Thursday, October 20, 2011

Tanzania yangu....Na UNAFIKI wa kumuenzi Mwl J. K Nyerere

"Speak the truth and speak it over. Love God and live is my only destination. Yeah, i heard your speeches, man and your empty promises (promise is a confortto a fool), but now that i know, your words are dangerous" NASIO FONTAINE
"If you stand for the truth, you'll always stand alone" Lucky Dube
Kama hauko kwenye kurasa za jamii (kama Facebook) basi umeshindwa kuona "wiki ya Nyerere". Yaani kulikuwa na matumizi makubwa ya picha za hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere pamoja na kauli na FALSAFA zake. Lakini wiki inakamilika leo na MAISHA YANASONGA.
Yanasonga kwa maana ya kwamba FALSAFA, KAULI NA HATA KAZI ZAKE ZINAENDELEA KUPUUZWA NA KUTOFUATWA.
Nianze na "hapa karibu" na nilipo (maeneo ya Washington DC) ambapo kwa mwaka wa nne mfululizo kumekuwa na maadhimisho ya kuenzi KAZI NA MAISHA ya hayati Baba wa Taifa, na blogu hii ilihudhuria maadhimisho hayo (kama ilivyofanya miaka mitatu iliyopita) ili kuweza kujuvya wananchi kile kilichotokea.
NA NDICHO NINACHOFANYA SASA.
Kama ilivyokuwa katika maadhimisho ya miaka mitatu iliyopita (mwaka mwaka 2008 hapa na hapa, mwaka 2009 hapa na mwaka 2010 hapa, maadhimisho ya mwaka huu yalikuwa na mambo mengi mema kwa waTanzania na wote wenye mapenzi mema na Tanzania.
Jambo moja ambalo lilikosekana na kwa hakika kuonekana kusikitisha wengi (nami nikiwemo) ni kukosekana kwa mwakilishi yeyote kutoka ubalozini.
Na hili limesikitisha zaidi kwa kuwa ubalozi wetu ulipata barua pekee kadhaa za kuomba mwakilishi baada ya taarifa kuwa Balozi asingeweza kufika lakini hakukuwa na majibu wala mwakilishi. Na zaidi ni namna ambavyo uBalozi wetu ambao umeonyesha ushirikiano kwenye mambo mbalimbali (mengine madogo kabisa) umeshindwa kutuma mwakilishi hata mmoja katika maadhimisho ya kiongozi ambaye amekuwa sehemu ya mafanikio makubwa katika ukuaji wao na ambaye amekuwa akikaririwa kwenye hotuba kadhaa za watumishi wa hapo ubalozini.
Na siku moja baadae, ubalozi umetuma uwakilishi kwenye mchezo wa soka baina ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga (achilia mbali matukio mbalimbali ambayo tunaona yakiripoti uwepo wa Balozi ama mwakilishi toka ubalozini).
Maadhimisho haya yameandaliwa na mMarekani mwenye asili ya AFRIKA ambaye alikuwa na bado ana mapenzi na kazi za hayati Baba a Taifa.

