaka Mtanga kutumia jina lake kama kipengele kimojawapo ndani ya blogu yangu ambacho hujikita katika kuonesha kile nijuacho juu ya watu ambao wamejitolea kunufaisha jamii nzima.
Ni katika kutimiza miaka hii mitatu ya blogu hii ya MWANANCHI MIMI ninapoojumuika na kaka Fadhy na wana-changamoto wengine kutafakari muelekeo wa wanablog / wananchi sisi.
Tujiulize tuliko na tupendako kwenda na hata namna tunavyoweza kukamilisha hilo.
Kaka Fadhy tuko PamoJAH na naamini kwa ushirikiano uutoao mara zote, TUTAFIKA TUUU.
Happy Third Birthdate MWANANCHI MIMI BLOG. Let's Keep On Moving

Mkaribishe Denzel Musumba ndani ya Blog Radio Talk

Denzel alipokuwa ndani ya Radio Umoja
Akiwa na askari wa Reggae LUCIANO baada ya mahojiano yake Radio Simba Fm
Jana wakati nasikiliza kipindi cha Jarida la Jumapili toka Idhaa ya Kiswahili ya VOICE OF AMERICA, nikasikia mahojiano kati ya Dada Esther Githui-Ewart na Denzel Musumba. Kijana ambaye anatumia huduma ya Blog Talk Radio kuendesha radio yake iitwayo East African Radio.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuhusu huduma hii na kisha nikajitoma huko kujua hili na lile juu yake. Kisha nikaungana naye na kumsikiliza alipokuwa "live" kwa masaa matatu.
Kwa hakika nilivutiwa na kazi yake. Ilikuwa Jumapili hivyo alitenga muda maalum wa nyimbo za dini na kisha akaendelea na burudani ya muziki mchanganyiko toka nchi zote zizungumzazo kiswahili. Uwiano wa muziki ulikuwa mzuri.
Na kisha likaja jingine la kupiga simu na kushiriki mada ambayo ilikuwa "Nini kikukeracho zaidi". Na hapo nikashangazwa na idadi ya watu toka nchi mbalimbali zizungumzazo kiswahili walio nchi mbalimbali ambao walichangia na kutuma salaam.
Nikashawishika kumpigia simu kujua hili na lile kuhusu redio yake na ndipo aliponiambia kuwa ni redio changa kwa wale wazungumzao Kiswahili na imekuwa ikijiongezea wasikilizaji kila uchao na licha ya kuwa na "umri" wa miezi miwili tu,imekuwa ikijipatia wasikilizaji mpaka 1000 kwa siku. Denzel ana uzoefu wa utangazaji tangu 2005 na amefanya kazi kwenye vituo vya West Fm nchini Kenya, Rock Fm huko Uganda,Radio Simba na kisha Radio Umoja huko Kenya
Waweza kusikiliza matangazo yake ya moja kwa moja na yale yaliyopita kwa kutembelea mtandao wake HAPA
BLESSINGS

Sunday, March 21, 2010

Yaaani ni kuwaza tuuu!!!!

"..kila kitu duniani lazima uwaze, hakuna litendekalo bila ya mawazo...". Haya ni maneno ya Da'Mkubwa Lady Jay Dee katika wimbo wake MAWAZO aliomshirikisha Ambwene Yesaya (A.Y)

Na humu alisema mengi kuhusu mawazo kwa wote, ukiwa na pesa, kichaa, mtoto, mkubwa yaani KILA MTU. Hii ina maana wenye kuwaza busara na ujinga pia., wenye kuwaza mema na mabaya vivyo hivyo. Ukweli wa kauli zake waendelea kujidhihirisha kila siku ulimwenguni

Wiki hii nilipokuwa nabarizi vibaraza vya wenzangu KUJIFUNZA hili na lile, nikatua kwa kakangu Prof Matondo akizungumzia POLISI ALIYETUHUMIWA KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO KWENYE SIMU YAKE AKIWA KAZINI (Isome hapa) na nikaona ni vema tukaangalia namna watu wanavyotumia vibaya mitandao na kuathiri kazi ama shule.

Lakini kabla hatujaenda huko, wacha nianze na hii ambayo ilikuwa ni WOW!! kubwa kwa wiki nzima.
Image from Catholic Conference of Ohio
Na hii ni habari juu ya mfungwa Lawrence Reynolds Jr wa Ohio ambaye alitakiwa kuuawa kwa sindano ya sumu kutokana na kukutwa na hatia ya mauaji ya Loretta Foster, 67, siku ya Jan. 1, 1994. Lakini kifo chake kiliahirishwa kwa kuwa "hakuwa kwenye hali nzuri kiafya kuuawa". WALIWAZA NINI??
Hii ilitokea baada ya mfungwa huyo kujaribu kujiua kwa kunywa vidonge vingi. Jaribio lake halikufanikiwa na hivyo alikuwa "unconsious enough to be executed". Mmmmmhhhhh!!!
Nilidhani alikuwa anawasaidia kupunguza gharama na taratibu za kumuua, lakini walimhudumia mpaka alipokuwa kwenye hali nzuri kiafya ili auawe. Na ndicho kilichotokea. Lawrence Reynold Jr aliuawa kwa sindano March 9, 2010.
Kwa habari zaidi Bofya hapa
Hii ilikuwa mara ya pili kwa kuuawa kwake kuahirishwa. Mwaka jana, mahakama ya rufaa iliahirisha kuuawa kwa Lawrence kwa kuwa walikuwa wana wasiwasi na utaratibu mzima wa kuwaua wafungwa huko Ohio baada ya mfungwa Romell Broom kuchomekwa sindano mara 18 wakati wakijaribu kutafuta mishipa ya kuweka drip za sumu na baada ya masaa mawili wakashindwa kupata mishipa hivyo kuahirisha uuaji wake. Kwa mujibu wa mahakama, hilo lilikuwa likivunja kile walichosema "Eighth Amendment constitutional rights against cruel and unusual punishment.."
Ili kujikumbusha mkasa huu na mingine ifananayo na hii, BOFYA HAPA
Image from Thinking On The Margin blog
Tukirejea kwenye TEKNOLOJIA, hapa Maryland kuna kesi inayoendelea kuunguruma baada ya wanafunzi 8 wa Winston Churchill High School kutumia kifaa cha kutunza kumbukumbu USB DEVICE "kuiba" taarifa muhimu na za siri (user ID and Password) zitumikazo kuingia katika akaunti ya mwalimu wao na kubadilisha grades zao na za wanafunzi wengine 46. WALIWAZA NINI???
Hili liliathiri wanafunzi wengi kwani majibu ya grades za wanafunzi 700 wa shule hiyo yalikabidhiwa kwa Polisi kwa uchunguzi na ilimlazimu mkuu wa shule hiyo kuwaalika wazazi wote na kuwaarifu kilichotokea. Lakini pia, vyuo vilivyo na wanafunzi toka shule hiyo ambayo ina rekodi ya kufaulisha asilimia 98 ya wanafunzi vilionesha wasiwasi wa usahihi wa wanafunzi wao kuwepo vyuoni mwao.
Soma habari kamili HAPA
Image from iStockphoto
Na mwisho kwa wiki hii ni ilee habari ya askari wa Israeli aliyehukumiwa baada ya kuvujisha taarifa za kina juu ya shambulio la siri lililokuwa likipangwa kufanywa na jeshi la nchi hiyo. Alifanya hivyo kwa kutumia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK. ALIWAZA NINI??? Hili la kuwa na uangalifu wa namna tunavyotumia mitandao hii niliwahi kuliandika HAPA.
Matokeo yake ilikuwa ni kuahirishwa kwa shambulio na kupelekwa mbele ya sheria kwa askari huyo.
Soma mkasa kamili wa askari huyo HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

