Wednesday, September 16, 2009

Ni Bambataa ya Malkia Sophy

Dadangu mwenyewe Malkia wa Bambataa Sophy binti Kessy
"Trup" nzima ya wana-Night Express (L-R) Dj Bulah (nice dreadlocks Brother), Dj Too Short, Malkia wa Bambataa Sophy, Antonio Nugaz na Maestro wa Michezo Extra.
Baaada ya Mwaka mmoja wa kuendesha blog inayohusu masuala mbalimbali ya wanamuziki na muziki wa kiAfrica, nimefanikiwa kujifunza mambo mengi sana licha ya ugumu wa kazi. Ni kwa hili ninamshukuru Mungu kwa kunipa moyo wa kukabiliana na watu na mambo mbalimbali.
Leo hii narejea kuitambulisha kwa mara nyingine tena blog yangu ya Bambataa, kwa wale wasioifahamu na wale ambao wanaoifahamu naomba sana tuendelee kushirikiana na kuendelea kuutanga Muziki wa Kiafrika ndani na nje ya mipaka yetu.
Kama unapenda kujua lolote kuhusu muziki au una lolote kuhusu muziki wa Africa unataka kunishirikisha ili tujalidi na wengine nao wafaidi basi nifikishie nami nitayafanyia kazi. Unaweza kuwasiliana nami kwa anwani pepe ambayo ni sophia80tz@yahoo.com lakini pia waweza kutembelea http://www.africabambataa.blogspot.com/ kwa habari na burudani zaidi.
Kutana nami Malkia wako nikiuenzi muziki wetu wa kiAfrica kupitia Clouds Fm "the peoples station" kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kila Jumatatu mpaka Ijumaa
Asanteni na karibuni sana .
Asante saana Dada Sophy kwa kuendelea kurindimisha burudani ya kiAfrika. Najua tutafika kwani tunasonga kiaina. Blogu hii yakushukuru kwa ushirikiano na twakutakia kila lililo jema katika kila jema utendalo.
Blessings

No comments:

Post a Comment