Showing posts with label Kutoka kwa bloggers. Show all posts
Showing posts with label Kutoka kwa bloggers. Show all posts

Thursday, January 19, 2017

KAMPENI MAALUM YA KUINUA MAADILI KITAIFA JAN - DEC, 2017

Jumamosi Jan 14, kiongozi wa kampeni ya kuinua maadili kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge akishirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington alizindua kampeni hiyo yenye lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa.
Kampeni hiyo imeanza rasmi na itaendelea hadi mwezi Desemba mwaka huu ikijikita zaidi katika kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.

Sunday, June 19, 2016

Maalim Seif ahitimisha ziara yake nchini Marekani

Na Mwandishi wetu Washington 
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad, jana alimaliza ziara yake nchini Marekani iliyochukua muda wa wiki moja.
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad (Picha na http://swahilivilla.blogspot.com/) Maalim Seif alikhitimisha ziara yake hiyo kwa mkutano wa hadhara ambapo alipata nafasi ya kuongea na Watanzania waishio nchini humu.
Katika Mkutano huo, mwanasiasa huyo gwiji nchini Tanzania alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuuelezea ulimwengu kukhusu kile kilichotokea Zanzibar kufuatia uchaguzi wa Oktoba 25 na mwelekeo wa demokrasia nchini Tanzania kwa ujumla.
Aliielezea ziara yake hiyo nchini Marekani kuwa imezaa matrunda. “Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa tumeeleweka na ziara yetu imezaa matunda” alisema Maalim Seif.
Sehemu ya hadhira wakimsikiliza kwa makini Maalim Seif
Kukhusiana na zoezi la uchaguzi wa mwaka jana Visiwani Zanzibar, Maalim Seif alisema kuwa, uchaguzi huo ulihudhuriwa na waangalizi wa Kimataifa na wa ndani kutoka pande zote za Muungano, Bara na Zanzibar, na wachunguzi wote hao walithibitisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. “Waangalizi wote, wote kabisa, walikiri kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki”, alisisitiza kiongozi huyo na kuongeza kuwa “Ulikuwa uchaguzi bora kabisa kuliko chaguzi zote zilizotangulia Zanzibar”
Aliuulezea mchakato wa uchaguzi kuwa ulikwenda vizuri mpaka kufikia tarehe 27 Oktoba ambapo jumla ya Majimbo 34 ya uchaguzi yalikuwa tayari yameshatangazwa, na mengine 9 yakiwa yameshahakikiwa ikiwa bado kutangwazwa tu. Na kwa upande wa udiwani na Uwakilishi, uchaguzi ulikuwa umeshakamilika na washindi kupewa shada zao za ushindi.

Thursday, January 7, 2016

TANGAZO LA MSIBA LONDON: MAREHEMU ABEID SAID MPATE

A'alaykum warahmatuLlahi wabarakatuh, 
Ina Llillah waina ilaih rajiun.
Ndugu zetu wa kiislam, tumepata faradh katika mji wetu wa coventry, Jana (06/01/2016)  ndugu yetu Abeid said (MPATE) ametangulia mbele ya haki. Ni wajib  wetu waislam kumstiri muislam  Mwenzetu.  
Tunaomba  michango yenu ili tuweze  kumstiri  ndugu yetu kwa chochote utakacho  jaaliwa inshAllah.
Jina : Mohamed Saleh 
Account number: 19891363
Sort :  30-92-33
Lloyd.  
: 07939294471 (wanawake)
:07801750508 (wanaume )
Maziko tutawajulisha baada ya kupatikana  mwili wa marehemu, InshAllah. 
Tafadhali ukipata ujumbe huu mtumie na mwenzio
Shukran  wa JazakumLlah khayran.

Thursday, December 24, 2015

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MAULID DAR

 Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


Tuesday, November 3, 2015

SHUJAAZ RADIO SHOW NA DJ TEE KUANZA KURUKA HEWANI KUPITIA EAST AFRICA RADIO.

Unamkumbuka yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake nyumbani kwao? Bila shaka umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila mwezi kiitwacho SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda vya Coca Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote wanaomfuatilia. Nyota imeanza kung’ara upande wake na sasa redio kubwa Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze kusikika hewani na show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.

“Show yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla, bila kusahau burudani kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa katika kufikia malengo yao maishani. Pia, utawasikia vijana mbali mbali wakijadiliana kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO, UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ Tee.

Show hiyo itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa TISA alasiri, inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa kuwa itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe alivyoelezea.

Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwake mwenyewe kwa kujiunga naye kupitia Facebook jina ni DJ Tee (http://on.fb.me/1FUl1hX), Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4)

Wednesday, October 21, 2015

SERIKALI YA TANZANIA YATAKIWA KUDUMISHA AMANI WAKATI WA UCHAGUZI

NA MWANDISHI WETU WASHINGTON 
Serikali ya Tanzania imetakiwa kuhakikisha kuwa amani na usalama vinakuwepo wakati na baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Tanzania tarehe 25 mwezi huu.
Profesa Nicholas Boaz,
Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa Mawasiliano na Sera katika Chuo Kikuu cha Maryland nchini Marekani, Profesa Nicholas Boaz katika mahojiano maalum na Swahilivilla.
Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake, Profesa Boaz ambaye amerejea nchini Marekani hivi karibuni baada ya ziara yake Tanzania, alisema kuwa nchini Tanzania kuna joto kali sana na vuguvugu la mabadiliko."Kuna joto kali sana la uchaguzi. Kwa kweli naona watu wengi wanaitikia wito wa kutaka mabadiliko", alisistiza profesa Boaz.
Alisema kuwa hali duni za wananchi katika nyanja mbalimbali za maisha baada ya miaka mingi ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na miaka kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, ndiyo iliyopelekea mwamko wa vuguvugu la kutaka mabadiliko. 
"Baada ya muda mrefu wa CCM kuwa madarakani, na miaka kumi ya Rais Kikwete, basi watu wamepata mwamko kuwa maisha na maendeleo yao yamekuwa duni.
 Kwa hivyo wanataka wapate mabadiliko ya kiongozi na kimtazamo juu ya namna ya kuweza kuwasaidia watu hasa katika maswala ya kazi, afya, mamno ya shule na mambo mengine mengi".
Aliyataja mambo hayo mengine kuwa ni swala la uhuru wa watu kujieleza na kuuliza juu ya kitu ambacho kinawakera.
Akijibu swali iwapo kweli wananchi wa Tanzania wamepata mwamko wa mabadiliko au wanaimba tu nyimbo za wanasiasa, Bwana Boaz alisema "Huwezi kuingia akilini mwa watu kuwajua nini wanakitaka. 
Lakini ukiona watu wanakusanyika wakasema wanataka mabadiliko, kuna kitu gani cha kuuliza zaidi ya hicho?" alidadisi msomi huyo na kuongea, "huu ni ushahidi kuwa watu wanataka mabadiliko ya kweli"
Aidha alisema kuwa wimbi hilo la mabadiliko linatokana na hali ya watu kukata tamaa na ahadi zinazotolewa na viongozi wa CCM wakati wakitafuta ridhaa ya wananchi kuingia madarakani na badala yake hali za maisha kuendelea kuwa duni.