Saturday, March 20, 2010

Burudani yarejea...............Asante kwa Da Subi

Doktori mkuu wa blogu hii, Subi binti Wavuti.
Kwa wasomaji wa blogu hii mtakuwa mmetambua kuwa habari nyingi ndani ya blogu hii hukamilishwa na muziki. Ama maelezo ya muziki ama nukuu toka kwenye muziki. Lakini pia kuna VIPENGELE MAALUM ambavyo vyazungumzia muziki ama viko hapa kufikisha ujumbe kupitia muziki.
Lakini kwa bahati mbaya, aliyekuwa host wa muziki wangu (www.imeem.com) alipotea bila taarifa na matokeo yake ni mimi kupoteza nyimbo zooote zilizokuwa zimehifadhiwa huko na hata codes ya zile zilizokuwa zimebandikwa hapa. Hilo liliniathiri na kuathiri "mmalizio" wa habari hapa. Nikaomba radhi na kuanza kusaka mahala pengine pa kutunza na kupata codes za muziki.
Daktari mkuu, fundi mkuu, mshauri mwandamizi na kadhalika na kadhalika wa blogu hii, Dada Subi alisikia kilio chngu na kunionesha mahala ninapoweza kuweka miziki.
Uzuri wa huko (ukilinganisha na niliyokuwa nahifadhia) ni kuwa web ya sasa yakuwezesha kucheza miziki hata kwenye webs ambazo wamefunga mitandao ya kushirikiana (mf Facebook, Youtube n.k)
Vipengele vya I & THEM pamoja na kile cha ZILIPENDWA sasa hivi vina miziki yote iliyopotea. Naendelea kujaza miziki ndani ya post za labels nyingine..
ASANTE SAANA KWA UVUMILIVU WAKO WAKATI WOOOTE NILIOKUWA SINA MUZIKI NA ASANTE SAANA KWA DA SUBI KWA MSAADA USIOISHA
Nakupenda, Nakuthamini na Nakuheshimu sana.
Zaidi ya yote, NAWAOMBEA MEMA WASOMAJI WANGU

Friday, March 19, 2010

Them, I & Them....NEVER GIVE UP....Luciano

Luciano kwenye onesho lake Zanzibar On The Waterfront 2008
Them, I & Them nayo ilikuwepo kudaka hili na lile
"Many of life's failures are people who did not realize how close they were to success when they gave up." Thomas A. Edison (1847 - 1931)
Nukuu hii ina ukweli mwingi na wa maana maishani mwetu hivi sasa. Wapo wengi ambao kutokana na mfumo wa maisha ulivyo na mkanganyiko wa uchumi wa sasa wameamua kuachana na kile wanachoamini na kukipenda na kujikuta wanajipotezea nafasi za kusonga mbele katika kukamilisha "mafanikio" yao maishani.
Pia nukuu hiyo hapo juu yanikumbusha kile alichokiimba hayati Lucky Dube katika wimbo wake TOUCH YOUR DREAM alipouliza "have you ever see the dream walking?, have you ever hear the dream talking? ....You are THE MASTER of your dream, if you pull the right string it'll be talking to you, don't hesitate, grab the chance before it's too late .... REACH OUT AND TOUCH YOUR DREAM"
Tunalokumbushwa hapa ni kuwa maisha yetu yako mikononi mwetu. Tunaweza kuamua kufanyia kazi kile kilichopo mawazoni mwetu (ambacho wengine wanakiita NDOTO) na kisha kukifanya kuwa kweli (na hapo watakibatiza jina la UFUNUO).
Ama twaweza kubaki na "kumbukumbu" ya tulichokiota na kushindwa kusonga mbele.
Lakini maisha yetu hayajaumbwa kuwa marahisi na ndivyo ilivyo na inavyotakiwa iwe. Kwa maana nyingine, kupambana na majaribu ni sehemu ya maisha tuliyopangiwa.
Ni katika hili, tunakutana na Jephter Washington McClymont ambaye anafahamika zaidi kama LUCIANO, anapotueleza kuwa MAISHA YAMEPANGWA NA MUNGU na kupanda na kushuka ni sehemu ya maisha.
Ukisikiliza ubeti wa kwanza, Luciano anazungumzia wakati ambao maisha hutuendea vema nasi tukadhani ni haki yetu kuwa hivyo nasi kusahau kuwa MUNGU ndiye chanzo cha mtiririko wa maisha yetu na ni wajibu wa kila mmoja kulitambua hilo.
Anasema "Just like a river moving water on and on to the sea. Like an Ocean always in motion, that is how you got to be. Just like the wind that blows on a constant flow that gives us life wherever we go. Like the sun that shines and allows our days to go.. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW."
Na katika kiitikio, Luciano anaendelea kutusisitiza kuwa licha ya ugumu wote huo, twatakiwa kuendelea kupigania kile tuaminicho mioyoni mwetu akisema "you should never give up, NEVER GIVE UP. Just keep on tyring. Never give up, believe in what you're doing. You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Lakini pia Luciano anaelezea wakati ambao mambo huwa yanakwenda kombo na baadae kuja kunyooka akituasa kuwa huo "ndio mfumo wa maisha" ambao MUNGU ameupanga na kwa kuwa yeye ndiye chanzo cha yoe, "hatutakiwi kushangaa".
Anasema "sometimes the crops refuses to bear and the harvest isn't really there. No rain the soil is cracked and dry, mothernature seems to die. Then one day shower came and the earth smiled again...... DON'T BE SUPRISED, 'CAUSE THAT'S NATURAL FLOW. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW"
Na kwa wale ndugu zangu wote walio katika magumu ya uchumi, maradhi, ukiwa, kuuguliwa, ama harakati nyingine zionekanazo kukwamisha kile ambacho umekuwa ukipanga kufanya kwa muda mrefu, nakwambia alivyosema Luciano kuwa "You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Msikilize hapa chini katika wimbo wake huo NEVER GIVE UP uliopo kwenye albamu yake ya Jah Is Navigator

