Sunday, July 28, 2013

Kanisa kuadhimisha miaka mitano ya huduma Washington DC

Kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries linalotoa huduma za kiroho na kijamii katika eneo la DMV (Washington DC na vitongoji vyake) linataraji kuwa na siku tatu za maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
Katika maadhimisho hayo yatakayofanyika kuanzia Agosti 9 - 11, kutakuwa na mafundisho ya neno la Mungu yatakayoongozwa na Mchungaji Nathanie Kigwila pamoja na Mwinjilisti Ezekiel Mwalugaja.
Pia kutakuwa na Tamasha la uimbaji litakaloshirikisha waimbaji wa hapa Marekani pamoja na waimbaji wa injili wa kimataifa toka Tanzania Upendo Kilahiro na Christina Shusho.
Mwisho kutakuwa na ibada maalum itakayokuwa ni kilele cha maadhimisho hayo ambayo itafanyika Jumapili ya Agosti 11.
Anwani ni
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

NYOTE MNAKARIBISHWA

No comments: