Showing posts with label Politics. Show all posts
Showing posts with label Politics. Show all posts

Wednesday, October 9, 2013

Dr Slaa afanya mahojiano na radio mbili za kitaifa nchini Marekani


Dr Slaa akifurahia jambo ndani ya studio za WIBC 93.1FM Indinnapolis
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa ambaye yupo kwenye ziara ya "VISION TANZANIA" nchini Marekani,. leo amefanya mahojiano na vituo viwili vya radio hapa nchini kueleza mambo mbalimbali kuihusu Tanzania.
Saa tatu asubuhi kwa saa za Marekani ya Mashariki, Dr. Slaa alikuwa katika studio za 93.1 WIBC Indiannapolis kwenye Garrison Show
Bofya hapa chini kusikiliza mahojiano hayo
Mchana wa leo (saa saba mchana kwa Marekani ya Mashariki), Dr Slaa alifanya mahojiano kwa nia ya simu na WPFW Radio ya Washington, D.C.
Bofya hapa chini kuyasikiliza

Tuesday, October 1, 2013

[AUDIO]. Maswali na majibu katika mkutano wa Mhe. Mwigulu Nchemba DMV

Kwa hisani ya Vijimambo Blog
 Wadau hii ni sehemu ya maswali na majibu kwenye mkutano wa CCM DMV uliofanyika jana Jumapili Sept 29, 2013 kesho tutajitahidi kuwaletea sehemu nyingine na hotuba ya Mhe. Mwigulu Nchemba
Chini ni maswali na majibu kutoka mkutano wa CCM DMV na waliojibu maswali ni Mhe. Mwigulu Nchmba akisaidiwa na msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete Mhe. Rajab Luhwavi

Sunday, September 29, 2013

Mhe. Mwigulu Nchemba aunguruma DMV

Habari na picha kwa hisani ya VIJIMAMBO BLOG
Mhe. Mwigulu Nchemba akijianda kuingia kwenye ukumbi wa Mirage  uliopo Hyattsville akiambatana na Msaidizi wa Rais Mhe. Rajab Luhwavi huku wakisindikizwa na wenyeji wao Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo( kushoto), Katibu wa CCM New York Bwn. Shabani Mseba(kulia). Katikati mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa zamani wa CCM DMV Bi Loveness Mamuya.
Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea na Watanzania DMV kwenye ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryland pamoja na mambo aliyoongea ni kuwaomba Watanzania ughaibuni kupima wanayoongea wapinzani huku akisikitishwa na kauli za upinzani wanaodai barabara si maendeleo huku akitoa mfano wa barabara za Marekani ni kielelezo cha maendeleo ukilinganisha na barabara Tanzania.
 Juu na chini ni viongozi wa dini wakiomba dua kabla ya mkutano
 Kikundi cha kwaya cha CCM DMV kikitumbuiza kwa nyimbo

Mhe. Mwigulu Nchemba kuongea na waTanzania wa DMV leo...USIKOSE

KUMBUKA
1: Mkutano utaanza saa kumi kamili jioni (4:00pm)
2: Anwani ni
The Mirage Hall.  
1401 University Blvd. E,  
Hyattsville, MD, 20873
Nyote mnakaribishwa 

Sunday, September 15, 2013

Mkutano wa Dr Willibrod Slaa na waTanzania DC


Viongozi na wanachama wa CHADEMA DMV wanapenda kuwakaribisha Watanzania wote Kuhudhuria mkutano na Katibu Mkuu wa CHADEMA (Taifa) Dr. Willibrod Slaa utakaofanyika Jumapili ya Septemba 22, 2013 kuanza saa saba mchana mpaka saa kumi na mbili jioni (1:00pm - 6:00 PM)
Anwani ni:  
1401 Unirvesty Blvd. (Mirage Hall)
Langley Park. Md 20783 
Karibuni tuje tujadiliane kuhusu maendeleo ya nchi yetu.
Maelezo zaidi wasiliana na
Liberatus Mwang'ombe  (240) 423-3331  
Baby Mgaza  (202) 200-5031 
Hussein Kauzela  (614) 653 - 1137 
Wote mnakaribishwa



Sunday, June 30, 2013

Young African Leaders Initiative Town Hall

At the University of Johannesburg - Soweto, President Obama discusses youth empowerment and leadership with young African leaders in a town hall meeting June 29, 2013.

Sunday, March 3, 2013

Kenya...MTACHAGUA VIONGOZI WENU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

Leo (March 4, 2013) wananchi wa Kenya wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya KATIBA MPYA.
WaKenya wamesikiliza kampeni za muda mrefu toka kwa wagombea wajazao nafasi mbalimbali.
Swali kwa ndugu zangu waKenya ni kuwa, mmeshajiuliza mtamchagua nani kuwa rais katika uchaguzi ujao?
Hapa sisemi kuchagua kwa jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Na je! Ndugu zangu wa Kenya mmeshajiuliza kuwa mnataka kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi?
Ama mliwasubiri waje na UONGO WAO ndio muanze kujipanga jinsi ya kukubaliana na uongo wao?
Ama mpaka waje na pesa ndio muangalie namna zinavyoweza kuwafaa?
Natumai hamkusubiri waje kuwaambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwenu.
Ama hamkusubiri waje na takwimu njema zisizoeleza mlivyo na kisha kuwaaminisha kuwa mnawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yenu.
Je!! Umeshawasiliana ama kujadiliana na yeyote masuala haya?
Nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
MTACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

Kila la kheri Kaka Denzil Musumba


Wednesday, November 7, 2012

Hotuba ya Rais Obama baada ya kutetea kiti chake

"I want to thank every American who participated in this election, whether you voted for the very first time or waited in line for a very long time. 
By the way, we have to fix that. Whether you pounded the pavement or picked up the phone, whether you held an Obama sign or a Romney sign, you made your voice heard and you made a difference. 
I just spoke with Gov. Romney and I congratulated him and Paul Ryan on a hard-fought campaign. 
We may have battled fiercely, but it's only because we love this country deeply and we care so strongly about its future. 
From George to Lenore to their son Mitt, the Romney family has chosen to give back to America through public service and that is the legacy that we honor and applaud tonight. 
In the weeks ahead, I also look forward to sitting down with Gov. Romney to talk about where we can work together to move this country forward."
 
Kabla yake, mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Republican Mitt Romney alitoa hotuba yake kukubali kushindwa.
"I ran for office because I'm concerned for America," and added, "Like so many of you, Paul and I have left everything on the field. We have given our all to this campaign." 

Monday, November 5, 2012

TRUTH WILL REVEAL

"You see their faces but you never know their thoughts,.. you see their actions but you never know their reactins, Time and Time-alone will prove the story and every eye will see, TRUTH WILL REVEAL"
Nimesema saana juu ya Nasio. Mmoja kati ya "darubini" kali za maisha ya wengi kupitia muziki halisi wa Reggae. Na japo nilimzungumzia wiki iliyopita, basi hapa ninaye tena katika kibao hiki TRUTH WILL REVEAL kutoka albamu yake ya Revolution.
Umati mkubwa nyakati za kampeni. Ukitaka kujua wawazalo juu ya mgombea, angalia matokeo. Kama unabisha muulize Mrema (1995)
Kwa hapa Marekani tumeona namna ambavyo uchaguzi wa mwaka huu umegeuka kuwa funzo kwa wengi.
Kuwaonesha kuwa MABADILIKO yajapo hayazuiwi kwa vitisho wala mtazamo wa mtu. Watu walipiga kura za maoni kwa namna ya kuweka uwiano na wengine hata kutopiga kabisa ilhali wakijua walichonacho mioyoni mwao.
Hilo liliwapa watu mtazamo kuwa uchaguzi ungekuwa mgumu kiasi na wengine kubashiri mambo kugeuka siku ya mwisho kulingana na "enthusiasm" waliyokuwa wakiiona kwenye kampeni zao. Walilosahau ni hilo lililoimbwa na Nasio ambalo pia nimeliandika hapo juu.
Wanadanganywa na sura bila kujua mawazo, na kuangalia matendo bila kujua madhara yake na wakati unapofika kila mtu akafanya kilichokuwa mioyoni na UKWELI UTADHIHIRIKA kiasi hata cha kuwashangaza walioshindwa.
NASIO ALIKUWA NA BADO YUKO SAHIHI.
Tusubiri usiku wa leo kujua, ni umati gani ulioshangilia na kisha kwenda kupiga kura?
 