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Wednesday, March 17, 2010

Nguvu ndogo ndani mwetu, iliyo kubwa kwetu na chanzo cha mafanikio na maanguko yetu.

Mwanzoni mwa miaka ya 200 nakumbuka nilikuwa nasikiliza kipindi cha KUMEPAMBAZUKA cha Radio One ambapo muongozaji wa kipindi hicho Kaka Godwin Gondwe aliyekuwa akihojiana na mwathirika wa virusi vya UKIMWI alitoa kauli ya hitimisho ambayo mpaka leo naamini ina ukweli maishani mwetu.
Alisema KAMA HUTAKI KITU, USISIKILIZE CHOCHOTE KUHUSU KITU HICHO. Kauli hii ilikuja baada ya binti mwathirika aliyekuwa akihojiwa kusema namna ambavyo alikuwa amejiwekea "nadhiri" ya kutomkubali mtu yeyote kwa uhusiano wa kimapenzi, lakini baada ya kumpa nafasi ya kuongea mwanaume mmoja, alijikuta akikubali kuwa na mahusiano naye kisha kufanya naye mapenzi na kusambaziwa virusi hivyo.
Ukiangalia kwa jicho la ndani, utagundua NGUVU YA KUSIKILIZA NA KUELEWA ilivyokuwa chanzo cha hayo yote.

Ni nguvu hii hii ambayo imeleta maanguko kwa familia nyingi. Familia ambazo zmeshindwa kutatua matatizo ya wazai na kuishia kwenye talaka kwa kuwa mmoja ama wazazi wote wanajiona kuwa sahihi na hakuna aliye tayari kusikiliza upande wa pili. Ni kutosikiliza huku ambako kumeyafanya mataifa makubwa kuelekea vitani na kugharimika kwa mamilioni ya pesa na baadae kuja kutambua kuwa walichokuwa wanadhani kuwa ndicho sasa sicho ama walichodhani kimefichwa hakijafichwa na mwisho wa mambo yajulikana kuwa waliofanya maamuzi HAWAKUSIKILIZA WALA KUELEWA.
Na hakuna ubishi pia kuwa nguvu hii ya KUSIKILIZA NA KUELEWA huwaponya wengi wanapoamua kutosikiliza yale ambayo yanaweza kuwaweka matatani. Nguvu ya USHAWISHI inayopitia kusikiliza huweza kuwatumbukiza wengi katika matatizo ama shughuli ambazo si sahihi ama salama kwa maisha yao na jamii kwa ujumla. Wapo ambao si makahaba, wezi, majangili, wauaji ama wakabaji kwa kuwa hawakuwapa nafasi ya kutosha wale ambao walitaka kuwashawishi kuingia huko.
Vivyo hivyo, wapo ambao si wafanyabiashara, watangazaji, waigizaji, waalimu, madereva, wachungaji na hata ma-Sheikh kwa kuwa hawakusikiliza na kuwaelewa wale ambao wangewashawishi kufanya hivyo.
Ina maana KUNA NGUVU KUBWA SANA YA KUSIKILIZA NA KUELEWA AMBAYO INAWEZA KUTUFANIKISHA NA KUTUANGUSHA
Lakini pia tukitafakari vema, kuna mengi tunayoweza kuyatambua na ambayo yatakuwa SULUHISHO la matatizo meengi hapa ulimwenguni
Nilichogundua ni kuwa HAKUNA MJINGA kwani kwa kukaa chini na kumsikiliza unaweza kujua kile ulichodhani kuwa ni ujinga na kutoka kwa "mjinga" huyo utaweza kujifunza namna walivyo wajinga hivyo utakuwa umeerevuka. Na huwezi kuerevushwa na mjinga. Hivyo, kama utamsikiliza mtu yeyote, utagundua kuwa si mjinga (hata kama hudhani kuwa ana busara na uelewa kama ulionao wewe katika uelewalo wewe kwa namna uelewavyo wewe)
Machi 5 mwaka jana niliandika kuhusu Nguvu baina yetu isiyo na nguvu ndani mwetu, yenye nguvu kwetu.(Isome hapa) ambapo nilizungumzia kwa kiasi nguvu hii kwa mtazamo mwingine na kisha Desemba 3 2009 nikaandika juu ya Nguvu ndani mwetu isiyo na nguvu kwetu bila nguvu miongoni mwetu.(Isome hapa) ambayo inajikita katika KUSHIRIKIANA ambako ni sehemu kubwa ya mafanikio ya kila mmoja wetu.
Dunia ya sasa inaongozwa na watu ama taasisi ambazo hazijihusishi na kusikiliza upande wa pili wa tatizo na matokeo yake hakuna suluhisho. Angalia mashariki ya kati kisha utaelewa. Bushman aliwahi kusema "United Nation should be dealing with equal rights, it is the only chance it can give us INTERNATIONAL PEACE, they only pretend to be what they're not. One day, one day, i know there'll be PEACE. There will be peace on earth" Dwight Bushman Duncan
Msikilize huyohuyo Bushman katika wimbo huohuo aliowaomba watu wapunguze kuongea na kuanza kusikiliza kisha watende aliouita TALKATIVE

