Showing posts with label Thanx and Praises. Show all posts
Showing posts with label Thanx and Praises. Show all posts

Wednesday, August 7, 2013

Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wikiendi hii

Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za  Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.
Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
 Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
 
            USIKOSE!!!!!
Na hizi ni baadhi ya nyimbo zao mpya
NI KWA NEEMA wake Christina Shusho (hit as always)

Na huu...NKIZA
Moja ya nyimbo mpya za Upendo Kilahiro kutoka katika albamu yake mpya aliyoimba kwa lugha ya kiRundi ya SINZOGIT'ICO NTIYA
IMAGINE
Hawa wote katika JUKWAA MOJA wikiendi hii

Sunday, July 28, 2013

Kanisa kuadhimisha miaka mitano ya huduma Washington DC

Kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries linalotoa huduma za kiroho na kijamii katika eneo la DMV (Washington DC na vitongoji vyake) linataraji kuwa na siku tatu za maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
Katika maadhimisho hayo yatakayofanyika kuanzia Agosti 9 - 11, kutakuwa na mafundisho ya neno la Mungu yatakayoongozwa na Mchungaji Nathanie Kigwila pamoja na Mwinjilisti Ezekiel Mwalugaja.
Pia kutakuwa na Tamasha la uimbaji litakaloshirikisha waimbaji wa hapa Marekani pamoja na waimbaji wa injili wa kimataifa toka Tanzania Upendo Kilahiro na Christina Shusho.
Mwisho kutakuwa na ibada maalum itakayokuwa ni kilele cha maadhimisho hayo ambayo itafanyika Jumapili ya Agosti 11.
Anwani ni
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

NYOTE MNAKARIBISHWA

Friday, July 5, 2013

Mchungaji Emmanuel Mgaya (MASANJA MKANDAMIZAJI) kuhubiri Washington DC Jumapili hii

Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara maalum, atahudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya kesho (Jumapili 07/07/2013)
Bwn. Mgaya ambaye pia hufahamika kama Mchungaji Mtarajiwa  na ambaye amekuwa akifanya huduma ya uhubiri nchini Tanzania, atahubiri katika ibada ya jumapili katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES katika ibada ya kawaida ya kila jumapili ambayo hufanyika kuanzia saa saba kamili mchana mpaka saa tisa kamili alasiri (1:00pm - 3:00pm)
Anwani ni
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii itakuwa ni huduma ya kwanza nchini Marekani kwa Mtumishi huyu ambaye ni Mchungaji msaidizi katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lililopo Kariakoo jimbo la Temeke jijini Dar Es Salaam likiongozwa na Askofu Bruno Mwakibolwa na ameshafanya huduma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Mtumishi Emmanuel Mgaya akihubiri Neno la Mungu katika viwanja vya kanisa la Tanzania Assemblies of God, Mbagala Dar Es Salaam
Photo Credits: Ramsoict.com
Masanja akiwa kwenye moja ya mikutano ya Injili wilayani Nzega mkoani Tabora, katika Mkutano wa Injili ulioongozwa na Mtumishi wa Mungu Daniel Kulola
Photo Credits: Strictly Gospel
Bwn. Emmanuel Mgaya, ambaye pia anafahamika zaidi kama Masanja Mkandamizaji kupitia kazi za uchekeshaji wa kwenye luninga, yuko nchini Marekani kwa ziara maalum ya Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili linalofanyika leo Jumamosi (June 6, 2013)

Tuesday, May 7, 2013

The Bees Group...Watoto na TALANTA zao kwa Mungu

Waite The Bees Group.
Watoto wa kiTanzania wanaoishi hapa Washington DC ambao kwa muda wao wa ziada wanafanya mazoezi ya nyimbo mbalimbali za dini na kutumika katika kumtangaza Mungu kwenye ibada, matamasha na makusanyiko ya kidini hapa Washington Metro.
Na hapa wameonyesha wanavyomfurahia Mungu katika wimbo huu wake Zak Mtumishi uitwao Yesu Ameniokoa.
Kuna vipaji humu, na sasa ni kazi kwetu wazazi KUVIKUZA NA KUVITUNZA

Thursday, April 5, 2012

Mkutano wa Pasaka DMV

Karibu katika ibada / mkutano mkubwa wa Pasaka utakaofanyika Jumamosi na Jumapili kwenye kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries.
Siku ya jumamosi, itakuwa saa 10 jioni mpaka saa 1 usiku na jumapili saa 7 mchana mpaka 9 alasiri na baada ya hapo itafuatiwa na TAMASHA LA UIMBAJI.
Ibada na tamasha vitahudumiwa na mwimbaji Flora Mbasha na Mchungaji Emmanuel Masanja kutoka Tanzania.
Karibu upokee muujiza wako.
Mahala ni:
The Way of the Cross Gospel Ministries.
3621 Campus Drive,
College Park. MD. 20705