Saturday, September 15, 2012

Hotuba kamili ya Mhe. Freeman Mbowe kwa waTanzania wa Washington DC



Freeman Mbowe akihutubia waTanzania
Sehemu ya umati uliohudhuria ukifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa chama Mhe. Freeman Mbowe 













Photo Credits: Abou Shatry wa Swahilivilla Blog
Hotuba kamili ya Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe alipokutana na waTanzania waishio Washington DC na vitongoji vyake jioni ya Sept 1, 2012.
Msikilize

Saturday, August 25, 2012

Uzinduzi wa tawi la CCM DMV leo

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tawi la CCM hapa DMV Mhe. Abdulrahman Kinana amewasili jana na kulakiwa na na viongozi wa matawi ya CCM DMV na New York.
Kushoto ni Katibu wa Tawi la CCM DMV Bw. Jacob Kinyemi, Katibu wa Tawi la New York Bwn. Shabani Mseba na Mwenyekiti wa Tawi CCM DMV Bi Loveness Mamuya.

Mhe Abdulrahman Kinana, ambaye ni kanali mstafu wa jeshi, ni mmoja wa wanasiasa wakongwe na mahiri nchini Tanzania. Ni mjumbe wa taifa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki na Meneja wa Kampeni wa Mhe Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.
 Ufunguzi wa Tawi la CCM unafanyika leo Jumamosi Aug 25, 2012 katika ukumbi wa Martin Luther King Jr Hwy Lanham, Jijini Maryland likiwa ni tukio maalum na la kipekee kwa wanachama wa CCM chini ya kauli mbiu ya CHANA GWANDA NA GAMBA, VAA UZALENDO

Monday, July 23, 2012

Uzinduzi wa tawi la CCM Washington DC

Tarehe 25 mwezi ujao, Chama Cha Mapinduzi kitazindua tawi lake dogo kwa wakazi wa Washington DC na vitongoji vyake.
Ili kuwekana sawa katika harakati hizi, mwenzangu Abou Shatry wa Swahilivilla Blog aliwasaka viongozi wa muda wa CCM hapa DMV na kufanya nao mahojiano. Wafuatilie hapa chini

Tuesday, November 15, 2011

Mahojiano. Waziri Mkuu Pinda na Urban Pulse

Katika kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, Urban Pulse Creative wanakuletea mtiririko wa Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kutuelimisha na kutupatia changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu.
Hizi ni sehemu ya kwanza, ya pili na ya tatu

Wednesday, November 4, 2009

Mwaka mmoja baada ya HISTORIA

Tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita ulimwengu ulitambua kuwa HISTORIA ilikuwa ikiandikwa nchini Marekani. Ambacho hakikujulikana ni kuwa NI HISTORIA GANI ambayo ingeandikwa.
Je!! Ni ya kwa na Rais mwenye umri mkubwa zaidi aingiapo madaakani?
Je!! Ni ya kuwa na Rasi wa kwanza mwenye asili ya Africa?
Ama ni ya kuwa na Rais toka chama kidogo cha siasa? (kumbuka walikuwepo wagombea 5 wa Urais nchini Marekani)
Na ndio maana siku ya uchaguzi (Nov 4, 2008) nikaandika kuwa Kushinda si kazi, Akishinda sasa!!!!!(Bofya hapa kuirejea) na kama ilivyotakiwa akapatikana MSHINDI ambaye ni rais wa sasa Mhe Barack Obama. Ilikuwa ni historia ambayo wengi hawakujua ilikoanzia na kwa waliokosa, basi mwaweza kusoma nililoandika nikisema A NEW DAY: Toka Frederick Douglas mpaka Barack Obama (Bofya hapa)Tazama hotuba ya kukubali Urais aliyoitoa Grant Park, Chicago. November 4th, 2008 ama maandishi yake HAPA
Labda safari ilikuwa ndefu ndio maana watu waliamua "kupumzika" mara baada ya uchaguzi, lakini kwa uongozi huu uliopo madarakani, nahisi kuna wanaojilaumu kwa madaraka waliyonayo. Uchumi unazidi kuporomoka (japo wao si waanzilishi wa hali hii), vita vya Irak na Afghanistan navyo vinazidi kuwa tatizo na wameshaanza kuviita Vita Vya Obama wakimaanisha kuwa maamuzi yake yatatathmini uwezo wake kuongoza nchi, wameanza uangalia ahadi alizokuwa akisema na utekelezaji wake, na kwa hakika ulimwengu umekuwa kwenye hali mbovu kiuchumi kuliko wengi tulio hai tunavyoweza kusimulia.
Mwaka wa kwanza umepita na haujawa na pumziko.
Ni vipi hali ya tathmini ya mwaka wa u-Rais wa Obama itaathiri imani za waMarekani? Ni kweli wengi wanajua ni zipi lawama zake na zipi si stahili yake? Ni kweli watu watatambua kuwa uchumi na maisha ya sasa ni tofauti ukilinganisha na wengi tujuavyo???
Na ni kweli kuwa ataweza kuwaeleza waMarekani ni kwanini hajawa TUMAINI kama ambavyo walitegemea?
Mwaka mmoja katika HISTORIA ya uongozi unamalizika leo.
NINI KITAFUATA???

