Wednesday, March 16, 2011

Mchango wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika elimu

"...the only way to get our economy strong, is to have an educated nation. And if you think affirmative action is the way out... no way... no way." Lucky Dube
Ofisa mtendaji Mkuu wa CBA, Yohanna Kaduma akisindikizwa kukagua majengo ya shule hiyo
.Afisa mtendaji Mkuu wa benki ya Commercial Bank of Africa (CBA) akikabidhi msaada wa madawati 172 yenye dhamani ya Sh 4.6 million kwa shule ya secondary Nkunga iliopopo wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya juzi. Anayayepokea ni mwanafunzi shuleni hapo Victoria Jodeph kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
BENKI ya Commercial Bank of Africa (CBA)Tanzania, imetoa msaada wa madawati 172 yenye thamani ya shilingi million 4.6 kwa shule ya sekondari Nkunka iliopo wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana na benki hiyo tawi la Mbeya, CBA iliweza kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma kirahisi kutokana na kuwa na upungufu wa madawati hapo awali.

Wakati wa kukabidhi msaada huo, Ofisa mtendaji Mkuu wa CBA, Yohanna Kaduma alisema wataendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa maendeleo ya shule hiyo na washule nyingine itakapoonekana hivyo.

Kaduma alisema CBA, inathamini jitianda zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo shuleni na kwa kupitia mfuko wa benki kwa ajili ya kuwekeza kwenye jamii, anafarijika kuona msaada huo utasaidia wanafunzi shuleni hapo.

“Sisi kama benki tunafarijika sana kuona tunashiriki katika maendeleo ya shulle hii. Kuwepo kwetu hapa leo kunatoa fursa kwetu kushiriki katika kutatua matatizo moja wapo ya shule hii, lakini pia kuunga mkono juhudi za serikali za kuendeza elimu nchini.” Alisema Kaduma.

Kwa upande wake msoma risala katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkunga wilayani hapo Bwana Joseph Mwalyammbwile alisema shule hio inakabiliwa na tatizo kubwa ya utoro hasa kwa wanafunzi wa kike ambao wanapata mimba hovyo na kuacha shule.

“Tunashukuru sana kwa msaada huu wa madawati. Ila niseme tu kuwa tatizo la kwanza limekwisha, Sasa tunaomba tusaidiwe kujenga hosteli ya wanafunzi hasa wa kike. Kuna tatizo kubwa sana la utoro linalosambabishwa na mimba. Tuwajengee hawa watoto hosteli hili tuwasaidie wamalize masomo yao.” Alisema Mwalyambwile

Shukrani kwa Ndg Andrew Chale kwa kutushirikisha habari hii.

1 comment:

emu-three said...

Kama kuna kitu muhimu sana cha kusaidia ni hiki; elimu...na kama inawezekana nyie mabenki anzisheni shule zenu, na kipaumbele wasiojiweza, na wafanyakazi wenu!
NI USHAURI TU