Thursday, January 7, 2010

Utakumbukwa kwa "deshi" ya maisha yako

Picha toka http://www.iawwai.com
Ninaposema "deshi" namaanisha uwazi ambao wengi hawajui wataujaza na nini kati ya kuzaliwa na kufa.

Maisha yana hatua tatu muhimu na mbili kati ya hizo (KUZALIWA na KUFA) hazina mjadala, na moja ambayo ndiyo tusiyoijua, ndiyo muhimu kwetu. Ndio hiyo niitayo "deshi". Na kwa kuwa kila mtu anazipitia mbili nilizozitaja, basi hakuna anayezijali wala kumkumbuka mtu kwazo.

Ina maana maisha yetu yamebaki kwenye hiyo hatua iliyo kati ambayo ndiyo tunayoihangaikia.

Kaka Kamala amekuwa akisema saana kuhusu kuhangaikia yasiyotufaa. Leo hii kila aitwaye shujaa ama fisadi ama mshkiliza rekodi, ama mtakatifu ama mkatili ama mwenye cheo chochote ulimwenguni anakumbukwa kwa kile alichofanya kwa muda wake wa "deshi" ambao ni wa katikati ya kuzaliwa na kufa.

Basi tuchuje vema maisha yetu na kuangalia na kutambua kuwa kwa kila utendalo sasa ndilo lenye kuweka historia yako mbeleni.

Amani kwenu

5 comments: