Saturday, July 11, 2009

Ngoma Africa band kukiwasha cha moto ! Fest Afrika, Finland 18 Julai 2009

The Ngoma Africa Band aka FFU ! watatumbiza mjini Tampere,Finland katika onyesho la aina yake Fest-Afrika! litakalo fanyika siku Jumamosi 18 Julai 2009,katika sehemu ijulikayo kama Klub, mjini Tampere,Finland.
Kiongozi wa bendi Ebrahim Makunja aka Ras Makunja atakiongoza kikosi chake kuelekea mjini Tampere,Ufini kwa ajiri ya kuwapa burudani ya asiye na mwana abebe jiwe! washabiki wa Ufini,ambao ngoma africa imewapa cheo washabiki hao kuwa ndio wahajili wao huko ufini!.
Bendi hiyo mashuhuri kwa kuwatia kiwewe washabiki barani ulaya imeshawahi kutumbuiza huko ufini mwanzoni mwa februari mwaka huu 2009 nyakati za msimu wa baridi na kutoana jasho na washabiki! wameitwa tena kwa kazi moja tu ya kutoa burudani ya kukata na mundu.
Wadau wa Ufini na scandinavia kwa ujumla chereko chereko na mwenye mwana!
watumishi wenu The Ngoma Africa Band wanakuja kuwapa burudani
wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica ukiwataka ngoma4u@googlemail.com

2 comments:

  1. Mzee wa changamoto nipitie na twenda huko kuburudika.....lol

    ReplyDelete
  2. Natamani nami ningekuwa huko wakati huo!!

    ReplyDelete