Tuesday, March 16, 2010

ASANTE Dk. KINASHA... MAISHA MEMA UYAANZAYO SASA

Dr Abednego Kinasha (kati) ambaye alikuwa Rais wa The College of Surgeons of East, Central and Southern Africa (COSECSA) akiwa na Makamu Rais wa The Royal College of Surgeons in Ireland (RCSI) Profesa Frank Keane (shoto) na Rais wa The Royal College of Surgeons in Ireland (RCSI) Profesa Gerald O'Sullivan katika picha hii ya Mei 8, 2008.
Image from RCSI.IE
Nilipofunzwa somo la UJASIRIAMALI chuoni Dodoma, nilifunzwa sababu kuu tatu za kufanya kazi ambazo ni SABABU ZA KIUCHUMI ambazo ni kwa zile kazi ambazo wafanyao wanafanya ili kupata pesa hata kama hawapendi wafanyalo. Pia kuna SABABU ZA KIJIOGRAFIA ambazo ni kwa wale ambao wanapenda kusafiri na kupanua uwigo wao wa ulimwengu ikiwa ni pamoja na kazi zihusishazo kusafiri. Kisha kuna SABABU ZA KI-UTU ambazo huusisha watu ambao WANAFANYA KAZI ZA WITO na kwa hakika wafanyalo ni huduma zaidi ya kile walipwacho. Ndipo hapa tukutapo waalimu, waokozi / zimamoto na hata madaktari na wauguzi.
Ugumu wa elimu juu ya kazi na nia za watu kufanya kazi ni kuwa mwenye nia yoyote kati hizo tatu anaweza kuwa popote kwa sababu yoyote, na namna pekee ya kujua ama kuona nani anafanya kazi kwa nia gani ni kwa kumuona akitenda kazi hiyo.
Nami maishani mwangu nilibahatika kumuona Dr Kinasha akitenda kazi ya wito.
Kwa wanaofuatilia hapa wanakumbuka post yangu ndeefu ya Desemba 22 2009 iliyokuwa na kichwa cha habari MIAKA 10 BAADAE (Loooong Personal story) Isome hapa ambayo ilizungumzia ajali niliyopata. Katika post hiyo nikazungumzia juu ya msaada nilioupata toka kwa Dada ambaye nikingali natafuta mawasilianao naye, Dada Renatha Benedicto.
Ambalo sikuendeleza kwenye habari hii, ni kuhusu matibabu ambayo nilianza kuyapata kutibu mgongo wangu. Nakumbuka nikiwa chuoni Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2000, nilipata maumivu makali saana ya mgongo kiasi cha kushindwa kutembea na nilihofia maisha yajayo kwa kuwa sikuwa na imani kama kuna siku ningeondokana na maumivu yale. Nilipopata nafuu nilirejeshwa nyumbani kwa matibabu. Ni hapo nilipopelekwa Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) na kuonwa na Dk Abednego Kinasha.
Nilitibiwa na Dk Kinasha na Dk Ismail Shariff (kwa sisi wagonjwa tupendao kujimilikisha twasema "ndio wakawa madaktari wangu") kwa muda wote niliohudhuria pale na hata nilipokuwa narejea likizo niliendelea kuangaliwa nao.
Lakini licha ya kunitibu, Dk Kinasha na Dk Shariff waliendelea kufuatiia maendeleo yangu hata nilipokuwa nje ya Dar wakiuliza ndugu waliokuwa na mawasiliano juu ya maendeleo ya mgongo wangu.
HAPO NDIPO UJUAPO KUWA KUTIBU NI ZAIDI YA KAZI KWAO.... NI WITO.
Nimekuwa na maumivu haya kwa muda mrefu lakini sasa niko vema. Na natambua kuwa haijalishi ningepata Daktari bingwa wa vipi huku nilipo, kama Dk Kinasha na Dk Shariff wasingefanya lililo sahihi, basi pengine sasa hivi nisingekuwa na uwezo wa kusogeza mwili wangu bila msaada wa mtu. Ni usahihi wa matibabu ya awali walionipa ambao umenifanya niendelee kuwa nilivyo sasa.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, nilizungumza na Dadangu ambaye alinitaarifu kustaafu kwa Dr Kinasha. Ilikuwa ni HISIA MCHANGANYIKO. Zile za kufurahi kuwa anaenda kupumzika baada ya utumishi wa miaka mingi. Lakini pia kukawa na hisia za kuwafikiria mamia ya wagonjwa ambao watakosa huduma sahihi na ya ukarimu ambayo mimi na wengine wengi tumepata katika kipindi kirefu cha utu na utumishi wa Dr Kinasha. Najua kuwa hata "anapostaafu" bado ataendelea kuwatumikia wengi kama ambavyo aliendelea kunijulia hali hata kama sikuwa Dar kwa matibabu. Ni haya mema ambayo watu wanafanya kama sehemu yao ya maisha ya kila siku, yanayotufanya binadamu kuuona UBINADAMU WA KWELI kama alivyoandika Kakangu Matondo akikumbuka SIKU ALIYOKUTANA NA UBINADAMU WA KWELI PALE MUHIMBILI (isome hapa)
Ni wema huu wa kuwa msikivu, mkarimu, mkweli na mwenye busara aliouonesha Dr Kinasha wakati na baada ya matibabu unaonifanya kuendelea kumuona miongoni mwa HEROES waliopata kugusa maisha yangu. Kama alivyosema Lucky Dube kwenye wimbo wake hapa chini kuwa "Do you see the smile on their faces after you've done what you're doing? Do you see satifaction on their faces, after you have blessed them with your gift. You dont think it's much, but for them it means a WORLD. They wake up in the morning and wish you were there. You don't have to lie to gain their trust"

Leo hii natembea, nakimbia, nacheza na hata kufanya kazi na kulea familia yangu changa kwa kuwa Dk Kinasha alishiriki katika matibabu yangu ya awali.
Nakutakia maisha mema katika "ustaafu" uuanzao Dokta na popote uendapo tambua kuwa NATHAMINI SAANA MCHANGO WAKO.

ASANTE SAANA Dk. KINASHA...NAKUTAKIA MAISHA MEMA UYAANZAYO SASA

Monday, March 15, 2010

Za Kale vs Maisha ya sasa........MASUDI

Kwa wazazi wengi, hatua za mwisho kabla ya kumuona ama kumpokea mwana wao anapozaliwa ni kumfikiria na pengine "kupiga picha" ya nini ama vipi mwana wao atakuwa pale atakapokua mkubwa.
Ni hizi hisia ambazo wazazi wengi (haijalishi wana asili ama wanaishi wapi) huwa wanafikia na wengine KUMUOMBEA MWANA WAO na kuweka MATUMAINI kuwa na mtoto mwema.
Si kila mzazi huiona "ndoto" hiyo ikitimia na kwa masikitiko wazazi wengi huona ulimwengu kama umewageuka na kujiona kama wana mikosi.
Haya ni mambo yaliyoanza zamaaani na yaliimbwa na wasanii miaka mingi iliyopita.
Jumatatu ya leo nakuacha na kisa hiki kilichosimuliwa naye Marijani Rajabu katika maisha halisi ya wana-wapotevu katika kibao hiki MASUDI.
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa** . Ama ili kuweza kujua tasnia nzima ya muziki na wanamuziki wa Tanzania BOFYA HAPA