Friday, March 16, 2012

Flora Mbasha kuhudumu Washington DC Metro jumapili hii

Msanii wa muziki wa injili toka nchini Tanzania, Bi Flora Mbasha amewasili nchini Marekani na jumapili hii (March 18, 2012) atakuwa mhudumu mgeni kwa wakazi wa Washington DC na vitongoji vyake katika Kanisa la Huduma ya Injili kwa njia ya Msalaba (The Way of the Cross Gospel Ministries).
Kwa mujibu wa Mchungaji Shideko wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministires, msanii huyo na wenzake watamtukuza Mungu kwa nyimbo kanisani hapo ambapo pia kundi wenyeji la Sounds of Glory Singers litahudumu.Pia Mchungaji Deogratias Lubala kutoka Tanzania atahubiriIbada hiyo inategemewa kuanza saa saba mchana na kumalizika saa tisa.
Anwani ya kanisa hilo ni:
3621 CAMPUS DR,
COLLEGE PARK. MD. 20740
NYOTE MNAKARIBISHWA

Tuesday, October 11, 2011

Mahojiano na J Sisters

Dada wawili kati ya wanne wa JSisters Jenny (pili kushoto) na Julie Julz Julius (wa pili kutoka kulia) wakiwa na Sunday Shomari wa Idhaa ya Kiswahili ya VOA na pia www.sundayshomari.com (kushoto) na Mari Damian (kulia) wa www.strictlygospel.wordpress.com baada ya mahojiano ya video hapa chini
J Sisters wakiwa pamoja na kwaya ya kanisa wenyeji la The Way of The Cross pamoja na waimbaji waalikwa Upendo Kilahiro, Upendo Nkone na Christina Shusho walipopanda jukwaani pamoja
J Sisters wakishambulia jukwaa
Ndugu wawili kati ya wanne wanaounda kundi la J Sisters wakieleza mengi kuhusu historia ya kundi lao, wakifafanua utata juu ya wao kusikiliza nyimbo za wasanii ambao hawajaokoka, muziki wa injili kwao ni nini, ukabilianaji wa ratiba baina ya shule na huduma, mambo wanayokabiliana nayo kama wasanii wa nyimbo za injili na mengine mengi.
Video imezalishwa na Mubelwa Bandio (www.changamotoyetu.blogspot.com) na waliketi na Dada Mary Damian (www.strictlygospel.wordpress.com)
KARIBU

Shukrani za pekee kwa J SISTERS ambao walitoa muda wao kuwezesha hili.
Baraka kwenu

Saturday, October 8, 2011

Mahojiano na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho.

Shukrani za pekee kwa waimbaji hawa ambao waliweza kutoa muda wao wa mapumziko (ambao wangeweza kufanya lolote watakalo) kuweza kuzungumza machache kuhusu HUDUMA wanayoitoa. Wameeleza historia zao kwa ufupi, kufafanua kile wafanyacho (kama ni huduma, kazi, usanii, hobby ama ni vipi?), hujuma zinazofanywa katika soko na biashara ya muziki nchini, namna wanavyotunga nyimbo zao, tofauti ya INJILI ya Tanzania na nchi walizotembelea pamoja kile / vile walivyojifunza katika ziara yao ya hapa Marekani ambacho wanaamini hawatakisahau.
KARIBU

Thanks and Praises ni kipengele kinachozungumzia masuala ya imani na kurejesha SIFA NA SHUKRANI KWA Muumba. Kwa matoleo zaidi ya kipengele hiki, BOFYA HAPA
Photo Credits: Vijimambo

Friday, September 30, 2011

Mkutano wa Neno la Mungu na Tamasha la uimbaji

Mkutano mkubwa wa Neno la Mungu pamoja na tamasha la Uimbaji wa aina yake utafanyika katika kuanzia Jumapili tarehe 2 hadi 9 Oktoba 2011 kuanzia saa 11jioni hadi saa 3 usiku ( 5pm-9pm).
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali za kimwili na Kiroho wataombewa.
KUMBUKA...
Ni kuanzia tarehe 2-9 Oktoba.
Mahala ni :

University Methodist Church
3621 Campus Drive,
College Park. MD. 20705

Kwa maelezo zaidi, tembelea http://www.thewayofthecrossgpspelministries.org ama wasiliana kwa simu nambari 703-863-2727 ama 202-367-3267 na / 240-706-0351
NYOTE MNAKARIBISHWA

Monday, September 19, 2011

Revival Gospel Conference Washington DC Metro

Ni kuanzia tarehe 2-9 Oktoba.
Mahala ni :
University Methodist Church
3621 Campus Drive,
College Park. MD. 20705
Kwa maelezo zaidi, tembelea http://www.thewayofthecrossgpspelministries.org ama wasiliana kwa simu nambari 703-863-2727 ama 202-367-3267 na / 240-706-0351

