Toleo la jana nimezungumzia kuhusu Tanzania yangu ilivyo katika pilika za kuionesha jamii sehemu ndoho ya mafanikio ikisema imeendeleza nchi ilhali wanaohitaji maendeleo kuiendeleza wanapuuzwa. Na sasa tunapoelekea uchaguzi ujao najua tumeanza kusikia meengi toka kwa waomba kura wakija na mbinu mbalimbali kutudanganya kuwa wanatujali. Wanarejea tena na tena kutueleza mipango ya kututoa katika lindi la taabu na umaskini ambao walipaswa kutuwezesha kidogo tu ili tujikwamue wenyewe. Hawfanyi hivyo kwa kuwa UMASKINI WA WENGI NDIO KULA YAO. Ndipo wanapopata la kusema na ndipo wanapowapumbaza watu kwa sukari, kanga na fulana.
Lakini kwanini tunawaacha wakisema wanatujali ilhali tunajua fika kuwa SI KWELI? Mbona kila nikitazama maisha ya vijijini yanasikitisha kuliko maelezo? Watu wanaendelea kunyanyasika katika kutafuta haki zao. Shule na makazi ya wafanyakazi wa serikali (ambazo zilijengwa na mkoloni) hazikarabatiwi hivyo kutufanya kuamini kuwa MKOLONI ALITUJALI ZAIDI YA WATAWALA WETU WA SASA. Majengo mapya ya kuvutia yanajengwa bila mpangilio wa maana kiasi cha kutilia shaka kama ukifika wakati wa ukarabati wa miundombinu ya majitaka hatutahitaji kutindua zaidi na kusababisha nyufa. Rushwa na Ufisadi viko kwenye kiwango cha juu mpaka walio juu hawavioni. Ni kama sehemu ya maisha. Na yote haya yanafanywa na WATANZANIA ambao wameamua kujichumia mali na jasho la waTanzania wenzake. Ni nani asiye na utu kati ya mkoloni ambaye hakuwa na uhusiano nasi na huyu mTanzania mwenzetu anayetufilisi zaidi ya tuliyemuita mkoloni?
AIBU!!!!
Bob Marley katika wimbo wake SURVIVAL aliwaeleza kwa uwazi watu hawa ambao sasa wanaanza kufanya mikutano na matamasha na makongamano na hata "maongezi" na wananchi kuwa "unawezaje kukaa hapo na kuniambia unajali wakati kila nikiangalia pembeni naona watu wakiumia kila siku?"
Lakini anamalizia kwa kuwaambia kuwa licha ya kuwa na watu tofauti, wenye kitu na wasio nacho, wenye aibu na wasio nazo, watenda mema na maovu, bado wanaokandamizwa isivyo halali watayapita haya na kuishi. Lakini pia anawakumbusha wanaokandamizwa kuwa "wakati umefika"
Najua MACHUNGU YA MAISHA YA waTanzania wengi na naamini licha ya kutokuwa na kitu, bado tunaweza ku-survive kwani "muda wa kuwaondoa wasiotenda wanenayo unawadia"
Msikilize Bob Marley katika Survival. Pitia mara kadhaa na tafakari maneno mekundu ukihusiaha na maisha ya waTanzania.(Ow, ow-ow-ow-ow!
Ow, ow-ow-ow-ow!)
Yeah, yeah, yeah!
How can you be sitting there
Telling me that you care -
That you care?
When every time I look around,
The people suffer in the suffering
In everyway, in everywhere.
Say: na-na-na-na-na (na-na, na-na!):
We're the survivors, yes: the Black survivors!
I tell you what: some people got everything;
Some people got nothing;
Some people got hopes and dreams;
Some people got ways and means.
Na-na-na-na-na (na-na, na-na!):
We're the survivors, yes: the Black survivors!
Yes, we're the survivors, like Daniel out of the lions' den
(Black survivors) Survivors, survivors!
So I Idren, I sistren,
A-which way will we choose?
We better hurry; oh, hurry; oh, hurry; wo, now!
'Cause we got no time to lose.
Some people got facts and claims;
Some people got pride and shame;
Some people got the plots and schemes;
Some people got no aim it seems!
Na-na-na-na-na, na-na, na!
We're the survivors, yes: the Black survivors!
Tell you what: we're the survivors, yeah! - the Black survivors, yeah!
We're the survivors, like Shadrach, Meshach and Abednego
(Black survivors),
Thrown in the fire, but-a never get burn.
So I Idren, I-sistren,
The preaching and talkin' is done;
We've gotta live up, wo now, wo now! -
'Cause the Father's time has come.
Some people put the best outside;
Some people keep the best inside;
Some people can't stand up strong;
Some people won't wait for long.
(Na-na-na-na-na!) Na-na-na, na-na-na na!
We're the survivors
In this age of technological inhumanity (Black survival),
Scientific atrocity (survivors),
Atomic misphilosophy (Black survival),
Nuclear misenergy (survivors):
It's a world that forces lifelong insecurity (Black survival).
Together now:
(Na-na-na-na-na!) Na na-na na na! (Na na-na na na!)
We're the survivors, yeah!
We're the survivors!
Yes, the Black survivors!
We're the survivors:
A good man is never honoured (survivors)
In his own yountry (Black survival).
Nothing change, nothing strange (survivors).
Nothing change, nothing strange (Black survivors).
We got to survive, y'all! (survivors) - /fadeout/
[*Sleeve notes:
But to live as one equal in the eyes
Of the Almighty.]
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Kaka nakubaliana na wewe kwa hili.
ReplyDeleteNi changamoto ambayo wanasiasa wetu wantakiwa kuitafakari.
Ukweli ni kwamba falsafa ya BOB iko hai na itaendlea kuwa hai vizazi na vizazi....Blessings
maweeeeeee
ReplyDeletebob marley.....great jamaican
ReplyDeleteHili ni darasa kwa wanasiasa wetu....
ReplyDeleteMimi nadhani wanasiasa wanatambua na kuelewa fika kile ambacho Bob amekieleza, tatizo hawaioni thamani,utu na wala hawana huruma kwa binadamu wenzao.
ReplyDeleteBOB Marley namchukulia kama mhanga wa matokeo ya uongozi mbovu barani Afrika na kwingineko. Ameweza kufungua mdomo kama mwanaharakati mkombozi, basi na sisi kama wahanga wa uongozi mbovu twahamasishwa kutokukaa kimya na kutoridhika na hali tulonayo.
Ni kweli hili ni darasa la wanasiasa. IJUMAA NJEMA NAWE PIA NA FAMILIA YAKO.
ReplyDelete♪ Taaaaanzania Tanzaniaaaaaa, nakupenda kwa moyoooooo woteeeeee ♪
ReplyDelete...wait...wote au nusu or just none?...I don't know...anyway first time since I started "following" you (blog) kumuweka Mzee mwenyewe BOB! :)
kaka sikiliza kutoka nyahbingi worriors.
ReplyDeletehttp://nyahbingiworriors.blogspot.com/
Robert Nesta Marley...ahsante kaka kwa Survival.
ReplyDelete