Sunday, March 14, 2010

Pacquiao amshinda Clottey kwa pointi

Usiku wa kuamkia leo, bondia Manny "Pacman" Pacquiao amedhihirisha kuwa yeye ni KING OF POUND FOR POUND pale alipomshinda kwa pointi bondia Joshua Clottey wa Ghana. Ushindi huu ambao umekuja kwa njia ya pointi, umekuja baada ya Pacquiao kushinda mapambano yake manne ya mwisho kwa KnockOut na likumbukwalo zaidi ni lile dhidi ya Miguel Cotto. Pia Clottey alipoteza pambano lake dhidi ya Cotto licha kuwa alionesha upinzani mkali na hata kumwangusha.
Lakini sasa kinachoangaliwa zaidi ni "nini chafuata baada ya pambano hili?"
Mei Mosi, Floyd Mayweather (aliyekimbia pambano dhidi ya Pacman) atapanda ulingoni kupambana na Shane Mosley. Na kwa kuwa kila mmoja wa watatu hawa ( Pacquiao, Mayweather na Mosley) alishajitangazia ama kutangazwa kama mfalme wa pound for pound, ushindi wa Pacquiao unafanya pambano la Mei Mosi kuwa la ushindani zaidi likitegemewa kutoa mpinzani wake
Je!! Ni nani atakayejipatia nafasi ya kupambana na Pacman kumsaka MFALME HALISI?
TUSUBIRI HIYO MEI MOSI
Tazama highlights za pambano la Pacquiao vs Clottey toka ESPN.COM

Na mahojiano ya Pacman baada ya pambano hapa chini

Ama kweli mawazo yetu hayafanani.

Hii ilikuwa ya wiki-jana lakini nikaiweka kando kupisha SIKU-KUU ya Da'Mogo wangu Faith.
Ni mwisho mwingine wa wiki na kama kawaida, twaendelea kujiuliza mengi mema na ya kushangaza wayawazayo wenzetu.
Nilipoanza ku-blog nilishangazwa na kuamua kuibandika habari ya huyu ndugu ambaye aliacha usia kuwa akifa, watakaokuja kumuona wamuone akiwa amesimamishwa NA NDIVYO ILIVYOKUWA (kama ionekanavyo hapa). Nimeikumbuka hii kwa kuwa wiki iliyopita nilikuwa natembelea "vibaraza" nikakutana na hii ya huyu ambaye alisema akifa, jeneza lake liwekwe UKWELI WA KILICHOMUUA MSOME HAPA KWA DA SCOLA. Nililowaza ni kuwa WALIWAZA NINI kuacha usia wa hivi?
Tuwaangalie wezi katika mwisho wa wiki hii.
Huyu wa nchini Brazil alienda kuiba kwenye sehemu ya mlo hukoo Brazil. Lakini bahati mbaya alishukia kwenye chimney isiyo sahihi kwani aliyoshukia ilikuwa imetumika kutengeneza BBQ hivyo alilazimika kuomba msaada. Waokozi wa zimamoto waliokuwa wameambatana na polisi walimuokoa na waweza kujua alipoelekea baada ya hapo. ALIWAZA NINI kushukia kenye chimney? Tazama "mnaso" na alivyookolewa hapa chini.

Hawa wameenda kuiba mahala na "wakafanikiwa" katika wizi wao. Ambalo hawakuwa wamelipanga vema ni namna ya kuondoa "troop" nzima waliyokuwa nayo katika kukamilisha "kazi" yao. Wakasahau mtoto. Easy catch. WALIWAZA NINI kwenda "kazini" na mtoto? Na pia WALIWAZA NINI kumuacha mtoto wao ambaye angekuwa na aligeuka kuwa "GPS" ya kujua walikotoka? Tazama taarifa hapa chini

Tumalizie na huko Florida (kwa kina Kaka Maondo) ambako simu ilipigwa kwenye kituo cha DHARURA (911) kuhusu wizi wa gari uliokuwa ukiendelea. Kilichokuja kugundulika baadae ni kuwa simu hiyo ilijipiga kwa bahati mbaya toka kwa mmoja wa wasichana hao waliokuwa wanaiba. Hebu ifuate kwa ufupi wake HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

