Tuesday, July 21, 2009

Changamoto yetu na uanamitindo wetu

"Jamani nakaribia kuanzisha tuzo za mwanasiasa bora wa Tanzania ila kigezo awe na uwezo wa kubeba uzito mkubwa kwenye gym."
Ndio!!! Unashangaa nini?
Ndio maisha yalivyo sasa katika Tanzania yetu. Unapoamua kuangalia uwezo wa mtu kwa kuuficha na kutumia namna nyingine kueleza kile unachotafuta tena kwa kigezo kingine.
Hivi umeshafuatilia mashindano mbalimbali ya "kujionesha" yanayoendeshwa nchini kwetu? Umeshajiuliza kuhusu vigezo vinavyotumika na matokeo yanayopatikana? Sasa la kusikitisha ni kuwa wanachagua watu ambao (kiasi fulani) wana-fit yale mahitaji ya watafutaji (ambayo wakati mwingine hayafanani ya ya wal wanaowaiga) kisha wanakwenda kumpambanisha na huyo mwenye vigezo wakitegemea atashinda.
Luciano aliimba kuwa "THERE'S NO IN-BETWEEN RIGHTEOUSNESS AND EVIL, SO PICK THE CHOICE" na naamini wana mitindo na maonesho wanatakiwa kufikiria hili.
Tunaona watu wakiweka vigezo vya kumsaka mlimbwende katika mashindano ambayo kihalali hayako sawa na maisha ama mazoea (sitasema maadili) yetu na bado tunayafanya ndani ya mipaka ya mazoea yetu ilhali huko waendako wawakilishi wetu wanalazimika kuwa nje ya mazoea tuliyonayo. Ina maana tunatumia vigezo visivyo kusaka mtu atakayekwenda kushindana na vigezo halisi. Na kibaya zaidi ni kuwa katika michuano inayohusisha ambayo yako ndani ya tamaduni zetu, hatujishughulishi. Well! Ziggy Marley alipoeleza pale tunapojitokeza akisema "where we lose ourselves just to find who we are,.....where we escape from the surface of what we've become."
Sasa nasoma kuhusu hayo mashindano ya Sexiest Man in Dar na siku ya kwanza niliposoma kuhusu hilo nikataka kujua kuwa kwa kuwa ni kumsaka Sexiest, "ina maana majaji watakuwa ma-changudoa ama ma-nguli wa mapenzi na mashindano yenyewe yatafanyikia danguroni?" Maana nilipoona jina la shindano nikaanza kuhisi vigezo vitakuwa ni vipi, lakini nilipokuja kusoma vigezo vyao, nikajiuliza uhalali wa kutumia jina hilo.
Labda mimi ndiye "mporipori" nisiyejua ukuaji wa lugha (na hasa lugha za biashara) lakini nakumbuka hata Kakangu Nzunzulima Matondo alilizungumzia hili HAPA. Hakuna ubishi kuwa kuna kuiga ambako hakutupeleki tunakotakiwa kwenda na kama tunaamua kuiga, basi na tusijali tunachoiga na kuamua kuiga nusu kwani hilo hutufanya tuwe kama mihogo iliyopikwa lakini haijaiva hivyo HAILIKI. Tukubali kuwa wabichi (yaani kubaki tulivyo) ama tujibadili kwa kujipika kuwa kama tuwaigao na tukishaamua kuwaiga na tuwaige kwelikweli.
Najua TUNAJIPOTEZA na kabla hatujajipoteza zaidi, na tujiulize alilotuuliza Nasio kuwa Where we belong?
Ni mtazamo tuu, na naamini kuna TATIZO. Labda ni namna nionavyo "tatizo" ama namna uonavyo nionavyo tatizo. Kumbuka. Namna tuonavyo tatizo, ndio tatizo

3 comments:

  1. Nionavyo mimi, mambo mengi sana tunafanya kwa kufuata mkumbo, bendera hufuata upepo ndo na sisi tumekuwa hivyo hivyo, ama kutokana na utandawazi wa kielektroniki au wa kawaida tu wa kutembea duniani na kutembelewa, tumelimbuka na ulimbukeni wetu hauishi leo, alimradi hatujawa na 'chetu' kwa maana ya mila na desturi tunazoshikilia, basi ulimbukeni utaendelea kwa kasi kadiri ya mabadiliko ya huko tunakoiga yanavyotokea. Najiuliza kama itafika mahali dunia hii ikawa na aina mbili za tamaduni na kila mtu akalazimika kuchagua mrengo wa kufuata. Kwa sasa naona Umagharibi umeshika hatamu. Kazi ni kuiga tuuu, kuiga tuuu yenye maana na yasiyo na maana. Ndiyo maisha tena, ah!

    ReplyDelete
  2. hey! just stopping by. wondering did you forget me or not. lol. just kidding. how are you doing now? hope all went fine. hey, i changed my yahoo messenger : nindyaaydnina@yahoo.com
    and if you have windows live messenger : nindyaaydnina@live.com

    ReplyDelete
  3. ndugu yangu utaweza katika hilo kwa sababu mchakato ni mrefu sana.

    Lakini sikukatishi tamaa kila jambo hufanywa kwa nia.

    ReplyDelete