Friday, August 11, 2023

Darasa 38: Hakuna asiye na cha kutoa na hakuna asiyehitaji

Darasa linakukumbusha kuwa.......… Usiache kuwa jambo zuri kwa watu wengine hata wakati ule unapopitia magumu yako. Kuna watu wanaishi maisha ya kulalamika kila siku. Wao hivi wao vile. Kuna watu ni wenye kujiona wanastahili kupokea tu na si kutoa kwa sababu hawana pesa, au hawana hiki au kile. Kuna watu wamejipa hatimiliki ya kutendewa mema na si kutenda. Rafiki, hata katikati ya magumu yako nenda ukawe jambo zuri kwa mtu. kuna namna nafsi yako itainuka. Kuna baraka utaichota. Nenda kawe jambo zuri kwa mtu. Kwa maneno au vitendo; kwa maneno na vitendo. Kaweke tabasamu usoni pa mtu. Darasa linakutakia tafakuri njema.DARASA la Laura Pettie ni makala zinazokujia kila Jumanne na Alhamis kupitia akaunti yetu ya YouTube. Unaweza kusikiliza makala zote kwa  leo kubofya PLAYLIST HII au tembelea akaunti yetu hii ya YouTube

No comments: