Friday, July 3, 2009

Born to suffer???????????

Katika taswira hii iliyopo kwenye Blogu ya Profesa Matondo, nimekumbana na maswali mengi kuhusu kile kinachotendeka kwa watoto hawa na kinachostahili kutendeka kuwasaidia vijana wengi kama hawa wanaojihusisha na maisha ya namna hii. Ni makosa ya nani kwa watoto kuwa walivyo? Na kama alivyouliza Prof Matondo, nani atalaumiwa kama watakuwa waharibifu wa maisha ya jamii?
Sikiliza wimbo huu wake Lucky Dube ambao unaimba kwa umakini kuhusu hali hii. SIKILIZA TAFADHALI

4 comments:

  1. Lucky Dube nyimbo zake zote ni nzuri anazungumzia maneno mazuri mimi nazipenda sana, We are born to suffer say aireee.

    ReplyDelete
  2. Wengi watasema ni sababu ya wazazi kutowalea wazazi wao kikamilifu. Lakini kwa mtazamo wangu nadhani ni kwa sababu vijana na watoto wengi wanadanganya kwenda mjini kuna kazi nzuri. matokeo yako ndo hayo

    ReplyDelete
  3. Bila mkakati wa kuhakikisha kwamba watoto kama hawa wanapatiwa elimu ni wazi kwamba Tanzania inakoelekea si kuzuri. Cha ajabu ni kwamba hata watoto wenye wazazi - lakini masikini- muda si mrefu hawataweza kujipatia elimu (ya juu). Usipojenga mashule basi jiandae kujenga magereza!

    ReplyDelete