Thursday, August 13, 2009

Yaliyofichwa kwa viongozi, yalifunuliwa kwa wasanii II

Lazima kuna atakayebeba laana ya kilio hiki picha toka http://www.edondaki.blogspot.com/
OKTOBA 29 MWAKA JANA NILIBANDIKA TOLEO HILI NA MPAKA LEO NAONA MATESO YA WENZETU YANAENDELEA. Leo tena nimeendelea kuulizwa kwanini napenda Reggae na majibu yanabaki kuwa yaleyale kuwa naiona IKITETEA WANYONGE ZAIDI YA MIZIKI MINGINE huku ikihimiza jamii kujikomboa kutoka katika utumwa wa kiakili. Sehemu ndogo ya BUSARA za watu hawa zisizosikilizwa na jamii ni hizi hapa. Ilikuja hiviii.........
Najaribu kupata pa kuanzia lakini nahisi ntaanza na swali la ni nini hiki?
Alisema Galinoma na nikaandika katika kipengele cha kila Ijumaa cha THEM, I & THEM niki-quote sentensi yake alipoimba "only this time, the downpressor man happens to be my own brother. Africans where are we going from here?". Ndiyo maswali tunayotakiwa kujiuliza kila wakati kwani ni sisi sisi tunaouana kila iitwayo leo kwa kutaka madaraka tunayopangiwa na wasioathirika na vita hivi. Namkumbuka Lucky Dube alipoimba kwenye wimbo wake uliobeba ajina la albamu wa Victims akionesha tofauti ya maovu waliyotendewa Babu zetu na wakoloni na ya sasa ambayo walio nje wanaangalia tunavyochinjana bila huruma akisema"Bob Marley said How long shall they kill our prophets while we stand aside and look. But little did he know that eventually the enemy will stand aside and look while we slash and kill our own brothers, knowing that alreadythey are the victims of the situation. Still licking wounds from brutality, Still licking wounds from humiliation" Kinachosikitisha ni kuwa anayesababisha kilio, majeraha na madhara haya ya kiakili, kimwili na kimazingira ni ndugu yetu. Ambaye anasema anapigania haki ya yule anayemuua. Na kati ya hao ni wale tuwaitao VIONGOZI. Nasio Fontaine aliimba kwenye wimbo wake wa Babylon You Doom alipowazungumzia hawa wanaosimama kupinga vita ilhali silaha zenye nembo za nchi zao ndizo ziuazo watu ambao viongozi wao wanaendelea kuua kwa kisingizio cha kusaka maisha mema kwa wawauao aliposema "babylon you speak of peace yet you make more war, you suppress the innocent to deceive the poor, death and destructions, hungry Baby Mother breasts run dry, yet you plan more war in your private sessions". Akaendelea kusema "you building more bombs and guns, yet babies are dying for hunger. We're the victims of your oppression. Blood of the innocent that you slaughter is upon your hands. You gave the gun, you set the fight, you sit aside and watch the slaughert."
Kuna mengi yaliyosemwa hapo awali na yanaendelea kuimbwa na kusemwa lakini sijui kwanini "viongozi" hawabadiliki na kuthamini utu na utaifa kuliko pesa.
Well. Kuna pande mbili. Ya wenzetu kaka zetu ambazo kwa manufaa yao na biashara za watengeneza silaha wanaamua kutothamini uhai wa wenzao na kuteketeza jamii kwa kisingizio cha kuleta maendeleo nchini mwao. Morgan Heritage waliimba kwenye swimbo wao so much more to come wakisema "these are the days known as eve of destructions, with POLITRIX just leading every nation" na ndilo tuonalo sasa. Wanaoathirika ni wale ambao hata hawajui maana na sababu ya vita. Watoto na kinamama na wenye ulemavu na mahitaji ya ziada ndio wanaobaki kuwa wahanga wa haya machafuko. Kusema hakumaanishi uoga, ila ni kuwa sauti ya wale wasioweza kupata nafasi ya kuandika haya maana wako kwenye mbio za angalau kusogeza dakika za maisha yao.
Kina mengi ya kuandika na kuna mengi ya ku-quote toka kwa wasanii hawa wema walioitetea na wanaoitetea Afrika na pengine wengine wanadhani kuandika haya ni ndoto kwani hayawafikii wahusika, lakini Tanya Stephens alisema "may be hoping for a change is a dream, may be life ain't as bad as it seems, but if dreaming is the best i can do then i'll be dreaming my whole life through." Nami ntaendelea kuota na kuomba kwa kuwa amani ni jambo nimuombealo kila mmoja. Si kwa kuwa naogopa kifo, bali kwa kuwa nawasilisha maneno ya wasanii wanaowasemea wasioweza kufanya hivyo. Lucky katika War and Crime alisema "I' m not saying this, because I' m a coward. But I' m thinking of the lives, that we lose everytime we fight Killing innocent people Women and children yeah Who doesn' t know about the good Who doesn' t know about the wars"

