Showing posts with label Mwananchi Mimi. Show all posts
Showing posts with label Mwananchi Mimi. Show all posts
Tuesday, December 2, 2014
Monday, December 2, 2013
[AUDIO]: Maandalizi ya matembezi ya hisani: NCHI YANGU, WAJIBU WANGU, TAIFA KWANZA
Matukio Chuma, muandaaji wa matembezi ya hisani akizungumzia matembezi hayo yatakayofanyika Januari 11, 2014 yenye kauli mbiu Nchi yangu, wajibu wangu, taifa kwanza.
Katika mahojiano haya Chuma anazungumzia mambo mbalimbali kuhusu matembezi hayo, ikiwemo sababu ya kuyaandaa, sababu za kuyafanya katika njia waliyoamua kuyafanya (Dar-Moro), mambo ya kufanya kabla hujashiriki matembezi haya na mengine mengi.
Unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0784 311-056, 0772 545-562 ama barua pepe ambayo ni kwetutanzania@yahoo.com

Monday, April 8, 2013
CHINA IS MORALLY BANKRUPT!!.... ALL THEY NEED IS OIL AND MINERALS
By Liberatus Mwangombe “Libe”
To my fellow Africans and Tanzanians
who praise and give China credit for building a coalition with African nations. The Chinese government doesn’t care about you
– their intentions are not transparent,
they do not care about human rights,
and corruption is as natural to them
as breathing. Even if no one else will
tell you what China’s true motivation is, I will. They need our natural resources such as oil
and minerals.
I wonder if President, Jakaya Mrisho
kikwete, considers the ultimate impact on Tanzania from forming trade alliances
with China. Through my personal research
I have found historical facts that reveal significant growth in the volume of
trading between Tanzania and China. In
1997 Tanzania’s total export of goods and services to China was Tsh 10 billion. In the same year, China’s export of goods and
services to Tanzania was Tsh 37 billion. In 2005, a mere 8 years later, these two
countries exchanged goods and services worth Tsh 347 billion! Tanzania’s
exports represented Sh 101 billion of the total and China’s exports represented
Sh 245 billon, more than twice that of Tanzania! (The Citizen, March 2013)
The numbers in 2005 already suggest
a Tanzanian dependence on China’s goods and services. In addition, in 2009 the divide widened even
further when Chinese President, Hu Jintao, met with Tanzanian President, Jakaya
Mrisho Kikwete and trading was at Tsh 1.37 trillion between the two countries,
again, disproportionately! History demonstrates
that China has never been a genuine trading partner since they have slowly
widened the gap to form a reliable source of income for themselves by providing
largely low quality goods and services at inflated prices. As of 2011 the export value between the two
countries was at Tsh 2.28 trillion!! I
don’t have to tell you which country has the lion’s share of that Tsh 2.28
trillion.
Wito kwa Vijana Wote Watanzania- Zamu Yetu Kuliongoza Taifa Imefika
The Kilian Kamota’s Call to All Tanzanian Youth: Our Turn to Lead the Nation is Now.
By
Kilian Muya Kamota
The task is ours, the
Tanzanian youth, to decide the future and the fate of our Nation. Our fathers,
the first generation of leaders, have done their part; they fought political
colonialism and afforded us the political independence. The time has come for them
to pass on the torch to us, so we can fight for socio-economic independence. We
must show up, accept the torch and lead our Nation into new horizons. The
future of Tanzania is in our hands – the Tanzanian youth. This is the task we cannot
ignore; this is the task we cannot pass to someone else. It is our task, it is
our duty. The question is what are we going to do about it? Are we going to
show up for this noble task? Are we going to report for duty? Or are we going
to let our Nation stray into wilderness and chaos without leadership? Are we
going to decide the fate of our own future or are we going to let few
politicians decide our fate and our future?
Our fathers – the
first generation of leaders – have grown old. Their actions and leadership can
attest to that. The time has come for them to pass on the torch and for us to
take the realm. Let us help them retire in peace as we take over the noble task
of leading our nation.
Letter to
the First Generation of Leaders – Good Bye and Good Luck
On behalf of all Tanzanian
youths’, i wish to express sincere gratitude to our fathers – the first
generation of leaders – for all the hard work and dedication to our Nation.
Your hard work and efforts is truly appreciated, it will not be forgotten and
will not perish in vain. We will always cherish all that you were able [and not
able] to achieve. And to that end, we want to wish you good health and good
luck as you retire in peace. Please take on your new task of advising the new
generation and
To Read more
click here
Thursday, August 18, 2011
DWIGHT HOWARD awezesha ujenzi wa bweni Tanzania
"Do you see the smiles on their faces after you have done what you do best?
Do you see satisfaction on their faces after you have blessed them with your gift?
You don't think it's much but to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there, you don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize they have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day"
Lucky Dube

Ni jana tu nilipokuwa ninapitapita mtandaoni nilipokutana na habari kuhusu ziara ya mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani DWIGHT HOWARD alivyotembelea Tanzania na kuwezesha kupatikana ama kujengwa kwa Bweni katika shule ya sekondari Kipok.
