Wednesday, August 12, 2009

Happy Birthdate Lolly

Hi Lolly. Ni salamu za upendo kukutakia kila lililo jema katika kusherehekea ama kukumbuka siku yako ya kuzaliwa. Nakuombea mafanikio kwenye mipango uliyonayo na naamini juhudi zako njema zazidi kufanikiwa. Shukrani saana kwa ukarimu ulionionesha nilipokutembelea hapo Moro na naomba salamu zangu uzifikishe kwa Subira pia.
Amani kwako na BARAKA TELE ZIKUANDAME.
Ni siku nyingine katika mapambano ya MAISHA, na hakuna kukata tamaa. Just keep on moving
HAPPY BIRTHDATE LOLLY

3 comments:

  1. Who is Lolly? Muwe mnatuambia basi. Ndiyo kifaa chako Mzee wa Changa??? Let us know...

    ReplyDelete
  2. Heshima kwako Anon. Lolly ni rafiki yangu saana. Si kifaa kama udhaniavyo bali ni kati ya watu ninaojivunia kufahamiana nao. Na kwa yeyote nifahamianaye naye nikikumbuka siku yake ya kuzaliwa huwa nasherehekea naye. Nilijifunza umuhimu wa siku hizi siku moja baada ya niliyedhani ningemuonesha umuhimu wake kwangu aliposhindwa kufikia siku niliyoamini ningeweza kufanya hivyo. Akawa ameondoka. Kwa sasa, kila nipatapo nafasi ya kuonesha kuthamini mchango wa mtu huwa nafanya hivyo. Haijalishi ni nani kwangu. As long as amekuwa mwema kwangu, nahitaji kuwa mwema na kumthamini. Ukiangalia katika "label" ya Jungu kuu (http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Jungu%20kuu) na pia ile ya Greetings (http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Greetings) utaona hilo.
    Asante kwa swali na naamini nimeondoa utata
    Blessings

    ReplyDelete
  3. Acha kuzuga mzee. Wewe mwenyewe mtu wa Rege. Huyu Lolly naye kavaa tisheti ya Reggae. Coincidence??? Please!

    ReplyDelete