Thursday, July 30, 2009

Luciano na Tanzania

Jana nimemsoma Da'Yasinta na uTANZANIA wake anaojivunia (msome hapa) . Nikafurahia saana. Katika maoni kama kawaida nikamsoma Kaka Kamala aliyeleta CHANGAMOTO nyingine akiuliza "tanzania nini na mtanzania ni nani?" na hilo likanifanya nirejeshe mawazo kwa wale ambao wanajua wanatokea Afrika lakini hawana hakika na watokeako. Hivi wana pa kupenda ama wataipenda Afrika kwa ujumla wake? Lakini kuna mengi ndani ya Afrika ya kumfanya mtu asiyelazimika kuipenda aipende? Vita, Ubadhirifu, Ufisadi ama? Tarehe 7 Aprili nilikumbuka saana nyumbani kisha nikaandika kuhusu siku nitakayorejea nyumbani (Bofya hapa kuisoma post hiyo). Nilijiuliza kuhusu nyumbani kisha "nikasindikiza" toleo hilo na wimbo wake Luciano uitwao When Will I Be Home (Bofya hapa kuusikiliza) ambao pia (kwa mshangao wangu nilipousikia mara ya kwanza) unaitaja TANZANIA kama nchi anayojiuliza kama ndiko iliko asili yake ama la.
Nakumbuka mwanzo wa miaka ya 2000, Kaka-Rafiki Gotta Irie aliniandikia mail kunieleza kuwa alikuwa na mpango wa kumualika Luciano kwenda kufanya onesho nyumbani. Nilifurahi kusikia hivyo kwa kuwa mimi ni msikilizaji na mpenzi wa muziki wa Luciano, na aliporejea toka huko (katika onesho ambalo niliambiwa kuwa lilifana licha ya mahudhurio kuingiliana na matukio ya kidini), lakini hata aliporejea toka huko, Luciano ameendelea kuizungumzia Tanzani ana anasema katika kukaa nchini na kutembea alijifunza mengi na kisha akaandika wimbo wa Remember When ambao kama aelezavyo kwenye mahojiano haya yajayo, alipata wazo hili akiwa Tanzania. Nikajiuliza MAPENZI aliyonayo kwa nchi ambayo inazidi kumong'onywa na wabadhirifu na namna anavyojitahidi kuielimisha jamii juu ya uzuri wa Tanzania nikaguswa saaaana. Luciano ni msanii nimpendaye (wacha nikiri) na haipiti siku bila kumsikia.
Msikilize hapa katika mahojiano (ANZA DAKIKA YA 2 NA SEKUNDE 31) umsikie hisia zake kuhusu Tanzania na Africa kwa ujumla


Blessings

2 comments: