Tuesday, April 7, 2009

When will i be home again???

"Sometimes I wonder when will I be home again?" Haya ni maneno ya Luciano ambaye katika wimbo wake aliouita hivyohivyo (when will I be home) ameimba mengi kuanzia walivyopoteza asili ya kwao kwa wazazi wao kupelekwa utumwani, kisha anazungumzia asakavyo asili yake na anajiuliza kama asili yake yaweza kuwa TANZANIA na kisha akazungumzia vitu vya kujivunia avionavyo na kuvipenda barani Afrika kama kuchomoza kwa jua kulivyona machweo yake, michezo ya watoto mitaani, kuoga mtoni (kwa wale walio karibu na mito) mpaka utayari wake wa kufika huko AFRIKA na kuendeleza kuimba kuwa "sometime i wonder when will i be home again?"Maswali ni mengi na wengi wanaweza kujiuliza mengi, lakini nami nitoe changamoto hapa kuwa ni kipi ukumbukacho zaidi unapofikiria safari ya nyumbani? Hapa namaanisha kule iliko asili yetu. Na leo nilipokuwa naendeleza kazi nilikuwa nasikiliza huo wimbo mara kadhaa. Ni kwa kuwa nilikumbuka sana nyumbani, kisha nikarejea kwenye kompyuta yangu na kuanza kujikumbusha taswira za nyumbani. Nakubali kuwa tumebarikiwa.
Mbali na ndugu na jamaa, UHALISIA NA USAILIA WA NYUMBANI ni kitu kingine ninachokikumbuka saaaana. Naishia kujiuliza tena WHEN WILL I BE HOME AGAIN?????

HAPA KWENYE MLO NDIO KABISAAAA. Sijui lini tena???
Msikilize Luciano katika wimbo huu When will i be home

11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Wow! hapo umeniacha hoi kabisa. ni kumbukumbu nzuri sana na huo msosi mmh nimetam,ani kwelikweli mpaka mate yamevuja

Fadhy Mtanga said...

Moyoni unatamani,
Kuwepo kwenu nyumbani,
Pengine hujui lini,
Wajiuliza!

Ndugu zako wa nyumbani,
Bado wanakutamani,
Wakwone japo machoni,
Wajiuliza!

Hujasahau nyumbani,
Uliko ughaibuni,
Basi utarudi lini?
Twajiuliza!

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta unatamani msosi wa home? Si juzi juzi ulikula hadi ukachoka ukakwea pipa huyoooo ukasepa.!
Kaka mkubwa mambo vp?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nakuona sijui uko viunga vya kashura sijui wapi hapa. kwa hakika umenikubusha sana home lakini niko njiani kueleke bukoba next wee.

nikumbukapo home huwa nakumbukamarafiki zangu wa shule za msingi, disco toto, nk. nakumbuka wazee wa vijijini na busara zao za ukubwani, nakumbuka ukwasi wa baadhi yao, kuoga mtoni na kulewa na washikaji.

nakumbuka msosi wa mviringo kama huo. mkubwa kiasi kwamba huwezi amani kuwa mtaumaliza lakini unaisha tu labda hamjaukalia.

bahati mbaya wiki ijayo narudi home nikiwa siwazi kula tena ndnizi nyama wala samaki, nikiwa siwezi kunywa tena kakonyagi wala lubisi. njiuliza itakuwaje nymbani na watu wa kwetu watanipokeaje na uamzi wangu mpya.

ikibidi nitasingizia ugonjwa daktari kaknikataza

napenda home

Simon Kitururu said...

Tukumbuke kuwa nyumbani kwa wengine nyumbani kwao ni china.


Na maswala ya nyumbani ni bora yana undugu na sisi ni bora kuliko wao!

Kumbuka nyumbani BOMBA ingawa kwa wengine nyumbani ni majukumu kuliko furaha!:-(
Na majukumu yanafurahisha kama unaweza.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nakumbuka vizuri sana mara yangu ya kwanza kukalia hizo nyasi. Nilikuwa form two pale Kahororo Sec. Wikiendi tulikuwa tunakwenda kule ziwani na kuna mawe kama hayo. Asante kwa kuniletea kumbukumbu za ujanani. Nyumbani daima ni nyumbani ati!

Koero Mkundi said...
This comment has been removed by the author.
Koero Mkundi said...

Ama kweli nyumbani ni nyumbani...

sophiasclub said...

Wow!Ebitoke!asante sana kwa kunikumbusha nyumbani.

Unknown said...

Kaka huo msosi umenikumbusha mbaaaaali kweli yaani ni chijijini kabisa kasoro hapo ni iyo sinia tu, si kule msosi wamiminwa moja kwa moja kwenye mbabi hizo au majini ya migomga na ako kanyasi ndo usiseme tena. ahhha we acha tu.

Mary Damian said...

Kaka Kamala umesharudi? chakula kimenikumbusha mbali kweli, nilipokua Ishozi Kijiji cha Katano.....Tweyambe Sec. Niliandaliwa chakula cha namna hii nilipokaribishwa na jamaa zangu Asante kwa picha, Nimepakumbuka jamani!