IMETOSHA

IMETOSHA

KUMRADHI

Kutokana na kubanwa na masomo, mabandiko hayatakuwa kila siku kama awali.
NAWAPENDAThursday, January 7, 2016

TANGAZO LA MSIBA LONDON: MAREHEMU ABEID SAID MPATE

A'alaykum warahmatuLlahi wabarakatuh, 
Ina Llillah waina ilaih rajiun.
Ndugu zetu wa kiislam, tumepata faradh katika mji wetu wa coventry, Jana (06/01/2016)  ndugu yetu Abeid said (MPATE) ametangulia mbele ya haki. Ni wajib  wetu waislam kumstiri muislam  Mwenzetu.  
Tunaomba  michango yenu ili tuweze  kumstiri  ndugu yetu kwa chochote utakacho  jaaliwa inshAllah.
Jina : Mohamed Saleh 
Account number: 19891363
Sort :  30-92-33
Lloyd.  
: 07939294471 (wanawake)
:07801750508 (wanaume )
Maziko tutawajulisha baada ya kupatikana  mwili wa marehemu, InshAllah. 
Tafadhali ukipata ujumbe huu mtumie na mwenzio
Shukran  wa JazakumLlah khayran.

Saturday, January 2, 2016

Sherehe ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Geofrey Kinyashi

Geofrey Kinyashi na mkewe Maria wakipata picha ya kumbukumbu baada ya Maria kushirikiana na Eddah Elegant Catering kumfanyia mumewe sherehe ya miaka 50 ya kuzaliwa ambayo mpaka wakati wa tukio, ilikua siri kwa "mzaliwa".
Ilifanyika usiku wa Ijumaa January 1, 2016 The Signature Blue Beltsville, Maryland nchini Marekani.
Geofrey Kinyashi akiwa na mkewe meza kuu.
Watoto Francis na William (kulia) wakiwa na marafiki zao kwenye meza kuu na baba na mama yao kwenye sherehe ya kuzaliwa ya miaka 50 ya mzazi wao.
Marafiki waliosoma na Geofrey Kinyashi tangia Sunday school, shule ya msingi na sekondari kutoka kushoto ni Duncan Silayo, Mariam Kalala Nyang'oro na William Kibaja wakiongea jinsi walivyomfahamu Birthday Boy enzi hizo. Duncan na William wanatokea jimbo la Massachusetts na Mariam anatokea jimbo la North Carolina.
Francis Kinyashi akimtakia baba yake kheri ya siku ya kuzaliwa huku mdogo wake William akifurahia anchoongea na baadae nae alimtakia baba yake kheri ya siku ya kuzaliwa.
Baba na mama Kinyashi wakifarahia jambo, kushoto Vero mdogo wa Maria aliyekuja toka jimbo la Georgia kwenye sherehe ya miaka 50 ya siku ya kuzaliwa ya Geofrey Kinyashi siku ya Ijumaa January 1, 2016 ilipofanyikia The Signature Blue Beltsville, Maryland nchini Marekani.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.

Thursday, December 24, 2015

KILIMANJARO STUDIO INAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU YA MAULID, CHRISTMAS NA MWAKA MPYA


Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland inatoa salamu za kheri ya sikukuu ya Maulid, Christmas na mwaka mpya kwa wadau wote wa Vijimambo Blog, Kwanza Production na Nesi Wangu Blog. Sikukuu iwe ya upendo na amani na muweze kusherehekea kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.

Kama hukutimiza malengo mwaka 2015 usijali mwaka 2016 ni mwaka wa kujipanga upya na Kilimanjaro studio inakutakia kila la kheri kwa mwaka mpya 2016 uwe mwaka wa mafanikio makubwa kwako na kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema palipokua na giza 2015 mwaka mpya apatie mwanga, palipokua na chuki 2015 mwaka mpya apaweke amani yote na tunaimani utafikia malengo na sisi kujipanga kwa mambo mapya kwa kuongeza vipindi kwenye Radio na kukuhabarisha kwenye Blogs zetu.

SOTE KWA PAMOJA TUNASEMA KHERI YA SIKUKUU YA MAULID, CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MAULID DAR

 Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


AKINA MAMA NA VIJANA NI NGUZO KUBWA YA KULETA MABADILIKO KATIKA VIJIJI.


 Bwana Bony Lukas akieleza jinsi anavyofanya uraghbishi hasa katika kuwasaidia vijana kujua haki zao na kujitambua.

Na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
Ni suala ambalo lipo wazi kuhusu tofauti za kimaisha baina ya wakazi wa mijini na vijijini, ila changamoto nyingi zaidi zinaonekana kuwakabili zaidi wale wanaoishi vijijini. Huko wananchi wanakosa huduma ambazo kimsingi ni haki zao na hivyo kutokuwa na usawa baina yao na wale wa mijini.
Picha kubwa inayojionesha vijijini kwa upande wa wanawake ni hasi kwa kiasi Fulani ukilinganisha na ile ya wanaume. Usawa wa kijinsia na kielimu baina yao na wanaume ni mkubwa sana, kesi za unyanyasaji kwao ni nyingi zaidi.  Pamoja na jihudi nyingi za kuwawezesha wanawake bado hawajapata nafasi ya kutoshwa kuweza kusikilizwa. Wanaume wameendelea kuwa watoa maamuzi na wanufaikaji wa kimfumo. 
 Mmoja wa waraghbishi akiwa anaonesha ripoti ya wanafunzi watoro katika shule ya msingi ya Nyandekwa .

Monday, December 14, 2015

TAMASHA LA MITIKISIKO 2015 LAACHA HISTORIA MKOANI IRINGA


Msaani maarufu wa bongofleva, Linex akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
Msaani maarufu wa Hip hop,Darasa akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
Umati wa wananchi wa Iringa waliojitokeza  katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Msaani maarufu wa Hip hop, Roma Mkatoliki akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Wazanzibar wa Sweden Waandaman

  
  
Taswira za Maandamano ya waZanzibar Diasporan waTanzania pamoja na wapenda amani na Demokrasia kote ulimwenguni. leo Jumatatu Dec 14, wameandamana huko Stockholm Sweden kwenye Parlament (Riksdag) kutaka Bunge na Serikali ya nchi hiyo kuibana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili iheshimu maamuzi ya wananchi wa Zanzibar waliyoyafanya kupitia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

Saturday, December 12, 2015

Reggae Time ya PRIDE FM Dec 12 2015.......Uhuru Afrika

Desemba 9, ilikuwa ni siku ya uhuru wa Tanganyika.
Desemba 12, ni uhuru wa Kenya
Katika kipindi hiki, tumeangaza machache juu ya UHURU wa nchi za Afrika na UHURU WA AFRIKA kwa ujumla.
Je! Tuko huru? Tunauenzi uhuru wetu? Na pengine nini kifuate baada ya kutoka kwa wakoloni?
KARIBU tujadili haya kupitia muziki wa Reggae.
Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio.
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658

Tuesday, December 8, 2015

Mahojiano na DC Paul Makonda katika kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 7 2015


Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.
Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.
Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu
KARIBU

Tuesday, December 1, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 30 2015 (Full Show)


Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali yatano ya Tanzania
Yanayofanyika yanaleta taswira gani kwa Tanzania? Na Je!
Yataendelea ama?