Dwight, ambaye kupitia tovuti ya foundation yake ya D12 amesema alikuwa katika maandalizi ya kuelekea Tanzania, Haiti, India na China ametoa msaada wa shilingi milioni 90 kusaidia ujenzi wa jengo hilo.
Mbali na kutoa mchango huo, Dwight, alishiriki kwenye kujenga sehemu ya msingi wa bweni hilo na kuzindua rasmi ujenzi huo kama aonekanavyo pichani.
Ukweli mwingine ni kuwa Dwight Howard ni mtu mwenye pesa, na pengine Shilingi milioni 90 si kitu kwake, lakini MATOKEO ya hicho ambacho wengine wanaweza kuona ni kidogo ndiyo ninayopenda kuyazungumzia hapa. Kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa mabinti hawa si kitu kidogo na ni hilo linalonifanya nimpe heshima na shukrani zaidi.
Ni maisha ya mabinti wengi yatakayobadilika na kuboreshwa kwa ushirikiano wake. Ni upendo wa aina yake alioonyesha kwa kushirikiana na wapendwa wa eneo hilo kuwezesha ujenzi huu.
Hili ni jambo ambalo halistahili kupita bila kupongezwa (kama ambavyo ningependa yeyote anayeshuhudia jambo kama hili kuleta hapa tupongeze).
Ni kwa sababu hii, napenda kumuunganisha Dwight Howard katika orodha ya watu walioingia kwenye MWANANCHI MIMI. Kipengele kinachohusu wale walioenda zaidi ya kazi ama fani zao, kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.
You're a hero D.
Photo Credits: D12 FOUNDATION FACEBOOK PAGE
Do you see the smiles on their faces
After you have done what you do best
Do you see satisfaction on their faces
After you have blessed them with your gift
You don't think it's much
But to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there
Don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize
They have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day
[Chorus:]
You're a hero, you're a hero
Big it up, big it up for the fireman
Big it up, big it up for the street cleaners
Big it up for the man and the woman who take care of abandoned children
Big it up, big it up for the grandmothers
Who are left to take care of the children
Big it up, big it up Wo!
MWANANCHI MIMI ni kipengele kinachoonesha, kuthaminisha na kuendeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi wenzetu / sisi wananchi katika kuisaidia jamii yetu. Hapa ni mahala ambapo hata wewe msomaji unaweza kuungana nasi kuonesha unathamini kazi ya mtu fulani kwa jamii yetu. Wapo wengi saana lakini hawapati thamani ya kazi zao kama ambavyo ingestahili na pengine ni kwa kuwa hawako katika "channel" ya kuvutia vyombo vyetu vya habari. Kwa habari zaidi nani ya label hii BOFYA HAPA
Do you see satisfaction on their faces after you have blessed them with your gift?
You don't think it's much but to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there, you don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize they have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day"
Lucky Dube

Ni jana tu nilipokuwa ninapitapita mtandaoni nilipokutana na habari kuhusu ziara ya mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani DWIGHT HOWARD alivyotembelea Tanzania na kuwezesha kupatikana ama kujengwa kwa Bweni katika shule ya sekondari Kipok.Dwight, ambaye kupitia tovuti ya foundation yake ya D12 amesema alikuwa katika maandalizi ya kuelekea Tanzania, Haiti, India na China ametoa msaada wa shilingi milioni 90 kusaidia ujenzi wa jengo hilo.
Mbali na kutoa mchango huo, Dwight, alishiriki kwenye kujenga sehemu ya msingi wa bweni hilo na kuzindua rasmi ujenzi huo kama aonekanavyo pichani.
Ukweli mwingine ni kuwa Dwight Howard ni mtu mwenye pesa, na pengine Shilingi milioni 90 si kitu kwake, lakini MATOKEO ya hicho ambacho wengine wanaweza kuona ni kidogo ndiyo ninayopenda kuyazungumzia hapa. Kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa mabinti hawa si kitu kidogo na ni hilo linalonifanya nimpe heshima na shukrani zaidi.Ni maisha ya mabinti wengi yatakayobadilika na kuboreshwa kwa ushirikiano wake. Ni upendo wa aina yake alioonyesha kwa kushirikiana na wapendwa wa eneo hilo kuwezesha ujenzi huu.
Hili ni jambo ambalo halistahili kupita bila kupongezwa (kama ambavyo ningependa yeyote anayeshuhudia jambo kama hili kuleta hapa tupongeze).
Ni kwa sababu hii, napenda kumuunganisha Dwight Howard katika orodha ya watu walioingia kwenye MWANANCHI MIMI. Kipengele kinachohusu wale walioenda zaidi ya kazi ama fani zao, kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.
You're a hero D.Photo Credits: D12 FOUNDATION FACEBOOK PAGE
Do you see the smiles on their faces
After you have done what you do best
Do you see satisfaction on their faces
After you have blessed them with your gift
You don't think it's much
But to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there
Don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize
They have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day
[Chorus:]
You're a hero, you're a hero
Big it up, big it up for the fireman
Big it up, big it up for the street cleaners
Big it up for the man and the woman who take care of abandoned children
Big it up, big it up for the grandmothers
Who are left to take care of the children
Big it up, big it up Wo!
MWANANCHI MIMI ni kipengele kinachoonesha, kuthaminisha na kuendeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi wenzetu / sisi wananchi katika kuisaidia jamii yetu. Hapa ni mahala ambapo hata wewe msomaji unaweza kuungana nasi kuonesha unathamini kazi ya mtu fulani kwa jamii yetu. Wapo wengi saana lakini hawapati thamani ya kazi zao kama ambavyo ingestahili na pengine ni kwa kuwa hawako katika "channel" ya kuvutia vyombo vyetu vya habari. Kwa habari zaidi nani ya label hii BOFYA HAPA
Wednesday, March 16, 2011
Mchango wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika elimu
"...the only way to get our economy strong, is to have an educated nation. And if you think affirmative action is the way out... no way... no way." Lucky Dube
Ofisa mtendaji Mkuu wa CBA, Yohanna Kaduma akisindikizwa kukagua majengo ya shule hiyo
.Afisa mtendaji Mkuu wa benki ya Commercial Bank of Africa (CBA) akikabidhi msaada wa madawati 172 yenye dhamani ya Sh 4.6 million kwa shule ya secondary Nkunga iliopopo wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya juzi. Anayayepokea ni mwanafunzi shuleni hapo Victoria Jodeph kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
BENKI ya Commercial Bank of Africa (CBA)Tanzania, imetoa msaada wa madawati 172 yenye thamani ya shilingi million 4.6 kwa shule ya sekondari Nkunka iliopo wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana na benki hiyo tawi la Mbeya, CBA iliweza kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma kirahisi kutokana na kuwa na upungufu wa madawati hapo awali.
Wakati wa kukabidhi msaada huo, Ofisa mtendaji Mkuu wa CBA, Yohanna Kaduma alisema wataendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa maendeleo ya shule hiyo na washule nyingine itakapoonekana hivyo.
Kaduma alisema CBA, inathamini jitianda zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo shuleni na kwa kupitia mfuko wa benki kwa ajili ya kuwekeza kwenye jamii, anafarijika kuona msaada huo utasaidia wanafunzi shuleni hapo.
“Sisi kama benki tunafarijika sana kuona tunashiriki katika maendeleo ya shulle hii. Kuwepo kwetu hapa leo kunatoa fursa kwetu kushiriki katika kutatua matatizo moja wapo ya shule hii, lakini pia kuunga mkono juhudi za serikali za kuendeza elimu nchini.” Alisema Kaduma.
Kwa upande wake msoma risala katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkunga wilayani hapo Bwana Joseph Mwalyammbwile alisema shule hio inakabiliwa na tatizo kubwa ya utoro hasa kwa wanafunzi wa kike ambao wanapata mimba hovyo na kuacha shule.
“Tunashukuru sana kwa msaada huu wa madawati. Ila niseme tu kuwa tatizo la kwanza limekwisha, Sasa tunaomba tusaidiwe kujenga hosteli ya wanafunzi hasa wa kike. Kuna tatizo kubwa sana la utoro linalosambabishwa na mimba. Tuwajengee hawa watoto hosteli hili tuwasaidie wamalize masomo yao.” Alisema Mwalyambwile
Shukrani kwa Ndg Andrew Chale kwa kutushirikisha habari hii.

Wednesday, May 12, 2010
Hongera kwa Da Vicky Ntetema
Vicky NtetemaClaudia Duque of Colombia, Tsering Woeser, a Tibetan living in China, and Vicky Ntetema of Tanzania will Receive 2010 Courage in Journalism Awards from the International Women’s Media Foundation. Mexican Journalist Alma Guillermoprieto is Lifetime Achievement Award Winner.
An investigative journalist from Colombia who has been robbed and kidnapped and who has received threats against her life and that of her daughter; a Tibetan journalist who is one of China’s best known bloggers, even though she is under constant scrutiny from the government, and a Tanzanian journalist whose investigations into a series of murders have put her in danger are winners of the 2010 International Women’s Media Foundation’s Courage in Journalism Awards.
“The work that these remarkable journalists do brings to light the dark corners of our globe,” said Judy Woodruff of the PBS News Hour, IWMF Courage in Journalism Awards chair. “They risk everything, including their livelihoods, their safety and the safety of their families, to unearth the truth and enlighten us all.”
Vicky Ntetema, 51, a freelance Tanzanian reporter who contributes to the BBC World Service. Ntetema uncovered one of her country’s horrible secrets when she began to investigate the brutal killings of albinos and their families. Working undercover, she learned that witchdoctors were murdering albinos to dismember their bodies and sell potions made out of their hair, legs and arms. Customers were told the potions would bring them good fortune. Witchdoctors are especially dangerous because they hold powerful positions in African traditional society, often use hired killers and are protected by local police. Ntetema has received death threats since she started her reporting. She has twice left Tanzania for her safety. She now reports wearing hijab to disguise her identity and often travels with a security guard. According to the BBC, some 170 witchdoctors have been arrested for the killings.
The IWMF Courage in Journalism Awards honor women journalists who have shown extraordinary strength of character and integrity while reporting the news under dangerous or difficult circumstances. The Lifetime Achievement Award recognizes a woman journalist who has a pioneering spirit and whose determination has paved the way for women in the news media. Including this year’s honorees, 69 journalists have won Courage Awards and 19 journalists have been honored with Lifetime Achievement Awards. The awards will be presented at ceremonies in New York on October 19 and in Los Angeles on October 21.
Founded in 1990 and now celebrating its 20th Anniversary, the International Women’s Media Foundation is a vibrant global network dedicated to strengthening the role of women in the news media worldwide as a means to further freedom of the press. The IWMF network includes women and men in the media in more than 130 countries worldwide.
Source: www.wavuti.com/4/post/2010/05/congratulations-to-victy-ntetema.html
SHUKRANI ZA PEKEE KWA DADA SUBI KWA KUTUSHIRIKISHA HILI NA PIA KWA DADA VICKY NTETEMA KWA KAZI ULIYOIFANYA KUIBUA MAOVU HAYA
Tuesday, May 11, 2010
Isaya Zephania Yunge......Kijana wa sasa, kwa Tanzania ya sasa
Destiny.Nimekuwa nikisema kuwa MPAKA KESHO ITAKAPOHESABIKA KUWA LEO, BASI VIJANA HATUTAENDELEA. Maana kubwa ya sentensi yangu ni kuwa mambo ya msemo wa VIJANA NI TAIFA LA KESHO hauna maana.
Hauna maana kwangu kwa kuwa wazee wanaendelea kung'ang'ania madaraka mpaka vijana wanapoelekea kuuacha ujana na wakati huo ndipo tunapojikuta tumekosa la kufanya kwa kuwa tulikuwa tukisubiri hiyo KESHO ambayo haijawahi kufika na haitafika. Hakuna ubishi kuwa wazee wengi na hasa kwenye siasa za nyumbani na ambao ndio wanaoonekana kuhusika katika maamuzi mengi yahusuyo Taifa na Vijana wanategemea saana uzoefu na wanatueleza kuwa hatuna UZOEFU katika kushauri na kuamua, lakini wanasahau kuwa "The trouble with experience is that by the time you have it you are too old to take advantage of it. " — Jimmy Connors
Lakini kati ya watu wachache ambao wameonesha kuanza harakati za kuibadili dhana hiyo potofu na kuamua kujikita katika kuibadili jamii yetu akiwa na umri wa ujana ni Kaka mdogo ISAYA ZEPHANIA YUNGE. Ni kijana mdoog ambaye ameweza kuwa na mipango halisi ya kuibadili jamii yetu. Niliweza kuwasiliana naye kwa njia ya mahojiano ya maandishi na kisha kupanga kufanya mahojiano ya sauti na kuyarekodi kwa njia ya simu. Mipango yangu ilishindikana ila alikuwa mkarimu saana kunieleza kila nilichohitaji kujua kuhusu yeye kwa njia ya maandishi na nikaona nishirikiane nanyi katika kipengele hiki cha MWANANCHI MIMI ambacho ni maalum kwa wale waliokwenda "mwendo wa ziada" kuiokoa jamii.
Isaya alizaliwa 23/03/1990 katika kijiji cha Nyangunge, wilaya ya Magu, mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa kwanza katika kwa wazazi wake ambao walitengana akiwa na miezi michache tangu kuzaliwa. Akielezea anavyokumbuka maisha yake ya utotoni, anasema "nikiwa na umri mdogo mama yangu alilazimika kunipeleka kuishi na bibi yangu wilayani Magu ambapo Bibi alikuwa akijishughulisha na Siasa, Kilimo na Ufugaji hivyo kukua na kulelewa hapo na bibi yangu ambaye alinifunza kilimo cha mpunga na ufugaji wa ngombe, mbuzi na mondoo, nikiwa na umri wa miaka mitano tayari nilikuwa Mchungaji bora wa Mbuzi na Mhamiaji wa ndege katika mashamba ya Mpunga."Harakati za Isaya katika kuikomboa jamii ziliznza mwaka 2005 ambapo alianza kufanya kazi za kujitolea katika shirika lisilo la kiserikali liitwalo KULEANA na akiwa hapo, walikuwa na kikundi cha watoto kilichoitwa SAUTI YA WATOTO,ambacho kiliwawezesha kupata mafunzo mbalimbali ya haki za watoto na wajibu wao na kupitia mafunzo hayo, waliweza kuelimisha jamii kwa njia ya redio, ambapo walikuwa na kipindi kila Jumamosi katika kituo cha Radio free Africa ya jijini Mwanza, kipindi ambacho kilikuwa kinafadhiliwa na UNICEF.
