Sunday, July 26, 2009

Give Thanks and Praises....CELEBRATE by Luciano

Katika maisha tuishiyo, kuna lipi la maana ambalo tunatakiwa kujivunia? Ni lipi la muhimu tunalostahili kusherehekea? Na ni vipi twatakiwa kuishi maisha ambayo yatadhihirisha usherehekeaji wetu wa jinsi tulivyo?
Pengine wengi hawajui na wanaishi maisha ambayo ni kinyume cha namna ambavyo tunastahili kuishi. Na wapo wanaoishi hivyo kwa kuwa hawajui ni kwa kiasi gani wamebarikiwa kuwa walivyo.
Ni wakati wa kusherehekea kila sekunde ya maisha yetu, kwani si wote waliotamani kuwa tulipo, walioishi kama tuishivyo na kujitahidi kuwa tulivyo wameweza kuwepo tulipo wakati huu.
Tuungane na Luciano asemaye "come let's Celebrate, it's time for us to appreciate the gift of life that God has given to us..."

1 comment:

  1. Uliyosema ni kweli hapa duniani watu tunaishi mara moja tu. (we just live once) Kwa hiyo kila dakika ni mali ni lazima uifurahie. Ahsante kwa hili.

    ReplyDelete