Saturday, March 22, 2014

Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011. Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.
Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 22, 2014

1 comment:

Nicky Mwangoka said...

Worthy calling it "The Modern miracle"