Kwa upande wa Tanzania kumbuka mwaka jana tuliwaza nini ningejibiwa kama NINGEPATA NAFASI YA KUONGEA NA RAIS WANGU SIKU YA UHURU (Bofya hapa)

Wednesday, February 11, 2009

Gari moja = matrekta 20. Uwiano mzuri, malengo mazuri, utekelezaji ........


Serikali imesema katika mwaka ujao wa fedha wanategemea kuweka mkazo zaidi katika kununua magari ambayo yanaisaidia zaidi jamii na kuongeza ufanisi katika kilimo na si yale ambayo wamekuwa wakinunua kila mwaka kwa ajili ya watendaji wake.
Katika mahojiano yake kuhusu mwaka mmoja aliokaa ofisini yaliyorushwa na kipindi cha MCHANA HUU cha redio ya taifa TBC ( yanapatikana Dullonet Feb 12, 2009), Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda amekiri kuwa "katika mifumo ya bajeti, tunazo pesa zinazoweza kupunguza matatizo ya kweli ya watanzania, lakini sehemu kubwa ya fedha hizo haziendi huko na badala yake zinakwenda katika maeneo ambayokwa sehemu kubwa kabisa yanatuhusu sisi watendaji na viongozi". Mhe Pinda amesema alipopitia orodha ya maombi iliyopelekwa hazina amegundua kuwa magari ya viongozi ndiyo yaliyochukua sehemu kubwa ya kipaumbele na kuyapa kisogo magari ya wagonjwa, matrekta na magari ya zimamoto hivyo akaamua kuwa hizo bilioni 50 zilizotengwa kwa ajili ya magari ya viongozi na ambayo huhitajika kununuliwa kila mwaka zitumike kwa malengo mengine japo wa miaka miwili ijayo kwa manufaa ya wakulima na wafugaji.
Amesema amegundua kuwa awapo ziarani, kila gari moja linakaribia thamani ya matrekta madogo 20 na kuamua kuwa ni bora kwa mkulima kupata matrekta kuliko ofisi yake kuendelea kugawa "mashangingi" kwa viongozi. Amesema ni mahesabu tu ambayo anataraji kukaa na viongozi wenzake serikalini na ana imani kuwa "kwa hakika tukiamua jambo hili, linawezekana".
Waziri mkuu amesema "tumedhamiria kuwa bajeti inayokuja, kama kutakuwa na ununuzi wowote wa magari, basi yatakuwa yale yanayomlenga zaidi mtanzania wa kawaida. Magari ya wagonjwa, magari ya zimamoto, magari ya kuzoa taka ngumu na taka za kawaida, vitu abavyo naona ni kero ya kila siku hapa Tanzania."

Ni kweli kuwa kuna baadhi ya miji na manispaa ambazo hazina magari ya zimamoto wala vizoa taka na vikusanya taka ngumu, na kuna uhitaji wa zana za kilimo nchini kote, hivyo kuliona hili ni hatua kubwa sana na nampongeza saana Waziri Mkuu kwa kuliona hili na nampongeza kwa "utafiti" huo ulioleta namba ya uwiano wa magari. Pia nafurahi na nasubiri kusoma bajeti ijayo kuona ni yapi kati ya yaliyosemwa hasa hili la "kuwanyima" viongozi "mashangingi" mapya. Maana mara zote viongozi wamesema na kutoa kauli nzuri, zenye mvuto na matumaini na kisha utekelezaji hauonekani.
Changamto yetu sote ni kuweka kumbukumbu za haya na ukifika wakati basi TUHOJI UTEKELEZAJI WA AHADI HIZI KWA UPENDO NA HESHIMA.

