Friday, October 14, 2011

Natamani ungekuwepo ukayaona haya

Mwl Julius Kambarage Nyerere. 1922 - 1999
Naangalia uchumi wa dunia unakoelekea na namna mataifa yanavyochukua umiliki wa uendeshaji wa shughuli muhimu za kiuchumi kisha naishi kujiuliza kama hii si sehemu ama aina mpya ya ujamaa?
Nikisoma MAKALA HII napata ka-picha kadoogo kwa mbali kuwa kama Mheshimiwa Baba wa Taifa Mwl Nyerere angekuwepo, basi angeweza kurejea kusema mawili matatu ambayo alishawahi kusema miaka kadhaa iliyopita na ambayo yamekuwa katika hotuba zake na nukuhu zilizopo sehemu mbalimbali.
Angekupweo leo hii angesemaje? Hakuna mwenye jibu sahii lakini kwa kuwa alishaonya kwenye hotuba zake, ninaloweza kuhisi ni kuwa angekumbusha kile alichosema ambacho wengi hawakudhani kuwa kingetimia na ungekuwa wakati wa kudhihirika tena kwa maono yake.
Miaka 12 tangu atutoke, bado unakumbukwa na binafsi natamani ungekuwepo ukanona viongozi wengi wa barani Afrika ambao wanayumbishwa misimamo yao na hata kupindisha ilani zao zilizowapa nafasi ya kuwatumikia wananchi, na kuwa kama hawatambui maslahi ya wananchi wao mpaka WAPANGIWE na mataifa makubwa ambayo baadhi ya viongozi wao hawajui lolote kuhusu nchi hizo.
Natamani ungekuwepo ukaona viongozi wetu wa sasa ambao hawawezi kusimamisha mapigano mpaka watishiwe na mataifa fulani, ama wawekewe vikwazo na fulani.
Natamani ungekuwepo ukaona viongozi wasiothamini uhai wa wananchi wao kwa kuendeleza vita baina ya wanachi wa nchini mwao mpaka waamriwe kuacha na mataifa ya nje.
Ungekuwepo basi ungeona viongozi wanaotumia mwanya wa elimu na mfumo m'bovu wa utawala kujilimbikizia mali kwa jasho la wahitaji (sio maskini) wengi Barani mwetu.
By the way, hayo ni ya Afrika kwa ujumla, ya nyumbani Tanzania yanasikitisha zaidi. Utayasoma kwingine ukipata nafasi.
Ni viongozi wachache tunaoweza kujivunia na ambao msimamo wao unaendelea kuonekana kuwa wazi an usioyumbishwa na "viranja" wa dunia. Wengi wanamjua Mandela kama kiongozi hodari, shupavu na jasiri katika Afrika na wenbgi wanakubaliana na hilo, lakini pia kama alivyosema Mchambuzi na Mwandishi hodari Freddy Macha, kabla ya Mandela alikuwepo Nyerere na ujasiri, uwezo na upeo wake bado unaheshimika miongoni mwa wengi.
KAMA UNAYAONA HAYA NA MENGINE MENGI BASI ENDELEA KUTUOMBEA NA KAMA HUYAONI BASI TWAKWAMBIA YALIYOPO LAKINI KAMA HUTUSIKII, NDIO MAANA TUNAENDELEA KUTAMANI TU KAMA UNGEKUWEPO.

Ulitekeleza sehemu yako na huko uliko PUMZIKA KWA AMANI.

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo ni kwamba marehemu hawezi kuwaombea walioko hai!! ila ujamaa ni utu, kuupinga ujamaa ni sawa na kuupinga utu, wakati kuupinga utu ni ndoto tu ya mchana tena

Simon Kitururu said...

Hivi huyu jamaa angekuwepo na akayaona angekuwa na lakufanya zaidi ya kuloloma tu kama wengine?


Kwani hawa jamaa walioshika patamu (samahani -hatamu)sikuhizi wanajali maneno ya mtu?


Nawaza tu kwa sauti!

emuthree said...

Hayupo lakini mungu yupo nasi , ipo siku!

Anonymous said...

I am with you kaka, very good , sema ukweli