Showing posts with label Darasa. Show all posts
Showing posts with label Darasa. Show all posts

Thursday, September 7, 2023

Darasa 45: Maisha yetu kama zoezi la matofali


Darasa linakukumbusha kuwa...… Watu watatu ni mimi na wewe. Watu kumi ni mimi na wewekwa sababu kuna watu tumesimama nyuma yao. Lakini pia, ni watu wetu wa karibu wanaosimama nyuma yetu. Mtu wa kwanza ni yule ambaye anapokuwa na kitu cha kutimiza hasubiri watu wakimbie pamoja naye. Huchakarika kadiri ya uwezo wake bila kulalamika wala kuvunjika moyo kwa kuwa hana msaada. Mtu wa pili ni yule ambaye anapokuwa na jambo lake ni lazima apate msaada ndiyo alifanye kwa kasi. Mtu wa hivi bila kusukumwa haendi wala hawajibiki ipasavyo. Ni ngumu kutimiza mambo yake ipasavyo bila kuegemea wengine. Mtu wa mwisho ni yule ambaye ni mlalamishi. Hutaka jambo lake watu wote waache shughuli zao kwa ajili yake. Hata kwenye ambayo ni wajibu wake kwanza, hulazimisha wengine kuwajibika kwa ajili yake, ama sivyo hununa au huzira na hata kuvunja ukairbu na mtu kwa sababu tu hakusaidiwa jambo ambalo ni wajibu wake. Wale watu 10 nyuma ya watu. kila mmoja ajitafakari anavyowatendea watu wake wa karibu pale wanapotegemea sapoti yake. Tujiulizetunaangukia kwenye kundi gani? Darasa linakutakia tafakuri njema.

Friday, August 11, 2023

Darasa 38: Hakuna asiye na cha kutoa na hakuna asiyehitaji

Darasa linakukumbusha kuwa.......… Usiache kuwa jambo zuri kwa watu wengine hata wakati ule unapopitia magumu yako. Kuna watu wanaishi maisha ya kulalamika kila siku. Wao hivi wao vile. Kuna watu ni wenye kujiona wanastahili kupokea tu na si kutoa kwa sababu hawana pesa, au hawana hiki au kile. Kuna watu wamejipa hatimiliki ya kutendewa mema na si kutenda. Rafiki, hata katikati ya magumu yako nenda ukawe jambo zuri kwa mtu. kuna namna nafsi yako itainuka. Kuna baraka utaichota. Nenda kawe jambo zuri kwa mtu. Kwa maneno au vitendo; kwa maneno na vitendo. Kaweke tabasamu usoni pa mtu. Darasa linakutakia tafakuri njema.



DARASA la Laura Pettie ni makala zinazokujia kila Jumanne na Alhamis kupitia akaunti yetu ya YouTube. Unaweza kusikiliza makala zote kwa  leo kubofya PLAYLIST HII au tembelea akaunti yetu hii ya YouTube