Hata hivyo, nia ya kujielimisha haikuishia hapo, kwani Isaya amenieleza kuwa "mwaka 2006 nilipata mafunzo ya uelimishaji rika juu ya masuala ya UKIMWI chini ya mradi ulioitwa Abstinence and Behaviour Change to Youth (ABY) uliokuwa unadhaminiwa na International Youth Foundation. Tangu hapo nimekuwa nikifanya kazi kama muelimishaji rika wa kujitolea mashuleni na katika jumuiya na kwa sasa natoa zaidi mafunzo hayo ya UKIMWI na stadi za maisha kwa Watoto wa mitaani , vile vile kupitia kipindi cha redio-katika redio iitwayo Passion FM nimeweza kutoa mafunzo hayo kwa hadhira kubwa zaidi juu ya masuala ya UKIMWI, stadi za maisha, na haki za watoto. "
Mwaka 2006, Kaka Isaya alichaguliwa na wajumbe wa baraza la watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambalo liko chini ya usimamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Akiwa na washiriki wenzake wa Junior 8Mwaka unaofuata (2007) alichaguliwa kuwakilisha Tanzania kama UNICEF-Youth Ambassador katika Mkutano wa Junior 8 ambao ni mkutano tangulizi wa vijana wa nchi za G8, katika mkutano huo uliokuwa na vijana 75 kutoka nchi za G8 na nchi zinazoendelea ambazo ni Brazil,China, Tanzania, Sierra Leone, Central Africa Republican, Ethiopia, India, Moldova, Algeria na Cameroon ambapo nchi hizi zilitoa vijana 10 ikiwa ni mmoja kila nchi. Anaendelea kunijuvya kuwa "nikiwa katika mkutano huu nilichaguliwa kuwa UNICEF-Africa Youth ambassador na nikahudhulia kikao cha G8 ambapo nilipata nafasi ya kuongea na kuwakilisha maoni yangu."
Akiwa na viongozi George Bush na Tony Blair katika mkutano wa G8Mwaka 2007, Isaya alianzisha shirika lisilo la kiserikali liitwalo JUNIOR 9 FOUNDATION, ambalo linashughulika na watoto wa mitaani na waishio katika mazingira magumu. "Junior 9 Foundation inawasaidia kwa kuwapeleka shule watoto wa mitaani ili wapate elimu ya msingi na kutoa vifaa na mahitaji ya shule kwa watoto waliokatika mazingira magumu."
Kwa hakika niliguswa, nimeguswa na nimefurahishwa saana na HARAKATI za Kaka mdogo Isaya na nimeona ni vema kumleta hapa KUENZI juhudi zake za kuibadili jamii akiwa na umri muafaka.
Kwa sasa anasoma kidato cha tano TAQWA HIGH SCHOOL-Ghana Campus.
HEKO KAKA ISAYA NA MUNGU AKUJAALIE
Naomba nisindikize pongezi zangu kwa UJANA WA LEO wa Isaya na kibao hiki kiitwacho YOUTHS TODAY
Thursday, November 19, 2009
TUWA-USA.......MASHUJAA WETU
Wasomi, wanaharakati wanaosaidia elimu nyumbani

"Do you see the smiles on their faces
after you have done what you do best.
Do you see satisfaction on their faces
after you have blessed them with your gift.
You don't think it's much
but to them it means the world.
They wake up in the morning and wish you were there
You don't have to lie to gain their trust.
You have never won a Nobel prize,
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day
YOU ARE A HERO, YOU ARE A HERO."
Haya maneno ndiyo aliyoanza nayo Phillip Lucky Dube katika wimbo wake HERO alipokuwa akitoa heshima kwa wale ambao wana nafasi ndogo katika jamii lakini wakizitumia ipasavyo kuleta MABADILIKO CHANYA KWA JAMII YAO. Nami leo sina ninaloweza kupunguza ninapowafikiria hawa wanachama wa Chama Cha Wanawake Wasomi wa kiTanzania waliopo nchini Marekani ama The Tanzanian University Women's Association (TUWA-USA)ambao hivi karibuni walifanikisha moja ya adhma zao kuu kwa kuwezesha kupatikana kwa madawati 32 yenye zaidi ya thamani ya shilingi 1,892,000 kwa shule ya msingi Mtakuja ambayo ni moja kati ya shule nyingi sana zenye uhaba wa madawati nchini.
Mlezi wa TUWA-USA Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya akimkabidhi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni Bwn Faustine Kikove moja ya madawati 32 yaliyochangwa.
Madawati hayo yaliyokabidhiwa na mlezi wa Chama hicho Meja Jenerali Mstaafu Benjamin Msuya ni hatua kubwa katika kusaidia kuimarisha mazingira ya elimu nchini hali itakayosaidia kuwafanya wanafunzi kufanya vema darasani.
Si kwa wanafunzi tu, bali pia mchango huu uliwezesha ajira kwa mafundi seremala
Kinachonipa faraja zaidi ni namna ambavyo wanachama wa TUWA-USA wameweza kufanikisha hili licha ya MAJUKUMU MENGI waliyonayo kimaisha. Chama hiki kinaendeshwa kwa kujitolea na wanachama wake wana majukumu ya kifamilia zaidi (wengine wakiwa ni kinamama wanaolea familia na wengine wakisafiri kutoka majimbo ya nje ya hapa DC Metro ili kufanikisha nia yao) na wamekuwa wakifanya hata mikutano kwa njia ya simu ili kufanikisha adhma yao. Leo hii kuona wanafanikisha hili katika mazingira magumu kama haya inaongeza furaha na kunikumbusha alichoimba Nasio Fontaine kuwa "harder the battle, yougher the fight, SWEETER THE VICTORY"
Blog hii ilibahatika kushiriki katika matukio ya kusaidia kutunisha mfuko ili kiweza kufanikisha jambo hili (kama ilivyoliripoti HAPA)na ilijionea CHANGAMOTO mbazo kinamama hawa wanakabiliana nazo katika kusonga mbele, na leo NAWIWA furaha kubwa kuleta shukrani kwa wanachama wote kwa kusimama imara katika azma yao na kuifanikisha jambo hili ambalo ni ZAWADI KWA JAMII NZIMA YA KITANZANIA.
