Tuesday, October 21, 2008

"If you can't go back, look back and make sure you stay connected to the Motherland" Ms Holland

Ms Mazie Green Holland akizungumza katika siku ya Maisha na Kazi za Mwl Nyerere

WaTanzania, waAfrika na wote wenye asili ya Afrika wamekumbushwa kutosahau walikotoka na kisha kufanya kila wawezalo kusaidia jamii ya "nyumbani" mahali popote walipo.
Rai hiyo imetolewa na Bi Mazie Green Holla kutoka The Diaspora African Forum wakati akitoa neno kwenye siku ya kukumbuka na kusherehekeha maisha na kazi za Mwalimu J. K. Nyerere iliyofanyika jioni ya Jumamosi ya tarehe 18 Oktoba kwenye ukumbi wa Kanisa la Mosaic lililopo 16th Street, NW jijini Washington DC.
Bi Mazie amesema japo si wote wenye kujua sehemu halisi iliko asili yao, lakini kwa pamoja weusi wengi twatambua kuwa tumetoka Afrika na ni wajibu wa kila mmoja wetu kuungana na kulisaidia bara hilo. Amesema kwa wale wasioweza kurejea barani Afrika kwa kutotambua chimbuko lao halisi, bado wanaweza kurejesha fikra zao nyuma na kutafuta namna njema ya kuunganishwa na Bara lao.
Akizungumzia kuhusu muunganisho wa waAfrika kupitia Diaspora hiyo yenye makao makuu yake nchini Ghana, Bi Hollad amesema imeweza kuwakusanya na kuwashirikisha waAfrika wengi waishio nje ya Bara lao kusaidia kukamilisha malengo na madhumuni makubwa ya Diaspora hii ya Afrika.
Kati ya madhumuni makuu ya The Diaspora African Forum ni kusaidia kuondoa kiwango cha umaskini katika nchi za Afrika zinazotegemea misaada ya nje kuendesha bajeti zao jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine imeziweka nchi hizo katika hali iliyopo.
Pia amesema Diasporas wanasaidia kunyanyua hali ya maisha ya waAfrika wenzao kupitia uboreshaji wa miundombinu, uwezeshwaji wa kijamii, chakula, makani na mambo mengi mengi.
Forum hiyo pia ni kati ya makundi yenye uwezo mkubwa kiuchumi ambayo yanasaidia kuboresha uchumi wa nchi zenye uhitaji.
Waweza kusoma mengi juu ya The Diaspora African Forum kwa kubofya http://www.diasporaafricanforum.org/home.htm


Ni CHANGAMOTO YETU sote DIASPORAS kuwa msaada wa namna yoyote katika kufanikisha nia njema za kuisaidia Afrika na waAfrika kwa ujumla.


DIASPORA: any population sharing common ethnic identity who were either forced to leave or voluntarily left their settled territory, and became residents in areas often far removed from the former. It is converse to the nomadic lifestyle

No comments: