Thursday, March 15, 2012

Haki za UTU WETU na uhuru wa UANDISHI WETU


Katika maandalizi ya mkutano wa Diaspora wa mwaka 2010 nchini Uingereza, blogger Issa Michuzi alinukuliwa akisema kuwa "Kwa mahesbu ya haraka haraka hivi sasa kuna blog zinazotumia lugha ya kiswahili zipatazo 200 ambapo pia blog takriban 10 zinaanzishwa kila siku, na kuifanya Tanzania kuw nchi zinazoendelea katika tasnia ya habari kwa njia ya mtandao."
Hayo yalikuwa mahesabu ya mwaka 2010. Sasa hivi blogu ni nyingi saana. Yaani hata sisi bloggers hatujuani. Na wingi wa blogs hizi hauendani na wingi wa mafunzo (japo ya awali) kuhusiana na suala zima la uandishi na maadili yake.
Na hapa linalosemwa si kwamba kila blogger lazima awe mwandishi ama awe na elimu ya uandishi, lakini ninalomaanisha ni kuwa kuna MAADILI ya uandishi ambayo NILAZIMA tuyafuate kama tunajua kuwa kuna jamii inayotutegemea katika kuwahabarisha, kuwaelimisha na kuwakomboa kiakili.
Kwa siku za karibuni kumekuwa na matukio mengi mabaya na ya kutisha nchini Tanzania na mengine yamehusisha mauaji na matendo ya kikatili kwa wanajamii. Licha ya shukrani za dhati kwa wana-blog kwa kuweka wazi matendo hayo, bado narejesha OMBI la kuzingatia MAADILI katika kuweka picha na maelezo.
Ninaloomba ni kuzingatia UTU hata wa Marehemu na pia kuthamini HESHIMA ya marehemu na nduguze.
Kumekuwa pia na shida ya kuweka majina na / hata picha za watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.
Ni OMBI katika kuona namna ambavyo tunaweza kuendeleza UTU WETU wakati tukiendelea kutimiza UHURU WA UANDISHI WETU.

Tukingali pamoJAH.
Tuonane NEXT IJAYO

5 comments:

Unknown said...

kaka huu ujumbe wako nimeupenda kweli, kitu ulichokisema ni kweli na ni kitu amabacho kipo, nimefurahi sana kutembelea blog yako ambapo nimegundua kumbe mtu unapofungua blog unakuwa hujakosea bali, unakuwa unaisaidia jamii kuwa karibu na upatikanaji wa habari
KUTOKANA NA HILO BASI NAKUOMBA KAKA JARIBU KUTEMBELEA BLOG YANGU YA http:/sweetbertp.blogspot.com/ UONE MAPUNGUFU YALIYOPO PIA HATA MAELEKEZO YATAKAYOFAA KWANGU. MAANA JUZI JUZI KUNA MWANABLOGU MMOJA HAPA NCHINI ALINIKATISHA TAMAA BAADA YA KUNIANDIKIA KATIKA UKURASA WA TWITTER "oyaa mbona kwenye hii blog hujafanya lolote" NILIFEDHEHEKA SANA. MAWASILIANO NI +255 753 672 877
facebook: sweetbert philemon tz
twitter: sweetbertp
NITASHUKURU KWA UWEPO WAKO KAKA

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana kaka kwa kukumbusha jambo hili.

SarafinaLindiweMsuya said...

Ni kweli kabisa. Inasikitisha sana kuona kuwa wanataka kuwa waandishi bila kujua code of ethics!

SarafinaLindiweMsuya said...

Ni kweli kabisa. Inasikitisha sana kuona kuwa wanataka kuwa waandishi bila kujua code of ethics!

SarafinaLindiweMsuya said...

Ni kweli kabisa. Inasikitisha sana kuona kuwa wanataka kuwa waandishi bila kujua code of ethics! Mbaya zaidi hamna sheria zinazowabana kufuata regulations.