Monday, January 25, 2010

ADIMIKO

Image from Metal Blades Logos
Kutokana na kupanga na kufuatilia masuala fulani ya mustakabali wa maisha, nategemea kuadimika kwa muda hapa. Haimaanishi kuwa sitakuwa naweka mabandiko, na si kwamba sitakuwepo kwa muda mrefu. Nitakuwa nikishughulikia mambo mengi na hivyo naweza kutokuwa na wakati wa kutosha kutazama mambo kwa "jicho la ndani" kuniwezesha kuyabandika hapa.
Najua ntapata nafasi ya kupitia "sebule" za wapendwa na pale niwezapo kuacha maoni yangu kwani hiyo ni SEHEMU YA RATIBA YA KILA SIKU
Kwa wakati huu wa u-adimiko langu, endelea kuwa salama, mwenye furaha na amani ndani na mazingirani mwako

UPENDO KWAKO

7 comments:

  1. Ahsante kwa taarifa. Hivi ndivyo inavyotakia KUTOA TAARIFA:-) Kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Upendo kwako pia Mkuu! Tuko pamoja!

    ReplyDelete
  3. Asante kwa taarifa.Inaeleweka kabisa kwamba kuna wakati mtu inabidi ukimbie kidogo kutoka bloguni ili kuweka sawa mambo mengine.Kila la kheri

    ReplyDelete
  4. Naamini kwamba unaadimika sasa ili uje upatikane huko mbele. Kwa hiyo yote ni sawa. Tutakusubiri!

    ReplyDelete