Tuesday, January 20, 2009

A NEW DAY: Toka Frederick Douglas mpaka Barack Obama

Safari ya rais wa anayechukua madaraka siku ya leo nchini Marekani yaonekana kama ilianza miaka miwili iliyopita alipoanza kampeni zake, lakini ukweli wa harakati za kumfanya mtu mweusi kupata nafasi aliyoipata Barak Obama zilianza miaka mingi iliyopita. Mtandao wa MSN umeweza kuweka majina ya wale wanaoaminika "kumsafishia njia" Mhe Barack mpaka kupata nafasi ambayo leo anaiapia rasmi. Na hapa chini ni watu hao kumi kuanzia Frederick Douglas mpaka Mch Jesse Jackson. Habari na picha zote zapatikana hapa

1: Frederick Douglass: Many of you may immediately associate Douglass with his groundbreaking book, My Bondage and My Freedom, but did you know that Douglass was our nation’s first African-American vice-presidential candidate? He ran alongside Equal Rights Party candidate Victoria Woodhull, the first woman to run for president in the United States. They didn’t win, but their political aspirations inspired many.

2: Hiram Revels: Barack Obama owes a lot to Hiram Revels. Known as a great orator, Revels was the first African-American appointed to the United States Senate when Mississippi’s state legislature voted 81 to 15 to send him to Washington in 1870.

3: Joseph Rainey: Unlike Revel, who was appointed to the Senate, South Carolinian Rainey was the African-American elected to the United States Congress and was the African-American to sit in the House of Representatives, which he did for nine years. Not too shabby, eh?

4: Booker T. Washington: With the founding of the Tuskegee Institute, Washington provided a great education for countless African-Americans. He eventually became known as the most powerful African-American in the nation and, for his efforts, became the first African American to receive an invitation to dinner at the White House.

5: Martin Luther King Jr: Do we really need to explain MLK’s inclusion? This man, one of the most respected civil-rights leaders in history — if not the most respected — helped break down the nation’s color barrier and set the course for a more inclusive American dream. Without him, well, it’s likely Obama never would have made it to the primary. Or, for that matter, the Illinois state Senate!

6: Thurgood Marshall: Thurgood Marshall rose to fame for winning case after case before the Supreme Court, including 1954’s seminal Brown vs. Board of Education, which desegregated schools. A little more than a decade later, Marshall would become the high court’s first African-American jurist.

7: Robert C. Weaver: Weaver left an indelible mark on Washington when, in 1966, he became the first African-American to hold a Cabinet-level position. Weaver served as Lyndon Johnson’s Secretary for Housing and Urban Development, which was created that very year.

8: Douglas Wilder: The first African American to be elected as governor of a state (Virginia), serving from 1990-1994.

9: Colin Powell: Powell was the first African-American to serve as Secretary of State, but he was the first — and so far only — black man to serve on the Joint Chiefs of Staff.

10: Jesse Jackson: Jesse Jackson and Barack Obama may have had their political differences in the past, but it can certainly be argued that Jackson’s 1984 campaign for the Democratic presidential nomination — and, also, his 1988 efforts — helped lay the groundwork for Obama’s historic election.

Hakika ni siku mpya kwa wenye tumaini jipya na mtazamo mpya wa jamii ya waMarekani. Msikilize Luciano alipoimba A NEW DAY .

Thursday, November 20, 2008

Hotuba: Mwl Julius Kambarage Nyerere Pt 2


Wiki iliyopita tuliisikiliza sehemu ya kwanza ya hotuba bofya hapa kuirejea aliyoitoa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hoteli ya Kilimanjaro (Kempinski) mnamo siku ya Jumanne mwezi wa Machi tarehe ya 14 ya mwaka 1995.
Hii Bofya hapa ni sehemu ya pili kati ya sehemu tatu za hotuba hiyo.

Subi
www.nukta77.com & nukta77.blogspot.com

Asante sana Da Subi

Thursday, November 6, 2008

"Not over until it's done"


