Hii inakuwa wiki nyingine ninayorejesha SIFA NA SHUKRANI kwake Mungu kwa kuwa mkuu kwangu na kwa familia yetu kwa ujumla. Ni wiki ambayo Kaka Mdogo Binomutonzi Bandio (pichani juu) anakumbuka kuzaliwa kwake. Nasi tunaungana naye katika kuikumbuka siku hii njema kwake. Tunajua namna tulivyopata ulinzi wake na namna ambavyo Ka Mdogo huyu amekuwa akimtegemea Mungu katika harakati zake za kimasomo. Najua kwa sasa unajiandaa na mitihani ya MOCK na kisha mitihani ya kumaliza kidato cha sita. NAKUTAKIA KILA LILILO JEMA KAKA na pia endelea kuwa na IMANI kwa MUNGU umwaminiye kwani kwake ndiko utokako msaada tuhitajio. Leo pia napenda kutoa SIFA NA SHUKRANI kwa Mungu kwa namna alivyoweza kumnusuru Kaka-mdogo mwingine Sheme Bandio katika ajali mbaya ya gari. Kakangu huyu aliyekuwa akielekea katika kituo chake cha kazi alipata ajali hii mbaya maeneo ya MANYONI na kwa maneno yake mwenyewe ameniandikia akisema "huwezi amini kama nilitoka salama! Mungu alikuwa upande wetu!" Kwa taswira za gari (kama zionekanavyo hapo juu), ni vigumu kuamini kuwa Kakangu huyu hakuwa na majeraha na alipata huduma ya kwanza tuu.
Ni kwa haya niliyoandika hapa leo na mengine mengi yaendeleayo maishani mwetu, ninaporejesha SIFA NA SHUKRANI kwa MUNGU kwani amejidhihirisha kuwa MLINZI NA KIONGOZI WETU.
Ndivyo tunavyomalizia wiki yetu kwa kukumbushana aimbayo Luciano kuwa MSAADA WETU NI KATIKA BWANA ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI.
Msikilize
JUMAPILI NJEMA
Nimechelewa kidogo Jumapili njema nawe na pole kwa yote.Na ka mdogo pia Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa. Mungu awe nawe daima.
ReplyDeletechangamotoyetu.blogspot.com is very informative. The article is very professionally written. I enjoy reading changamotoyetu.blogspot.com every day.
ReplyDeletepayday advance loan
pay day loans