Darasa linakukumbusha kuwa...…
Watu watatu ni mimi na wewe.
Watu kumi ni mimi na wewekwa sababu kuna watu tumesimama nyuma yao. Lakini pia, ni watu wetu wa karibu wanaosimama nyuma yetu.
Mtu wa kwanza ni yule ambaye anapokuwa na kitu cha kutimiza hasubiri watu wakimbie pamoja naye. Huchakarika kadiri ya uwezo wake bila kulalamika wala kuvunjika moyo kwa kuwa hana msaada.
Mtu wa pili ni yule ambaye anapokuwa na jambo lake ni lazima apate msaada ndiyo alifanye kwa kasi. Mtu wa hivi bila kusukumwa haendi wala hawajibiki ipasavyo. Ni ngumu kutimiza mambo yake ipasavyo bila kuegemea wengine.
Mtu wa mwisho ni yule ambaye ni mlalamishi. Hutaka jambo lake watu wote waache shughuli zao kwa ajili yake. Hata kwenye ambayo ni wajibu wake kwanza, hulazimisha wengine kuwajibika kwa ajili yake, ama sivyo hununa au huzira na hata kuvunja ukairbu na mtu kwa sababu tu hakusaidiwa jambo ambalo ni wajibu wake.
Wale watu 10 nyuma ya watu. kila mmoja ajitafakari anavyowatendea watu wake wa karibu pale wanapotegemea sapoti yake.
Tujiulizetunaangukia kwenye kundi gani?
Darasa linakutakia tafakuri njema.
No comments:
Post a Comment