"..once you got life there's a chance you'll be able to overcome. Where there's will, there's a way, IT'S NOT OVER UNTIL IT'S DONE, if you believe you will achieve, everything can just turn around" Hayo ni maneno yaliyoimbwa naye mkongwe wa Lover Rock Beres Hammond katika wimbo wake Not Over Until It's Done.
Maneno hasa ndio ambayo hunipa moyo pale ninapokuwa na ndoto ama mipango na kisha kuhisi kuwa ninakumbana na vikwazo mbalimbali katika kuyatekeleza. Na ndipo nikumbukapo kuwa It's not over until it's done. Na ukimsikiliza zaidi kwenye wimbo huo anaendelea kusema kuwa "while you are wondering what suit to wear, the family's worry is what a meal to share" na hiyo hunipa mwanga kuwa pamoja na matatizo tuliyonayo, lakini wengine wana zaidi. Kwa hiyo badala ya kulalamika basi tuendelea kukamilisha mikakati ya kufanikisha ndoto zetu. Na kwa juhudi, maarifa, utii na imani kutakuwa na njia sahihi ya kutufikisha kule tutakako kwenda. Lakini juu ya yote kuwe na Baraka zake akupaye uhai.
Nimesema haya kutokana na ushindi wa Rais Mteule wa Marekani Mhe Barack Obama.
Hajatoka kwenye familia ya kitajiri, hakuwa katika familia yenye jina kubwa (kama kina Martin Luther ama Malcom X), hakulelewa malezi ya wazazi wote kumfanya awe na mtu wa kuiga majukumu ya kimalezi ya mwanaume, hakutoka katika jimbo lenye uwezeshwaji mkubwa na wala si mtu aliye ndani ya siasa kuu za nchi kwa muda mrefu. Lakini kwa miezi 21 aliyopiga kampeni, ameonesha nia halisi ya kushinda uchaguzi huu na mara zote katika harakati zake amekuwa akikumbana na "kigingi" cha kuwa yeye ni mweusi na isingekuwa rahisi kwa raia wabaguzi wa nchi hii kumpa kura. Alichofanya ni kuamini katika nia yake ya kuwa kiongozi wa nchi na yanaweza kusemwa yasemwayo lakini "it's not over until it's done". Na watu wakasema kuwa historia haiwezi kubadilika kwa mtu ambaye hajawa na uzoefu wa kuongoza hata jimbo lake akapewa dhamana ya kuongoza taifa hili lenye ukubwa wa matatizo zaidi ya wema, lakini msemo unaonekana kuwa uleule kuwa "it's not over until it's done". Wamemhusisha na Magaidi, kutumia jina lake la pili la Hussein kama njia ya kuwatisha watu, kuzungumza juu ya uwezo wake mdogo katika masuala ya kimataifa lakini alionekana kujiamini katika kile atendacho akiamini kuwa mwisho wake ni Nov 4 na kwa kuwa ilikuwa haijafika, kwake ni yaleyale "it's not over until it's done".
Obama amekuwa na mafanikio makubwa saana katika "kuiunganisha jamii" tangu akiwa Community Orgernizer huko Chicago. Ni uwezo huohuo alioutumia katika kujipanga na kueleza vema mtazamo, msimamo, imani, changamoto na matarajio yake na namna anavyojipanga kukabiliana na hayo yote katika kipindi cha utawala akipewa dhamana. Alionesha kujipanga vema katika ku-organize kampeni na kuvunja rekodi ya kukusanya kiasi kikubwa saana cha pesa kwa ajili ya kampeni kitu kilichowafanya wapinzani wake waanze kutaka kufanya uchunguzi kama watu hao hutoa pesa zao wenyewe na kwa hiari. Lakini hakusita kuonesha kuwa ana lengo na kwa kuwa muda ulikuwa haujafika, "it's not over until it's done"
Ni Jumanne ya wiki hii, tuliposhuhudia kile kilichowaliza wengi. Kuona ambacho miaka mitano iliyopita hakikuwa hata mawazoni mwa watu. Kile ambacho wengi hatukutegemea kutokea katika kizazi chetu. Tukaona kwa ushindi wa wingi wa kura na kura za kimajimbo tena kwa historia ya wapiga kura wengi tangu mwaka 1908, Barak Obama akachaguliwa kuwa Rais wa 44 wa Marekani, Rais wa kwanza mwenye asil ya Afrika na kwa hilo akadhihirisha kuwa "anything can just turn around"
CHANGAMOTO YETU ni kujifunza kutoka katika njia aliyoionesha badala ya kutegemea kuleta mabadiliko Barani na nchini mwetu. Kuamini katika kuvunja mipaka iwekwayo na "maadui" na kuamini katika kile sahihi kilichopo ndani ya mioyo yetu. Namaanisha kuwa wengi hawaoni mafisadi wakiweza kusafishwa nchini Tanzania, hawaoni kama rushwa yaweza kuondolewa nchini Tanzania, hawaoni viongozi wazembe wakiwajibishwa nchini Tanzania, hawaoni mtu akigusa na kuinua maisha ya wahitaji wengi wa vijijini nchini Tanzania na wala hawaoni mageuzi ya kweli kuelekea matumaini kwa waTanzania wengi, lakini nionalo mimi ni kuwa "IT'S NOT OVER UNTIL IT'S DONE"

BLESSINGS