Showing posts with label Dakika 90 za dunia. Show all posts
Showing posts with label Dakika 90 za dunia. Show all posts

Saturday, October 11, 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA. Kumalizika kwa mkutano wa DICOTA 2014


Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (DICOTA) limemaliza mkutano wake wa mwaka Jumapili ya Oktoba 5 jijini Durham jimbo la North Carolina ambao kwa wengi waliohudhuria, wameonyeshwa kuridhishwa nao
Mwenzangu Mubelwa Bandio, anayo taarifa kamili.

Hii ni sehemu ya ripoti za Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 11, 2014

Saturday, April 12, 2014

[AUDIO]. DAKIKA 90 ZA DUNIA: Maadhimisho ya Kwibuka20, Washington DC

 Wiki kama hii, miaka 20 iliyopita, nchi ya Rwanda ilishuhudia kuanza kwa mauaji ambayo kwa siku 99 zilizofuata, yaliacha historia mbaya na ambayo itaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Ndani ya siku 100, watu wanaokadiriwa kufika milioni 1 waliuawa katika mauaji ya kimbari.
Miaka 20 baadaye (mwaka huu), dunia nzima imeungana na Rwanda kukumbuka kile ambacho wengi wanaona kuwa kilitokea na kuachwa kuendelea kutokana na Jumuiya ya kimataifa kutoingilia kati na kutoa msaada muafaka kwa wakati muafaka.
Kumekuwa na matukio mbalimbali kukumbuka mauaji ya kimbari ya Rwanda ambayo yamefanyika duniani kote, Kutoka Kigali Rwanda mpaka hapa Dar-Es Salaam na hata huko Washington DC.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Aprili 12, 2014

Sunday, April 6, 2014

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Mauaji kwenye kambi ya jeshi Fort Hood

Jenerali Mark Milley, Kamanda wa Fort Hood akizungumza na waandishi wa habari
Wiki iliyopita, nchi ya Marekani ilikumbwa na mauaji mengine yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi huko Fort Hood, Texas.
Jumatano Aprili 2, askari mmoja wa Jeshi la nchi hiyo, Ivan Lopez ambaye inasemekana alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo, aliwafyatulia risasi na kuwaua wanajeshi wenzake 3, kujeruhi 16 kabla hajajigeuzia bastola na kujiua
Mauaji haya, yanarejesha kumbukumbu ya mauaji makubwa kabisa kutokea kwenye kambi za jeshi nchini humo, yaliyotokea kwenye kambi hiyohiyo takriban miaka 5 iliyopita.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Aprili 5, 2014

Saturday, March 22, 2014

Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011. Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.
Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 22, 2014

Saturday, March 15, 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Mfungwa aliyekuwa akisubiria KIFO aachiwa huru

Picha iliyopigwa na mwanasheria wake, ikimuonyesha Bwn Ford, siku ya kwanza kama mtu huru baada ya miaka 30 jela kwa kosa ambalo hakufanya. Photo Credits: theatlantic.com
Wiki hii, mmoja wa wafungwa nchini Marekani, ambaye alikuwa kwenye orodha ya wanaosubiri kunyongwa kutokana na kuhukumiwa kifo kwa mauaji  aliyotuhumiwa kufanya mwaka 1984 aliachiwa huru baada ya Jaji kukubali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa ni yeye aliyeshiriki mauaji hayo.
Sasa, mfungwa huyu atalipwa dola 25,000 kwa kila mwaka aliotumikia kifungo hicho, lakini, kwa mujibu wa sheria ya Louisiana, kiwango cha juu anachoweza kulipwa ni dola 250,000
Ina maana, atalipwa kwa miaka 10 tu kati ya 30 aliyokaa gerezani
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 15, 2014

Saturday, February 22, 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?

Photo: Mobile88.com Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi kifupi tu. Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni 19 kununua WhatsApp. Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?
Bahati Alex (L) na Mubelwa Bandio (R)
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM). Hii ilikuwa ripoti ya Februari 22, 2014

Saturday, February 8, 2014

Rekodi katika michuano ya Olimpiki Sochi

Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia.
Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake
Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake.
Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Februari 8, 2014