Nyote mnakaribishwa

Saturday, August 20, 2011

Give Thanks and Praises....COME DOWN FATHER..Beres Hammond

"In my heart I know that you wont let ur chosen people suffer, (too long) I know u would never let us down.
Many times I coulda pick up a gun, I coulda go out a street and play big john, that's no fun no, sure ain't no fun, oooh no, cause I think
What would happen if the other man, thinks the same, then bullets fall like rain, It's no fun no, no it's no fun.
Oh I see greed and I see selfishness, everyman is for themself. Only u can talk to them father, cause they listen to no one else.
Come Down Father"
Ndivyo asikikavyo kuimba Beres Hammond katika wimbo huo ambao ni kama maombi kwa yale yaendeleayo duniani. Beres anaendelea kumuomba Mungu juu ya wenye mamlaka ambao sasa wanajigeuza miungu-watu akisema "To the hearts of those responsible, let them know their actions are despicable. Remind them that IS YOU WHO WEARS THE CROWN" Na pia anawakanya wale wenye kudhani wataweza kuikimbia hukumu ya mabaya wanaoendelea kuyatenda kuwa "Oh, unto the ones who think you can do these wrongs and get away, Woe unto u, and watch out for ur day"
Msikilize HAPA
Beres Hammond akimuomba Mungu arejee kusawazisha hali

Saturday, May 21, 2011

Give Thanks and Praises...COME DOWN FATHER

"In my heart I know that you wont let ur chosen people suffer, (too long) I know u would never let us down.
Many times I coulda pick up a gun, I coulda go out a street and play big john, that's no fun no, sure ain't no fun, oooh no, cause I think
What would happen if the other man, thinks the same, then bullets fall like rain, It's no fun no, no it's no fun.
Oh I see greed and I see selfishness, everyman is for themself. Only u can talk to them father, cause they listen to no one else.
Come Down Father"
Ndivyo asikikavyo kuimba Beres Hammond katika wimbo huo ambao ni kama maombi kwa yale yaendeleayo duniani. Beres anaendelea kumuomba Mungu juu ya wenye mamlaka ambao sasa wanajigeuza miungu-watu akisema "To the hearts of those responsible, let them know their actions are despicable. Remind them that is u who wears the crown" Na pia anawakanya wale wenye kudhani wataweza kuikimbia hukumu ya mabaya wanaoendelea kuyatenda kuwa "Oh, unto the ones who think you can do these wrongs and get away, Woe unto u, and watch out for ur day"


Msikilize mwenyewe Beres Hammond akimuomba Mungu arejee kusawazisha hali


KISHA BURUDIKA (TENA) NA VIDEO HIZI ZA AFRIKA MASHARIKI
ATEGISIN by Emmy Kosgei

OMULIRO by Judith Babirye

KIATU KIVUE by Anastazia Mukabwa & Rose Muhando

SALUTI by Dady Owen & Friends

TAUNET NELEL by Emmy Kosgei

Sunday, March 20, 2011

Give Thanx and Praises......East African Praises

ATEGISIN by Emmy Kosgei

OMULIRO by Judith Babirye

KIATU KIVUE by Anastazia Mukabwa & Rose Muhando

SALUTI by Dady Owen & Friends

TAUNET NELEL by Emmy Kosgei

Sunday, March 13, 2011

Give Thanks and Praises. TIME CHANGES by Lady Comfort

Maisha ya sasa yanakwenda tofauti na wengi tulivyotarajia. Maisha yamegeuka na si katika imani baina ya watu, bali uchumi na nyanja ama niseme sehemu nyingine nyingi. Watu wamekosa amani ndani mwao (ndani ya mioyo yao), wamekosa amani ndani ya familia zao, wanakosa imani kwa jamii yao, kwa viongozi na hata ulimwengu kwa ujumla. Lakini haya si mageni na wala si kitu kipya masikioni mwa wengi. Hali hii yaweza kuwa mpya maisha mwa wengi maana wamekuwa wakisikia yakitokea kwa wengine na hivyo hawakuweza kuhisi ugumu wake halisi.
Lakini haya ni mabadiliko ya nyakati, na hili laweza kuwa funzo kuwa tujaribu kugeukia pale ambapo tunaamini ndipo palipo na uwezo wa kutufanikisha katika haya yote. Nako ni kwake MUNGU.
Wimbo wa leo ni kuhusu hilo ambapo mwimbaji Dada Comfort Osei-Wusu anatukumbusha kuwa kila kitu kina nyakati. Kama ilivyo kkatika kuzaliwa na kufa, kupanda na kuvuna, hivyo muda / wakati wa kupata amani halisi ni sasa na amani hiyo yapatikana kwake MUNGU.
Msikilize Lady Comfort katika wimbo huu TIME CHANGES uliobeba jina la albamu yake TIME CHANGES

>Nami nakwambia kuwa kila jambo lina mwisho, na "mwisho wa bonde ni mwanzo wa mlima kukupeleka kileleni" NEVER GIVE UP
JUMAPILI NJEMA

Sunday, November 7, 2010

Give Thanks and Praises.......BEHOLD by Culture

@ www.photosforsouls.com/nature57.html
I was travelling up the mountaine one day
And suddenly, I heard the voice coming to I and say,
Behold i come quickly to pay every man
According to the work that they have done.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
Say BEHOLD, BEHOLD I Come quickly


This world is like a mirror, reflecting at what you do,
and if you face it smiling, it will smile right back to you.
So do unto others as you would have them do,
So you days, will be many many much longer
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
Say BEHOLD, BEHOLD I Come quickly


JUMAPILI NJEEEEEMA