Wednesday, October 12, 2011

Happy EARTHDAY Pau. Namshukuru Mungu kwa......

SIRI YA MAISHA niliyojifunza ni kuwa UNAFUNZA UNAPOFUNZWA. Binafsi NIMEKUA NILIPOKUZA / NIKIKUZA.
"Mshiko wa kwanza". Mengi akilini.
Leo namshukuru Mungu kuwa mwanetu mpenzi Paulina Arianna ametimiza miaka 2. Safari yake haikuwa nyororo na wala sikutegemea iwe hivyo, lakini kuna mengi mema niliyookoteza njiani. Na la kwanza (ambalo si siri) ni UJASIRI WA MAMA YAKE. Kwangu.......NAMSHUKURU MUNGU KWA UWEPO WAKE.
Duh!!! Mara si mimi ama sisi tena, bali naye.
Namshukuru Mungu kwa uhai wa asomaye hapa, kwani lengo si kusherehekea nami siku hii ya "stress buster" wetu, bali pia kushiriki hisia na mafunzo tuyapitiayo njiani. Katika miaka miwili hii nimejifunza mengi. Kuhusu wengi na kwa namna nyingi. Kuanzia ushauri wa MALEZI mpaka namna ya kukabiliana na mambo mengi ya utoto na watoto. NAWASHUKURU WOTE KWA HILO
Nimejifunza kushukuru kwa kuonyeshwa kilicho upande wa pili ambao sikupata kuujua (kama NICU) na pia tumaini kulingana na mahitaji ya wengine. Nimefunzwa UVUMILIVU na pia TUMAINI.
Uanaharakati kauanza mapema hivi? T-Shirt inapingana na "dubwana" lililo nyuma yake.
Lakini yote juu ya yote Paulina amekuwa chanzo cha furaha. Kumuona nirejeapo nyumbani toka kazini ilikuwa ni sababu tosha kurejesha tabasamu ambalo wakati mwingine hupotezwa na watu wenye fikra "kandamizi" tunaofanya nao kazi. Lakini si kwetu tu (mimi na mamaye), bali pia ametuunganisha na wengine wengi ambao walipata muda wa "kuserebuka naye"
Hapa ni yeye na "KAKA MUKUBWA" Idd Ligongo.
Japo hajawahi kuwa mtulivu pichani, lakini zile apigwazo akiwa HANA utulivu hutulia. Ama? Lol
Namshukuru Mungu kwa familia hii. Ambayo kwa miaka miwili sasa imekuwa zaidi ya ilivyokuwa kabla. Upendo ndio umekuwa MKUU ZAIDI
Hii ni BARAKA kuu ambayo haijalishi kuna "laana" gani mbele yangu, namshukuru Mungu kuwa hii ya hawa wawili (so far. Lol) nikingali nayo. NAMSHUKURU KWAYO
Lakini bado safari ya UPENDO huu haikuwa rahisi kama wengi wanavyoweza kudhani. Kuanza malezi ukiwa mbali na msaada wowote hakikuwa kitu rahisi. Lakini mara zote nilifarijika kwa kumsikiliza mwanamuziki Darius Rucker alipoimba "It won't be like this for long. One day we'll look back laughing at the week we brought her home.
This phase is gonna fly by, so baby, just hold on. It won't be like this for long"
Na ukweli ni kuwa sasa ni mwaka wa pili (japo kuangalia nyuma ni kama juzi tu).
Na kwa sasa ukiwa na Bibi, Babu, Baba na Mama wakubwa na wadogo, Wajomba, Shangazi na ndugu wengine ndani ya Tanzania...NAPENDA KUWAAMBIA (wewe na Mamako) kuwa NAWAPENDA SANA, NAWAKUMBUKA SANA, NA NAJUA "It won't be like this for long". Punde tutakuja kuungana tena na kuendelea kusherehekea maisha tuliyobarikiwa kuwa nayo.
Happy EARTHDAY Paulina.
Nakupenda na nakukumbuka sana. Punde tukijaaliwa tutaungana tena
NIUSIKIAPO WIMBO HUU, NAKUKUMBUKA SANA.
Love you

11 comments:

Subi Nukta said...

Libras balance the world!
Pongezi kwenu wazazi.
Heko sana!
Heri kwa sikuku ya kuzaliwa Pau!
Love you lil angel!

Mary Damian said...

Hongereni kaka! Mungu azidi kumtunza Pau! Mungu awatunze wazazi wake!

Ebou's said...

M/Mungu akujalie Kheri na baraka tele Prencess wetu Pau, Mzee wa swahilivilla pamoja na wadau wote wanakutakia kila la kheri popote pale ulipo, we still love you.. si urudi ujee kumpa kibano baba huku anakumiss!

Ebou's said...

Ohh nimerudi tena nimesahau kusema Happy Birthday Princess Paul

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

uuuuuwwwwwiii mwombeki anakusubiria ufike bukoba na kukupa salamu na kukupongeza pia.

waiyhukage kaisiki

Yasinta Ngonyani said...

HERI SANA KWA SIKU YA KUZALIWA SHANGAZI/RAFIKI pAU. PIA HONGERA NYINGIIIIII SANA KWA WAZAZI.

Rachel Siwa said...

Hongera sana da'Pau,Mungu akubariki n katika yote,Hongereni Wazazi na Mungu awape hekima kwenye malezi ya mtoto wetu.

Anonymous said...

HAPO MUBELWA UMEPATA MKE SISTER ESTHER HUWA NA MKUBALI SANA YAANI HUWA ANA AKILI SANA UMEBARIKIWA SANA AF HUWA MSAFI SANA HADI RAHA,PIA NICE FAMILY MUBELWA JAMANI NA WISH NAMI MUNGU ANIJALIE NAMI FAMILIA NZURI KAMA YAKO.

Anonymous said...

HE NIMERUDI TENA JAMANI HAPPY BIRTHDAY MY DEAR PAU.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera Paulina na Mungu Aendelee kukubariki. Utaonana lini na somo yako Arianna (japo tunaandika Ariana) aliyeko huku Florida?

Simon Kitururu said...

Happy Birthday Paulina Arianna!