Nikiangaza maisha yangu, najivunia wakubwa wangu wawili hapo juu walioambatana na Mama. Ndio Dada zangu walionitangulia. Na leo, Dada Mkubwa-Mdogo Ajuna ndiye akumbkaye siku ya kuzaliwa. Huyu ndiye "aliyeniachia titi" na pengine ndiye niliyeishi naye kwa muda mrefu zaidi ya ndugu wengine. Ndiye niliyekwaruzana na kuelewana naye zaidi na ndiye aliyeonekana kuwa karibu zaidi pia.
Dadangu huyu alikuwa mfano-hai wa maisha kwa namna alivyopambana na pilika za maisha baada ya shule na alifungua njia ya kujaribu kwangu.
Katika siku yako muhimu leo, NAPENDA KUKUTAKIA KILA LA KHERI, BARAKA TELE NA MAKUZI MEMA YA "WAJOMBA"
Wajua TWAKUPENDA NA TWAKUOMBEA na TUNAJIVUNIA UNAVYOENDELEA KUWA MFANO KWA WENGI
Baraka kwako na kwa familia nzima.
HAPPY BRITHDATE DADA AJUNA
Hongera Ajuna! Ubarikiwe sana!
ReplyDeleteHongera dada Ajuna, uwe na siku njema.
ReplyDeleteMmefanana na Ajuna.
Stay blessed.
Hongera sana dada Ajuna, nakutakia maisha marefu na mafanikio mema katika maisha yako. Ni kweli mmefanana huwezi kubisha kuwa sio ndugu. Ubarikiwe sana
ReplyDeleteHongera dada ajuna, hongera Mzee wa Changamoto kwa kuwa na dada wa mfano!
ReplyDeleteMungu na akuongezee miaka mingiiiiiiii, HAPPY BIRTHDATE Dada.
ReplyDeleteYaani nobody will ever "argue" that it is your sister! Yaani mlivyofanana wote...do you have a picture mliopiga wote pamoja? Should be a great one...anyway Happy Birthday dada Ajuna. I hope your brother sends you these wishes we all write here...(mmh)
ReplyDeleteHappy birthday dada
ReplyDelete