Showing posts with label Kilimanjaro Studio. Show all posts
Showing posts with label Kilimanjaro Studio. Show all posts

Monday, May 7, 2018

Kipindi cha JUKWAA LANGU. Mei 7, 2018

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo ndani ya Kilimanjaro Studios, wageni wetu studioni ni kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoitumikia jamii ya wahitaji nchini Tanzania.
Katika saa la kwanza tutakuwa na uongozi wa SHINA INC ambao tangu mwaka 2002 wamekuwa wakisaidia jamii zenye uhitaji nchini Tanzania. Wana mengi ya kutushirikisha

Kwenye saa la pili tutakuwa na wakuu wa Help for Underserved Communities Inc. (HUC-USA) ambao wanajishughulisha kutoa textbooks mashuleni, VETA Scholarships na kusaidia matibabu ya macho nchini Tanzania.

Lakini tutaanza na mrejesho wa maadhimisho ya TANZANIA DAY 2018 yaliyofanyika Dallas Texas.

Ni kipindi cha JUKWAA LANGU, leo Jumatatu (Mei 7, 2018) na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Facebook live (Mubelwa Bandio na Kwanza Production) ama Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama piga simu 202-683-4570
*******************************
PRODUCER: Mubelwa Bandio

Wednesday, February 7, 2018

JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 2 TANO LADIES

Katika sehemu ya pili ya kipindi cha Jukwaa Langu Jumatatu hii tumetembelewa na TANO LADIES.
"Wadada" walioamua kuwa sehemu ya msukumo wa maendeleo ya wanawake na mabinti zetu.
Wamezungumzia (pamoja na mambo mengine) nafasi na mchango wao kama Diaspora kwa Tanzania, na pia wanavyopanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake duniani.
Unaweza ona sehemu ya video yao hapa
https://vimeo.com/253461804

JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi na waalikwa wengine kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

Kipindi cha JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 1 SARATANI

Katika sehemu ya kwanza ya kipindi cha Jukwaa Langu, tumezungumzia kuhusu siku ya SARATANI DUNIANI iliyoadhimishwa  Feb 4.
· Takwimu za maradhi haya zinaonyesha kwamba kifo 1 kati ya 6 hutokana na maradhi haya.
· Wajua, namna yanavyoathiri nchi zinazoendelea? Ni 20% tu zenye takwimu sahihi kuwezesha kupambana na maradhi haya.
Unajua ni tabia gani maishani zinaweza kuondoa 30% ya Saratani?
· Unafahamu harakati zinazofanywa na Diaspora katika kupambana na maradhi haya?
· Tulikuwa na Mwanasayansi na Mtafiti wa aina mojawapo ya Saratani, pamoja na mwanaharakati kujadili haya.
......
JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe na waalikwa wengine studioni kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf

Sunday, March 19, 2017

Mahojiano na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A


Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.
Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.
Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2
Karibu usikilize

Saturday, September 24, 2016

Kipindi cha Reggae Time, Pride Fm... Sept 24 2016

Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658

Kipindi cha Ongea Na Shangazi. Sept 23, 2016.... USAFI

Kipindi cha ONGEA NA SHANGAZI hukujia kila Ijumaa kutoka Kilimanjaro Studio. Aunty Asha Akida anakuwa akijadili mambo mbalimbali kuhusu mahusiano kwa wapendanao, maisha ya familia, malezi ya watoto na mengine mengi, huku ukipata nukuu mbalimbali kuhusu mada husika na muziki murua
Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) na hii ni kila siku ya ijumaa kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093