Na licha ya juhudi zote za kugharamia maadhimisho hayo, BADO HAPATI USHIRIKIANO TOKA UBALOZINI. Mimi nilishirikishwa katika kujaribu kuitangaza na ndipo nilipotengeneza video hiyo hapo juu (AMBAYO NAWASHUKURU SAANA BLOGGERS WENZANGU KWA KUISAMBAZA MARA KADHAA), na kisha nikashirikishwa kwenye maendeleo ya maandalizi yake ikiwa ni pamoja na kupata nakala za barua pepe zilizokuwa zikitumwa uBalozini kuomba mwakilishi. Lakini si barua wala simu iliyorejeshwa. Swali la kwanza mimi kujiuliza ni kuwa NI NANI HASA ALIYEKUWA NA WAJIBU WA KUANDAA HILI? Huyu mMarekani aliyekutana na Hayati Baba wa Taifa nchini China (kama alivyosema kwenye hiyo video hapo juu) ama maadhimisho haya yalistahili kufanywa na Ubalozi wakishirikiana na jumuiya za waTanzania wa hapa + DICOTA?
Umati mzima uliohudhuria maadhimisho ya mwaka huu kuenzi kazi na maisha ya Hayati Baba wa Taifa
Katika maadhimisho ya miaka Hamsini ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyoandaliwa na Ubalozi kwa ushirikiano na DICOTA, tuliona bango la ukaribisho wa wageni likiwa na nukuu ya Nelson Mandela. Na hii si kusema kuwa Mandela hakustahili kuwepo, ama hana hadhi ama hana nukuu za kutosha, lakini kuzungumzia UHURU wa TANZANIA na kumuweka / kuwaweka kando walioshiriki kwa asilimia kubwa kuusaka, ni DHIHAKA.
Na sasa kuona ubalozi huohuo "unasahau" kupeleka mwakilishi kwenye maadhimisho hayo, ni jambo ambalo binafsi lilinisikitisha sana. Lakini kilichonisikitisha zaidi, ni kutojibiwa barua pepe niliyoomba mawasiliano na yeyote mwenye kuweza kufafanua jambo hili.
Lakini kwa kuwa leo ni Ijumaa, siku ambayo huwa tunapata BURUDANI, UELIMISHAJI na UKOMBOZI WA KIAKILI kupitia kazi za wasanii wa reggae, basi twende visiwa vya Dominika ambako tunakutana naye Nasio Fontaine, anayesisitiza "tittle" ya post kwa wimbo HYPOCRITES.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante kaka kutujuza hili. Pengine mshangao wako unaweza usiufikie ule wangu kuhusiana na Nyerere Day. hapa nyumbani siku hiyo palifanyika uzinduzi wa mbio za mwenge kule Butiama ikiwa ni sambamba na miaka 50 ya uhuru kwa kuenzi juhudi za Mwalimu. jambo ambalo nilishangazwa nalo ni kitendo cha mkuu wa kaya kutohudhuria wakati huweza kuhudhuria matukio mengi tu madogo madogo ambayo kwa mtazamo wangu umuhimu wake hauufikii umuhimu wa siku hiyo.

ni hayo tu!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Mtanga.
KARIBU UWANJANI.
Ya hapa yalisikitisha maana sina hakika kuwa Ni nani hasa aliyestahil kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere. Huyu mMarekani ambaye alikutana na Nyerere China ama waTanzania waishio hapa?
Sasa na Mkuu wa Kaya naye "katia timu"?
Kaaazi kwelikweli

sam mbogo said...

Mzee wa changamoto,nasema pole sana.hapo umekumbusha kitu kimoja juu ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu walioajiliwa na serikali.waweza kuta hapo ni uzembe wa mtu mmoja ambaye alitakiwa kuwajibika katika swala hilo. sasa wakija kutahamaki tayari washaharibu wakiulizwa wanabaki wanajikanyakaga.niaibu kushindwa kutoa mwakilishi kwa shughuli kubwa kama hiyo.kaka s.

Albert Kissima said...

Inasikitisha sana kwa hakika. Inawavunja moyo wale wote wenye nia njema ya kuisaidia Tanzania kufikia malengo yake. Ni dhahiri kabisa kuwa Tanzania ilipuuza maadhimisho hayo.

Hili bado ni tatizo sugu kwa watawala wetu. Ukijaribu kufuatilia ni mikakati gani madhubuti iliyowekwa na serikali ya Tanzania ili kuepusha majanga yanayogharimu maisha ya watu kama la kuzama kwa meli, hutopata mkakati endelevu hata mmoja. Makosa ya Mv Bukoba, ndio hayo yaliyogharimu maisha ya mamia ya watu katika Ajali ya Mv islender. Watawala wanaPUUZA kwa kutoa salamu za rambirambi na mambo yanaishia hapo.