Picha toka kwa Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog
Umuhimu wa Blogs unaanza kuonekana na kuthaminika, lakini huwezi kuzungumzia blogu zetu za kiswahili bila kumtaja Future Hall Of Famer katika hili Kaka Muhidin Issa Michuzi.
Huyu amekuwa chachu ya wengi kujifunza na kuanzisha blogs zao na alikuwa mtu wa kwanza kunihimiza ama kunishawishi kuanzisha blogu baada ya kuwa namtumia posts kadhaa. Amekuwa pia akinielekeza meengi kuhusiana na Kamera na Picha na kwa kupitia taswira mbalimbali katika blogu zake, nimeweza kujifunza mengi kuhusu "fani" hiyo.
Kila mtu anaweza kuwa na yake ya kusema kuhusu yeye, lakini kwangu amekuwa "mwalimu wa vitendo" katika suala la upigaji picha.
Na leo anapoongeza umri kwa kukamilisha siku nyingine maishani, NAUNGANA NA WOTE WAMTAKIAO MEMA KUMUOMBEA KILA LILILO JEMA KATIKA YALE ATENDAYO.
Happy Birthdate Brother Muhidin
Kwa kuwa unasherehekea siku hii, ina maana uko duniani, na kama uko duniani basi tambua kuwa uko kwenye UWANJA WA FUJO. Kwa wewe mkongwe utakumbuka meengi yasemwayo.
BLESSINGS
Happy Birthday Brother Michuzi!
ReplyDeleteHongera sana kwa siku hii maalum.
ReplyDelete