Friday, March 18, 2011

Them, I & Them...VICTIMS... Lucky Dube

"Bob Marley said 'how long shall they kill our prophets while we stand aside and look'? But little did he know that eventually the enemy will stand aside and look, while we slash and kill our own brothers knowing that already they are the victims of the situation. Still licking wounds from brutality, still licking wounds from humiliation...We are the victims everytime. We got double trouble everytime" Lucky Dube Photo Credits: Left foot forward.org
Hivi sasa tumeona "maendeleo" ya kile kinachoonekana kama vuguvugu la KUDAI DEMOKRASIA ambalo linaonekana kutawala AFRIKA na MASHARIKI YA KATI. Lakini lililo kubwa ni namna ambavyo WATAWALA ambao wamesema "wanazipenda nchi zao kiasi kwamba wako tayari kuua kila mtu anayewaomba wapumzike, ili wabakie madarakani". Kibaya ni kuwa WATAWALA hawa na hata familia zao hawaathiriki na mapigano wanayoanzisha. Wao wako salama, wao wanapata kila wanachotaka, wao wanaendeleana maisha ya kawaida (ambayo ni zaidi ya mwananchi wa kawaida anapokuwa katika hali tulivu), ila anayeumia, anayeteseka ni MWANANCHI. Mwananchi ambaye hata katika hali ya utulivu tayari ana maisha magumu.
Ni haya maisha ambayo hata Lucky Dube aliyazungumzia katika wimbo wake VICTIMS akisema "tayari wananchi hawa walishakuwa waathirika wa hali ya maisha" na sasa ndugu tuliokuwa tukitegemea watusaidie ndio wanatuua na kutuchinja". Na mfano ni huko Libya ambako Kanali Gadafi anatumia majeshi yake kushambulia "waasi" na matokeo yake ni kuuawa na kujeruhiwa kwa wasiohusika hasa watoto. Photo Credits: Newsmild.com
TAZAMA VIDEO HII UONE JINSI RAIA WANAVYOFANYWA NA WANA-USALAMA WAO. Wanaolipwa mshahara kwa kodi yao. Wenzao, ndani ya nchi yao


Msikilize Lucky Dube katika wimbo wake VICTIMS kutoka albamu aliyoipa jina hilohilo la VICTIMS.

Didn, t know she was crying, until now as she turns to look at me
She said boy o' boy you bring tears to my eyes. I said what?
She said boy o' boy you bring tears to my eyes
Bob Marley said "How long shall they kill our prophets hile we stand aside and look
But little did he know that eventually the enemy will stand aside and look
While we slash and kill our own brothers
Knowing that already they are the victims of the situation


Still licking wounds from brutality
Still licking wounds from humiliation
She said all these words and the wrinkles on her face became perfect trails for the tears
and she said;

Chorus: (x3)
We are the victims everytime
We got double trouble everytime

She took me outside to the churchyard showed me graves on the ground
and she said;
There lies a man who fought for equality there lies a boy who died in his struggle
Can all these heroes die in vain while we slaughter and kill our own brothers
Knowing that already they are the victims of the situation

Still licking wounds from brutality
Still licking wounds from humiliation

Chorus till fade.....


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe unaagalia habari hizi kwenye vyombo vya habari vya kimarekani vinavyotafuta sababu za kumtungua Qadafi ili vijichotee mafuta kama vilivyofanya kule Iraq na kuwaingiza watu kwenye matatizo ya milele

angalia vizuri na kufuikiri utagundua hilo then uwe upande wa Qadafi

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kamala.
Ni kweli kuwa naangalia habari hizo kwenye vyombo vya kiMarekani. Lakini UKWELI KAMILI ni kuwa naziangalia kupitia MITANDAO mingine isiyo na maslahi na Marekani. Labda nikujulishe tu kuwa vyombo vingi vya habari unavyosoma hapo nyumbani vime-subscribe kwa AP na Reuters n.k na ndio maana wanaweza kuandika habari kama wako pale japo hawana mwakilishi. Ina maana ninyi mnapata MATAKWA ya watu wa magharibi kuliko mimi ninayetazama Al Jazeera na vyombo vingine vya kiArab.
Na kuhusu post yenyewe na hasa nilipomtaja Gadhafi nimesema (na hapa nanukuu) "Na mfano ni huko Libya ambako Kanali Gadafi anatumia majeshi yake kushambulia "waasi" na matokeo yake ni kuuawa na kujeruhiwa kwa wasiohusika hasa watoto".
Mimi nawe tunajua kuwa majeshi ya Libya YANAPIGANA. Na tunajua kuwa wanawake na waoto wasiojua hata tafsiri na sababu ya vita hivi nao wanakumbwa na haya. Na ndipo niliposema kuwa sasa si nchi iliyotawala Libya inayoua watu, bali wao wamekaa pembeni wakiwatazama waLibya wakichinjana.
NA HUO KAKA.....HUO NDIO UKWELI

Koero Mkundi said...

Bado najiuliza ni upande upi uko sahihi, Waasi au Ghadafi?

Fadhy Mtanga said...

mimi ni mtembeleaji mzuri sana wa mtandao wa Aljazeera pengine kuliko mitandao yote. lakini nina kila sababu ya kuamini enzi ya Ghaddaf inapaswa kumalizika.

pamoja na hayo, mimi si shabiki wa mataifa mengine kuingilia taifa jingine....lakini ni mtu ninayedhani ikibidi ibidi.

mimi si shabiki wa kuingiliwa kwa taifa lolote kuambatane na maslahi ya kiuchumi na wala si maslahi ya wananchi wake....

mimi si shabiki wa kiongozi yeyote kutumia ubabe wa kijeshi uuao raia wake ili aendelee kubaki madarakani...ukishawauwa raia wako utawaongoza panya?

lakini mie si shabiki wa vita.

Mungu uwalinde wananchi wa kawaida wa Libya maana hali si hali.

kaka Mubelwa, muda mrefu kaka. bila shaka uzima upo wa kutosha.