Friday, March 12, 2010

Them, I & Them....ONE TIN SOLDIER.....Bushman

Pichani ya kwanza, wanawake wakiomboleza huko Jos na inayofuatia ni mazishi ya pamoja ya waliouawa huko Nigeria
Image from REUTERS
Walipowaua wenzao na kwenda kufunua jiwe, wakakuta LIKIOMBA AMANI DUNIANI.
Image from http://www.disabledartistsnetwork.net
Kati ya habari za kusikitisha wiki hii ni ile ya kuuawa kwa watu wanaokadiriwa kuzidi 500 huko Nigeria kwa sababu ambazo wengine wanaziona kama za kidini. WATU 500. HII SI TAKWIMU TU, BALI NI MAISHA YA WATU.
Na kibaya zaidi ni kuwa wanaouana ni wanandugu. Ni hili tukio linalonikumbusha kuhusu toleo nililowahi kuandika kuhusu wimbo huu wa ONE TIN SOLDIER. Na hapa naomba niurejee wimbo huu ONE TIN SOLDIER ambao uliimbwa miaka ya 1960 na ambao ni utunzi wao Dennis Lambert na Brian Potter. Kama umeusikia unaweza kuwa umejiuliza maswali mengi kuhusu maana yake. Nimeusikiliza mara kadhaa na kujiuliza kama yaliyoimbwa (ama niseme kutabiriwa) miaka hiyo ndiyo tuliyoyaona wiki hii nchini Nigeria?
Wimbo unazungumzia watu wa "Mlimani" na "Bondeni" ambao kwa pamoja wanajua kuwa kuna "MALI YA THAMANI" iliyozikwa mahala lakini hawajui ni nini. Na kwa kuwa kuna UROHO wa kutopenda kugawana mali hiyo, wale wa "bondeni" wanapoomba kushiriki katika umiliki wanahakikishiwa hilo lakini wanaishia kuuawa wanapokwenda kuiona kama walivyoahidiwa na wa "mlimani".
Na baada ya "kuwafyeka" wale wa bondeni, watu wa mlimani wanakwenda kufunua ilipo mali hiyo ili kujimilikisha na wanakuta HAZINA iliyopo inawaomba kudumisha AMANI DUNIANI lakini hiyo ni baada ya kuwa wameshatenda mauaji na kuwateketeza wenzao. Katika kufananisha nielewavyo mimi na "wachambuzi" wengine, nimekutana na mmoja wa walioelezea maana yake akisema na hapa nanukuu kuwa "... greed won't get you anywhere and that betraying your friends will ultimately leave you with nothing but loneliness." Sijui ni lini ndugu zetu wa Nigeria (na sehemu nyingine) watalitambua hili na kuacha "kuwaangamiza" wananchi wenzao wakitaka kujilimbikizia mali zisizodumu? Unapomuua nduguyo kwa sababu ya ki-Dini ama Itikadi za kisiasa unategemea nini? Bob Marley aliwahi kuuliza kuwa "Would you make the system make you kill your brotherman?". Na sasa jibu twaliona. Mfumo wa maisha, imani za kidunia na za kuamini tunakoweza kuwa zatufanya tuwaone wenzetu hawastahili kuishi bali sisi. Tukumbuke hotuba ya Emperor Haille Sellasie I kwenye Umoja wa Mataifa Oktoba 4, 1963 ambapo alisema "That until there are no longer first-class and second class citizens of any nation;..... Until bigotry and prejudice and malicious and inhuman self-interest have been replaced by understanding and tolerance and good-will; Until all Africans stand and speak as free beings, equal in the eyes of all men, as they are in the eyes of Heaven; Until that day, the African continent will not know peace."
MUNGI IBARIKI AFRIKA
Ukiusikiliza na kuusoma unaelewaje? Fuatilia wimbo huu katika toleo hili lililoimbwa naye Bushman.

"Listen people to a story
that was written long ago,
Bout a kingdom on a mountain
and the valley folks below
On the mountain sit a treasure,
buried deep beneath the stone
And the valley people thought
they'd have it for their very own.

Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.

So the people of the valley
sent a message up the hill
Asking for the buried treasure,
tons of gold for which they'd kill
Came an answer from the mountain,
"with our brothers we will share
All the secrets of our mountain,
all the riches buried there."

Now the mountain cried with anger,
"Mount your horses, draw your swords"
And they killed the valley people,
so they won their just rewards
Now they stood beside the treasure,
on the mountain, dark and red
Turned the stone and looked beneath it,
"PEACE ON EARTH" that all it said.


Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.".... x2


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA