Wednesday, October 7, 2009

Happy Birthdate Mr President

Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya M Kikwete anakumbuka siku yake ya kuzaliwa. Rais Kikwete alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika kijiji cha Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. Luteni Kanali (Mstaafu) huyu alianza kung'aa katika ulimwengu wa siasa mwaka 1982 alipochaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ana mwaka 1997 akawa mjumbe wa Kamati Kuu. Mwaka 1994 akaweka rekodi ya Waziri wa Fedha mwenye umri mdogo zaidi (miaka 44) nafasi aliyoitumikia mpaka mwaka 1995 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya nje. Nafasi hiyo aliishikilia mpaka alipotwaa madaraka ya Urais wa nchi mwaka 2005
Ni jambo la kheri kuifikia siku hii na twapenda kumpongeza saana kwa kuifikia. Na kama kiongozi wa nchi yenye matatizo mengi, tunamuomba aitumie siku hii kutafakari mwaka alioumaliza na ulio mbele yake kwa manufaa ya wananchi waliompa dhamana ya kuwaongoza

Heri ya siku ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais.

1 comment:

  1. HERI YA SIKU YA KUZALIWA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MSRISHO KIKWETE.

    ReplyDelete