Monday, September 7, 2009

Tumsaidie ndugu yetu Emmanuel Urio

Picha kwa hisani ya Kaka Michuzi
Picha kwa hisani ya Dada Flora
Kaka Issa Michuzi na Dada Flora wameweka ombi la msaada kwa Kaka Emmanuel Urio. Nami naungana nao kuomba kila mwenye uwezo wa kumsaidia kujitoa kwa hali na mali katika kiwango chochote kumuwezesha ndugu yetu kutimiza lengo lake. Akiwezeshwa anaweza kuwa mtu muhimu maishani mwetu, kuwa ushuhuda kwa wengine wanaokata tamaa na pia anaweza hata kutoa ajira kwa wengine.
Ndugu Emmanuel Urio alizaliwa jijini Mwanza akiwa na upungufu wa mikono na miguu na licha ya ugumu wa mazingira yake, anapenda saana kusoma na kuimba na mambo mengine mengi ambayo anaamini akiwezeshwa atafanikiwa. Kwa mujibu wa Blog ya Dada Flora, "Emah anafanya mambo mengi saa japokuwa hana miguu wala mikono, ana uwezo wa kusoma na kuandika vizuri, anaweza kuimba, ana uwezo wakutumia gitaa, anatunga shanga. Kwa kifupi Emah anafanya mambo ambayo baadhi yetu ambao tumekamilika hatuwezi kuyafanya."
Kwa pamoja tumsaidie ndugu yetu ambaye anapatikana kirahisi zaidi kwa kutumia simu namba +255 757 839 674
Tumeshuhudia jinsi Kijana Nick alivyo SAUTI NA MFANO wa mafanikio ya wale walio na tofauti nasi. Mtazame hapa chini kijana huyu ambaye alizaliwa bila mikono wala miguu lakini anacheza pool, golf na hata kuogelea. Ni sauti kwa mamilioni ulimwenguni

Katika kipengele kipya cha MWANANCHI MIMI, tutakuwa tukileta habari za wale wanaoisaidia jamii na pia wanaohitaji msaada kutoka kwa jamii.
Sisi ni sehemu kubwa ya kuwezeshana kufanikisha haya.

No comments:

Post a Comment