Mwl Albert Juakali wa Shule ya Msingi Iboma wilayani Chunya mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya m'buyu.
Vyama ni vingi, JUMUIYA ni nyingi na mahitaji ni mengi, na ni sisi wenyewe tunaohitaji kusimama kidete kuweza kufanikisha tatizo hili na kuboresha mazingira na maisha bora kwa kila mwanafunzi kwa kujitolea kile tuwezacho katika kufanikisha azma hii. Si lazima kiwe kikubwa, bali tukitoa kwa moyo kitafaa. Kama alivyosema Mother Theresa kuwa "I can do no great things. Only small ones with GREAT LOVE." Nasi tuungane katika kuchangia na kufanikisha kuwaondoa watoto katika mazingira haya. Kama TUWA-USA wameweza kusimama katika MALENGO yao kama walivyoeleza HAPA, ni kwanini vyama na jumuiya nyingine zisiweze??
Licha ya kusaidia kuinua elimu kwa watoto (hasa mabinti) nchini anzania, TUWA-USA imekuwa ikijitahidi kufanikisha njia za kuwezesha waTanzania walio hapa kujua namna ya kupata elimu bora hapa nchini (BOFYA HAPA)
Unaweza kujua na kujifunza mengi kuhusu TUWA-USA kwa kutembelea tovuti yao HAPA
Kwa Dada zangu wa TUWA-USA.
ASANTENI SAANA. TWAWATHAMINI, TWAWAPENDA, TWAWAOMBEA NA KUWATAKIA HERI KATIKA KILA JEMA MPANGALO KUFANYA KWENU NA KWA JAMII YETU
Kwa blog ya Changamoto Yetu, ninyi ni HEROES
BLESSINGS
Picha toka Blogs za Kaka Issa & Ahmad Michuzi
after you have done what you do best.
Do you see satisfaction on their faces
after you have blessed them with your gift.
You don't think it's much
but to them it means the world.
They wake up in the morning and wish you were there
You don't have to lie to gain their trust.
You have never won a Nobel prize,
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day
YOU ARE A HERO, YOU ARE A HERO."
Haya maneno ndiyo aliyoanza nayo Phillip Lucky Dube katika wimbo wake HERO alipokuwa akitoa heshima kwa wale ambao wana nafasi ndogo katika jamii lakini wakizitumia ipasavyo kuleta MABADILIKO CHANYA KWA JAMII YAO. Nami leo sina ninaloweza kupunguza ninapowafikiria hawa wanachama wa Chama Cha Wanawake Wasomi wa kiTanzania waliopo nchini Marekani ama The Tanzanian University Women's Association (TUWA-USA)ambao hivi karibuni walifanikisha moja ya adhma zao kuu kwa kuwezesha kupatikana kwa madawati 32 yenye zaidi ya thamani ya shilingi 1,892,000 kwa shule ya msingi Mtakuja ambayo ni moja kati ya shule nyingi sana zenye uhaba wa madawati nchini.
Madawati hayo yaliyokabidhiwa na mlezi wa Chama hicho Meja Jenerali Mstaafu Benjamin Msuya ni hatua kubwa katika kusaidia kuimarisha mazingira ya elimu nchini hali itakayosaidia kuwafanya wanafunzi kufanya vema darasani.
Kinachonipa faraja zaidi ni namna ambavyo wanachama wa TUWA-USA wameweza kufanikisha hili licha ya MAJUKUMU MENGI waliyonayo kimaisha. Chama hiki kinaendeshwa kwa kujitolea na wanachama wake wana majukumu ya kifamilia zaidi (wengine wakiwa ni kinamama wanaolea familia na wengine wakisafiri kutoka majimbo ya nje ya hapa DC Metro ili kufanikisha nia yao) na wamekuwa wakifanya hata mikutano kwa njia ya simu ili kufanikisha adhma yao. Leo hii kuona wanafanikisha hili katika mazingira magumu kama haya inaongeza furaha na kunikumbusha alichoimba Nasio Fontaine kuwa "harder the battle, yougher the fight, SWEETER THE VICTORY"
Blog hii ilibahatika kushiriki katika matukio ya kusaidia kutunisha mfuko ili kiweza kufanikisha jambo hili (kama ilivyoliripoti HAPA)na ilijionea CHANGAMOTO mbazo kinamama hawa wanakabiliana nazo katika kusonga mbele, na leo NAWIWA furaha kubwa kuleta shukrani kwa wanachama wote kwa kusimama imara katika azma yao na kuifanikisha jambo hili ambalo ni ZAWADI KWA JAMII NZIMA YA KITANZANIA.
