Friday, March 16, 2012

Flora Mbasha kuhudumu Washington DC Metro jumapili hii

Msanii wa muziki wa injili toka nchini Tanzania, Bi Flora Mbasha amewasili nchini Marekani na jumapili hii (March 18, 2012) atakuwa mhudumu mgeni kwa wakazi wa Washington DC na vitongoji vyake katika Kanisa la Huduma ya Injili kwa njia ya Msalaba (The Way of the Cross Gospel Ministries).
Kwa mujibu wa Mchungaji Shideko wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministires, msanii huyo na wenzake watamtukuza Mungu kwa nyimbo kanisani hapo ambapo pia kundi wenyeji la Sounds of Glory Singers litahudumu.Pia Mchungaji Deogratias Lubala kutoka Tanzania atahubiriIbada hiyo inategemewa kuanza saa saba mchana na kumalizika saa tisa.
Anwani ya kanisa hilo ni:
3621 CAMPUS DR,
COLLEGE PARK. MD. 20740
NYOTE MNAKARIBISHWA

1 comment:

emuthree said...

Mkuu tupo pamoja