WE NEED TO "RISE UP, WISE UP, WAKE UP AND SHAKE UP"
NB: Nyimbo nyingi za reggae zapatikana kila Ijumaa katika kipengele ama LABEL ya I & THEM (hapa)

6 comments:

  1. Kwa kweli inasikitisha sana. Kuona watu wanateseka kama wanyama kuondolewa sehemu ambayo wamejijenga bila kupenda. Kuna wakati nikiangalia picha kama hizi nalia na nasema kwa nini?

    ReplyDelete
  2. bila kujitambua na kuitambua nafsi yetu kuu (our higherSelf / God realization) bado tuna wakati mgumu na mambo hayatabadilika wala nini yaani.

    people fail to know that even the early ages richest guys died, that even dictators like Hitler Amin, Musolin etc died. but also the believed to be good politicians like Nyerere, Washington etc, died that even the present leaders will die that each and everything's life span in this world is very very limeted and eternal life/ eternal love, supreme one and endless one is what matters.

    they kill fellows to get some very few situpid cents for their crazy bodily life!! sounds crazy, doesnt it?

    ReplyDelete
  3. Hawajali! Binadamu, japo kajipa cheo cha "uhomo sapiens" bado ni MNYAMA tena mnyama katili ajabu!

    ReplyDelete
  4. yani kilio hiki si chako peke yako ni cha wote.kila nikiona yanayoendelea tanzania nalia.nasema kwanini.hebu anaglia janga la ukimwi, wazazi,marafiki, watoto wanapukutika wakati hela za misaada ya ukimwi zinakuja kila siku. jamani hii na genocide ya rwanda natofauti gani, wote watu wanakufa. jamani nilikutana na mzungu akaniambia ukimwi unawaua sana waafrika hasa wa vijiji, niliumia maana alikua anakosea alitakiwa kusema, w2 wa vijijini hawafi kwa ukimwi bali kwa njaa na kukosa lishe na huduma za afya.ila nililia sana kuona tafiti zinasema waafrika wanakufa sana na ukimwi.waafrika hatufi na ukimwi ila nikwa njaa, mawazo, lishe duni na ukosefu wa huduma za afya. na walioathirika wengi ni viongozi wetu wala rushwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi,wanauwezo wa kununua maziwa,mayai na uhakika wa matunda kila siku. jamani viongozi wetu mbona ivi. ila kama mungu yupo kweli lakini hukumu ni hapa duniani.

    ReplyDelete
  5. jamani tuamke watanzania huu ni wakati wakuijenga upya nchi yetu. vijana tuko wengi kuliko wazee, na sisi ndo tunateseka. ivi wenzangu mnaweza kunipa umuhimu wa bung? minaona hakuna haja ya kuwa na wabunge. pesa ambazo wangelipwa wabunge tungejenga mashule, mahospitali na kununua madawa. hakuna kinachotushinda watanzania basi tu kugandamizwa na viongozi wanaojipenda wenyewe, na hawapo kwa ajili ya nchi hii bali kwa ajili ya nchi za magharibi. wakati si ndo tunaowapigia kura.ivi tusipopiga kura 2010 nani atauliza.itamaanisha hatutaki mtu yeyote. tunataka tuijenge nchi yetu upya. hebu ona mabomu yanatumika kuiba, hii si tanznaia ya jana, na mambo yataendelea maana w2 wamekata tamaa.nchi zote zenye vita ni kwasababu watu walikata tamaa,jamani kwanini haya yatokee. tuungane jamani.tuache ukabila,udini wala usomi.sisi ni wamoja, watanzania,waafrika. kidole kimoja hakiuui chawa,kumbukeni msemo huu jamani.

    ReplyDelete
  6. Hakuna mnyama mharibifu kama binadamu. Tumeiharibu sana dunia yetu.

    ReplyDelete