Mwl Albert Juakali wa Shule ya Msingi Iboma wilayani Chunya mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya m'buyu.Vyama ni vingi, JUMUIYA ni nyingi na mahitaji ni mengi, na ni sisi wenyewe tunaohitaji kusimama kidete kuweza kufanikisha tatizo hili na kuboresha mazingira na maisha bora kwa kila mwanafunzi kwa kujitolea kile tuwezacho katika kufanikisha azma hii. Si lazima kiwe kikubwa, bali tukitoa kwa moyo kitafaa. Kama alivyosema Mother Theresa kuwa "I can do no great things. Only small ones with GREAT LOVE." Nasi tuungane katika kuchangia na kufanikisha kuwaondoa watoto katika mazingira haya. Kama TUWA-USA wameweza kusimama katika MALENGO yao kama walivyoeleza HAPA, ni kwanini vyama na jumuiya nyingine zisiweze??
Licha ya kusaidia kuinua elimu kwa watoto (hasa mabinti) nchini anzania, TUWA-USA imekuwa ikijitahidi kufanikisha njia za kuwezesha waTanzania walio hapa kujua namna ya kupata elimu bora hapa nchini (BOFYA HAPA)
Unaweza kujua na kujifunza mengi kuhusu TUWA-USA kwa kutembelea tovuti yao HAPA
Kwa Dada zangu wa TUWA-USA.
ASANTENI SAANA. TWAWATHAMINI, TWAWAPENDA, TWAWAOMBEA NA KUWATAKIA HERI KATIKA KILA JEMA MPANGALO KUFANYA KWENU NA KWA JAMII YETU
Kwa blog ya Changamoto Yetu, ninyi ni HEROES
BLESSINGS
Picha toka Blogs za Kaka Issa & Ahmad Michuzi
Friday, October 9, 2009
ULEZI........CHANGAMOTO YETU kwa JAMII BORA
Kutokana na CHANGAMOTO zilizo nje ya uwezo wangu, nimeshindwa kuweka kipengele cha Them, I & Them kwa siku ya leo. Ila, nina CHANGAMOTO YETU SOTE KUHUSU ULEZI NA MALEZI
Taswira toka http://co.humboldt.ca.usKuna wakati maisha yetu hayaendi kama tupendavyo. Yaani uwezo wa kutimiza ndoto zetu unazidiwa na ukweli wa ugumu wa maisha. Na kwa kuwa hatutimizi malengo yetu, haimaanishi kuwa hatuwezi kuishi maisha mema. Tunaweza kwa KUTAMBUA wapi palipo na uwezekano wa kusaidiwa kutimiza ndoto ama malengo yetu kwan ufasaha na mafanikio zaidi ya tunavyoweza. Ni hapa ambapo tunatakiwa kuwa wasaidizi wa wenzetu. Wa ndugu na jamaa zetu na kuwaonesha njia sahihi ili wafanikiwapo wawe na uwezo wa kutusaidia sisi na jamii kwa ujumla.
Juzi nilikuwa nasoma ukurasa wa rafiki yangu kwenye facebook. Nikakutana na picha njeeema saana ya Mamaye kisha nikaeleza ukweli kuhusu jukumu la kinamama. Aliponijibu nikajikuta nakaribia kutiririsha chozi. Alinieleza kuhusu UPENDO, UJASIRI NA IMANI aliyonayo mama yake. Sikushangaa sana kwani na yeye yuko hivyo. Kisha nikarejea kwa wazazi wengi niwajuao (namtanguliza Mamangu mpenzi) na kugundua kuwa wengi wanafanya mengi ambayo sasa hivi yanaigusa jamii kubwa kuliko ambavyo ingekuwa kama wangeamua kujilimbikizia wao. Najaribu kufikiri kama Mama zetu wangepata muda wa kuelimishana kwa namna tufanyavyo (hata kama wangekuwa na ma-pc kila chumba cha nyumba na muda wa kufanya hivyo). Lakini hii ni sehemu ndoooogo saaaana ya faida ambayo Mama zetu (na wazazi + walezi kwa ujumla) wameiwekeza kwetu na sasa ulimwengu mzima unanufaika.
Niliwahi kuandika kuwa HUWEZI KUWASHUKURU WOTE WALIOKUSAIDIA, BALI WAOMBEE. Waombee kwa moyo wa kuwekeza katika kile unachokitumia sasa kutuelimisha na kutupa changamoto za maisha.
Na hii sasa ni CHANGAMOTO YETU SOTE kubadili mawazo ya u-mimi na kuwekeza katika kile tuwezacho, lakini pia kile tunachoweza kuwawezesha wenzetu na tufanye hivyo.
Narejesha habari hii toka kwake Dr Ben Carson aliyoizungumza katika kipindi cha Morning Edition cha NPR ambapo kila Jumatatu huwa wanaleta watu tofauti kueleza wanachoamini. Yeye alisema anaamini kuwa THERE IS NO JOB MORE IMPORTANT THAN PARENTING. (Bofya hapa kusoma na kusikiliza wengine wasemavyo)
Labda tujiulize kuwa ni matendo mangapi yanayoimong'onya jamii kwa kuwa watu hawakulelewa vema?? Hawakuoneshwa njia sahihi ya kupia, hawakufunzwa kujitambua na kutambua na kuheshimu tofauti na mafanano yetu, hawakuelezwa kuwa sisi ni zaidi ya muonekano, ni zaidi ya pesa, ni zaidi ya mali, ni zaidi ya sifa za mtaani na hata zaidi ya vile ambavyo wasiotujua wanatufanya tujione????
Ni mangapi yanayotokea sasa na kuonekana dhahiri kuwa ni matokeo ya ULEZI M'BOVU???
Naungana na Dr Carson kuwa HAKUNA KAZI ILIYO MUHIMU ZAIDI YA KULEA NA NAWASHUKURU WAZAZI NA WALEZI WANGU WOOOTE WALIONILEA NA WANAOENDELEA KUNILEA (kwa namna moja ama nyingine)
Bonyeza "play" umsikilize na / msome Dr Carson hapa chini
The simplest way to say it is this: I believe in my mother.
My belief began when I was just a kid. I dreamed of becoming a doctor.
My mother was a domestic. Through her work, she observed that successful people spent a lot more time reading than they did watching television. She announced that my brother and I could only watch two to three pre-selected TV programs during the week. With our free time, we had to read two books each from the Detroit Public Library and submit to her written book reports. She would mark them up with check marks and highlights. Years later we realized her marks were a ruse. My mother was illiterate; she had only received a third-grade education.
Although we had no money, between the covers of those books, I could go anywhere, do anything and be anybody.
When I entered high school I was an A-student, but not for long. I wanted the fancy clothes. I wanted to hang out with the guys. I went from being an A-student to a B-student to a C-student, but I didn't care. I was getting the high fives and the low fives and the pats on the back. I was cool.
One night my mother came home from working her multiple jobs and I complained about not having enough Italian knit shirts. She said, "Okay, I'll give you all the money I make this week scrubbing floors and cleaning bathrooms, and you can buy the family food and pay the bills. With everything left over, you can have all the Italian knit shirts you want."
I was very pleased with that arrangement but once I got through allocating money, there was nothing left. I realized my mother was a financial genius to be able to keep a roof over our heads and any kind of food on the table, much less buy clothes.
I also realized that immediate gratification wasn't going to get me anywhere. Success required intellectual preparation.
I went back to my studies and became an A-student again, and eventually I fulfilled my dream and I became a doctor.
Over the years my mother's steadfast faith in God has inspired me, particularly when I had to perform extremely difficult surgical procedures or when I found myself faced with my own medical scare.
A few years ago I discovered I had a very aggressive form of prostate cancer; I was told it might have spread to my spine. My mother was steadfast in her faith in God. She never worried. She said that God was not through with me yet; there was no way that this was going to be a major problem. The abnormality in my spine turned out to be benign; I was able to have surgery and am cured.
My story is really my mother's story -- a woman with little formal education or worldly goods who used her position as a parent to change the lives of many people around the globe. There is no job more important than parenting. This I believe.
N.P.R (National Public Radio)
Monday, September 7, 2009
Tumsaidie ndugu yetu Emmanuel Urio
Kaka Issa Michuzi na Dada Flora wameweka ombi la msaada kwa Kaka Emmanuel Urio. Nami naungana nao kuomba kila mwenye uwezo wa kumsaidia kujitoa kwa hali na mali katika kiwango chochote kumuwezesha ndugu yetu kutimiza lengo lake. Akiwezeshwa anaweza kuwa mtu muhimu maishani mwetu, kuwa ushuhuda kwa wengine wanaokata tamaa na pia anaweza hata kutoa ajira kwa wengine.
Ndugu Emmanuel Urio alizaliwa jijini Mwanza akiwa na upungufu wa mikono na miguu na licha ya ugumu wa mazingira yake, anapenda saana kusoma na kuimba na mambo mengine mengi ambayo anaamini akiwezeshwa atafanikiwa. Kwa mujibu wa Blog ya Dada Flora, "Emah anafanya mambo mengi saa japokuwa hana miguu wala mikono, ana uwezo wa kusoma na kuandika vizuri, anaweza kuimba, ana uwezo wakutumia gitaa, anatunga shanga. Kwa kifupi Emah anafanya mambo ambayo baadhi yetu ambao tumekamilika hatuwezi kuyafanya."
Kwa pamoja tumsaidie ndugu yetu ambaye anapatikana kirahisi zaidi kwa kutumia simu namba +255 757 839 674
Tumeshuhudia jinsi Kijana Nick alivyo SAUTI NA MFANO wa mafanikio ya wale walio na tofauti nasi. Mtazame hapa chini kijana huyu ambaye alizaliwa bila mikono wala miguu lakini anacheza pool, golf na hata kuogelea. Ni sauti kwa mamilioni ulimwenguni
Katika kipengele kipya cha MWANANCHI MIMI, tutakuwa tukileta habari za wale wanaoisaidia jamii na pia wanaohitaji msaada kutoka kwa jamii.
Sisi ni sehemu kubwa ya kuwezeshana kufanikisha haya.

Subscribe to:
Posts (Atom)