Showing posts with label Jukwaa Langu. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa Langu. Show all posts

Monday, May 7, 2018

Kipindi cha JUKWAA LANGU. Mei 7, 2018

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo ndani ya Kilimanjaro Studios, wageni wetu studioni ni kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoitumikia jamii ya wahitaji nchini Tanzania.
Katika saa la kwanza tutakuwa na uongozi wa SHINA INC ambao tangu mwaka 2002 wamekuwa wakisaidia jamii zenye uhitaji nchini Tanzania. Wana mengi ya kutushirikisha

Kwenye saa la pili tutakuwa na wakuu wa Help for Underserved Communities Inc. (HUC-USA) ambao wanajishughulisha kutoa textbooks mashuleni, VETA Scholarships na kusaidia matibabu ya macho nchini Tanzania.

Lakini tutaanza na mrejesho wa maadhimisho ya TANZANIA DAY 2018 yaliyofanyika Dallas Texas.

Ni kipindi cha JUKWAA LANGU, leo Jumatatu (Mei 7, 2018) na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Facebook live (Mubelwa Bandio na Kwanza Production) ama Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama piga simu 202-683-4570
*******************************
PRODUCER: Mubelwa Bandio

Wednesday, February 7, 2018

JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 2 TANO LADIES

Katika sehemu ya pili ya kipindi cha Jukwaa Langu Jumatatu hii tumetembelewa na TANO LADIES.
"Wadada" walioamua kuwa sehemu ya msukumo wa maendeleo ya wanawake na mabinti zetu.
Wamezungumzia (pamoja na mambo mengine) nafasi na mchango wao kama Diaspora kwa Tanzania, na pia wanavyopanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake duniani.
Unaweza ona sehemu ya video yao hapa
https://vimeo.com/253461804

JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi na waalikwa wengine kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

Kipindi cha JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 1 SARATANI

Katika sehemu ya kwanza ya kipindi cha Jukwaa Langu, tumezungumzia kuhusu siku ya SARATANI DUNIANI iliyoadhimishwa  Feb 4.
· Takwimu za maradhi haya zinaonyesha kwamba kifo 1 kati ya 6 hutokana na maradhi haya.
· Wajua, namna yanavyoathiri nchi zinazoendelea? Ni 20% tu zenye takwimu sahihi kuwezesha kupambana na maradhi haya.
Unajua ni tabia gani maishani zinaweza kuondoa 30% ya Saratani?
· Unafahamu harakati zinazofanywa na Diaspora katika kupambana na maradhi haya?
· Tulikuwa na Mwanasayansi na Mtafiti wa aina mojawapo ya Saratani, pamoja na mwanaharakati kujadili haya.
......
JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe na waalikwa wengine studioni kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf

Monday, September 12, 2016

Kipindi Cha Jukwaa Langu Sep 12 2016....Tetemeko Bukoba

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania
Wadau Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini humo.
Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .

Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093
Karibuni

Monday, March 28, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu March 28 2016 (Full)


 Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA.
Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kujadili kuhusu Jumuiya za waTanzania nje ya nchi na changamoto zake, na pia kuhusu DICOTA na mkutano wao mkuu wa mwaka huu
KARIBU

Tuesday, December 8, 2015

Mahojiano na DC Paul Makonda katika kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 7 2015


Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.
Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.
Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu
KARIBU

Tuesday, December 1, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 30 2015 (Full Show)


Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali yatano ya Tanzania
Yanayofanyika yanaleta taswira gani kwa Tanzania? Na Je!
Yataendelea ama?

Monday, November 23, 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Nov 23 2015 (MJADALA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Magufuli akizindua Bunge la 11
Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali ya Tanzania baada ya kuzinduliwa kwa Bunge la 11.
Mjadala huu ambao ulifuata HABARI kutoka magazeti mbalimbali, umehusisha wadau toka Marekani, Canda na India
Karibu
Waweza kutusikiliza kupitia tovuti zetu www.kwanzaproduction.com na www.vijimamboradio.com

Tuesday, November 3, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 2, 2015 (Full Show)

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015

Monday, October 26, 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Okt 26 2015 (FULL)

Photo Credits: dw.com/sw

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Na leo, tulizungumzia Tanzania baada ya Uchaguzi wa jana Oktoba 25, 2015

Tuesday, October 20, 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Oct 19 2015 (Full)

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Ni kipindi cha mwisho kabla ya uchaguzi, na washiriki wengi walishiriki kutoa mchango wao kuhusu mchakato ulivyokuwa, na neno ama wosia wao kwa waTanzania wote
KARIBU

Tuesday, August 11, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu wiki hii (Aug 10, 2015)

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tulijadili kuhusu kung'atuka uongozi kwa Prof Ibrahimu Lipumba na pia kukua kwa ufuasi kwa mgombea uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa.
Pia, hotuba ya Zitto Kabwe huko Iringa, na mengine mengi
Ungana na Dj Luke Joe (wa hapa), Rose Chitallah, Shamis Abdul (wa hapa) na Mubelwa Bandio (wa hapa) toka Kilimanjaro Studio, Beltsville Maryland na Jeff Msangi (msome hapa) kutoka Toronto Canada kujadili haya.
Pia, kulikuwa na simu za wasikilizaji kadhaa
KARIBU

Tuesday, August 4, 2015

Mahojiano na Balozi Limerata Mulamula kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU

 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Tuesday, July 28, 2015

Mahojiano na Balozi Amina Salum Ali kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU

Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali
Karibu

Mazungumzo na mtangazaji Rose Chitallah kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU

Mubelwa Bandio na Rose Chitallah studioni
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na mtangazaji Rose Chitallah
Karibu

Kipindi cha Jukwaa Langu Julai 27 2015 (FULL)

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
KARIBU

Monday, July 13, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU, Julai 13, 2015

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali akiwemo Katibu Uenezi na Itikadi wa CCM Ndg. Nape Nnauye kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
KARIBU