Friday, March 16, 2012

RIVERSIDE.......Culture

Hapa ndio RIVERSIDE kwangu. Ninapopatumia ku-edit Video na Picha mbalimbali, kuwasiliana na wapendwa mbalimbali, kusoma blogs na mambo mbalimbali, kusikiliza miziki mbalimbali na pia "kurusha" CHANGAMOTO mbalimbali. Umeshagundua Riverside yako?
Dunia imekumbwa na hali mbaya ya uchumi ambayo inasababisha watu kushindwa kuzikabili hasira na kupoteza ubinadamu na kutenda yasiyotendeka kwa kuwa tu uchumi umewafanya waishi waishivyo. June 12 2009 niliandika kuhusu Bw. James von Brunn, aliyekuwa na miaka 88, aliyeingia makumbusho ya Holocost hapa Washington DC na kuanza kufyatua risasi zilizoua na sababu zikiwa ni chuki za kibaguzi na pia akilalamikia kumong'onyoka kwa mafao yake ya uzeeni (Soma habari yake hapa) . Mzee huyu alipata stress na hakujua pa kuzitua. Akaishia kufanya maafa. Novemba 5 mwaka huo huo wa 2009, askari mmoja Meja Nidal Malik Hasan alifanya ufyatuaji risasi kwenye kambi moja ya jeshi na kuua askari wenzake 13 na kujeruhi wengine 30 (Soma habari yake hapa).
Matukio kama haya yameendelea kuathiri na kutokea zaidi na zaidi katika nchi mbalimbali. Na lililotokea hivi karibuni, ni la askari mmoja wa Marekani aliyeko Afghanistan ambaye aliamua kuingia mtaani na kuanza kufyatua risasi na kuua watu zaidi ya dazeni moja.
YOTE HAYA YAMEHUSISHWA NA MSONGO WA MAWAZO.
Katika taarifa hii iliyotolewa na mwanasheria John Henry Browne aliyeteuliwa kumuwakilisha, kuna chembe za ukweli kuwa mhusika wa tendo hili alikuwa amekabiliwa na mambo zaidi ya uwezo wa kichwa chake kuhimili na kujikuta aki-SNAP na kutenda aliyotenda. Lakini askari huyu ambaye alikuwa kwenye ziara ya nne ya kikazi vitani na ambaye alipata majeraha makubwa kichwa huko nyuma, hakufurahia kupelekwa tena vitani na alishaonyesha kuchukizwa ama kutoridhishwa na hatua hiyo. Mwanasheria wake anasema "He wasn't thrilled about going on another deployment," na kisha anaongeza kuwa "He was told he wasn't going back, and then he was told he was going."
Hawa ni maskari na watumiaji wa silaha ambao matukio yao yameweza kutangazika. Lakini tunao wengi kwenye jamii zetu. Ambao kwa kusongwa na mawazo wanashindwa kuonyesha upendo kwa watoto wao. Wanakuwa wakali kwa jamii zao na wanaathiri furaha miongoni mwao.Lakini yote haya huja na dalili kiasi, japo si zote huonekana mapema.
NI NANI ANAYEONA DALILI HIZI ZA WAPENDWA HAWA?
NI NANI ANAYECHUNGUZA KUONA NDUGU ZETU WANA MAHALA PA KUTUA MIZIGO YAO YA MAWAZO?
Ndilo haswa lengo la kuingia kwenye album ya TRUST ME yake Joseph Hill ama Culture ambaye humo tunakutana na wimbo RIVERSIDE.
Katika wimbo huu, Culture anazungumza umuhimu wa kwenda pembeni ya mto na kupata muda wa kutafakari uumbaji wa Mungu na kutua msongo ulio ndani mwetu. Utamsikia akizungumza "And I sat down quietly watch the fishes circle around the little stones.
Lay their burden on the riverside.
I cup my ears and I heard the little birds whistling in the tree like, so lay their burden on the riverside
Jah provides for the birds in the air and the fishes in the sea so what about me.
Lay their burden on the riverside
Look at the crow they toil not neither do they spin yet father provide far them.
Lay their burden on the riverside"
Kwa ujumla ni kuwa kila mmoja ana magumu yake, lakini kila mmoja ana mahala pa kupata unafuu.
Ni wakati wa kuisaka ilipo NAFUU yako ili kukuwezesha kuondoa msongo wa mawazo. Na kwa kufanya hivyo, utakuwa umeisaka na kuipata RIVERSIDE YAKO.
Jiunge na Culture katika kibao hiki kitaaamu cha RIVERSIDE

For I woke on Saturday morning
Feeling sticky and dirty after work
Took a walk down a riverside

I roll a little spliff
Sat down on a stone and start to cool off
With my burden down a riverside

For I check around the youths
And I try to teach the truth
Lay their burden on the riverside

I walk through every corner
Try to find someone to talk to but I have to
Lay their burden on the riverside

For I walk and I talk
And I linger and I search
Lay their burden on the riverside

And I walk, I met the youthman pocket
And I try to search around them
Lay their burden on the riverside

And I sat down quietly
Watch the fishes circle around the little stones
Lay their burden on the riverside

I cup my ears and I heard the little birds
Whistling in the tree like so
Lay their burden on the riverside

Live good among your neighbor
Like sister and brother and
Come with me a riverside

All you need is pray to Jah, quality
You see secret shall be revealed
Lay their burden on the riverside

(solo)

Jah provides for the birds in the air
And the fishes in the sea so what about me
Lay their burden on the riverside

Look at the crow they toil not neither do they spin
Yet father provide far them
Lay their burden on the riverside

Let us walk and talk
And pray quietly in search
Lay their burden on the riverside

Look at the color of those clothes, oh Jah
Make each and every one individually
Lay their burden on the riverside

Where is the love?
Where is the togetherness too?
Lay their burden on the riverside

I can't take the war and I can't take the shooting
Neither the looting, just
Lay their burden on the riverside

I tried around Rema
Even in The Jungle
To find a quiet rest

Round there in a Nannyville
My heart come to a trail
Lay their burden on the riverside

And I knock, and I search
And I whisper and I preach
Lay their burden on the riverside

Where is the quietness
And the love to be found in some corner?
Lay their burden on the riverside

Let us walk, let us search
Let us examine and let us see
Lay their burden on the riverside.


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Mija Shija Sayi said...

Bless u kaka, umesema kweli kabisa laiti watu tungegundua siri hii ya kwenda River side????!!! Mambo mengi yasingefika yalipofika sasa.

I salute You.

Ebou's said...

Ohhh yeahh sote bado hatujajua dada umuhimu huo ila wapo watu ambao wanatupa ushauri kama hawa, Good job Bandio blessing