Tuesday, October 11, 2011

Mahojiano na J Sisters

Dada wawili kati ya wanne wa JSisters Jenny (pili kushoto) na Julie Julz Julius (wa pili kutoka kulia) wakiwa na Sunday Shomari wa Idhaa ya Kiswahili ya VOA na pia www.sundayshomari.com (kushoto) na Mari Damian (kulia) wa www.strictlygospel.wordpress.com baada ya mahojiano ya video hapa chini
J Sisters wakiwa pamoja na kwaya ya kanisa wenyeji la The Way of The Cross pamoja na waimbaji waalikwa Upendo Kilahiro, Upendo Nkone na Christina Shusho walipopanda jukwaani pamoja
J Sisters wakishambulia jukwaa
Ndugu wawili kati ya wanne wanaounda kundi la J Sisters wakieleza mengi kuhusu historia ya kundi lao, wakifafanua utata juu ya wao kusikiliza nyimbo za wasanii ambao hawajaokoka, muziki wa injili kwao ni nini, ukabilianaji wa ratiba baina ya shule na huduma, mambo wanayokabiliana nayo kama wasanii wa nyimbo za injili na mengine mengi.
Video imezalishwa na Mubelwa Bandio (www.changamotoyetu.blogspot.com) na waliketi na Dada Mary Damian (www.strictlygospel.wordpress.com)
KARIBU

Shukrani za pekee kwa J SISTERS ambao walitoa muda wao kuwezesha hili.
Baraka kwenu