Thursday, July 30, 2009

Mkutano wa kuanzisha jumuia ya watanzania katika Jimbo la Gauteng

Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng (Johannesburg na Pretoria) wanatarajia kufanya mkutano wa kuanzisha jumuia yao tarehe 22 mwezi wa Agosti 2009 jijini Johannesburg.
Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu jumuia hii pamoja na kuchagua viongozi wa kudumu.

Watanzania wanaoishi kwenye miji ya Johannesburg na Pretoria ambao wangependa kuwa wanachama na pia kushiriki kwenye uchaguzi wa uongozi wa jumuia wanakaribishwa kuwasiliana na wajumbe wafuatao kwa maelezo zaidi:
Brian Mshana b_mshana@yahoo.com
Laurean Rugambwa bwanakunu@gmail.com
Faustine Ndugulile drfaustinen@aol.com

Shukrani
KAMATI YA MAANDALIZI

Binafsi na lwa miaba ya wana-Changamoto yetu wote tunawatakia kila la kheri katika kuanzisha Jumuiya hiyo tukiamini kuwa utakuwa mwanzo wa UMOJA NA MSHIKAMANO katika kukabiliana na matatizo mengi yawakubayo ndugu zetu.
Blessings

1 comment:

  1. Nashukuru Mkuu kwa msaada wako wa kutufikishia huu ujumbe.
    Faustine

    ReplyDelete