Monday, October 5, 2009

My Brothers, My Proud, My Silent HEROES

Hawa ndio "wakubwa wetu wa mwisho kuzaliwa". Kaka wadogo ambao wamezidi kuwa FAHARI kwangu. Kaka zangu hawa wananifariji kwa namna wajitahidivyo shuleni na mienendo yao ya maisha niifahamuyo. Ni faraja kuwa na watu ambao wanaweza kupanga nawe kitu kisha wakatimiza kwa manufaa ya familia nzima.

Na kama kuna wakati niliojivunia zaidi maisha ya ndugu zangu hawa, ni wakati huu walipokuwa likizo. Kila mmoja kwa wakati wake amedhihirisha upevu wa mawazo na ufikirivu na kuwa wabunifu katika kuonesha njia ya mafanikio yao kielimu.
Na sasa mnaporejea chuoni kwa mwaka wa pili, napenda mfahamu kuwa NAJIVUNIA SAAANA KUWA NA KAKA KAMA NINYI. Mmekuwa faraja yangu kwa mwenendo wa maisha yenu.

Najua ninyi si maarufu, ninyi si wenye kupamba taarifa na vyombo mbalimbali vya habari, ninyi si wenye kutambulika sehemu nyingi kama mashujaa, na pengine mwaweza msijue kuwa ni mashujaa. Lakini nataka kuwaambia kuwa NINYI NI ZAIDI YA KAKA ZANGU, NI ZAIDI YA MARAFIKI WA KUDUMU.
NINYI, NI MASHUJAA KWANGU

5 comments:

  1. Ni fahari sana kwa vijana hawa na wanatakiwa kujisifu kwani ndugu,jamaa na marafiki kutambua uwepo wao kwa kuridhika na wayafanyayo ni jambo jema sana na ni baraka kwao.


    Kuna vijana wengi wanakutana na maneno mabaya kutoka kwa ndugu,jamaa na jamii nzima ambayo si baraka kwao kabisa.Unakuta kijana anaambiwa maneno kama "ni bora usingezaliwa kwani huna msaada wowote" n.k,mpaka mtu kuambiwa hivi ina maana uwepo wake hautambuliki, ambapo si jambo jema kabisa.

    kwa hiyo vijana hawa wana kila sababu ya kujivunia na juhudi zao.Nawapa hongera saaana,wasichoke, wazidi kukaza buti.

    ReplyDelete
  2. Una haki ya kujivunia na kujivuna kuwa na ndugu/kaka kama hao. Hongera sana. Na usichoke kujivuna na kama hujawaambia ana kwa ana basi waambie sasa nadhani watafurahi zaidi.

    ReplyDelete
  3. Nyote mlipata malezi mema na mimi napenda niwapongeze wazazi wenu kwa kazi nzuri ajabu waliyofanya. Sote tunajivunia na jamii inafaidika sana. Bila shaka wewe kaka yao ndiyo taa hasa inayong'ara, taa ambayo daima haizimiki na iko tayari kuwaonyesha njia ya kurudi nyumbani pale wanapopotoka na kujaribu kupapasa kilichomo gizani. Watakuwa watu wa ajabu sana kama watashindwa kuiona taa hii na kung'ang'ania gizani. Nawatakia mema na Mungu aendelee kuwabariki daima!

    ReplyDelete
  4. Aaaaaaaw what a sweet love!!! Some brothers even SUE each other!!! can you imagine!!...nway I always wished to have a big brother...ok unnecessary story lol...so nice!!!

    ReplyDelete
  5. Ndugu, nimependezwa sana na ujumbe wako kuhusu ndugu zako! Kweli umeonyesha upendo wa dhati kwao.
    Mwenyezi Mungu awazishie na kuwabariki mpate mafanikio makubwa zaidi na kuzidisha upendo huo.

    ReplyDelete