Tuesday, October 20, 2015

WARIDHISHWA NA HUDUMA ZA KITUO CHA AFYA KIVUNGE, UNGUJA

IMG_20151016_175545
Pichani juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi wetu
BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha afya cha Kivunge.
Kituo hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na majeraha mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.
Alizitaja changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
IMG_9525
“Tunawashukru sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema Haji.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.
Alisema kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za afya kwa ufanisi zaidi.
“ Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”, alifafanua Bw.Rodriguez.
IMG_9533
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.
Naye Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.
Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na endelevu.
IMG_9557
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho huku akiwa ameambatana na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (nyuma ya Alvaro) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu. Kulia ni Daktari wa kujitolea anayehudumia wangonjwa katika kituo hicho Alexander Vogt.
IMG_9564
Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt akimwonyesha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez baadhi ya ripoti za magonjwa yanayowasumbua watoto chini ya umri wa miaka 5 wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho.
IMG_9574
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na Dr. Mohamed Abdallah (kulia) aliyekuwa akitoa huduma kwa mtoto Salma Shamis mwenye siku 10 ambaye anasumbuliwa na masikio wakati Bw. Rodriguez alipofanya ziara fupi ya kukagua kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” visiwani Unguja kilichojengwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
IMG_9591
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye vyumba vya madaktari kama walivyokutwa na kamera yetu.
IMG_20151016_175753 IMG_9612
Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James akizungumza na waandishi wa habari waliombatana kwenye ziara hiyo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_9621
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto Shekha Khamis (3) mkazi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” aliyefika kituoni hapo kupatiwa matibabu.

NDESAMBURO AMUOMBEA KURA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI JAFARY MICHAEL.

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo,akimnadi mgombea Ubunge katika jimbo hilo Jafary Michael (Chadema) katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata ya Ngangamfumuni.
Baadhi ya wananchi wakiwa kando ya barabara wakifuatilia mkutano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema,Jafary Michael akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Moshi mjini,Philemoni Ndesamburo (katikati) akiwa na mgombea udiwani kata ya Ngangamfumuni,Anthony (kulia ) na mgombea udiwani kata ya Longuo Raymond Mboya. (kushoto).
Mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini, Jafary Michael akiomba kura .
Baadhi ya wafuasi na wananchi waliofika katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimumbea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Ngangamfumuni,Anthony.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimuombea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Rau, Peter Kimaro wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,kandaya Kaskazini.

Video: Ewe Mgombea, wekeza katika kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU



Maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza kuenea kwa VVU.
Hata hivyo, ambukizo moja katika kila maambukizo kumi mapya huwapata watoto wanaozaliwa japokuwa asilimia 90 ya maambikizi haya yangeweza kuzuilika. Wasichana pia wamo hatarini zaidi kuambukizwa VVU kuliko wavulana. Kila ambukizo jipya la kijana aliye chini ya miaka ishirini linadhihirisha kushindwa kuwapatia vijana elimu ya afya ya uzazi, taarifa, stadi na huduma zitakazowawezesha kujilinda. Unyanyapaa na ubaguzi vinaendelea kudhoofisha uwezekano wa wanawake kupata huduma.


Fanya kazi pamoja na washiriki wote katika kupanua huduma na matibabu yatakayoangamiza kabisa maambukizi ya VVU ya mama kwa mtoto ifikapo mwaka 2015. Hakikisha kuwa watoto wote wenye VVU na UKIMWI wanapata matibabu wanayoyahitaji.

Toa ahadi ya kuongeza rasilimali katika kuwakinga vijana, hasa wasichana dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kuunga mkono mpango wa kitaifa wa kuzuia VVU.

Saidia katika kuanzisha huduma za afya zinazowalenga vijana na mipango madhubuti ya stadi za maisha ambazo zitawapa taarifa na kuwawezesha, hasa wasichana kupunguza uwezekano wao wa kuambukizwa VVU na UKIMWI.

Thursday, October 1, 2015

Tigo yatoa mchango wa madawati 700 kwa shule za umma mkoani Mbeya

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, (kushoto) akimkabidhi madawati yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Tigo imetoa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya 49 milioni kwa shule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, (kulia) akimkabidhi madawati Ofisa Elimu Shule za Msingi Jiji la Mbeya, Deusdedit Bimbalirwa, baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya Sh49milioni kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro  (kulia) akiwa ameketi kwenye dawati na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, mara baada ya kampuni ya Tigo kumkabidhi  mhe. Kandoro madawati 700 yenye thamani ya Sh49 milioni kwa shule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini .

Septemba 30, 2015 Jijini Mbeya: Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali linalotoa misaada katika jamii lijulikanalo kama Hassan Maajar Trust (HMT) wametoa mchango wa madawati 700 yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 49 kwenye shule za msingi 32  katika wilaya ya Rungwe, Mbozi na wilaya ya Mbeya Mjini.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika moja ya shule jijini Mbeya, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema: “ mchango huu ni sambamba na dhamira ya kampuni ya kuunga mkono mipango ya kijamii kupitia wigo wake wa kushirikisha jamii”.
“Kupitia mchango huu, kampuni ya Tigo inawajibika katika kutengeneza viongozi wa baadaye wakiwamo madaktari, wahandisi na wataalamu wengine wa nchi hii, "alisema Gutierrez.
Alisema, katika miezi ya hivi karibuni kampuni ilitoa mchango kama huo wa madawati katika mikoa ya Iringa na Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya dola za Marekani 50,000 kwa serikali, ahadi ambayo kampuni ya Tigo ilitoa mwaka jana ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za umma nchini.

Makabidhiano yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alisema madawati hayo700 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika wilaya hizo tatu, akitoa wito kwa wadau wengine wenye mapenzi mema kujitolea na kujiunga kwenye jitihada za kukabiliana na sehemu iliyobaki ya uhaba wa madawati mkoani humo.

                   Picha na habari kwa hisani ya http://bongodailyupdates.blogspot.com/



WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI USO KWA USO NA WAPIGA KURA WAO MUFINDI , WAULIZWA MASWALI MAZITO JUU YA AJENDA YA WATOTO


       Ndg Patrick Lalika, akiuliza Swali kuhusu Mazingira hatarishi kwa Watoto katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge

Mwalimu  Nico Mgala, Akiuliza swali kuhusu mrundikano wa wanafunzi madarasani katika .mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge
 
Ndg Castory Boniface Masangula Mgombea Udiwani kata ya Igowole kupitia CCM akijibu Swali  katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge 
Ndg Israel Mpina Msalilwa, mgombea Udiwani kata ya Igowole kwa tiketi ya CHADEMA akijibu swali katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge
 Wazazi wakifuatilia  mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kwenye mdahalo

 Frank Timothy Malata, mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kusini. Kwa tikeki ya Chadema akitoa maelezo.
Mwanafunzi Mangula akiuliza swali juu ya huduma bora ya Umeme
Thabiti Msofe Afisa Ustawi wa Jamii Mufindi, Akichangia mada kuhusu Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Lishe Bora katika  mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge
Zikiwa zimebaki siku 23 kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, hapo jana wakazi wa Jimbo la Mufindi kusini wamewataka wagombea Ubunge na Madiwani watakaopata nafasi ya kuwaongoza katika kipindi kinachofuata  kutafuta suluhisho la ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na adhabu kupita kiasi kutoka kwa walimu na wazazi, Mimba za utotoni na kukatishwa masomo kwa watoto kwa ajili ya ndoa ama ajira.

Hayo yalisemwa katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge Frank Timothy Malata (CHADEMA) pamoja na wagombea udiwani Castory Boniface Masangula (CCM) na Israel Mpina Msalilwa (CCM).

Aidha walisisitiza suala la upatikanaji wa viwanja vya michezo kwa watoto na kudai kuwa michezo ni njia mojawapo ya kumbadili mtoto kimwili na kiakili.

Akijibu hoja kutoka kwa wananchi, Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Frank Timothy Malata ameahidi kupatikana suluhisho la adha hizo na kukomesha ukatili dhidi ya watoto. Mgombea huyo pia ameahidi kuinua michezo kwa kuanza na upatikanaji wa viwanja bora vya michezo mbalimbali zaidi ya mpira wa miguu. 

Kwa upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Igowole kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Castory Boniface Masangula ameahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kamati za ulinzi za watoto na sekta nyingine zinazojihusisha na ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ukatili wowote.

Naye Israel Mpina Msalilwa ambae ni mgombea Udiwani wa kata hiyo kupitia CHADEMA aliahidi kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali kuondoa tatizo la mrundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na kupiga vita ukatili dhidi ya watoto zikiwemo adhabu kupita kiasi zinazotolewa na wazazi, walezi ama walimu.

Katika hatua nyingine, watoto ambao ndio walengwa wakuu wa Midahalo hii walitoa maoni yao kuwa nini kifanyike baada ya viongozi hao kushika nyadhifa wanazogombea ambapo walitaja kuwa wanakerwa na uhaba wa vitabu, vyoo, huduma bora za afya, umeme na usafiri na kupambana na mimba za utotoni hasa hasa kwa wanafunzi.

Wakati huo huo, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mufindi Navoneiwa Mfinanga amewataka wagombea hao kuwa karibu na kamati za watoto ili kuhakikisha wagombea wanatimiza ahadi zao

Midahalo hii ni muendelezo wa midahalo ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto kinachoandaliwa na Kampuni ya TRUE VISION Production chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ikishirikiana na UNICEF yenye lengo la kuibua ajenda ya watoto kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. 

Unaweza kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa tisa mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org nawww.facebook.com/WalindeWatoto

“Tuwape nafasi viongozi wanaojali watoto kwa kutetea haki zao” – Baraza la Watoto

Bi. Samia Suluhu Ahaidi Neema kwa Wakazi wa Musoma Mkutano wa Kampeni...!

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.
 Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.

INTERNATIONAL DAY OF OLDER PERSONS, SUSTAINABLE CITIES FOR ALL AGES

UNFPA's Executive Director, Dr. Babatunde Osotimehin.
UNFPA's Executive Director, Dr. Babatunde Osotimehin.
Population ageing and urbanization are major global issues of the 21st century. While cities are growing, their share of residents aged 60 years and over is also rising. Rapid urbanization is challenging both national and local governments in developing inclusive and integrated cities.
Today, as we observe the International Day of Older Persons, we must ensure that cities respond to the needs of persons of all ages and that older persons are as much a part of urban life as their younger counterparts.
This year’s theme of Sustainability and Age Inclusiveness in the Urban Environment fits in perfectly with the objectives of the recently adopted 2030 Agenda for Sustainable Development: leave no one behind! Together, we must ensure that older persons are fully integrated in cities’ economic, social, political and cultural life.
What can we do to make our cities more inclusive? We can start by ensuring that both younger and older generations are included in the urban planning process and their issues, needs and concerns are equally taken into account.
We need an approach to urban planning that focuses on well-being throughout the life cycle. We should invest in young people today by promoting healthy habits, ensuring education and jobs, and providing access to health services and social security coverage for all workers. This is the best investment to improve the lives of young people, help stem the increasing tide of out-migration, and improve the lives of future generations of older persons.
At the same time, we must provide affordable and accessible health-care services, lifelong learning and retraining opportunities, and flexible employment for older persons to improve their well-being and facilitate their integration into the fabric of communities.
Strengthening human capital by ensuring empowerment, education and employment of all citizens will yield a high return on investment and will help countries reap a demographic dividend that can lift millions out of poverty. Creating hope and opportunity for young people to develop their full potential can drive progress in the years to come and, ultimately, result in a second demographic dividend of healthier, wealthier and more productive older persons.
Today, we call on policymakers and urban planners to work together to ensure an inclusive urban environment for all ages. This means paying particular attention to the important pillars of urban living, such as housing, transportation, basic social services, and health care, to make them age-friendly. It means creating an ageless society, characterized by an urban physical environment that facilitates personal mobility, safety and security. It means creating an urban social environment that encourages respect, social inclusion, and participation. And it means protecting natural resources, preparing for natural disasters, and reducing risk so that current and future generations look forward to a sustainable future.
Today, we call on urban leaders to ensure the protection of the human rights of all urban residents, including the elderly who are more vulnerable, and to enforce zero tolerance of discrimination, neglect, violence and abuse of older persons.
Ensuring sustainability and age inclusiveness in the urban environment means creating a society for all ages where the voices of all generations are heard and where the needs of both young and old are met. It means empowering young and old to fully participate in the economic, social and political life of their communities. It means gathering data on city residents and their needs and working to ensure that they are adequately met. It also means sharing experiences about what makes a city a great place to live in for both young and old.
Age-friendly cities are not just elderly-friendly. They are better for everyone.

UBA’S ODUOZA WINS CEO OF THE YEAR AWARD AT INVESTMENT SUMMIT IN NEW YORK

Mr. Phillips Oduoza, GMD-CEO, UBA Plc
Group Managing Director and CEO, UBA Plc, Mr. Phillips Oduoza.
Group Managing Director and CEO, UBA Plc, Mr. Phillips Oduoza has emerged the 2015 Ai Socially Responsible Investment (SRI) 30 CEO of the year at this year's 8th annual Ai CEO Investment Summit. This is the second time he is winning the award after winning it first in 2013.
He was named the winner from a long shortlist that included Nassef Sawiris, CEO, Orascom Construction Company, Sifiso Dabengwa, CEO, MTN Group, SA, Guillaume Roux, CEO, Lafarge Africa, Segun Agbaje, CEO, GT Bank, Graham Clark, GMD, Dangote Sugar and Ben Kruger/Sim Tshabalala, Co-CEOs, Standard Bank. The event took place in New York at the sidelines of the UN General Assembly.
Africa investor (Ai), is a leading international investment and communications group based in South Africa. Every year it organises the institutional investment summit as a platform for public and private sector leaders in Africa to dialogue with global counterparts on ways to invest and grow businesses in Africa. As an integral part of the summit, Ai also hosts the investment and business leadership awards to reward exceptional business practices, economic achievements and investments across Africa, whilst recognising the institutions and individuals improving the continent’s investment climate.
At the summit and awards ceremony attended by over 250 of Africa’s most prominent and influential business, government and development finance leaders, as well as five African Heads of State, the UBA CEO won the Ai SRI CEO of the Year award in recognition of his exceptional achievements over the last year which according to the summit organisers, is an “inspiration for business and government leaders working to raise Africa’s investment profile”.
The judging panel considered excellent leadership skills, enhanced organisational image, innovation and originality as well as alignment with the millennium development goals (MDGs) in choosing the Socially Responsible Investment (SRI) 30 CEO of the year. Speaking on the award, Oduoza who has twice been recipient(the first time in 2013), said: 'as Africa’s global bank, The United Bank for Africa, UBA, has operations in 19 African countries and 3 global financial centres - New York, London and Paris, serving over 9 million customers. This award validates our efforts over the years in building a solid pan-African banking business that is profitable, sustainable and socially responsible. I dedicate it to all UBA people: customers, staff and other stakeholders in Africa and across the globe".
Other recognitions at the ceremony include: Venture Capital/Private Equity Award won by the Abraaj Group, whilst Institutional Investor of the Year and Investment Promotion Agency of the Year went to Public Investment Corporation of South Africa (PIC) and Centre de Promotion des Investissementsen Côte d'Ivoire (CEPICI) respectively. The Leadership in Sustainable Investment in Africa Award went to the Bill and Melinda Gates Foundation.
Uganda Pres + GM USA
Uganda President Yoweri Museveni with General Manager USA.

Thursday, September 24, 2015

TASWIRA ZA SALA YA EID AL-ADHW-HAA 2015 WAISLAM WASHINGTON DC

Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.( Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.